Uamuzi wa kuhamishia makao makuu ya polisi Dodoma ni wa kitaalamu au kisiasa?

Jeshi la polisi limetangaza kuhamisha makao yake makuu Dodoma mwezi ujao kwa mujibu wa magazeti ya leo. Binafsi nachukulia uamzi huu kama wa kukurupuka. Kwanza Jeshi hilo si taasisi au idara ya kisiasa hivyo uwepo wao sehemu si kwa kigezo cha siasa bali usalama.

Wangejiuliza mfano kwa nini Dar es Salaam kuna mikoa maalum ya kipolisi na Dodoma hakuna. Dar kuna uhalifu mkubwa kulinganisha na Dodoma. Polisi wapo kwa ajili ya kulinda viongozi tu? Au yale yanayosemwa kwamba liko kisiasa ni kweli? Tujiulize unapotokea uvunjifu wa amani sehemu kwa nini wataalamu wa jeshi la polisi hutoka makao makuu kwenda mikoani?

Mfano mauji ya Amboni, milipuko ya Arusha na Zanzibar, au mauji ya msikitini Mwanza polisi walilazimika kutuma wataalamu toka makao makuu. Hii inaonyesha polisi wanahitajika sehemu tokana na unyeti wa kiusalama na si viongozi wa kisiasa watakapokuwa. Lazima tuhoji uamzi wa kuhamia Dodoma ni wa kisiasa au unatokana na tathmini ya kitaalamu ya mahitaji kiusalama?
Kwa miundombinu ipi? Ndipo mjue ni uhamaji wa kisiasa na wala siyo wa kitaalamu. Tusubiri tuone mwisho wa hii tamthiliya. Kama nakumbuka vizuri kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha Ikulu ilitengewa a good amount of money. Ina maana hii ndoto ya kwenda Dodoma ilikuwa bado haijaotwa au?
 
Jeshi la polisi limetangaza kuhamisha makao yake makuu Dodoma mwezi ujao kwa mujibu wa magazeti ya leo. Binafsi nachukulia uamzi huu kama wa kukurupuka. Kwanza Jeshi hilo si taasisi au idara ya kisiasa hivyo uwepo wao sehemu si kwa kigezo cha siasa bali usalama.

Wangejiuliza mfano kwa nini Dar es Salaam kuna mikoa maalum ya kipolisi na Dodoma hakuna. Dar kuna uhalifu mkubwa kulinganisha na Dodoma. Polisi wapo kwa ajili ya kulinda viongozi tu? Au yale yanayosemwa kwamba liko kisiasa ni kweli? Tujiulize unapotokea uvunjifu wa amani sehemu kwa nini wataalamu wa jeshi la polisi hutoka makao makuu kwenda mikoani?

Mfano mauji ya Amboni, milipuko ya Arusha na Zanzibar, au mauji ya msikitini Mwanza polisi walilazimika kutuma wataalamu toka makao makuu. Hii inaonyesha polisi wanahitajika sehemu tokana na unyeti wa kiusalama na si viongozi wa kisiasa watakapokuwa. Lazima tuhoji uamzi wa kuhamia Dodoma ni wa kisiasa au unatokana na tathmini ya kitaalamu ya mahitaji kiusalama?
Tarime nako kuna kanda maalumu ya kipolisi mbona sio makao makuu ya polisi?
 
Ni vema kama kitu hujui uanze kuuliza na siyo judgemental statement
Kwa taarifa yako...IGP LAZIMA KILA SIKU ASUBUHI AHUDHURIE MORNING CALL YA KIKAO CHA BARAZA LA USALAMA LA TAIFA KINACHOONGOZWA NA RAIS..AKIWEMO MKUU WA MAJESHI...MKURUGENZI USALAMA WA TAIFA..NA WENGINE AMBAO SINA HAJA KUKUTAJIA
Kwa maana hiyo by any means usitegemee kama Rais wa nchi akihamia Dodoma wakuu wa majeshi na wakurugenzi wakuu wa ulinzi na usalama wabaki Dar....LAZIMA NA WAO WAWE PALE
Isitoshe....Kanda Maalumu Dar HAIJUMUISHI Headquarter ya Jeshi..Hizo hazihami na Ma RPC wa hizo Kanda wapo na Kamishna wa Kanda Maalumu wa Polisi ataendelea kuwepo

My take:pICHA AMBAYO NAIPATA HAPA TANZANIA KWA SASA NI KUWA UKIKOSOA NA KUPINGA KILA KITU KINACHOFANYWA NCHINI NDIPO UNAONEKANA UNA AKILI..LKN UKIUNGA MKONO KITU CHEMA UNAONEKANA HUNA MAANA!!!!!...Mhhh the attitude wa are now engaged in damage our destination. ..I stand to be corrected
mkuu nawe usikurupuke..
IGP anasema anahamia Dodoma September,wakati rais bado atakua yupo Magogoni...
logic yako iko wapi ya morning call ?
 
yeah,hiyo sababu ina logic,wakuu wa usalama lazima wambrief rais kuhusu mambo ya usalama daily na personaly
Logic iko wapi? Kwan nani kasema rais anahamia mwezi ujao ? kama sababu ulizosema ni kweli basi wangesubiri mh.rais ahamie au wao wahame mwezi mmoja kabla ya rais kwenda
 
hakuna hasara kubwa kama mtu anayeitwa msomi kuongozwa na mihemko na sio hoja na falsafa..
unakuta msomi kutwa ni kukurupuka ili kumridhisha mwengine !!
hana tena udhibiti wa akili yake !!
ninavyoelewa kuna taasisi zinapaswa kuhama pamoja na taasisi ya rais..
kwani hupaswa kua pamoja kila siku..
hebu tuangalie, taasisi ya rais hukutana na viongozi wa taasisi za ulinzi na usalama kila siku..
sasa wewe mkuu wa taasisi ushakurupuka na kukimbilia DOM, halafu rais wako bado yupo Dar na anakuhitaji katika vikao vya kila siku vya ulinzi na usalama !
ngachoka !!!!!!!
 
Nchi hii imekuwa na Mihemko sana awamu hii hata walio na upeo wamemezwa na kuogopa kutoa ushauri.
 
Na hii nadhani inatokana na kauli zake kwamba mtu akienda tofauti na anavyotaka yeye basi atalala naye mbele, hiki kitu kinatisha sana sidhani kama kuna mtu yupo tayari kulala na Rais
Nani anataka kuharibu ugali wake kazi yetu ni kutii amri halali ndiyo mkuu
 
Ni vema kama kitu hujui uanze kuuliza na siyo judgemental statement
Kwa taarifa yako...IGP LAZIMA KILA SIKU ASUBUHI AHUDHURIE MORNING CALL YA KIKAO CHA BARAZA LA USALAMA LA TAIFA KINACHOONGOZWA NA RAIS..AKIWEMO MKUU WA MAJESHI...MKURUGENZI USALAMA WA TAIFA..NA WENGINE AMBAO SINA HAJA KUKUTAJIA
Kwa maana hiyo by any means usitegemee kama Rais wa nchi akihamia Dodoma wakuu wa majeshi na wakurugenzi wakuu wa ulinzi na usalama wabaki Dar....LAZIMA NA WAO WAWE PALE
Isitoshe....Kanda Maalumu Dar HAIJUMUISHI Headquarter ya Jeshi..Hizo hazihami na Ma RPC wa hizo Kanda wapo na Kamishna wa Kanda Maalumu wa Polisi ataendelea kuwepo

My take:pICHA AMBAYO NAIPATA HAPA TANZANIA KWA SASA NI KUWA UKIKOSOA NA KUPINGA KILA KITU KINACHOFANYWA NCHINI NDIPO UNAONEKANA UNA AKILI..LKN UKIUNGA MKONO KITU CHEMA UNAONEKANA HUNA MAANA!!!!!...Mhhh the attitude wa are now engaged in damage our destination. ..I stand to be corrected
Kwa hiyo raisi na mkuu Wa majeshi na hao wengine wote ukiowataja na ambao hujawataja wote wameshaenda Dodoma?au IGP atakuwa anakuja kila asubuhi Ku attend hiyo meeting?
 
Swali la kujiuliza ni hili: Tunapoteza nini tusipohamisha serikali kwenda Dodoma? Kama hakuna tunachopoteza kwa namna yeyote twende Dodoma. Kama kuna tukakachopoteza kwa namna ya fedha, uchumi, usumbufu kibiashara, usalama, na mahusiano yetu na balozi zetu zilizopo Dar na kadha wa kadha kheri tubaki Dar.

Kama lengo letu ni kusambaza maendeleo mikoani basi njia sio kuhamisha ofisi za serikali bali kupeleka viwanda na miundo mbinu itakayochochea shughuli za kiuchumi huko mikoani. Vile vile ni vyema tukajiuliza swali la msingi kabisa: je sababu zilizomshawishi Nyerere kutaka kuhamia Dodoma bado ni sababu za muhimu kwa hali iliyopo sasa? Kwa maana nyingine mazingira yaliyohitaji Dodoma kuwa makao makuu bado yapo hivyo hadi sasa ukitilia maanni uimara wa makao haya wa muda mrefu wa Dar? Sambamba na hilo, je sekta binafsi zilizojiimarisha kwa kuhudumia uwapo wa makao makuu Dar zitamudu na kuendelea na biashara hata baada ya makao kwenda Dodoma, au zitajiju?

Naichukia siasa kwasababu jukwaa ndilo linalofanya maamuzi na sio maamuzi yanayoshirikisha utafiti wa kitaalamu. Nashawishika kwamba kuamia Dodoma ni uamuzi wa jukwaani.
 
Back
Top Bottom