Uchunguzi Wa Computer

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Komputer yako lazima iwekewe updates za kisasa , iwekewe antivirus pamoja na updates zake bila kusahau firewall , windows xp service park 2 inakuja na service park yake ingawa haikuhakikishii usalama sana kama haina angalau vitu hivyo 3 kuna uwezekano mkubwa zaidi kwa computer yako kuvamiwa au kushambuliwa kama imeunganishwa katika mtandao au hata kama haijaunganishwa .

MTANDAONI

Sasa hivi wengi tumeunganishwa katika mtandao na wengi zaidi wanazidi kuhamisha shuguli zao kwa njia ya mtandao au kutegemea zaidi mtandao kwa shuguli zao , kama kusoma email , kutembelea tovuti , manunuzi ya vitu , kuongea na mambo mengine mengi sana .
Kama nilivyosema hapo mwanzo kuunganisha computer yako katika mtandao unakuwa na nafassi kubwa zaidi kushambuliwa , katika dunia ya mtandao password pekee hazitoshi bila kuchukuwa hatua nyingine nzuri na rahisi zaidi .

UTAVAMIWA KAMA

- Ukifungua attachment yoyote ambayo hujui inahusu nini au chanzo chake .
- Kama ukiamini kila kitu unachosoma katika mtandao ni mali mfano ahadi za utajiri kama ukifungua attachement au tovuti Fulani
- Ukidownload programu ya ajabu kutoka katika mtandao kama screenserver za bure , games , picha na vingine vingi
- Kushiriki au kushirikiana na wengine data zako kwa programu za peer to peer kama kazaa , wares , au ares
- Ukishirikiana password yako na watu wengine


VITU VYA KUFANYA USIVAMIWE KWA URAHISI

- Hakikisha antivirus yako iko updated na saa zote iwe inafanya kazi
- Ujenge mazoea ya kuweka updates hizi zinapatikatika bure katika tovuti ya Microsoft au zile zinazohusika na programu unayoitumia . kumbuka lazima uwe na operating system ambayo ni genuine ili kiweka kupata updates nyingi na nzuri zaidi .
- Ni vizuri ukawa na password na account zaidi ya mbili katika computer yako moja administrator na ingine , moja ina weza kucorrupt au rafiki yako anaweza kuja kuomba compuer kwani ni lazima atumie account yako ?? unampa hiyo ingine .
- Weka firewall na hakikisha inafanya kazi katika computer yako au mtandao wa kazini kwenu .
 
Nimekuwa nikitumia mtandao kwa mda mrefu kidogo siwezi kujua haswa ni muda gani hata sijui ni muda gani nilianza rasmi kutumia mtandao lakini miaka hiyo haikuwa muhimu kwa mtu kuhofia kuhusu usalama wa computer yake na mtandao kwa ujumla hata sikushugulika kulinda vitambulisho vyangu katika mtandao .

Katika dunia ya sasa hivi vitu vimebadilika tena haraka sana bila kutegemea kama ingekuwa hivi miaka 10 iliyopita , kuna watu mamilioni wanatumia mtandao kila siku na saa zote ambao wanapenda kuiba vitambulisho vyako ,password zako , namba zako za siri na mambo mengine ya kifedha na masuala mengine mengi tu

Wanaweza kuiba utambulisho wako na nyaraka zingine kwenda katika account zako kuchukuwa pesa au mikopo kutoka sehemu zingine za dunia kwa kutumia majina yako au viambatanisho vyako na kuchukuwa hizo pesa au mali bila wewe kujua au kuwa na taarifa rasmi

Haiishii hapa pekee , sio tu tunaogopa kupoteza pesa na mambo yetu mengine kwa nji ya mtandao ,pia kuna watu wengine wanapenda kuharibu data na taarifa zako katika computer yako kwa furaha zao na upendo wao tu , tunaishi katika dunia ya ajabu kidogo watu wako tofauti sana

Siandiki kukutisha au kukuogopesha usitumie tena mtandao au computer yako la hasha , unachotakiwa ni kuuelewa mtandao na kuelewa tips na mambo mengine ya jinsi ya kujilinda na vitendo hivi wakati wowote ili usiogope na usiwe mashakani muda wote .

Kwanza kabisa ni lazima computer haswa ambayo imeunganishwa katika mtandao wa ndani au wa kimataifa iwe na firewall , unaweza kujiuliza hivi firewall ni nini ? inafanya kazi gani ? kwanini firewall ??

Firewall zinatengenezwa kutoruhusu au kuzuia computer ingine isiweze kutembelea computer yako bila ruhusa yako kuiweka vizuri firewall ni ukuta kati yako na mtandao , uwe wa kimataifa au wa hapo hapo officini kwako pekee , ukitaka mtu atembelee computer yako lazima umruhusu kupitia firewall yako .

Firewall ni nzuri sana kwa kujilinda na ghasia nyingi za mtandao , nimewahi kutumia nyingi kama ZoneAlarm , Norton hata mcafee , vile vile windows xp service pack 2 inafirewall yake yenyewe nayo inafanya kazi ntakueleza ubaya wa service park 2 firewall baadaye .

Unaweza kujikinga na firewall mtu asiweze kutembelea computer yako lakini ujue kwamba kuna aina nyingi za programu mtu huweza kutumia kutembelea computer yako bila wewe kuwa na taarifa au ruhusa

Virus , Trojan na Spyware za aina mbali mbali , kuna nyingi sana firewall haiwezi kukukinga na zote hizi lakini utahitaji msaada za ziada nao ni kuweka antivirus katika computer yako ambayo sio ya bure , itakayofanya kazi saa zote na kukupa taarifa

Antivirus zinaweza kukukinga na aina nyingi za virus katika mtandao , antispyware kwa ajili ya kujikinga dhidi ya spyware , Trojan kwa ajili ya Trojans na programu zingine nyingi saa .

Kwa dunia ya sasa , na maendeleo ya mtandao , antivirus moja inaweza kufanya vyote hivyo , kuondoa spyware , virus , Trojans , isokae hapo unatafuta programu za moja moja za kuondoa kitu kimoja kimoja katika compter yako kwa kufanya hivyo utajaza computer yako na vitu vingi sana na kuifanya iwe taratibu na nzito .

Lakini umepata picha ya nini ninachotoka kukuambia au sio ? unahitaji programu moja tu ya kufanya shuguli zote hizo katika computer yako kwa wakati unaokufaa na unaotaka wewe . Hakikisha umeweka antivirus nzuri pale unapoweka operating system mpya na ufanye updates hapo hapo .

Lingine na msingi zaidi ni kufuata ushauri huu , ukae mbali na tovuti za wakubwa na usidownload au kuweka programu za bure katika computer yako kumbuka hakuna kitu cha bure katika mtandao , lakini kuna ambazo ni nzuri sana ila uwe makini sana siwezi kuzitaja kila moja ina madhara yake .

Hakikisha programu zako ni za kisasa na zinaendana na wakati , na angalia hatua zako unapotembelea baadhi ya tovuti katika mtandao

Ahsante
 
Pengine umewahi kuota sikumoja unaweza kufanya uchunguzi kidogo katika computer yako au computer ya mtu mwingine , kujua alifanya nini , vitu anavyoweka katika computer yake na mambo mengine kuhusu computer yake si ndio ?


Leo nitakuonyesha njia chache ambazo unaweza kuzitumia kufanya uchunguzi mdogo katika computer yoyote ambayo utakutana nayo , kumbuka njia hizi zinatumika kwa bidhaa za Microsoft windows pekee .

Kabla ya kuanza maelezo haya kuna mambo muhimu ambayo mwenye computer anatakiwa awe anayajua au kuyatambua yeye kama mmilihi halali au mtumiaji wa computer husika nayo ni .

UTAMBULISHO

Right Click katika my computer , utaona general katika general utaona maelezo ya mwanzo kabisa kama aina ya operating system kama ni windows xp au 2000 , imesajiliwa kwa nani , aina ya CPU spidi yake , na ram iliyokuwepo katika computer hiyo

Kuna computer name hapo utaona jina la mwenye computer unaweza kubadilisha jina hili na kuweka jina lingine au kama utataka kujiunga na workgroup au domain Fulani makazini kwako hapo ndio pakuanzia , kubadilisha jina kunafanyika kama una mamlaka hayo yaani kama umelogin na account ambayo ina administrator Status kama sio administrator basi hutopata nafasi hiyo kamwe .

Ukifungua hardware kuna device manager hapo utaona hardware zote zilizochomekwa katika computer yako pamoja na driver zake kama ziko installed hapo na zinafanya kazi .

Kwa ufupi ukitaka maelezo ya kina ambayo hayahitaji sana utaalamu tafuta programu inaitwa Belarc Adviser au DriveMagician programu hizi ukitumia utaweza kuona hardware zote zilizomo ndani pamoja na watengenezaji wa vifaa hivyo na programu zilizomo ndani ubaya wake ni kwamba zitaonyesha mpaka licence za programu hizo maana yake mtu anaweza kuiba hizo licence au keys na kwenda kutumia kwingine kwa raha zake .

MAELEZO YA ZIADA


Kwanza fungua my computer – tools – folder options – view – show hide files and folders kuna baadhi ya watu wanapenda kutumia hatua ya hide kuficha folder na files zao ingawa njia hii ni ya kizamani kidogo kwa sababu kuna programu maalumu za kulock file au folders au file .

Njia hiyo ya hapo juu unaweza kufanikiwa kujua kama file zilizofichwa ukazipata , ila kama mtu alitumia programu maaalumu kulock hiyo folder hata ukiona huwezi kuifungua hapo ndio zinahitajika jitihada zingine ingawa kuna njia zaidi za kuweza kupata hizo file au folder .

Pili fungua my computer – fungua drive c (kama operating system iko drive c ) - Documents and settings – ( utakuta account nyingi kama computer yako unatumia jina mwehu basi utaona mwehu , la msingi wengi wanapenda kutumia administrator au user ) kama ni user fungua user – fungua templates ( utaona programu alizofungua muda mfupi uliopita au anazopenda kufungua au kutumia kumbuka usipofanya show hidden folders hutoweza kuona templates .

Hapo hapo katika user fungua My Recent Documents , ukifungua hiyo pia utaona files alizokuwa anatumia mtuhumiwa kwa kipindi kifupi kilichopita , pamoja na folder alizofungua , kama alichomeka flashdisk basi jina la flash disk utaliona pale au kama alichomeka kifaa chochote historia nzima utaiona pale pale .

Kuna cookies ,ambayo inapatikana katika user mara nyingi cookies ina maana kama computer husika huwa inatumia mtandao au imeunganishwa na mtandao , hapo utaweza kuona cookies na link fupi za tovuti ambazo mhusika amewahi kutembea au ambazo huwa anatembelea .

Watu wengine hupenda kuhifadhi link ya tovuti wanazotembelea katika browser zao , kwahiyo ukifungua favorites utaweza kuona link hizi za tovuti na kama mtu huyo anapenda kutembelea tovuti za ngono , au ambazo sio salama basi utaona hapo kwa sababu tovuti za hivyo huwa zinafanya hijack na kujihifadhi zenyewe kilazima .

Local Settings
Ndani ya local settings kuna Application Data , History , Temp ,Temporary Internet Files ,ukifungua history utaweza kuona tovuti zote alizowahi kutembelea mtuhumiwa na kama alikuwa anamtindo wa kuhifadhi password zake katika computer husika basi unaweza kufungua mpaka email zake na nyaraka zake zingine kwa kuwa zitakuwa zinafunguka moja kwa moja na ni rahisi kutumia programu zingine kuweza kutambua password husika .

Ukifungua Temporary Internet Files utaona file na programu zilizopatikana katika tovuti husika alizotembelea , mara nyingi hapo utakuta vitu haswa picha nakadhalika , pia virus huwa wanaanzia hapa katika folder hili , spyware na uchafu mwingine wa mtandao chanzo chake kikuu ni katika Temporary Internet Files .

Kama wewe ni mtumiaji wa windows 2000 kuna folder moja linaloitwa Recent hapo utaweza kupata mambo ya ziada kuhusu mtuhumiwa .

TAHADHARI

Maelezo ya hapo juu sio ya uhakika sana kwa sababu kuna programu za kuweza kufuta yote hayo kwa sababu huwa yanajaza computer na kusababisha ufumbufu mwingine kwahiyo ukikuta mtu ametumia programu ya kuondoa temporary Internet Files basi umeuwawa au programu ya Diskclean up basi napo umechemka .

Hata wewe unaweza kufuta baadhi ya vitu hivi

Start – Accessories – System Tools – Diskclean up – click Ok

Kisha kuna popup itakuja imeandikwa Disk Clean up for ( C) kama operating system yako iko Drive D basi chagua d na kadhalika , kuna programu zinazoweza kukusaidia na shuguli hii kama ccleaner , hijackthis na zingine nyingi zilizoko mitaani .

Utaona maelezo na cha kufanya kama unataka kufuta hizo files kwahiyo unaweza kuponyoka hapo kazini kwako kama unataka IT wetu asijue unafanya nini na umetembelea tovuti gani hapo unazifuta tu kiulaini .

Kuna sehemu zingine wanatumia server maalumu za kuhifadhi vitu ( BACKUP ) hii ina maanisha hata kama ukifuta au ukiformat Computer yako vile ulivyofanya vinakuwa viko katika hiyo server kwa ajili ya kumbu kumbu za baadaye kama chochote kikitokea , labda usijiunge na Domain ya Network husika ili usiwe unafanya backup na hiyo ni ngumu sana .
Hayo ni maelezo mafupi kuhusu uchunguzi na ndio mwanzo wake ingawa kuna programu maalumu zinaweza kutumika kuweza kuridisha vyote ulivyofuta na kuruhusu uchunguzi kuendelea kama kawaida .

Kuna wengine wanafikiri kufuta HDD ni suluhisho , siku hizi sio suluhisho hata ukifuta partition kuna programu za kuweza kurudisha pertition hizi pamoja na data zake ili ziweze kutumika hapo mbeleni au ziweze kutumika kama ushahidi mambo yanavyoweza kwenda kombo .

Katika kutumika kama ushahidi sijui kama Tanzania kuna sheria hizi za kutumia vifaa vya electroniki na kuwasilisha ushahidi mahakamani au la kama hamna basi ndipo tunapoelekea huko tujiandae kikamilifu

Kwaheri
 
Back
Top Bottom