Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,205
- 25,535
Ligi Kuu ya Hispania,maarufu kama La Liga imeendelea kuwadhihirishia wanazi wa soka la EPL na kwingineko kuwa ni ligi bora na yenye ushindani hadi mechi ya mwisho. Ligi zote kubwa Ulaya zimeshapata mabingwa wake hata kabla ya kuisha mechi zao isipokuwa La Liga.
Ujerumani,bingwa ni Bayern Munich. Uingereza,bingwa ni Leicester City. Ufaransa,bingwa ni PSG. Italia,Juventus ametwaa ndoo muda mrefu tu. Uholanzi,PSV Eindhoven wameshakuwa mabingwa. Tanzania,Yanga wamekuwa mabingwa na kadhalika.
La Liga bado hakuna bingwa. Kabla ya mechi za jana,Barcelona na Atletico Madrid walikuwa wakiongoza kwa alama 85 kila mmoja wakifuatiwa na Real Madrid aliyekuwa na alama 84,alama moja nyuma yao. Baada ya Barcelona kuisambaratisha Espanyol kwa 5-0, Madrid kuizima Valencia 3-2 na Atletico Madrid kulazwa na Levante iliyo mkiani kwa 2-1,Barcelona inaizidi Madrid alama moja na A. Madrid alama tatu.
Zinasubiriwa mechi za mwisho. Bingwa hadi mechi za mwisho zichezwe. Anaweza kuwa Barcelona au Real Madrid. Hiyo ndiyo La Liga,rugby ya EPL tupa kule!