SoC02 Uchungu mkopo wa elimu ya juu ulivyoyeyusha ndoto zangu za kuwa daktari

Stories of Change - 2022 Competition

Clark cian

Senior Member
Jul 3, 2021
153
139
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 24 kwa sasa,ambaye kwenye kundi la watu ambao hawajalelewa na wazazi wao ni mmoja wapo ni mzaliwa wa Moshi kilimanjaro na namshukuru mungu nilipata elimu yangu ya kidato cha nne na sita vizuri nikahitimu na hiyo yote ilikuwa ni nguvu za ndugu zangu hasa mashangazi walioamini uwezo wangu na kujitoa juu yangu.nikafanikiwa kumaliza kidato cha nne katika seminari moja iliyopo morogoro kisha nikabahatika kuchaguliwa kidato cha tano katika shule moja mkoani kilimanjaro ,nilizidi kusoma bila ya kukata tamaa ikiwa ndoto yangu kubwa moyoni kwangu nikufika chuoni kivyovyote vile ili kusomea ndaki ninayoihitaji; basi mapambano hayakuisha nikazidi kujikaza kusoma kwa bidiii hata nikashindwa kunywa na kula vizuri kama wenzangu kwakuwa nilifikiri watakao patiwa mikopo ya elimu ya juu ni wale waliofaulu vizuri ,basi vita kwenye madaftari na vitabu vyangu viitwacho 'chand' havikuisha mchana na usiku mpaka nikahakikisha nimejua vitu vyote,basi kama iivyo sikuzote mchumia juani hulia kivulia usemi haukunidanganya matokeo yakatoka nikafanikiwa kufaulu kwa daraja la kwanza kwa point 7.

wow ilikuwa ni jambo la kushangaza na naweza kusema ilikuwa ni miujiza ila ni mipango ya mungu juu ya maisha yangu ,basi hapo nikajipa akilini mwangu uhakika wa kupata mkopo asilimia mia . kwasababu ya uwezo wangu wa kifamilia ulikuwa haujitoshelezi na ndugu zangu walikuwa wameshaanza kunisema kwa chini chini huku nikibahatika kusikia neno moja kwa shangazi yangu ambaye alikuwa ni tegemezi sana kwenye elimu tangu mwanzo ,alilalama kichinichini akisema''kusema ukweli kwa sasa hela sina'' basi niliposikia hivyo nilitaka kukata tamaa lakini baada ya kugundua nimeshamezeshwa kuwa wanaofaulu ndio wanapata mikopo mikubwa basi nilipiga moyo konde.

Basi matokeo ya vyuo yalitoka nikabahatika kupata course ya medicine doctorkama kozi ya ndoto yangu katika chuo cha Dodoma huku nikiwa tayari kusubiri mkopo kutoka serikalini ili niweze kwenda kusomea course ya maisha yangu ,sio siri nilikuwa nimejawa na furaha moyoni mwangu na kila ninapopita najitambulisha naitwa Daktari.erasmy lashau kwa majirani hata marafiki zangu ingawa bado sijapata elimu hiyo.

Basi mwezi ukapita majibu ya mkopo yakatoka kwa mara ya kwanza kuangalia kama wamenipatia nikakuta hamna kitu nisubiri awamu ya pili,basi sikujikatia tamaa nikasubiri awamu ya pili pia nayo ikapita bila kupata, basi roho yangu ikaanza kuuma na kuhisi kwamba serikali inataka kuiyeyusha ndoto yangu na huku nikikumbuka maneno ya shangazi yangu tegemezi aliyekuwa ananisomesha alivyodai kuwa hana hela ya kunisomesha basi nilianza kujikatia tamaa huku nikisubiri awamu ya tatu ,basi kwamasikitiko nikakosa tena kwa mara ya tatu hapo ndo nilipata mshtuko mkubwa na simu nilidondosha chini nusura ipasuke ,lakini neno'' but wait for the 4 round'' yaani nisubiri kwa awamu ya nne likaniapa moyo tena nikawa na nguvu ya kuendelea kufikiria ndoto yangu jinsi nitakavyotibu wagonjwa na kivipi baada ya kupata elimu yangu.

Lakini siku zikapita ila lililoniuma zaidi na kunifanya nikose hamu ya kula chakula huku nikuwakumbuka wazazi wangu walipo daah ni pale nilipoona wameniandikia kwamba nisubiri mwaka mwingine tena ndo niombe mkopo daaaah kusema ukweli iliniuma sana hadi leo hii basi nilisubiri kuona ndugu zangu watajitokezaje kuhusu suala langu la kukosa mkopo ila bado mwitikio wao ukawa wa chini sana hadi kunipelekea kukata tamaa ya kupata elimu yangu ya kuwa daktari basi kwa majonzi nikaanza kufuta taratibu akilini ndoto yangu yakuwa daktari na kuanza kufikiria jinsi ya kuanza kpambania maisha yangu bila mategemezi ya ndugu na huku nikiacha malalamiko na laana kwenye bodi ya mikopo tanzania kwa kutonipa mkopo bila kufikiria ni wangapi tulikosa ila nilikuwa najichukulia kama ni mimi pekee nisiyena bahati.

Na mpaka sasa imepita miaka miwili sijafanikiwa kwenda kusomea ndoto ya maisha yangu nikisema waziwazi bodi ya mkopo imenipa donda kubwa kwenye moyo wangu ila mungu si athumani nilijitahidi kuwekeza nguvu zaidi kwenye kazi za jamii basi nika bahatika kufanya kazi ya bodaboda ili kuweza kujiingizia kipato huku nikiwa na malengo baada ya miaka mitano nitajisomesha elimu hiyo kwa hela zangu mwenyewe kwasababu naamini juu ya mikono yangu na mungu pia.

Ila kwa sasa napenda kumshukuru buriani rais magufuli kwa kuongeza fedha kwenye mfuko wa mikopo ya elimu ya juu ambapo inaaminisha umma kuwa wanafunzi wahitimu wa kidato cha sita watakuwa na uwezo wa kupata mikopo hiyo kwa usawa ,ila yote hayo yatawezekana kwa bodi husika kuondoa ubinafsi na upendeleo huku ikiwa na tamaa ya wanafunzi wote wahitimu kupatiwa mikopo hiyo kwani ina umuhimu sana kwa maisha yao pia kuondoa fikra potofu kwa baadhi ya watendaji wapangaji mikopo kwa wanafunzi kutokuzingatia shule aliyesoma mhusika kwani ada za elimu ya juu huwa ni kubwa kulinganisha na baadhi ya shule za private mfano seminary .

Pia watu wa bodi husika wapate uchungu na kuwawazia mawazo chanya wale wote waombao mkopo na sio kila aombao mkopo ni kwa ajili ya kujiongezea utajiri kwasababu kila mwaka unapoisha bodi inapokea vilio vya wanyonge bila ya wao kuvisikia ambavyo vyote vinalia juu ya ndoto zao kukatishwa na bodi kutokana na uwezo wao wa kujiendeleza kimasomo ni mdogo.

Pia upangaji wa mikopo uzingatie hali ya uchumi wa watanzania kwasasa watanzania wengi hatuna uwezo kwahiyo bodi iweze kupanga mikopo inayoweza kujitosheleza kwa waombaji ili kuondoa kero na malalamiko kutoka kwa waombaji mfano mwaka jana mtu kati ya ada yake ya mwaka milioni 1 na nusu bodi inamlipia laki mbili na elfu ishirini na nne tuuh huo ni unyonyaji kwa watanzania kwakweli inaumiza na kukatisha tamaa sana pale mhitimu anapokosa mkopo serikali iangalie hili.

Mwisho; wanafunzi wahitimu wa kidato cha sita wanapitia shida na changamoto kubwa kwenye kipindi hiki cha kusubiri kupangiwa mikopo yao basi serikali hasa kwenye wizara ya elimu itupie jicho upande wa bodi ya mikopo ili kuweza kuondoa dosari ambazo zipo ili wanafunzi wote waweze patiwa mikopo hiyo ili kuweza kuondoa malalamiko kutka kwa wahitimu kutokana na mikopo huchochea kwa kiasi kubwa wahitimu kufikia malengo waliyojiwekea.
 
Back
Top Bottom