Jumakidogo
R I P
- Jul 16, 2009
- 1,851
- 417
Mzito K,
Yaani miaka yote hii chama kilichosheheni wasomi hakina Accounting package inayoeleweka? Kuhusu huyo Tumbo, siku zote nimekuwa natahadharisha juu ya hawa wapima upepo wanaokimbilia kwenye vyama baada ya kushamiri kwa vyama hivyo, na sio wao wenyewe kushiriki kuvijenga vyama hivyo. CDM wapo wengi sana. Anton Komu, Joseph Selasini, Msafiri Mtemelwa nk. Watu aina hii ni hatari sana, nashangaa wanapokkuja na nyie kukimbilia kuwatunuku mavyeo. Hivi huyu aliyepumzishwa uhasibu, kama amesomea mbona nafasi ni nyingi tu, aliambiwa uhasibu wake lazima aufanyie CDM?
Umeandika waraka mrefu ambao kwa sehemu kubwa bado haujajibu tuhuma zilizoletwa. Sehemu kubwa ya waraka wako umejaribu kuwapambanua wale walioleta tuhuma hizo ni kina nani. Nadhani si muhimu kwetu kujua mleta tuhuma ni nani! Ili iweje, thibitisha hapa kuwa, tuhuma hizo si za kweli ili upingane na Dr Slaa mwenyewe ambaye ki msingi amekubali. Nilitegemea jambo moja kubwa baada ya Tuntemenke kushusha scud zile, nilitegemea wana CDM makini kuanza uchunguzi wa kutafuta ukweli kuhusu tuhuma hizo ili wasafishe chama, badala yake nao wanawashutumu waliosaidia kufukua maovu. Nikuulize swali dogo. Ikitokea tuhuma hizo zikathibitishwa kuwa ni za kweli, mtaweka wapi sura zenu?