Uchaguzi 2020 Ubunge Tarime Mjini: Ngicho ahamishia nguvu zake kwa Gerald Martin

nokwenumuya

JF-Expert Member
Jun 29, 2019
810
2,851
UBUNGE TARIME MJINI: NGICHO/WAITARA WAHAMISHIA NGUVU ZAO KWA GERALD MARTIN

Kura za maoni Jimbo la Tarime Mjini zilifanyika tarehe 21 Julai 2020 na Jackson Kangoye akafanikiwa kuongoza kwa idadi ya kura. Inafahamika kwamba Jackson Kangoye na Mwita Waitara walitengeneza muungano ili kusaidiana katika kura za maoni za Tarime Mjini na Tarime Vijijini.

Na wote wawili walitegemea msaada wa Kamati ya Siasa Tarime katika kupindisha tararibu ili waweze kupata upendeleo dhidi ya wagombea wengine. Itakumbukwa Kamati hiyo ya siasa inayoongozwa na Mwenyekiti Daudi Marwa Ngicho, mchimbaji mdogo wa madini ambaye pamoja na mengine ana tuhuma mbalimbali katika hizo biashara zake.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Daudi Ngicho alihakikisha anaweka wabunge ambao watakuwa watiifu kwake na mara nyingi sana amewatishia waliokuwa wakishindana na Mwita Waitara ili kuhakikisha kuwa anapata nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM katika jimbo la Tarime Vijijini.

Kura za maoni zilifanikisha mpango wao kwa wote kushinda kura za maoni, japo iko wazi kilichotumika kuwapa hizo kura ni rushwa ambayo iko wazi. Baada ya kura hizo wananchi wengi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wameonyesha wazi kutokubali mapendekezo hayo ya wagombea maana hayaendani na matarajio ya wapiga kura wa Jimbo la Tarime Mjini na pia Tarime Vijijini.

Baada ya kujiridhisha kuwa Jackson Kangoye hakubaliki, ameruka na kuangalia jinsi anavyoweza kuitumia kamati ya siasa kumpendekeza mshindi wa tatu, Gerlad Martin, ambaye naye alipata kura 20 baada ya kuwa mtoa rushwa pia na taarifa zake zipo wazi.

Ngicho, Waitara wamekubaliana ni bora katika kikao cha kamati ya siasa kujaribu kushawishi na kumpendekeza Gerald Martin, kwani kwao ni mtu dhaifu ambaye wanaweza kummiliki na akafanya yale wanayotaka wao.

Na ikumbukwe Jumuiya ya Vijana Tarime kwa muda mrefu walijigeuza kuwa kikundi cha kumpigia Kampeni kinyume na kanuni za Uchaguzi. Hivyo ilikuwa rahisi Mwenyekiti wa UVCCM Tarime kumshawishi Waitara na Ngicho kuwa bora waende na Gerald, ambaye naye pia kiufupi sio mtu anayekubalika kwa wananchi maana hana mchango wowote kwenye jamii ukilinganisha na Michael Kembaki aliyekuwa mshindi wa pili na ambaye anakubalika.

Ngicho hamtaki Michael Kembaki kwa sababu haoni kama anaweza kummiliki kwa sababu ni mtu anayejitambua, mwenye biashara zake na asiyetegemea mtu katika maamuzi yake binafsi. Hivyo ameona ni bora ampiganie Gerlad, na kwa kuwa kamati nzima ya siasa iko chini yake na huwa anawalipa wote posho basi bila shaka anajua mapendekezo yake yote yatapita kwa asilimia 100.

Tunaomba viongozi wa kitaifa wa Chama waangalie kwa undani hali ya Tarime kwani maamuzi mabaya yatakayofanyika yatapelekea majimbo yetu kuendelea kuwa chini ya CHADEMA.

Wenu,
Venance Marwa,
Mwana CCM Mkereketwa Tarime.
 
Tarime Mjini Rushwa imetembea sana. Nasikia mpaka Wapinzani walitoa pesa ili baadhi ya wagombea CCM wasipate kura (inashangaza!!). Mmeacha wagombea wa maana (kwa sabau hawakutoa Pesa). CCM wakitaka kushinda hili jimbo waweke mtu anayekubalika hapa si aliyetoa rushwa
 
Tarime Mjini Rushwa imetembea sana. Nasikia mpaka Wapinzani walitoa pesa ili baadhi ya wagombea CCM wasipate kura (inashangaza!!). Mmeacha wagombea wa maana (kwa sabau hawakutoa Pesa). CCM wakitaka kushinda hili jimbo waweke mtu anayekubalika hapa si aliyetoa rushwa

Ni kweli hizo tuhuma zipo, Chadema walipambana kutoa pesa ili mgombea anayepita CCM awe ambaye wataweza kumgaragaza kwa urahisi
 
Ni kweli hizo tuhuma zipo, Chadema walipambana kutoa pesa ili mgombea anayepita CCM awe ambaye wataweza kumgaragaza kwa urahisi
Hapo ndio wameingia mkenge. Ester alipaswa kupata Mtu strong, msomi na anayekubalika na jamii ya Tarime. Nyie mkang'ang'ania pesa
 
Shida ni nini Ngoja Yaendelee Kuwa Chini ya CHADEMA, Kama Wananchi Wanapata Maendeleo. Jimbo Kuwa Chini ya CCM Haiwaongezei lolote au Chochote Wana Tarime pote Mjini na Vijijini.

Nakupa 100, kwani lazima yawe chini ya CCM. Hawa wamerogwa, hao CCM watajijua wenyewe waweke Waitara , jiwe au mbuzi kama wanarangi ya kijani hakuna tofauti.
 
Back
Top Bottom