Ubora wa ligi: Ni La Liga tu ambao hawajampata bingwa wakisubiri mechi ya mwisho

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,198
25,517
Ligi Kuu ya Hispania,maarufu kama La Liga imeendelea kuwadhihirishia wanazi wa soka la EPL na kwingineko kuwa ni ligi bora na yenye ushindani hadi mechi ya mwisho. Ligi zote kubwa Ulaya zimeshapata mabingwa wake hata kabla ya kuisha mechi zao isipokuwa La Liga.

Ujerumani,bingwa ni Bayern Munich. Uingereza,bingwa ni Leicester City. Ufaransa,bingwa ni PSG. Italia,Juventus ametwaa ndoo muda mrefu tu. Uholanzi,PSV Eindhoven wameshakuwa mabingwa. Tanzania,Yanga wamekuwa mabingwa na kadhalika.

La Liga bado hakuna bingwa. Kabla ya mechi za jana,Barcelona na Atletico Madrid walikuwa wakiongoza kwa alama 85 kila mmoja wakifuatiwa na Real Madrid aliyekuwa na alama 84,alama moja nyuma yao. Baada ya Barcelona kuisambaratisha Espanyol kwa 5-0, Madrid kuizima Valencia 3-2 na Atletico Madrid kulazwa na Levante iliyo mkiani kwa 2-1,Barcelona inaizidi Madrid alama moja na A. Madrid alama tatu.

Zinasubiriwa mechi za mwisho. Bingwa hadi mechi za mwisho zichezwe. Anaweza kuwa Barcelona au Real Madrid. Hiyo ndiyo La Liga,rugby ya EPL tupa kule!
 
Huo ni ubora au ni ubovu wa timu nyingi kwenye hiyo ligi!!!! Hii inatoa maana kuwa ni timu chache kwenye hiyo ligi zinazoweza kutoa upinzani kwa timu kubwa kama Real Madrid, Barcelona na Atletico. Timu kama Espanyol hata Vpl haiwezi kuchukua ubingwa halafu unategemea iweze kuizuia Baca kweli!!!!?
 
Huo ni ubora au ni ubovu wa timu nyingi kwenye hiyo ligi!!!! Hii inatoa maana kuwa ni timu chache kwenye hiyo ligi zinazoweza kutoa upinzani kwa timu kubwa kama Real Madrid, Barcelona na Atletico. Timu kama Espanyol hata Vpl haiwezi kuchukua ubingwa halafu unategemea iweze kuizuia Baca kweli!!!!?

Mkuu mkolaj ,Barcelona na Leicester nani amefungwa mechi nyingi? Kwa taarifa yako,Barcelona amefungwa 5 na Leicester amefungwa 3 tu. Wakati Barcelona amefungwa na Socedad,Celta Vigo,Valencia na Madrid,Leicester amefungwa na Arsenal na Liverpool tu
 
Ligi ambayo hat trick zimejaa halafu unaiita bora? Kuna ligi hat trick inatafutwa kwa tochi. Tofautisha kati ya vilabu bora na ligi bora.
 
Ubora wa ligi unapimwa kwa level ya competition kwenye ligi husika.... Sasa kwenye la liga competition ni baija ya timu tatu, watu wanashinda goli 6 kila wiki hamna ligi hapo, sema kuna timu chache bora. Maana ya ligi ni ushindani, na hakuna kama EPL katika hilo.
 
Endeleeni na mabishano yasiyokuwa na tija. Mara EPL ndo bora mara La Liga n.k. Hongereni sana na ubishani wenu nadhani mwisho wa siku mtapata mgao wa fedha kutoka huko
 
Ubora wa ligi unapimwa kwa level ya competition kwenye ligi husika.... Sasa kwenye la liga competition ni baija ya timu tatu, watu wanashinda goli 6 kila wiki hamna ligi hapo, sema kuna timu chache bora. Maana ya ligi ni ushindani, na hakuna kama EPL katika hilo.
ni kweli mkuu sababu Bilbao alimpiga man u 5 sevila alimpiga Man u 3 Atletico alimzibua yokobus 4 na Granada alimtumbua Everton 3 Hapo Sijazuzungumzia Madrid na City
Mchezo huu hauhitaji ...
 
La liga ina timu bora tena chache uwez ona underground anachukua ubingwa uko milele ni ushindani wa izo timu tatu tofauti na epl ata kama la liga izo timu zisipokuwa form mabingwa na tatu bora ni hao hao na kama unataka kuamini angalia gap kati ya mtu wa tatu na wa 4 la liga afu angalia epl ndio ujue ushindani uko wapi barca kafungwa mechi tatu mfululizo na bado anaongoza ligi ebu yafanye epl uone kamuulize spurs ka droo mechi moja ndoto za ubingwa kwaeli
 
Hakuna kama La liga
Hakuna kama Barcelona
Hakuna kama KING10S

EPL tupa kwenye dustbin...
EPL hawatumii akili bali nguvu
EPL inawatoa jasho Segunda Division & Segunda B
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Back
Top Bottom