Matokeo ya Kidato cha Nne yamenikumbusha wakali hawa wa mwaka 2005 kutokea kule Mbeya

Execute

JF-Expert Member
Sep 21, 2022
3,000
7,285
Basi enzi zile kuna mitihani ya darasa la saba ikijumuisha shule za Maanga, Sinde, Mwenge, Nzovwe, Ilemi, Muungano na Ruanda nzovwe kulikuwa na wakali wao mwaka 2001.

Stephen Swetala, Ibrahim David, Daudi Mwala, Goodluck Mlwilo, Diligent Mmbaga, Wilson Ngole, Mbawala (wa muungano) na yule jamaa wa sinde simkumbuki jina. Walienda special schools kasoro huyo Diligent.

Matokeo ya form four 2005 kukawa na maajabu maana Mwala na Ibrahim waliangukia pua na kutupwa technical halafu huyo Diligent akaenda special akitokea shule ya kata. Sijui waliendeleaje huko advance na wako wapi siku hizi.
 
Basi enzi zile kuna mitihani ya darasa la saba ikijumuisha shule za Maanga, Sinde, Mwenge, Nzovwe, Ilemi, Muungano na Ruanda nzovwe kulikuwa na wakali wao mwaka 2001...
Kuna mwana pale mabatini alikuwa anapiga 50/50 siku akifeli sana basi ana 48/50.

Yule mwamba alienda Kibaha boys sijui siku hizi anaendeleaje hukoo..

Yaani tukikutana Nonde, Sisimba, Azimio, mabatini nzovwe lazima awe wa kwanza kila pepa.

Hakika wakati ni ukuta aiseee...
 
Aisee kuna mmakonde pale mzumbe mwaka 1998/1999 kidato cha nne alipata A zote ,hapo hapo mzumbe six akapata A zote saizi ni daktari bingwa huko uturuki Kwa mara ya Kwanza kushuhudia genius,maana kuna Raia ni kukariri mwanzo mwisho ila Jamaa ni nomaaaaa sio poa hakuna cha mathe wala physcs
 
siku hizi hakuna Tanzania One wala shule kumi bora. serikali imeachana na kuwapa zawadi vichwa

maana wamegundua ulimwengu wa internet unaabudu Entertainers. vichwa wa academic wanaonekana wapuuzi tu
 
Miaka ipi hiyo mkuu? Labda ungetaja jina ningeweza kumfahamu.
 
Aisee kuna mmakonde pale mzumbe mwaka 1998/1999 kidato cha nne alipata A zote ,hapo hapo mzumbe six akapata A zote saizi ni daktari bingwa huko uturuki Kwa mara ya Kwanza kushuhudia genius,maana kuna Raia ni kukariri mwanzo mwisho ila Jamaa ni nomaaaaa sio poa hakuna cha mathe wala physcs
Safi sana kuona mtu kichwa kuanzia darasani mpaka kwenye maisha.
 
siku hizi hakuna Tanzania One wala shule kumi bora. serikali imeachana na kuwapa zawadi vichwa

maana wamegundua ulimwengu wa internet unaabudu Entertainers. vichwa wa academic wanaonekana wapuuzi tu
Wamefanya ushindani uwe wa kimyakimya. Ila miaka ile ilikuwa moto sana. Nashangaa siku hizi vijana wanapata one za saba nyingi sana, sijui elimu imebadilika au ndio vijana wana akili zaidi.
 
Back
Top Bottom