Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

habari za hivi punde ni kuwa mkutano wa CCM ambao ulikuwa wa uzinduzi wa kampeni huko Busanda umeanza kwa kudorola kutokana na kuhudhuriwa na watu wachache sana kiasi cha kulazimika kuwaomba wanafunzi kuhudhuria katika mkutano huo wa kampeni.
hali hii ni tofauti na mikutano ya Chadema na Cuf ambayo ilizinduliwa Rasmi siku ya JUmamosi na kupata watu wengi.
inasemekana tayari viongozi wa CCM wameanza kulaumiana huku baadhi wakidai kuwa walipanga eneo hilo kutokana na kukwepa kumpeleka Msekwa Nyarugusu kwa kuhofia kuwa huenda angezomewa kutokan ana kutokuwa na ushawishi wa kutosha kubadili upepo kama Malecela.
Hata hivyo haijaeleweka Malecela ambaye alikuwa akitarajiwa kuhudhuria ameshidwa kufika kutokana na nini na badala yake chama kimempangia kuendela kesho na kampeni za Chama hicho enao la Nyarugusu. naendela kufuatilia ili kupata habari kamili.:rolleyes:
 
Wananchi wameshajua CCM hawana jipya la kuwaambia watu wa Busanda na TZA kwa ujumla. Watanzania walio wengi wameamka.

Ila tusijekushangaa mahudhurio hafifu ya kampeni kwa chama tawala halafu wapinzani wakawa na wafuasi wengi ktk viwanja vyao; MATOKEO YAKAWA KINYUME NYUME.

CCM WANAMBINU NYINGI CHAFU ZA KUPATA USHINDI. TUWE MACHOO KWA HILO. PIGA KURA THEN LINDA KURA YAKO, HAKUNA KURUDI NYUMBANI HADI UMEJUA MATOKEO YA KITUO CHAKO. Vinginevyo wapinzani itakula kwao tena km kuleeeee..... Mbeya
 
Weka antena yako vizuri mkuu uturushie vyema yatakayo jiri.

Mgombea ubunge wa CCM awapigia magoti wananchi wa Busanda

Na Frederick Katulanda, Busanda

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeanza vibaya uzinduzi wa kampeni zake za uchaguzi mdogo Jimbo la Busanda katika Kata ya Kaseme, Busanda baada ya kupata watu wachache tofauti na mikutano ya Chadema na CUF ambavyo vilizindua rasmi mikutano yao Jumamosi iliyopita katika maeneo tofauti.

Wakati ikiwa hivyo katika ufunguzi huo, mgombea wao Lolencia Masele Bukwimba alijinadi kwa kuwapigia magoti wapiga kura huku akiomba wampigie kura kwa kuwa ni mwenyeji wa eneo hilo.

Bukwimba alisema ameamua kugombea ili awatumikie baada ya kuwatumikia wananchi nje ya jimbo hilo kwa muda mrefu akiwa katika mikoa ya Arusha na Dar es Salaam.

Alisema ameamua kurejea Busanda kugombea ubunge ili kuwasaidia katika harakati za maendeleo na kwamba, atakaa huko kinyume na madai ya wanaosema atawatelekeza na kwenda kuishi Dar es Salaam.

“Nimekuja kugombea kwa ajili ya kuwasaidia wananchi, ingawa kuna watu wanadai kuwa mkinichagua nitakuwa nakaa Dar, siyo kweli kwetu ni katika kijiji cha Nyabulolo na mume wangu ni huyu hapa ameniruhusu kugombea, naye atakaa hapa Nyabulolo hivyo nawaombeni kura zenu,” alieleza Bukwimba huku akipiga magoti na kurejea kwa lugha ya Kisukuma.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa katika uzinduzi huo, Katibu wa chama hicho, Yusuf Makamba aliionya Chadema kuwa isitarajie kuibuka na ushindi katika jimbo hilo kwa vile jimbo hilo ni lao kutokana na kumilikiwa na marehemu, Faustine Kabuzi Rwiromba sawa na ilivyokuwa kampeni za uchaguzi mdogo wa Tarime ambapo Chadema walishinda.

Makamba alisema CCM wana hakika ya kushinda kama ilivyokuwa kwa Chadema Tarime, kutokana na umiliki wa awali wa jimbo hilo kuwa mikononi mwao na kufananisha uchaguzi huo ni kiraka katika suruali iliyotatuka ambayo unapotaka kuiziba ni lazima utumie rangi na aina ya kitambaa cha suruali halisi.

“Hiki ni kiraka. Sasa suruali ikitoboka na ukitaka kuziba kwa kiraka, utatumia kitambaa cha rangi gani kama si ilele ya suruali. Kwa hiyo Chadema na wenzako mnapaswa kujua kuwa jimbo hili ni mali ya CCM kama ilivyokuwa kwao katika jimbo la Tarime na wakalirejesha,” alisisitiza Makamba.

Akijibu hoja za upinzani ambazo zimekuwa zikitolewa katika mikutano ya kampeni kuwa CCM imejaa mafisadi, alisema ufisadi ni wa mtu mmoja na wala siyo chama, hivyo CCM isilaumiwe kwa hilo badala yake alaumiwe anayehusika na ufisadi.

Alisema chama kinao watu safi hivyo kukiita ni chama cha ufisadi kama wapinzani wanavyodai ni makosa na upotoshaji mkubwa, hivyo kuwataka wananchi kupuuza madai hayo.

“Hawa wakija hapa wanasema CCM ni mafisadi, hebu niambieni wao Chadema walipewa fedha kwa ajili ya kugawa pikipiki na baiskeli nchi nzima na wafadhili lakini hawakugawa, badala yake walipeleka stakabadi bandia kwa mfadhili huyo, hapa nani ni fisadi kama sio wao,” alihoji Makamba.

Akizindua kampeni hizo jana, Msekwa alisema wanao uhakika wa kushinda kutokana na nguzo kuu tano ambazo ni umoja, mshikamano, wingi wa wanachama, sera safi pamoja na mfumo bora wa uteuaji wagombea.

Alisema CCM ina uhakika wa kushinda katika uchaguzi huo kutokana na historia ya mageuzi na kwamba, kutokana na kuwa na wanachama wengi wamekuwa wakishinda katika chaguzi mbalimbali.

“Mwaka 2005 katika uchaguzi wa wabunge UDP na TLP vilipata kiti kimoja wakati CUF ilipata viti 19 kwa upande wa visiwani, Chadema viti vitano na CCM kuibuka kidedea kwa kupata viti 206 kikiwemo cha Busanda, hivyo nasisitiza kwamba tutashinda,” alieleza.

Hata hivyo mkutano huo ulihudhuriwa na watu wachache huku sehemu ya wahudhuriaji hao ikijazwa na wanafunzi wa sekondari ya Kaseme, jambo ambalo lilifanya baadhi ya viongozi wa chama hicho kukosoa kuwa mkutano huo wa ufunguzi ungefanyika alikozaliwa mgombea huyo au Katoro.

Licha ya John Malecela kukwama kufika katika kampeni hizo kutokana na kuchelewa kufika Busanda, CCM ilikuwa ikilitumia kundi la uhamasishaji la TOT, huku timu ya wabunge wa Kanda ya Ziwa akina, Samwel Chitalilo, Anthony Diallo, Lawrence Masha, Dalali Shibiliti na Festusi Limbu wakishuhudia.

Leo kampeni za chama hicho zitaendelea katika kata ya Nyarugusu na kuhutubiwa na Malecela.

Sasa mzee makamba anakataaa nini??? Waliokuwa wanashutumiana hivi karibuni kuwa fulani na fulani ni mafisadi papa nao wakasema fulani ni nyangumi; HAWA WOTE NI WANANCHAMA WA CHAMA GANI??? CHADEMA, CUF, NCCR AU CCM??? Nahisi ktk huo mkutano hakukuwa na kuuliza maswali au hao watoto wa shule ni wa bweni maana hata magazeti, tv hakuna huko

Sasa km CCM hawana jipya hao watu watatokea wapi???
 
habari za hivi punde ni kuwa mkutano wa CCM ambao ulikuwa wa uzinduzi wa kampeni huko Busanda umeanza kwa kudorola kutokana na kuhudhuriwa na watu wachache sana kiasi cha kulazimika kuwaomba wanafunzi kuhudhuria katika mkutano huo wa kampeni.
hali hii ni tofauti na mikutano ya Chadema na Cuf ambayo ilizinduliwa Rasmi siku ya JUmamosi na kupata watu wengi.
inasemekana tayari viongozi wa CCM wameanza kulaumiana huku baadhi wakidai kuwa walipanga eneo hilo kutokana na kukwepa kumpeleka Msekwa Nyarugusu kwa kuhofia kuwa huenda angezomewa kutokan ana kutokuwa na ushawishi wa kutosha kubadili upepo kama Malecela.
Hata hivyo haijaeleweka Malecela ambaye alikuwa akitarajiwa kuhudhuria ameshidwa kufika kutokana na nini na badala yake chama kimempangia kuendela kesho na kampeni za Chama hicho enao la Nyarugusu. naendela kufuatilia ili kupata habari kamili.:rolleyes:

Dalili ya mvua ni mawingu, hii ni habari njema sana yenye kuamsha matumaini!
 
Ajenda ya UFISADI ni kaa la moto kwa CCM na ndiyo maana wanatumia nguvu kubwa sana kujenga hoja kwamba CCM siyo chama cha mafisadi bali ufisadi ni wa mtu mmoja mmoja tu.

Swali la kujiuliza je hao watu ambao wanasemwa ni mmoja mmoja tu wamefanywa nini? Kama CCM ingekuwa makini na kweli inataka kuonyesha nia ya dhati ya kupinga ufisadi, wale wote wenye tuhuma za ufisadi wangepigwa chini kwanza then wachunguzwe na iwapo watagundulika kwamba tuhuma zao ni za kizushi then wangeweza kurudishwa kwenye nyadhifa walizo nazo.

Lekule (Mbunge wa Longido) na Mollel (Mbunge wa Arumeru) walituhumiwa kutumia rushwa kwenye uchaguzi wa chama, vikao vya chama vilifanya maamuzi ya kuwazuia wasigombee mpaka pale watakapothibitishwa na mahakama kwamba hawakutumia rushwa. Iweje, vikao hivyo hivyo vya Chama viwakomalie baadhi na wengine wabaki wanatesa na nyadhifa zao?

CCM ni chama cha mafisadi na ndiyo maana "gwiji" la ufisadi likiguswa Chama chote kinatikisika utawasikia akina Makamba (Katibu Mkuu), Chiligati (Katibu Mwenezi) na Mkuchika (Naibu Katibu Mkuu Bara) wakija juu na kusema hizo tuhuma ni uzushi, how do you judge kwamba ni uzushi bila kuzifanyia kazi? Je, walishazifikisha mikononi mwa Polisi/TAKUKURU na report ikarudi ikiwa imewasafisha watuhumiwa?

Mtu kama Chenge ambaye anatuhumiwa kwenye sakata la Radar bado ni mjumbe wa kamati ya maadili ya CCM, hivi huko kwenye maadili hawagusii maswala ya ufisadi, ama maadili ya huko ni yale yanayohusu matusi tu? Mtu kama huyo ikija ajenda ya kuhusu ufisadi hawezi kuchangia constructively kwa kuwa inamgusa moja kwa moja na akipendekeza hatua kali zichukuliwe dhidi ya watuhumiwa ni sawa na kujifunga kitanzi yeye mwenyewe.

Ili CCM ijipambanue na mafisadi inatakiwa kuwatosa wote ambao wanatuhuma na wazipeleke polisi ama TAKUKURU, hata kama jamii haina imani na vyombo hivyo, siku watu wakija na hoja ya tuhuma za ufisadi CCM itakuwa na uwezo wa kujitetea kwamba tuhuma zilichunguzwa na polisi na hazikuwa za kweli, na hapo watakuwa wamejisafisha japo ni kwa kutumia maji machafu kama TAKUKURU ilivyofanya kwa marehemu Richmond.

Uzuri wa UFISADI ni kwamba umekigawa chama kwenye mapande makubwa 2, wapo wanaopingana na ufisadi kikweli na wapo walio nyuma ya mafisadi ama watetezi wa mafisadi. Tatizo kubwa ni kwamba viongozi walio wengi kwenye CCM wanawalinda mafisadi including mwenyekiti wa chama na ndiyo maana inakuwa ngumu kwake kufanya lolote na akizidiwa nguvu ndipo hutekeleza mambo mengine japo kwa shingo upande hata kama alikuwa hapendi kufanya hivyo.

Nchi na Chama kwa sasa havina uongozi, kama ni ndege basi iko kwenye Auto Pilot, na tukikutana na dhoruba ya ukungu ama hali mbaya ya hewa basi tunaweza kujikuta tunapoteza mwelekeo ama kusambaratika kabisa.

CCM ijisafishe kwanza ama ionyeshe nia ya dhati kwamba inajipambanua na ufisadi na hilo hawawezi kulifanya kwa kuwa hela za ufisadi ziliwasaidia kwenye uchaguzi. Hao wanaotuhumiwa walifaidika kwa kuchota mabilioni na kiasi fulani wakakipeleka kwenye kampeni.
 
Tofauti na Dar es Salaam, huko mikoani watu wameamka na hawako tayari tena kusikiliza ngonjera za CCM za ahadi hewa. Watu wa mikoani kwa kweli wamechoka na porojo na stori za viongozi wa serikali ya CCM na wanataka kusikia vitu vipya. Mkoa wa Dar es Salaam umetokea kuwa pango la mafisadi na hivi sasa ni kikwazo kweli kewli katika harakati za kuleta mabadiliko nchini.
Shame on you Dar es Salaam.​
 
habari za hivi punde ni kuwa mkutano wa CCM ambao ulikuwa wa uzinduzi wa kampeni huko Busanda umeanza kwa kudorola kutokana na kuhudhuriwa na watu wachache sana kiasi cha kulazimika kuwaomba wanafunzi kuhudhuria katika mkutano huo wa kampeni.
hali hii ni tofauti na mikutano ya Chadema na Cuf ambayo ilizinduliwa Rasmi siku ya JUmamosi na kupata watu wengi..:rolleyes:

This is the best news i have reAd!!!.

Wanastahili sifa sana wananchi wa Busanda .At least sasa kelele za

viongizi wetu wa upinzani zinaanza kueleweka

BRAVO BUSANDA!!!!
 
Mi naona kumteua mwanamke yawezekana ikawa sababu huyo mama hana mvuto kwa wanachama na wapiga kura.
 
Jana niliangalia kwenye Tv ya CCM1 sorry kumbe ni tbc1 nimekosea kwa sababu hiyo ni tv ya chama cha mapinduzi.
Sikuamini porojo za Ma rope(Makamba) alizokuwa anawapa wana Busanda. Yaani kweli kama jina lake anawafunga kamba na ni Makamba kweli. Kufikia kuambia wananchi wa Busanda kuwa wana viongozi walio na mvuto? eti sijui wanajali shida zao? sijui Bra bra bra...................
Wakiwapa kura sisi m basi nitaamini ujuha ni wa wadanganyika kweli!
 
habari za hivi punde ni kuwa mkutano wa CCM ambao ulikuwa wa uzinduzi wa kampeni huko Busanda umeanza kwa kudorola kutokana na kuhudhuriwa na watu wachache sana kiasi cha kulazimika kuwaomba wanafunzi kuhudhuria katika mkutano huo wa kampeni.
hali hii ni tofauti na mikutano ya Chadema na Cuf ambayo ilizinduliwa Rasmi siku ya JUmamosi na kupata watu wengi.
inasemekana tayari viongozi wa CCM wameanza kulaumiana huku baadhi wakidai kuwa walipanga eneo hilo kutokana na kukwepa kumpeleka Msekwa Nyarugusu kwa kuhofia kuwa huenda angezomewa kutokan ana kutokuwa na ushawishi wa kutosha kubadili upepo kama Malecela.
Hata hivyo haijaeleweka Malecela ambaye alikuwa akitarajiwa kuhudhuria ameshidwa kufika kutokana na nini na badala yake chama kimempangia kuendela kesho na kampeni za Chama hicho enao la Nyarugusu. naendela kufuatilia ili kupata habari kamili.:rolleyes:

Hawa watu wa vijijini nao siku hizi wako informed. Hivyo wanajua vizuri kuwa CHAMA CHA MAFISADI, CHUKUA CHA MAPEMA, CHAMA CHA MATAJIRI etc. Hivyo wanajua kuwa chama kilichokuwa chao sasa hivi si chao ni cha wafanyabiashara na matajiri tu.

Hivyo jamaa wa upinzani inabidi wacheze karata zao vizuri kwani uwezekano wa kushinda ni mkubwa. Hao wazee waliopelekwa huko hawana jipya watu wamewazoea kuwa ni wasanii. HIVYO WAJIANDAE KWA ANGUKO LA PILI.
 
[COLOR="Red"][[/COLOR]COLOR="red"]Mgombea ubunge wa CCM awapigia magoti wananchi wa Busanda
[/COLOR]Na Frederick Katulanda, Busanda

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeanza vibaya uzinduzi wa kampeni zake za uchaguzi mdogo Jimbo la Busanda katika Kata ya Kaseme, Busanda baada ya kupata watu wachache tofauti na mikutano ya Chadema na CUF ambavyo vilizindua rasmi mikutano yao Jumamosi iliyopita katika maeneo tofauti.

Wakati ikiwa hivyo katika ufunguzi huo, mgombea wao Lolencia Masele Bukwimba alijinadi kwa kuwapigia magoti wapiga kura huku akiomba wampigie kura kwa kuwa ni mwenyeji wa eneo hilo.

Bukwimba alisema ameamua kugombea ili awatumikie baada ya kuwatumikia wananchi nje ya jimbo hilo kwa muda mrefu akiwa katika mikoa ya Arusha na Dar es Salaam.

Alisema ameamua kurejea Busanda kugombea ubunge ili kuwasaidia katika harakati za maendeleo na kwamba, atakaa huko kinyume na madai ya wanaosema atawatelekeza na kwenda kuishi Dar es Salaam.

"Nimekuja kugombea kwa ajili ya kuwasaidia wananchi, ingawa kuna watu wanadai kuwa mkinichagua nitakuwa nakaa Dar, siyo kweli kwetu ni katika kijiji cha Nyabulolo na mume wangu ni huyu hapa ameniruhusu kugombea, naye atakaa hapa Nyabulolo hivyo nawaombeni kura zenu," alieleza Bukwimba huku akipiga magoti na kurejea kwa lugha ya Kisukuma.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa katika uzinduzi huo, Katibu wa chama hicho, Yusuf Makamba aliionya Chadema kuwa isitarajie kuibuka na ushindi katika jimbo hilo kwa vile jimbo hilo ni lao kutokana na kumilikiwa na marehemu, Faustine Kabuzi Rwiromba sawa na ilivyokuwa kampeni za uchaguzi mdogo wa Tarime ambapo Chadema walishinda.

Makamba alisema CCM wana hakika ya kushinda kama ilivyokuwa kwa Chadema Tarime, kutokana na umiliki wa awali wa jimbo hilo kuwa mikononi mwao na kufananisha uchaguzi huo ni kiraka katika suruali iliyotatuka ambayo unapotaka kuiziba ni lazima utumie rangi na aina ya kitambaa cha suruali halisi.

"Hiki ni kiraka. Sasa suruali ikitoboka na ukitaka kuziba kwa kiraka, utatumia kitambaa cha rangi gani kama si ilele ya suruali. Kwa hiyo Chadema na wenzako mnapaswa kujua kuwa jimbo hili ni mali ya CCM kama ilivyokuwa kwao katika jimbo la Tarime na wakalirejesha," alisisitiza Makamba.

Akijibu hoja za upinzani ambazo zimekuwa zikitolewa katika mikutano ya kampeni kuwa CCM imejaa mafisadi, alisema ufisadi ni wa mtu mmoja na wala siyo chama, hivyo CCM isilaumiwe kwa hilo badala yake alaumiwe anayehusika na ufisadi.

Alisema chama kinao watu safi hivyo kukiita ni chama cha ufisadi kama wapinzani wanavyodai ni makosa na upotoshaji mkubwa, hivyo kuwataka wananchi kupuuza madai hayo.

"Hawa wakija hapa wanasema CCM ni mafisadi, hebu niambieni wao Chadema walipewa fedha kwa ajili ya kugawa pikipiki na baiskeli nchi nzima na wafadhili lakini hawakugawa, badala yake walipeleka stakabadi bandia kwa mfadhili huyo, hapa nani ni fisadi kama sio wao," alihoji Makamba.

Akizindua kampeni hizo jana, Msekwa alisema wanao uhakika wa kushinda kutokana na nguzo kuu tano ambazo ni umoja, mshikamano, wingi wa wanachama, sera safi pamoja na mfumo bora wa uteuaji wagombea.

Alisema CCM ina uhakika wa kushinda katika uchaguzi huo kutokana na historia ya mageuzi na kwamba, kutokana na kuwa na wanachama wengi wamekuwa wakishinda katika chaguzi mbalimbali.

"Mwaka 2005 katika uchaguzi wa wabunge UDP na TLP vilipata kiti kimoja wakati CUF ilipata viti 19 kwa upande wa visiwani, Chadema viti vitano na CCM kuibuka kidedea kwa kupata viti 206 kikiwemo cha Busanda, hivyo nasisitiza kwamba tutashinda," alieleza.

Hata hivyo mkutano huo ulihudhuriwa na watu wachache huku sehemu ya wahudhuriaji hao ikijazwa na wanafunzi wa sekondari ya Kaseme, jambo ambalo lilifanya baadhi ya viongozi wa chama hicho kukosoa kuwa mkutano huo wa ufunguzi ungefanyika alikozaliwa mgombea huyo au Katoro.

Licha ya John Malecela kukwama kufika katika kampeni hizo kutokana na kuchelewa kufika Busanda, CCM ilikuwa ikilitumia kundi la uhamasishaji la TOT, huku timu ya wabunge wa Kanda ya Ziwa akina, Samwel Chitalilo, Anthony Diallo, Lawrence Masha, Dalali Shibiliti na Festusi Limbu wakishuhudia.

Leo kampeni za chama hicho zitaendelea katika kata ya Nyarugusu na kuhutubiwa na Malecela.
Source: Mwananchi
 
Last edited:
Inashangaza sana kusikia mafisadi wanamsaport mgombea wa CUF,huu ni upotoshaji nina wasiwasi na uzalendo wako mwanakijiji inawezekana wewe ni fisadi lililobobea.

Nani hajui kwamba CUF tokea ilipoanzishwa mafisadi wamejipanga kuimaliza kuanzia seikalini hadi kwenye vyombo vya habari.
Anglia juzi kwenye ITV ya fisadi Mengi,taarifa ya habari walipotoa habari ya chadema waliitoa kwa ukamilifu huku wakimuonesha Dr.Slaa na mbowe pamoja na waliohudhuria kwa ukamilifu.lakini ilipo kuja habari ya CUF walimuonesha tu Mr.Hamad na hawakuionesha audiece(waliohudhria) NA UJUMBE ALIOUTOA JE HUU SI UFISADI KATIKA HABARI?

Tokea ianzishwe CUF imekuwa haipati cofreji ya maana katika vyombo vya habari apa tanzania hatuna vyombo huru vya habari si nipashe wala tanzania daima wala mwanahalisi.gazeti kidogo unaloweza kuliweka katika uhuru ni MWANANCHI.

Ni mafisadi ndo wamekuwa wakilisimamia hilo kwa ticket ya udini. na nyinyi kina mwanakijiji mkaingia kundini.
 
WanaJF,
CCM wanapaswa wajiulize maswali yafuatayo na kuyatolea majibu:
1.Kudorora kwa ununuzi wa pamba na kusababisha marobota yalundikane kwenye majumbani mwa wakulima.
2.Wamesaidiaje wakulima kuwatafutia mazao mbadala ambayo yana soko zuri?
3.Wametekelezaje mapendekezo ya Tume ya Madini ya Judge Bomani na yakitekelezwa ni manufaa gani wanageita watayapata.
4.Ni nini kimewazuia serikali ya CCM pamoja na kupewa ridhaa kubwa na wananchi wameshindwa kuboresha maisha ya wananchi richa ya kuongoza mfululizo kwa miaka karibu 50?
5.Ni matarajio gani kutoka kwa mgombea atakavyoshiriki dhidi ya vitendo vya kifisadi vinavyoshamilishwa na serikali ya CCM?Jibu hili alitoe sasa hivi kabla hajapewa ridhaa ya wapiga kura.Maana tumeona waliochaguliwa upande wa CCM wameshindwa kuonyesha msimamo wao(TUnduru,Kiteto na Mbeya vijijini)
Wakijibu maswali haya basi wapigakura na walipakodi wa Busanda wayatathmini majibu na kutoa maamuzi.Enzi za kupewa burudani na zawadi za kukidhi mahitaji ya mda mfupi zimeshapitwa na wakati.
 
Unajua.....ningepewa nafasi ya kuwafunda kambi ya upinzani ningewaambia yaani kwa jinsi CCM inavyoenda kwa sasa with scandals DAILY.....zinazowagusa wanachama wake...ni dhahiri wangecapitalize hapohapo.......they should drive the message home to all of us Tanzanians kwamba change haitaletwa na wageni ila sisi wenyewe tu.....These CCM guys have been running this country as they please .......na unajua jeuri wanakuwa nayo sababu kwa asili yetu Watanzania tuna "malaise" ya kufikiri...and we alwaiZ wait for the guy-next-door to come to our rescue.....haitatokea........we either kick these guys OUT or we eternally remain in poverty.....wananchi wa Busanda please help us DRIVE THE POINT HOME........WE ARE TIRED OF CCM!!!!!!!
 
Viongozi wa CHADEMA wakamatwa Geita

na Edward Kinabo, Geita

[Source: Tanzania Daima]

VIONGOZI wawili wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wilayani hapa, juzi jioni walikamatwa na polisi jirani na kituo kikuu cha mabasi mjini hapa, wakituhumiwa kumshambulia muuza magazeti, Abbas Omari.

Viongozi hao ni Katibu Mkuu wa chama hicho wilayani Geita, Rogers Ruhega (34) na Katibu wa Kata, Paul Vincent (33), ambao walikamatwa wakidaiwa kumshambulia muuza magazeti huyo katika eneo lake la biashara.

Muuzaji huyo wa magazeiti alifungua RB namba GE/IR/1055/2009 katika kituo kikuu cha polisi wilayani Geita, akielezea kushambuliwa na viongozi hao.

Viongozi hao wakizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, jana asubuhi, walisema chanzo cha tukio hilo ni kunyofolewa kwa habari zinazohusu wasifu wa mgombea ubunge wa CHADEMA, Jimbo la Busanda katika gazeti la Tanzania Daima Jumapili.

“Sisi tulipata simu kutoka Dar es Salaam, kwamba gazeti la Tanzania Daima la siku ile (Jumapili), lilitoa habari kubwa kwenye kurasa za ndani. Kwa hiyo, ilipofika jioni nilimwomba katibu wetu wa kata aende akatazame kama magazeti yameshafika Geita.

“Aliitazama nakala moja ambapo ndani yake aliona habari kuhusu mgombea wa CHADEMA. Alirudi kuongeza pesa ili kununua nakala nyingi zaidi, tukaongozana wote kwenda kununua magazeti ya sh 10,000.

“Tulipofika magazeti tuliyakuta, lakini nilipoanza kulisoma moja nikagundua halina ukurasa wa katikati uliokuwa na habari ya mgombea wetu. Tukatazama nakala zote za Tanzania Daima zilizokuwa pale, tukagundua kuwa zote zilinyofolewa kurasa zilizokuwa na habari kuhusu mgombea wetu wa Busanda.

“Kwa hiyo tulianza kumhoji yule bwana, nani amenyofoa kurasa kwenye magazeti haya na kwanini anawauzia watu magazeti yenye kurasa pungufu? Kukatokea ubishani mkubwa,” alisema Ruhega.

Alisema mabishano kati yao na muuzaji huyo wa magazeti yaliingiliwa sana na mtu mmoja, aitwaye David Azalia, ambaye walisema kuwa ni mjumbe wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wilayani Geita (UVCCM) na mwandishi wa habari wa gazeti la Habari Leo.

Ruhega alisema kuwa baada ya muda mfupi, mwandishi huyo wa Habari Leo, aliondoka eneo hilo na kuwaacha wao wakiendelea kulumbana na muuzaji huyo wa magazeti, lakini dakika chache walimsikia muuzaji wa magazeti akiongea kwa simu na mwandishi huyo, akipewa maelekezo ya kwenda kushitaki polisi.

Alisema, polisi walipofika eneo hilo, walikataa kuchukua ushahidi wa nakala hizo za gazeti la Tanzania Daima, badala yake wakawakamata na kuwaweka kizuizini katika kituo kikuu cha polisi mjini Geita, kwa dakika kadhaa, hadi walipokuja kutolewa kwa dhamana na mwenyekiti wa CHADEMA, tawi la Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine.

Alisema kuwa wanaamini kuwa kunyofolewa kwa nakala hizo, kuna mkono wa CCM kwani hawataki wananchi wa Busanda na wilaya nzima ya Geita waelewe sifa nzuri za kielimu na kiutendaji alizonazo mgombea ubunge wa CHADEMA, Jimbo la Busanda, Finias Magessa.

Aidha, muuza magazeti huyo alipoulizwa ni nani hasa amenyofoa nakala hizo, alisema: “Ni yule mwandishi wa Habari Leo.”

Ruhega, alisema kuwa katibu wao wa kata alipokwenda pale mara ya kwanza alimwona mwandishi huyo.

“Tulipokwenda wote mara ya pili tulimkuta pembeni na tulipomuuliza yule muuzaji magazeti mbona kurasa zimenyofolewa, yule mwandishi ndiye akawa wa kwanza kuanza kujibu kwa niaba yake,” alisema.

Hata hivyo, jitihada za gazeti hili kuzungumza na OCD kuhusu suala hili ziligonga mwamba kwani hakuwa tayari kulizungumzia kwa sababu ya kile alichodai kuwa yeye si msemaji rasmi.
 
Huyo fisadi anaenyofoa wasifu wa mgombea hafikirii kabisa. Huyo anatakiwa kurushiwa mabomu ya mbagala akafie mbali huko, ili akome kufanya hivo

Unajua Chama Cha Mafisadi (CCM) huwa hawana confidence wanachojuwa wao ni kuiba na si vinginevyo. Sasa basi sisi watanzania wenye uchungu wa nchi yetu tunatakiwa kuhakikisha kuwa SISIEMU haikamati majimbo ya kutosha ili kidhoofisha Bungeni. Wana JF wote ambao wanaumizwa na mambo yanayofanywa na SISIEMU inabidi kuandaa mkakati maalumu wa kuwasambaratisha hawa MAFISADI wa SISIEMU.
 
Ukweli ni kwamba wananchi wengi wa Tanzania wamechoswa na siasa za KIFISADI. Sasa kinachotakiwa ni kuisambaratisha kabisa hiyo SISIEMU hapo Busanda. Kwa kuwa SISIEMU wanambinu nyingi sana za kuiba kura, wananchi wa Busanda wanatakiwa kuwa waangalifu sana kwenye zoezi zima la upigaji kura na uhasabuji kura. kukiwa na ulegevu wowote hapa SISIEMU watatumia mwanya huo kubadilisha matokeo.
 
Kama wamechoshwa/mmechoshwa/tumechoswa inapaswa tushiriki kikamilifu ikiwa ni pamoja na kujiandikisha kupiga kura na kulinda kura zenyewe. Halafu kikubwa kuukata ufisadi, kwani wasimamizi wa vyama vya upinzani wananunuliwa kwa msimbazi mbili na kukubali kuhamisha kura. Ni ufisadi mkubwa, tukiukataa huu basi hata hiyo katiba tutaibadili hata kama hawataki.
 
Back
Top Bottom