Uchaguzi Mkuu Kenya unaendeshwa kwa misingi ya Kikabila?

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Tangu kuanzishwa kwa siasa za vyama vingi Kenya, somo moja ambalo vyama vya siasa vimejifunza ni mpango wa kuungana ili kuweza kupata ushindi wakati wa uchaguzi mkuu. Uanzishaji wa miungano umekuwa msingi wa siasa za Kenya tangu uchaguzi wa 2002. Muungano wa kwanza ulikuwa wa National Rainbow Coalition uchaguzi wa 2002, muungano ulioleta Pamoja vyama vyote vikuu vya upinzani wakati huo dhidi ya mgombea wa chama cha KANU.

Lakini imekuwa ikilalamikiwa kuwa katika kuunda coalitions hizo basi kikubwa kinachoangaliwa ni nguvu za makabila. Kwa Kenya makabila matatu ndio yanadhaniwa kuwa na nguvu sana kutokana na idadi ya watu waliopo. Makabila hayo ni Wakikuyu, Kalenjin na Wajaluo.

Tokea Kenya ipate uhuru imekuwa ikitawaliwa na Marais hawa kutoka Makabila mawili tu ambao ni
  • Jomo Kenyatta (1963–1978) - Kikuyu
  • Daniel Arap Moi (1978–2002) - Kalenjin
  • Mwai Kibaki (2002–2013) - Kikuyu
  • Uhuru Kenyatta (2013–2022) - Kikuyu
  • William Ruto (2013-...) - Kalenjin
Hayati Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa Dhambi ya ubaguzi ukishakuitenda inaendelea ni sawasawa na kula nyama ya mtu. Ukila nyama ya mtu utaendelea tu kuila.

Wajaluo wamekuwa wakipambana kutawala tokea enzi za Mzee Jaramogi Oginga Odinga lakini juhudi zao ziligonga mwamba, tumaini lao la mwisho lilikuwa Raila Amoli Odinga ambaye pamoja na kuungana na Uhuru Kenyatta lakini Ujaluo wake ulimponza na kuangukia pua

Hivyo Kenya itaendelea kutafunwa na dhambi ya ubaguzi wa kikabila katika kusaka madaraka.

Nimalizie kwa kumnukuu William Clay - "Kwenye siasa hakuna maadui wa kudumu na urafiki wa kudumu, isipokuwa maslahi tu"
 
Back
Top Bottom