proton pump
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 5,363
- 6,903
Mara nyingi nimekua nikiandika hili suala humu kuwa elimu ibadilishwe kwan haifai kabisa. Mwaka huu hawajatangaza shule Bora Wala mwanafunzi Bora.
Wachambuzi wa ITV wengi wametoa mawazo mazuri Sana kama vile;
Kubadilisha lugha ya kufundishia iwe ya Moja kwa Moja kuanzia msingi hadi chuo kikuu. Hapa ni vizuri kwa sababu aliyesoma shule za kiingereza mwanzo mwisho huwezi kumshindanisha na aliyesoma kwa KISWAHILI msingi, halafu Kiingereza sekondari ambaye ndio kwa anapambana kujua lugha kwanza ndio aendelee.
Naunga mkono Tena kwa sababu shule ya mjini huwezi kuishindanisha na ya kule kijijini Monduli ambapo shule Ina walimu wawili na watoto hawana muamko wa elimu, watoto wanatoka mbali, umasikini unawadumaza, japokua hata mjini pia umasikini upo.
Shule binafsi huwezi kuishindanisha na shule za serikali kwa sababu serikalini hakuna vifaa vya kutosha na idadi ya wanafunzi ni wengi kuliko shule binafsi.
Narudi kwa Huyu mchambuzi anayeitwa (BANTE) ajifikirie Sana kuwaita walimu vilaza (mambumbu) huku akijisifia alipata ONE form four, huyu huyu mwalimu aliyemfundisha ndiye aliyemtoa BANTE. Hiyo lugha anayotumia sio nzuri. Kama yeye alifundishwa na mbumbumbu sijui Leo hii angekaa hapo ITV aongee hicho anachozungumza saa hivi.
Hao wanaojiita Tanzania one ni Nini walichobadilisha au jipya lipi wamegundua? Wengi wao ndio wameharibika katika JAMII zetu chunguza vizuri utanijulisha.
Narudia huyu BANTE atafakari anayoyaongea unaweza ukawa na Elimu lakini hujaelimika.