Uchambuzi: Adhabu kwa wabunge Silaa na Gwajima ni funzo kubwa kwa watanzania

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,861
18,285
Kwema wakuu? Naingia kwenye hoja moja kwa moja bila kupindisha maneno. Leo tarehe 31/08/2021 bunge la JMT limetoa adhabu ndogo kwa wabunge wawili wa CCM – ndugu Jerry Silaa wa Ukonga na ndugu Josephat Gwajima wa Kawe. Bunge limetoa azimio la kuwasimamisha mikutano miwili ya Bunge.

Wengi tuliofuatilia maamuzi yale ya bunge tumebaki vinywa wazi kwani kuna mambo mengi yamefichwa ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya. Watanzania wamefichwa mambo mengi sana kufuatia adhabu hii ilyotolewa kwa wabunge hawa wa CCM.

Naomba nianze kuchambua adhabu iliyotolewa kwa Silaa na sababu zilizotolewa na kamati kuhusu adhabu husika. Hoja ya Silaa ilikuwa kwamba wabunge wanalipwa pesa nyingi sana ambazo hazikatwi kodi na hili hufanyika kwa makusudi ili wasilipe kodi stahiki kwa serikali kama wafanyakazi na watanzania wengine wanavyolipa.

Kwa bahati mbaya sana, Silaa amehukumiwa kwa kusema ‘uongo’ bila kamati kuonyesha ukweli ni upi. Kinachoonekana wazi ni kuwa kamati imeamua kufunika kombe ili mwanaharamu apite. Hawataki kusema ukweli kwa sababu wakisema ukweli wananchi watakuwa wakali kwani wananchi wanabebeshwa mzigo mkubwa wa kodi na tozo, huku wabunge wakila bata. Na kwa masikitikko makubwa, pamoja na mishahara minene wanayolipwa kuna mbunge aliwahi kudiriki kusema kuwa mishahara yao ni midogo na kuwa walipwe kwa dola. Nchi hii haitakuja kuisha maajabu.

Wananchi wamjia juu mbunge anayesema posho, mishahara yao haitoishi

Kwa mujibu wa taarifa zilizowahi kutolewa na Mh Zitto Kabwe mwaka 2017 wakati akiwa mbunge wa Kigoma Mjini, mshahara wa mbunge ni Tsh 3.8 kwa mwezi, posho ya ubunge ni milioni 8 kwa mwezi, posho ya kujikimu ni Tsh 120,000 kwa siku, kukaa kikao cha bungeni posho ni Tsh 200,000 kwa siku. Bado kuna fedha kwa ajili ya mfuko wa jimbo ambayo ni milioni 46 lakini hii hutegemeana na jimbo lenyewe na mbali na hapo kuna posho ya jimbo.

Kwa kuwa huu ulikuwa mshahara wa mwaka 2017 na kwa kuwa kila mwaka wabunge hujiongezea mishahara kimyakimya, kuna uwezekano mshahara wa mbunge kwa sasa upo juu sana kuliko tunavyofikiri.

Huu ndio ufafanuzi ambao ulipaswa kutolewa na kamati ya Bunge kwa umma wa watanzania ili kukata mzizi wa fitna. Lakini wameamua kukaa kimya ili wananchi wasijue jinsi wanavyokwepa kodi kwa kujilimbikizia posho za kukufuru huku wakijilipa kimshahara uchwara ambacho hukatwa kodi uchwara isiyotosha kuchangia chochote kwenye uchumi wa taifa.

Mimi nafikiri Silaa yupo sahihi sana anaposema kuwa wabunge hawalipi kodi. Kama kweli wabunge wa CCM wanataka kushiriki ulipaji kodi, hizo posho za kufuru wanazojilipa zihamishiwe kwenye mshahara ili zikatwe kodi. Sote tunafahamu kuwa posho huwa hazikatwi kodi. Ndio maana wameamua ku-divert mshahara kwenda kwenye posho ili wakwepe kodi. Hawa jamaa ni wahujumu uchumi wallah!

Kabla sijaenda mbali sana naomba nirejee kwenye suala la Gwajima na hoja nyingine zilizoibuka kutokana na kauli zake tata za kuwakataza watanzania kuchanjwa. Kukaangwa kwa Gwajima ni haki kabisa kwa makosa aliyofanya kuwapotosha wananchi kuhusu chanjo. Nasikitika tu amepewa adhabu ndogo sana licha ya kuwa kosa alilofanya ni zaidi ya uhujumu uchumi. Ni uuaji wa makusudi.

Je ni funzo gani tulilopata kutokana na adhabu hizi kwa wabunge wa CCM? Mosi, funzo kubwa ni kuwa kuna baadhi ya wanaCCM hawapendi uongozi wa mama Samia kwa sababu wanazozijua wao wenyewe (Ushahidi: Sikiliza clip hapo juu). Hawa ni wale masalia wa mwendazake waliojipa jina na MATAGA na kujifanya kuwa wao ni watanzania zaidi kuliko wengine. Dawa yao inachemka.

Pili, kuna baadhi ya watanzania aina ya Gwajima ambao wanamdharau mama Samia kwa sababu tu yeye ni mwanamke. Wanaoana eti hatoshi kuiongoza nchi. Kwa hiyo, wanajitahdi kuleta chokochoko na kumvuruga kusudi aache kujikita kuongoza nchi aanze kujishughulisha nao. Hii ni hujuma kubwa sana. Wabunge wengi waliochangia hoja kwenye klipu hapo juu, wamessikitsishwa mno na kitendo hiki cha baadhi ya watanzania wasioitakia mema nchi hii kufanya juhudi za kumkwamisha mama Samia. Hili halikubaliki hata kidogo.

Tatu, kitendo cha kamanda IGP Simon Sirro kugoma kumkamata Gwajima na kumfungulia mashtaka ya uhujumu uchumi kinaashiria kuwa kamanda Sirro yupo upande wa kundi linalomhujumu Rais Samia. Naomba mama Samia amfute kazi mara moja au amshauri ajiuzuru bila shuruti ili ampishe ateue IGP mwingine. Huwezi kuwa Amiri Jeshi Mkuu halafu kipande kimoja cha jeshi kikagoma kukutii ukabaki salama. Lolote laweza kutokea.

Nahitimisha kwa kusema adhabu hii aliyopewa Gwajima ni ndogo sana kwani suala lake limekuwa likifanyika kwa muda mrefu na kwa kurudiarudia. Ameonyesha dharau kubwa sana kwa rais wetu hasa pale alipomtuhumu kwamba alifanya chanjo ya maigizo na kwamba amehongwa na mabeberu ili kuleta chanjo ya kuwaua watanzania. Ilipaswa huyu bwana apewe adhabu kali zaidi.

Na akama Spika aliposhauri, naomba chama chake kiangalie uwezekana wa kumfuta uanachama ili liwe fundisho kwa wengine wasioheshimu mamlaka. Laiti kama mbunge wa upinzani ndiye anayefanya upotoshaji huu anaofanya Gwajima, nadhani angekuwa hata ameishauawa na watu wasioijulikana. Lakini kwa kuwa ni mbunge mwenzao ndio maana wamempa adhabu nyepesi.

Taarifa zaidi kuhusu sakata hili unaweza kulipata kwenye uzi huu hapa chini:

Ikiwa makato kwenye miamala ya simu, LUKU na mabenki hayatabadilika nini kifanyike?

Nawasilisha.​
 
Ugomvi wangu kuhusu hii sababu ni kuwa kama wamewasimamisha hadi january hawa wananachi wa majimbo yao nani atawasemea? Nani atachangia nani atatoa mawazo ya wananchi wa hayo majimbo, nadhani kama kuwapa adhabu nzuri wangeishia kuwakata tu hiyo mishahara then wahudhurie vikao vyote kama kulikuwa na ulazima wa kuwapa adhabu za kubumba
 
Yaani kuikosoa serikali ni kumdharau mama? Mbona tunawekana kwenye kona namna hii? Kama hakutaka kukosolewa kwa nini alikuabali kuwa raisi?!
Hiyo dhana ya mataga sijui masalio hiyo ni nadharia tu ya kulea baadhi ya watu.
Zamu yenu ya maamuzi mmemaliza sasa subirini zamu ya maamuzi ya Mungu na wananchi.
Kwanza naona kama mnajichanaganya tu. Nishachoka na tozo zenu na hamlipi kodi, nchi imekua yenu mnakula mema ya nchi na hamataki watu waseme. Kwanza mshachelewa na hatuchanji.
 
Ugomvi wangu kuhusu hii sababu ni kuwa kama wamewasimamisha hadi january hawa wananachi wa majimbo yao nani atawasemea? Nani atachangia nani atatoa mawazo ya wananchi wa hayo majimbo, nadhani kama kuwapa adhabu nzuri wangeishia kuwakata tu hiyo mishahara then wahudhurie vikao vyote kama kulikuwa na ulazima wa kuwapa adhabu za kubumba
Pamoja sana
 
Mimi nafikiri Silaa yupo sahihi sana anaposema kuwa wabunge hawalipi kodi. Kama kweli wabunge wa CCM wanataka kushiriki ulipaji kodi, hizo posho za kufuru wanazojilipa zihamishiwe kwenye mshahara ili zikatwe kodi. Sote tunafahamu kuwa posho huwa hazikatwi kodi. Ndio maana wameamua ku-divert mshahara kwenda kwenye posho ili wakwepe kodi. Hawa jamaa ni wahujumu uchumi wallah!
Hapo umekosea sana, Kwa mujibu wa sheria ya kodi, posho zinapaswa kukatwa kodi. Sema hizo posho za wabunge ndizo hazikatwi kodi.
Soma hii sec 7 ya income tax act 2008
7.-(1) An individual's income from an employment for a year of

income shall be the individual's gains or profits from the employment of

the individual for the year of income.

(2) Subject to the provisions of subsection (3), (4) and (5) in

calculating an individual's gains or profits from an employment for a year

of income the following payments made to or on behalf of the individual

by the employer or an associate of the employer during that year of income

shall be included:

(a) payments of wages, salary, payment in lieu of leave, fees,

commissions, bonuses, gratuity or any subsistence travelling

entertainment or other allowance received in respect of

employment or service rendered;

Kama kuna marekebisho yoyote hapa katikati, nakubali kukosolewa.
 
Kwema wakuu? Naingia kwenye hoja moja kwa moja bila kupindisha maneno. Leo tarehe 31/08/2021 bunge la JMT limetoa adhabu ndogo kwa wabunge wawili wa CCM – ndugu Jerry Silaa wa Ukonga na ndugu Josephat Gwajima wa Kawe. Bunge limetoa azimio la kuwasimamisha mikutano miwili ya Bunge.

Wengi tuliofuatilia maamuzi yale ya bunge tumebaki vinywa wazi kwani kuna mambo mengi yamefichwa ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya. Watanzania wamefichwa mambo mengi sana kufuatia adhabu hii ilyotolewa kwa wabunge hawa wa CCM. Kama hukupata nafasi ya kufuatilia mjadala moja kwa moja kutoka bungeni unaweza kusikiliza hapa chini:

Naomba nianze kuchambua adhabu iliyotolewa kwa Silaa na sababu zilizotolewa na kamati kuhusu adhabu husika. Hoja ya Silaa ilikuwa kwamba wabunge wanalipwa pesa nyingi sana ambazo hazikatwi kodi na hili hufanyika kwa makusudi ili wasilipe kodi stahiki kwa serikali kama wafanyakazi na watanzania wengine wanavyolipa.

Kwa bahati mbaya sana, Silaa amehukumiwa kwa kusema ‘uongo’ bila kamati kuonyesha ukweli ni upi. Kinachoonekana wazi ni kuwa kamati imeamua kufunika kombe ili mwanaharamu apite. Hawataki kusema ukweli kwa sababu wakisema ukweli wananchi watakuwa wakali kwani wananchi wanabebeshwa mzigo mkubwa wa kodi na tozo, huku wabunge wakila bata. Na kwa masikitikko makubwa, pamoja na mishahara minene wanayolipwa kuna mbunge aliwahi kudiriki kusema kuwa mishahara yao ni midogo na kuwa walipwe kwa dola. Nchi hii haitakuja kuisha maajabu.

Wananchi wamjia juu mbunge anayesema posho, mishahara yao haitoishi

Kwa mujibu wa taarifa zilizowahi kutolewa na Mh Zitto Kabwe mwaka 2017 wakati akiwa mbunge wa Kigoma Mjini, mshahara wa mbunge ni Tsh 3.8 kwa mwezi, posho ya ubunge ni milioni 8 kwa mwezi, posho ya kujikimu ni Tsh 120,000 kwa siku, kukaa kikao cha bungeni posho ni Tsh 200,000 kwa siku. Bado kuna fedha kwa ajili ya mfuko wa jimbo ambayo ni milioni 46 lakini hii hutegemeana na jimbo lenyewe na mbali na hapo kuna posho ya jimbo.

Kwa kuwa huu ulikuwa mshahara wa mwaka 2017 na kwa kuwa kila mwaka wabunge hujiongezea mishahara kimyakimya, kuna uwezekano mshahara wa mbunge kwa sasa upo juu sana kuliko tunavyofikiri.

Huu ndio ufafanuzi ambao ulipaswa kutolewa na kamati ya Bunge kwa umma wa watanzania ili kukata mzizi wa fitna. Lakini wameamua kukaa kimya ili wananchi wasijue jinsi wanavyokwepa kodi kwa kujilimbikizia posho za kukufuru huku wakijilipa kimshahara uchwara ambacho hukatwa kodi uchwara isiyotosha kuchangia chochote kwenye uchumi wa taifa.

Mimi nafikiri Silaa yupo sahihi sana anaposema kuwa wabunge hawalipi kodi. Kama kweli wabunge wa CCM wanataka kushiriki ulipaji kodi, hizo posho za kufuru wanazojilipa zihamishiwe kwenye mshahara ili zikatwe kodi. Sote tunafahamu kuwa posho huwa hazikatwi kodi. Ndio maana wameamua ku-divert mshahara kwenda kwenye posho ili wakwepe kodi. Hawa jamaa ni wahujumu uchumi wallah!

Kabla sijaenda mbali sana naomba nirejee kwenye suala la Gwajima na hoja nyingine zilizoibuka kutokana na kauli zake tata za kuwakataza watanzania kuchanjwa. Kukaangwa kwa Gwajima ni haki kabisa kwa makosa aliyofanya kuwapotosha wananchi kuhusu chanjo. Nasikitika tu amepewa adhabu ndogo sana licha ya kuwa kosa alilofanya ni zaidi ya uhujumu uchumi. Ni uuaji wa makusudi.

Je ni funzo gani tulilopata kutokana na adhabu hizi kwa wabunge wa CCM? Mosi, funzo kubwa ni kuwa kuna baadhi ya wanaCCM hawapendi uongozi wa mama Samia kwa sababu wanazozijua wao wenyewe (Ushahidi: Sikiliza clip hapo juu). Hawa ni wale masalia wa mwendazake waliojipa jina na MATAGA na kujifanya kuwa wao ni watanzania zaidi kuliko wengine. Dawa yao inachemka.

Pili, kuna baadhi ya watanzania aina ya Gwajima ambao wanamdharau mama Samia kwa sababu tu yeye ni mwanamke. Wanaoana eti hatoshi kuiongoza nchi. Kwa hiyo, wanajitahdi kuleta chokochoko na kumvuruga kusudi aache kujikita kuongoza nchi aanze kujishughulisha nao. Hii ni hujuma kubwa sana. Wabunge wengi waliochangia hoja kwenye klipu hapo juu, wamessikitsishwa mno na kitendo hiki cha baadhi ya watanzania wasioitakia mema nchi hii kufanya juhudi za kumkwamisha mama Samia. Hili halikubaliki hata kidogo.

Nahitimisha kwa kusema adhabu hii aliyopewa Gwajima ni ndogo sana kwani suala lake limekuwa likifanyika kwa muda mrefu na kwa kurudiarudia. Ameonyesha dharau kubwa sana kwa rais wetu hasa pale alipomtuhumu kwamba alifanya chanjo ya maigizo na kwamba amehongwa na mabeberu ili kuleta chanjo ya kuwaua watanzania. Ilipaswa huyu bwana apewe adhabu kali zaidi.

Na akama Spika aliposhauri, naomba chama chake kiangalie uwezekana wa kumfuta uanachama ili liwe fundisho kwa wengine wasioheshimu mamlaka. Laiti kama mbunge wa upinzani ndiye anayefanya upotoshaji huu anaofanya Gwajima, nadhani angekuwa hata ameishauawa na watu wasioijulikana. Lakini kwa kuwa ni mbunge mwenzao ndio maana wamempa adhabu nyepesi.

Taarifa zaidi kuhusu sakata hili unaweza kulipata kwenye uzi huu hapa chini:

Ikiwa makato kwenye miamala ya simu, LUKU na mabenki hayatabadilika nini kifanyike?

Nawasilisha.​
Mods unganisheni huu Uzi tafadhali na ile mingine inayomzungumzia Gwajima na Slaa kwa yale yaliyotokana na Bunge la leo.
 
Like serious, bunge linaacha kujadiri mambo ya msingi wanamjadiri Gwajima na slaa tena kwenye jambo la hiari !!?
Duh hii ndo Tz!
Hujauwa tu bado kuna mtu anataka kuwa spika kama kwa miaka 20? Japo wanamuangalia tu jina siku yake kulikata aibuuuuu
 
Hapo umekosea sana, Kwa mujibu wa sheria ya kodi, posho zinapaswa kukatwa kodi. Sema hizo posho za wabunge ndizo hazikatwi kodi.
Soma hii sec 7 ya income tax act 2008
7.-(1) An individual's income from an employment for a year of

income shall be the individual's gains or profits from the employment of

the individual for the year of income.

(2) Subject to the provisions of subsection (3), (4) and (5) in

calculating an individual's gains or profits from an employment for a year

of income the following payments made to or on behalf of the individual

by the employer or an associate of the employer during that year of income

shall be included:

(a) payments of wages, salary, payment in lieu of leave, fees,

commissions, bonuses, gratuity or any subsistence travelling

entertainment or other allowance received in respect of

employment or service rendered;

Kama kuna marekebisho yoyote hapa katikati, nakubali kukosolewa.
Fact. Wabunge hawa wa CCM walitukosea sana walipotunga sheria ya kukata kodi posho lakini posho za wabunge wakaziondoa kwenye makato ya kodi. Inauma sana.
 
Back
Top Bottom