Jeshi la polisi limetangaza kuhamisha makao yake makuu Dodoma mwezi ujao kwa mujibu wa magazeti ya leo. Binafsi nachukulia uamzi huu kama wa kukurupuka. Kwanza Jeshi hilo si taasisi au idara ya kisiasa hivyo uwepo wao sehemu si kwa kigezo cha siasa bali usalama.
Wangejiuliza mfano kwa nini Dar es Salaam kuna mikoa maalum ya kipolisi na Dodoma hakuna. Dar kuna uhalifu mkubwa kulinganisha na Dodoma. Polisi wapo kwa ajili ya kulinda viongozi tu? Au yale yanayosemwa kwamba liko kisiasa ni kweli? Tujiulize unapotokea uvunjifu wa amani sehemu kwa nini wataalamu wa jeshi la polisi hutoka makao makuu kwenda mikoani?
Mfano mauji ya Amboni, milipuko ya Arusha na Zanzibar, au mauji ya msikitini Mwanza polisi walilazimika kutuma wataalamu toka makao makuu. Hii inaonyesha polisi wanahitajika sehemu tokana na unyeti wa kiusalama na si viongozi wa kisiasa watakapokuwa. Lazima tuhoji uamzi wa kuhamia Dodoma ni wa kisiasa au unatokana na tathmini ya kitaalamu ya mahitaji kiusalama?