Mweka Hazina anachaguliwa kati ya wanachama kuunda sekretariet ya chama (Komu) na mhasibu ni mwajiriwa..Na labda, awe Mweka Hazina badala ya Mhasibu!
Mweka Hazina anachaguliwa kati ya wanachama kuunda sekretariet ya chama (Komu) na mhasibu ni mwajiriwa..Na labda, awe Mweka Hazina badala ya Mhasibu!
Rev.Mzito K. asante, maelezo yako yanajieleza yenyewe kuwa baada ya hiyo software mpya kuja na kuziba mianya ya watu ndipo chokochoko zilipoanzia. Haya mengine ya kufukuzwa kwa kuonewa is another case, wewe umeleta kutokana na uchunguzi wako, sasa kama kuna mtu anadhani Mwigamba alionewa atuletee uchunguzi wake na si kudhani alionewa kwa ku guess.sikukujibu mara ya kwanza uliposema Mwigamba ni mtaalam wa telecom, nilijua utakwama mahali. Nashukuru umeonyesha hekima yako kwa kuwa mkweli.
Kilichopo ni kuwa Mwigamba alikuwa na utaratibu wa kuleta ripoti zilizokuwa zimekaa kiubabaishaji na zilikuwa zinachelewa kutoka. Accounting package iliyoletwa na Josephine iliziba mianya ya wao kufanya ubabaishaji wao. Baada ya yeye kugundua hilo akaikataa kwa kujitetea kuwa ile ni database tu. Alipoambiwa ataje tofauti ya database na accounting package ndio ukawa mtihani. Nadhani umeelewa sasa
Nilichokiona hapa ni kuchafua watu bado sijapata connection ya watu hao na tunte/tii/paa. Madhara yake ni makubwa sana kwa cdm ni bora uzi ukafutwa
tatizo la cdm fans ni kuamini kila kitu bila kufikirisha ubongo kwa mapana
Mkuu Juma Kidogo, usiwe kipofu kwa mambo yanayoonekana waziUmeandika waraka mrefu ambao kwa sehemu kubwa bado haujajibu tuhuma zilizoletwa. Sehemu kubwa ya waraka wako umejaribu kuwapambanua wale walioleta tuhuma hizo ni kina nani. Nadhani si muhimu kwetu kujua mleta tuhuma ni nani! Ili iweje, thibitisha hapa kuwa, tuhuma hizo si za kweli ili upingane na Dr Slaa mwenyewe ambaye ki msingi amekubali. Nilitegemea jambo moja kubwa baada ya Tuntemenke kushusha scud zile, nilitegemea wana CDM makini kuanza uchunguzi wa kutafuta ukweli kuhusu tuhuma hizo ili wasafishe chama, badala yake nao wanawashutumu waliosaidia kufukua maovu. Nikuulize swali dogo. Ikitokea tuhuma hizo zikathibitishwa kuwa ni za kweli, mtaweka wapi sura zenu?
Mkuu u don't have to make an excuse upo sahihi kabisa
Kwa upande mwingine, hapo panaweza kuwa na tatizo. Pamoja na kuwa ni mtaalamu kwenye hayo mambo, pamoja na kwamba alikuwa ana volunteer, bado mlitakiwa kufikiria out of the box and probably a step further. Haya mambo ndio huwa yanaleta migongano baadae ndani ya organisation/institution.
Kama mngefuata taratibu za kawaida za kutafuta hiyo package kama kutangaza tenda, n.k kuna uwezekano mkubwa haya yasingetokea. Inawezekana kwa kumtumia huyo mama mlikuwa mnajaribu ku-save costs na pia kutumia ujuzi wake for free, lakini ni muhimu kujua kuwa vitu au services za bure zinakuja na gharama zake pia.
Naamini Chadema ni chama makini kama kinavyojiita. Sometimes, for the avoidance of any problem/conflict in future vitu kama hivi inabidi vifanyike kwa kufuata taratibu. Sidhani kama itakuwa ni utaratibu mzuri kama Chadema ikiingia madarakani, na Dr Slaa akawa Rais basi package za accounting system za Ikulu ziwe zinafanywa na huyu mama kwa sababu ni mjuzi na atafanya for free.
Wanachadema mtaniponda but I am just providing a constructive criticism.
Kuhusu walinzi wa Josephine kumpeleka kanisani.
Ukweli ni kuwa Josephine hana mlinzi. Yupo yeye kama yeye. Hata alipovamiwa na wale majambazi/vibaka josephine alikuwa peke yake. Hata hapa JF tulilalamika sana kwa nini yule mama hana walinzi.
Kimsingi walinzi waliopo ni wale wanaomlinda Dr. Slaa nyumbani kwake. Sasa hawa (Dr. na Josephine) wanaishi pamoja hivyo sio rahisi alindwe Slaa tu Josephine asilindwe.
Na walinzi hawa walipatikana katika mchakato halali kabisa. Walikuwa interviewed na kufanyiwa character assesment.
Coincidence ni kuwa katika walinzi walioajiriwa wapo ambao awali walikuwa Walinzi wa Askofu Gwajima ambaye pia ni askofu wa Josephine. Josephine hana mlinzi binafsi.
Waliotoa mada ile waje wathibitishe walinzi binafsi wa Josephine
Rev.Mzito K. asante, maelezo yako yanajieleza yenyewe kuwa baada ya hiyo software mpya kuja na kuziba mianya ya watu ndipo chokochoko zilipoanzia. Haya mengine ya kufukuzwa kwa kuonewa is another case, wewe umeleta kutokana na uchunguzi wako, sasa kama kuna mtu anadhani Mwigamba alionewa atuletee uchunguzi wake na si kudhani alionewa kwa ku guess.
Mkuu Maranya, baada ya kusoma uzi nimegundua kwamba kwa upande wa Mwigamba kuna elements za kuonewa. Hivi unaleta accounting package ambayo naamini imekuwa developed na siyo kuchukuliwa kutoka dukani (on the shelf) halafu unasema ameshindwa kuitumia; je alikuwa trained, alishirikishwa katika mchakato wa kui develop? Hii package inaonekana kama imekuwa imposed kwa akina Mwigamba bila kufuata utaratibu wa System Development Life Cycle. Siku zote system ambazo hazikufuata utaratibu huwa zina failkwa kuwa hukosa User Acceptance. Pia mkuu umeseme Mwigamba ni fundi mchundo; imekuwa tena aingilie mambo ya IFRS 9 au ni Mhasibu pia kwa maana ya Certified Public Accountant? Kama si mhasibu na mkampa uhasibu basi mlimuonea tangia mwanzo na hapa ni maendelezo tu ya kumuonea.
Kusoma B.Com bila kuwa na CPA ama equivalebt hakumfanyi mtu kuwa mhasibu wa kushika mapesa yote hayo. Sijui NBAA wako wapi manake kila mtu anajiita mhasibu ili hali si mhasibu bali Accounting Technician!
Mkuu wangu narudia tena kusema mtu yeyote hawezi kuifanya kazi ya accounting ikiwa hakufundishwa accounting na kuhitimu. Unachodai wewe sio kweli na nakuhakikishia kwa sababu ni profession yangu na nimeifanya kazi hiyo..Mtu anayetumiwa kuingiza data entry za accounting iwe excel au powerpoint hawezi kujua kutumia accounting software bila kuwa na elimu ya uhasibu.Mkuu kilichofanyika hapa ni ku analyse data za Rev. pamoja na Maranya na mwisho nikatoa conclusion. Ushahidi hapa ni post ya Rev na Maranya!! Au huoni una kiwi ya macho?
Mkuu wangu Rev.
Asante sana kwa nondo zako hizi.Roho yangu imetulia na sasa ninaweza hata kula chakula.Mkuu wangu endelea kutufumbua macho.Maandiko matakatifu yanasema hakuna litakalofichika siku itakapotimia.Yale yaliyofanywa mvunguni mwa kitanda yataanikwa juu ya paa la nyumba.Mkuu wangu watu wengine tumefunga na kusali tangu Tuntemeke & Co. wameanza uasi wao.Mungu wetu ni mwaminifu na ameanza kujibu maombi.
Sheria gani inaruhusu mwanaume kuoa mke wa mtu?!Mbele ya
sheria Dr Slaa sio single. Ukishakaa
na mwanamke kwa zaidi ya miezi
sita basi anahesabika kama mke. Hivyo kama 'mama mdogo' yuko
kwakO tangia mwezi August 2011
basi ndugu una mke! Tarumbeta na
ubwabwa ni juu yako lakini mke
tayari unaye ndani!
Kikubwa unachofanya kwenye huu uchunguzi wako ni kumsafisha Josephine, ili la walinzi Slaa mwenye pamoja na Josephine, hawakukanusha kwenye majibu yao.
Sasa wewe unakuja kukanusha uoni huko ni kujipendekeza na uchunguzi wako utaoneka porojo?
Katika huo uchunguzi wako Josephine ana kosa lolote?
Kimbunga,
Hayo mengine ya NBAA pamoja na mazagazaga mengine sina taarifa nayo. Lakini nimeambiwa kabla ya kuletwa makao makuu kwa kazi hiyo alikuwa anafanya kazi kama hiyo(ya uhasibu) katika shirika moja la kimataifa jijini Arusha.
Kama ndivyo basi atakuwa amepitia taratibu zote zinazomfanya awe mhasibu, na sidhani kama chama kiliamua kumpa kazi hiyo akiwa hana ujuzi huo, nitaendelea kufuatilia.
Hata mimi nashangaa badala ya kujadili issues tunajadili mtu na ndoa yake kaoa, hajaoa, mchumba nafikiri si sehemu yake hapa. Hili la Slaa ana mchumba tulishaliongelea sana, kinachotakiwa kwenye thread hii tujadili hizi tuhuma ni za kweli au za uongo.
No kwanini ufutwe no ndio kukomaa kwa siasa ,and that is life they chose all of them pamoja na Slaa lazima waongelewe lazima wazushiwe lazima wasifiwe itis a process! Lakini nasema hakuna thread kufutwa tujue ukweli ,tunaweza tusijue ukweli wote but at least 95% clue.
Hawa jamaa Tuntemeke & Co kule wameweka madai mengi na kuishia kujadili Josephine that was too low!Kwa hiyo hii yote imeletwa kutokana na watu kupigwa chini shit.
Watu kama hawa ni hatari hata wakienda sehemu nyingine watashabikiwa lakini watu watakuwa makini nao kuliko kawaida.Hilter alikuwa anawatumia watu kama hawa kisha anawamaliza anajua TRAITOR ipo siku will turn on you
Mkuu wangu kufanya installation ya Accounting software kwenye mifumo ya uhasibu wa chama kikubwa kama CDM unaona ni issue ndogo?Halafu mtaona jinsi tulivyo wastaarabu..Hii mada inamhusu Tuntemeke lakini hatujapiga makelele kumwita aje kujibu maswala haya ila tunazungumza na watu wengine kabisaa kujadiliana na hakutokea kwa sababu anajua aloyafanya..
Paulss, Mkuu wangu kuipata na weka software Bongo mnatangaza tender?.. haya maajabu makubwa sana yaani wewe ukiharibikiwa na gari utatangaza tender sio?