Uamuzi wa CHADEMA dhidi ya madiwani: "A Big Mistake!"

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Kitendo cha Kamati Kuu ya Chadema kuwavua uanachama madiwani wake wa Arusha, is "A Big Mistake"!, and there is a price to pay, so Chadema must pay very dearly and the price which is very high!.

Nimesoma ile taarifa ya maamuzi ya Kamati Kuu ya Chadema iliyoletwa humu jukwaani, na thread kadhaa kuhusu uamuzi huo, wengi wa wachangiaji wakiupongeza, hivyo nimeona nitoe maoni yangu, kuwa uamuzi huo is one of the "Big Mistakes*, Chadema had ever made!.

1. Ile sheria ya kulazimisha wawakilishi wa wananchi, lazima wadhaminiwe na vyama, its a bad law, na inakwenda kinyume cha Katiba ya JMT inayotoa uhuru kwa kila raia kushiriki katika uongozi wa serikali tangu ya mitaa hadi serikali kuu, hadi mahakama kuu ilishatoa rulling hicho kipengele kuwa ni 'unconstitutional' na kiwe struck out from the books of law!. Naamini Chadema hilo wanalifahamu, hivyo kitendo cha kutumia kipengele hicho hicho batili ambacho ni " a bad law", to its advantage, is "A Big Mistake!".

2. Ukishachaguliwa, Diwani au Mbunge, hata kama ulidhaminiwa na chama, wewe, unakuwa umechaguliwa na watu, wananchi, na unakuwa ni mtumishi wa watu na kule kwenye ngazi za maamuzi, Baraza la Madiwani na Bungeni, unawakilisha maslahi ya wananchi waliokuchagua ndio waliokutuma, na sio maslahi ya chama kilichokudhamini, japo katika uwakilishi wako, pia maslahi ya chama yatazingatiwa. Kitendo cha chama kuwafukuza wawakilishi halali wa wananchi kwa maslahi ya chama, is "A Big Mistake!".

3. Sisi ambao japo tuna vyama, lakini tuna shauku ya kuona Tanzania inaongozwa na chama mbadala, tumekuwa na imani kubwa sana na Chadema kama ndicho chama pekee ambacho kimeonyesha dalili kinaweza kuwa chama mbadala Kwa CCM ambacho kimethibitisha kikiaminiwa, kinaweza kuleta mabadiliko ya kweli. Hivyo tunategemea Chadema kitafanya maamuzi yanayofuata misingi ya haki. Kitendo cha kuwavua uanachama madiwani wake hawa, waliochaguliwa na wananchi, (sio chama) bila kuwasikiliza, ni kuwa "condem Unheard", which is against principles of Natural Justice, and this is a "A Big Mistake!".

4. Uzoefu wa siasa za Kanda ya Kaskazini, watu wanachagua watu na sio vyama, ndio maana CCM wanajua wazi kuwa, wao CCM, kuanzia Mwenyekiti wao, sekretariat yake, CC yao na NEC nzima ya CCM, hata wakapige kambi Moshi mjini, wakeshe kwa mwezi mzima, siku zote 30 mfululizo usiku na mchana huku wakipiga kampeni ya nguvu kwa kutumia mabilioni yao wanayofisidi, na kuwavisha Wanamoshi wote, zile T.Shirt na kofia, pamoja na kulisha pilau la nguvu siku zote 30, Ndesa hawatamng'oa!. Kitendo cha Chadema kuwavua uanachama watu wa watu mjini Arusha, it's "A Big Mistake!".

5. Wenzao CCM walipokuja na makelele ya kujivua gamba, nilisema CCM, kuanzia Mwenyekiti wao, na kelele zote za Nape na Chiligati, hawana ubavu wa kuwavua uanachama hao watuhumiwa wa ufisadi kwa kuhofia retaliation ya watu wao, ndio maana mtashuhudia kwenye kampeni za Igunga, CCM lazima impigie magoti RA. Amini nakuambia, hawawezi kuwafanya lolote EL na AC, sana sana watawabembeleza kujiudhuru nyadhifa zao, lakini sio kuwavua uanachama, kwanini Chadema, chama cha matumaini, kifanye makosa ambayo CCM iliyochokwa, haiwezi kuyafanya, ya kuwavua uanachama wachaguliwa wa wananchi?!. That is "A Big Mistake!".

6. Chama makini kama Chadema, is expected to do the right thing, at the right time. Hatua hii, ya kuwavua uanachama madiwani pendwa Arusha, hata kama it was the right step, imekuja at the wrong time!, wakati wakitafuta justification ya kulitwaa jimbo la Igunga, ndio chama kinaanzisha tifu kanda ya Kaskazini ambako ndiko kwenye mizizi yake, mimi sijui, Chadema, imeyafanya hayo kwa kutegemea nini?!.

7. Wakati nikiuleta ukosoaji huu, sio vibaya nikiwakumbusha Chadema baadhi ya maamuzi yake na matokeo yake. -Kumuengua Mwera Tarime, niliwaambia humu humu JF, kuwa it was a mistake, matokeo sote tunayajua!. Kususia kutangazwa kwa matokeo na kutomtambua rais, nilicoment humu humu, matokeo yake sote tunayajua, na jinsi Chadema ilivyonufaika na hatua hizo.

8. Niliwahi kuwapa Chadema, ushauri fulani, wapenzi na mashabiki wa Chadema, mlinibeza sana, including viongozi wenu. Mimi nikawasisitizia kuhusu, internal reforms na kujenga 'the winning coalition' including strategies kuelekea 2015, mpaka leo, bado sijaona, tuendelee kusubiri, 'the playing ground is not level, and never will it be, hivyo, 2015, tutaingia tena kwenye mechi ile ile, katika uwanja ule ule uwanja tenge, mazingira yale yale, halafu tutegemee matokeo tofauti?!.

9. Angalizo: Naomba kwenye kujadili mada muhimu zinazohusu maslahi ya taifa, nawaombeni sana tujadiliane kwa ustaarabu huku tukipingana kwa hoja na sio kuleta ushabiki wa vyama ama kupinga hoja kwa matusi, kejeli na matukano.

10. Nimetoa angalizo hilo makusudi, kwa vile nafahamu fika, kinachowapata wakosoaji wote wa Chadema humu kwenye forum hii, lakini kwenye kutoa honest opinion, lazima tuseme ukweli mchungu ambao utawacost Chadema Dearly!. Afadhali anayekukosoa kwa kukuambia ukweli, kuliko anayekusifia kwa kukudanganya ili hali anaelewa wazi mwishoni utaanguka na utaangamia!.

UPDATE.
Nime happen kukutana na mjumbe mmoja wa CC ya Chadema asubuhi hii, amenifafanulia A-Z ya kilichotokea. Chadema walifanya kila waliloweza ili kuwarudisha kwenye mstari lakini ilishindikana. Hao madiwani walizidi kuitunishia misuli CC ya Chadema, hivyo Chadema kama chama, was left with no option bali kuwatimua.

However, kwa vile Mhe. Lema ni major player on one side, na madiwani on the other, sasa na tusubiri jinsi CC ya Chadema, itakavyomshughulikia, na kwa vile yeye ni mjumbe wa CC hiyo ya Chadema, tutawaomba Chadema, wasilimalize suala lake ndani kwa ndani bila kutoa taarifa kwa umma, ili kupusha dhana ya double standards.

Sasa naanza kuwaelewa Chadema kidogo kidogo.

Wasalaam.

Pasco.

Pasco ni political comentator ambaye ni mwanachama wa chama cha siasa na sio Chadema, ila yuko objective bila kuegemea chama chake, bali mshabiki wa demokrasia ya kweli ndani ya vyama, na ndani ya Bunge. Comments zangu zina 'neutrality, objectivity, fairness na balance, bila kuendekeza ushabiki wa vyama, bali kutanguliza mbele maslahi ya taifa.
 
Suppose hawa madiwani wangekuwa wamekosa nidhamu kwa wananchi walio wachagua ambao ni wanachama wa chadema.

Je, wananchi wangetaka kuwawajibisha wangefanyaje, lazima wananchi wangepeleka malalamiko yao kwenye cc ya chadema ili cc wafanye disciplinary action

This is an obvious measure
 
suppose hawa madiwani wangekuwa wamekosa nidhamu kwa wananchi walio wachagua ambao ni wanachama wa chadema ..... je wananchi wangetaka kuwawajibisha wangefanyaje .... lazima wananchi wangepeleka malalamiko yao kwenye cc ya chadema ili cc wafanye disciplinary action ..... this is an obvious measure
Hili eneo jingine lenye udhafu katika viongozi wetu wa kuchaguliwa, mbunge au diwani akishachaguliwa, hakuna mechanisim ya kuwawajibisha hata wakiboronga vipi.

Hoja yangu ni wale viongozi ni wawakilishi wa wananchi hivyo walijiridhisha, wananchi wao wamechoka malumbano, hivyo wakakubali yaishe. Wametekelweza wananchi wao walichotaka.

Chadema kama chama, kimewakosea sana wananchi wa Arusha, kitakachofuatia uamuzi huu, wewe kisubirie!.
 
Chama chochote lazima kiwe na nidhamu tena ya hali ya juu vinginevyo chama hicho kitakuwa kinafanya usanii kama ilivyo sasa ndani ya CCM. Tatizo kubwa tunaloliona ndani ya CCM sasa hivi ni kukosekana kwa nidhamu kutokana na kutokuwepo anayeheshimiwa ndani ya chama hata zile taratibu zao za kuhakikisha kunakuwepo na nidhamu hazifuatwi kabisa.

Watu wanafanya madudu kila kukicha hawawajibishwi na hii ndio imefanya Watanzania wengi wakose na imani na chama hicho katika kila kona ya nchi yetu. Hongereni sana CHADEMA kwa maamuzi yenu mazito ili kudumisha nidhamu ya hali ya juu ndani ya chama.
 
Pasco nakuomba ukaoge ulale

Hata kama mtu amechaguliwa na wananchi kumbuka kwamba kwa siasa za bongo... chama kina nguvu kubwa sana ya ku-determine whether to go right or left... you can take alot of lessons from areas like bagamoyo, kigoma, tanga, kondoa, monduli etc


I like you alot but i think on this one... you better stick to what you do best and spend sometime dealing with your personal issues

usituletee mambo yako yale
 
Hili eneo jingine lenye udhafu katika viongozi wetu wa kuchaguliwa, mbunge au diwani akishachaguliwa, hakuna mechanisim ya kuwawajibisha hata wakiboronga vipi. Hoja yangu ni wale viongozi ni wawakilishi wa wananchi hivyo walijiridhisha, wananchi wao wamechoka malumbano, hivyo wakakubali yaishe. Wametekelweza wananchi wao walichotaka. Chadema kama chama, kimewakosea sana wananchi wa Arusha, kitakachofuatia uamuzi huu, wewe kisubirie!.

please substantiate your statement in red ....... otherwise admit that this is your own speculation
 
Chama chochote lazima kiwe na nidhamu tena ya hali ya juu vinginevyo chama hicho kitakuwa kinafanya usanii kama ilivyo sasa ndani ya CCM. Tatizo kubwa tunaloliona ndani ya CCM sasa hivi ni kukosekana kwa nidhamu kutokana na kutokuwepo anayeheshimiwa ndani ya chama hata zile taratibu zao za kuhakikisha kunakuwepo na nidhamu hazifuatwi kabisa. Watu wanafanya madudu kila kukicha hawawajibishwi na hii ndio imefanya Watanzania wengi wakose na imani na chama hicho katika kila kona ya nchi yetu. Hongereni sana CHADEMA kwa maamuzi yenu mazito ili kudumisha nidhamu ya hali ya juu ndani ya chama
BAK, Ushujaa ni pale chama kinapoamua kufanya maamuzi magumu, ila kitendo cha kufanya maamuzi, bila kujali the consequenses za maamuzi hayo, at the end of the day, maamuzi hayo yanakuja kugeuka liabilities.

Hawa madiwani ni watumishi wa wananchi na sio watumishi wa chama, kwa kawaida wakosaji hupewa barua za onyo, zikifuatiwa na karipio kali, na ndipo huadhibiwa. Mimi niliwasikia hao madiwani wakisema hawakupewa nafasi kujieleza. Japo uamuzi huu ni wa kishujaa na kwa sasa unapongezwa, kilio cha kusaga meno ndicho kinachofuatia!.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Pasco, Hata kama mtu amechaguliwa na wananchi kumbuka kwamba kwa siasa za bongo... chama kina nguvu kubwa sana ya ku-determine whether to go right or left... you can take alot of lessons from areas like bagamoyo, kigoma, tanga, kondoa, monduli etc
Udhamini wa chama kwa viongozi ni kinyume cha katiba, kiongozi akishachaguliwa ni kiongozi wa watu na sio kiongozi wa chama, ni mtumishi wa watu na sio mtumishi wa chama. Muafaka wa madiwani wale ni kwa maslahi ya wananchi wao na sio maslahi ya chama.

Wote mnaopongeza hatua hii kwa sasa, mtanielewa ninasema nini, pale yatakapoikuta Chadema, hayo ya kuikuta!.
 
please substantiate your statement in red ....... otherwise admit that this is your own speculation
LAT, nilifikiri unajua hao madiwani waliovuliwa uanachama, walifanya nini, sababu za kufanya walichokifanya pia naamini, unazijua, kama hukuwasikia wakisema wenyewe, then, better count it, my own speculations.
 
BAK, Ushujaa ni pale chama kinapoamua kufanya maamuzi magumu, ila kitendo cha kufanya maamuzi, bila kujali the consequenses za maamuzi hayo, at the end of the day, maamuzi hayo yanakuja kugeuka liabilities.

Hawa madiwani ni watumishi wa wananchi na sio watumishi wa chama, kwa kawaida wakosaji hupewa barua za onyo, zikifuatiwa na karipio kali, na ndipo huadhibiwa. Mimi niliwasikia hao madiwani wakisema hawakupewa nafasi kujieleza. Japo uamuzi huu ni wa kishujaa na kwa sasa unapongezwa, kilio cha kusaga meno ndicho kinachofuatia!.

Kwa maoni yangu hawa Madiwani walikuwa na muda wa kutosha kurekebisha kile walichokosea lakini hawakufanya hivyo hata wakafikia kutoa kauli hadharani za kukaidi kauli za Viongozi wao wa juu kutokana na sakata hili.

Hivyo hawahitaji kutafuta vijisababu visivyo na kichwa wala miguu ili kujitetea, wamevuna walichopanda.
 
Kwa kuwa ni uchambuzi poa.

Kwa baadhi yetu issue si hizo "speculations" ulizoandika. Kwetu baadhi yetu ni yale tunayoyamini kuwa ndiyo sera, mkakati na utekelezaji mbadala ndani ya mazingira yaliyopo.

1. Kumefanyika uchaguzi batili wa umeya ambao wahusika waliahadi kutafutia ufumbuzi baada ya kipindi fulani (Kabla ya 5/02). UFUMBUZI haukutolewa.

2. Maandamano halali kushinikiza UFUMBUZI yalitolewa taarifa toka Nov 2010 yalifanyika kwa amani; serikali iliua watu kwa kutumia nguvu nyingi, na kuwafungulia viongozi wa CDM kesi feki. Pinda kalidanganya Bunge.

3. Serikali imejikanyaga kutaka muafaka kwa milango ya nyuma. Wapuuzi (madiwani) wakadhani wemefikia muafaka.

4. Baada ya hatua (3) kuwasihi madiwani wahalifu wajirudi wamekaidi amri halali ya uongozi wa chama.

5. Chama kimewafukuza uanachama madiwani waasi. WEWE UNASEMA "A BIG MISTAKE"

By definition a mistake is made knowingly. Kwako wewe CDM wamefanya maamuzi mabaya kwa kujua na kufahamu. Ni contradiction ya maudui yako.

Kwa kuamini wanachokiamini wamefanya maamuzi kwa kujua na kufahamu wakiwa tayari kuingia gharama yo yote. Kama ulikuwa na premise nyingine kama madaraka na siyo chama kinachoamini unajifariji. MAAMUZI KAMA HAYO YANAHITAJIKA SI NA CDM TU BALI NA KILA INSTITUTION kwa kile wanachokiamini.
 
Hili eneo jingine lenye udhafu katika viongozi wetu wa kuchaguliwa, mbunge au diwani akishachaguliwa, hakuna mechanisim ya kuwawajibisha hata wakiboronga vipi. Hoja yangu ni wale viongozi ni wawakilishi wa wananchi hivyo walijiridhisha, wananchi wao wamechoka malumbano, hivyo wakakubali yaishe. Wametekelweza wananchi wao walichotaka. Chadema kama chama, kimewakosea sana wananchi wa Arusha, kitakachofuatia uamuzi huu, wewe kisubirie!.
Hapo kwenye highlight naomba nitofautiane na wewe kidogo. nadhani zipo taratibu za kuwashughulikia na njia mojawapo ni kama hii waliyoitumkia Chadema.
 
Udhamini wa chama kwa viongozi ni kinyume cha katiba, kiongozi akishachaguliwa ni kiongozi wa watu na sio kiongozi wa chama, ni mtumishi wa watu na sio mtumishi wa chama. Muafaka wa madiwani wale ni kwa maslahi ya wananchi wao na sio maslahi ya chama. Wote mnaopongeza hatua hii kwa sasa, mtanielewa ninasema nini, pale yatakapoikuta Chadema, hayo ya kuikuta!.

Narudia CDM inajua na kufahamu yatakayowakuta huna haja ya kuspeculate. Lengo la kuchukua maamuzi kwa sababu ya kutunza katiba ya chama na uongozi wake umefanyika sahihi come what may. MAISHA YANAENDELEA (Life goes on kwa msisitizo)
 
Kwa maoni yangu hawa Madiwani walikuwa na muda wa kutosha kurekebisha kila walichokosea lakini hawakufanya hivyo hata wakafikia kutoa kauli hadharani za kukaidi kauli za Viongozi wao wa juu kutokana na sakata hili. Hivyo hawahitaji kutafuta vijisababu visivyo na kichwa wala miguu ili kujitetea, wamevuna walichopanda.
BAK, natumaini umefuatilia sakata hili tangu mwanzo, nimesikiliza amri za chama na majibu yao. Madiwani hao walipinga amri halali za chama simply because hazikufuata principles of natural justice. Ile barua ya kuwalazimisha kujiuzulu nyadhifa zao, ilitolewa kwa maamuzi ya 'kiimla', na uamuzi wa kuwavua uanachama nao pia ni uamuzi wa kiimla.

Kama maamuzi magumu yenyewe ndio haya ya kiimla, watu wakitinga magogoni sio ndio watanyonga kabisa watu hadharani, ili liwe fundisho kwa wanaodharau maagizo, hata kama maagizo hayo sio halali?.
 
Narudia CDM inajua na kufahamu yatakayowakuta huna haja ya kuspeculate. Lengo la kuchukua maamuzi kwa sababu ya kutunza katiba ya chama na uongozi wake umefanyika sahihi come what may. MAISHA YANAENDELEA (Life goes on kwa msisitizo)
Mimibaba, Yes chama kina haki kuchukua maamuzi yoyote kwa mujibu wa katiba yake, kitu muhimu kwangu ni 'what for'?. I thought Chadema is party of the people, by the people and for the people!. Jee uamuzi huo wa Kamati Kuu ya Chadema is it for the people of Arusha or for the party?

Maamuzi yanayofanywa regardless of what come out may, ndiyo yatakuja kuicost zaidi Chadema, na what come out may, ni kuishia kulalamika na kulalama!. 2015 siyo mbali kihivyo!.
 
Hapo kwenye highlight naomba nitofautiane na wewe kidogo. nadhani zipo taratibu za kuwashughulikia na njia mojawapo ni kama hii waliyoitumkia Chadema.
Mpita Njia, nakubaliana na wewe, dhana ya diwani na mbunge kuwajibishwa na vyama, is wrong, CCM wanaliujua hilo, na Chadema pia wanalijua hilo, kitendo cha Chadema kukubali kuitumia wrong premise for its advantage, its a big mistake!.
 
BAK, natumaini umefuatilia sakata hili tangu mwanzo, nimesikiliza amri za chama na majibu yao. Madiwani hao walipinga amri halali za chama simply because hazikufuata principles of natural justice. Ile barua ya kuwalazimisha kujiuzulu nyadhifa zao, ilitolewa kwa maamuzi ya 'kiimla', na uamuzi wa kuwavua uanachama nao pia ni uamuzi wa kiimla. Kama maamuzi magumu yenyewe ndio haya ya kiimla, watu wakitinga magogoni sio ndio watanyonga kabisa watu hadharani, ili liwe fundisho kwa wanaodharau maagizo, hata kama maagizo hayo sio halali?.

Usitishe watu Mkuu, maamuzi haya yalistahili kabisa kufanywa ili kudumisha nidhamu ndani ya chama. Maamuzi haya hayaashirii kwamba CHADEMA kama watafanikiwa kuingia madarakani (hopefully 2015) basi wataanza kunyonga Watanzania hadharani. Sidhani kama CHADEMA wana mpango kama huo unaoufikiria wewe Mkuu.
 
Kwa kuwa ni uchambuzi poa.

Kwa baadhi yetu issue si hizo "speculations" ulizoandika. Kwetu baadhi yetu ni yale tunayoyamini kuwa ndiyo sera, mkakati na utekelezaji mbadala ndani ya mazingira yaliyopo.

1. Kumefanyika uchaguzi batili wa umeya ambao wahusika waliahadi kutafutia ufumbuzi baada ya kipindi fulani (Kabla ya 5/02). UFUMBUZI haukutolewa.
2. Maandamano halali kushinikiza UFUMBUZI yalitolewa taarifa toka Nov 2010 yalifanyika kwa amani; serikali iliua watu kwa kutumia nguvu nyingi, na kuwafungulia viongozi wa CDM kesi feki. Pinda kalidanganya Bunge.
3. Serikali imejikanyaga kutaka muafaka kwa milango ya nyuma. Wapuuzi (madiwani) wakadhani wemefikia muafaka.
4. Baada ya hatua (3) kuwasihi madiwani wahalifu wajirudi wamekaidi amri halali ya uongozi wa chama.
5. Chama kimewafukuza uanachama madiwani waasi. WEWE UNASEMA "A BIG MISTAKE"

By definition a mistake is made knowingly. Kwako wewe CDM wamefanya maamuzi mabaya kwa kujua na kufahamu. Ni contradiction ya maudui yako.

Kwa kuamini wanachokiamini wamefanya maamuzi kwa kujua na kufahamu wakiwa tayari kuingia gharama yo yote. Kama ulikuwa na premise nyingine kama madaraka na siyo chama kinachoamini unajifariji. MAAMUZI KAMA HAYO YANAHITAJIKA SI NA CDM TU BALI NA KILA INSTITUTION kwa kile wanachokiamini.
Mimi Baba, niliisikia kauli ya chama kuwataka wajirudi, na nilisikiliza kauli za madiwani hao, wakipinga msimamo wa chama kwa vile haukufuata taratibu. Kama maamuzi yenyewe ndio haya!, basi safari bado ni ndefu!.
 
Mimibaba, Yes chama kina haki kuchukua maamuzi yoyote kwa mujibu wa katiba yake, kitu muhimu kwangu ni 'what for'?. I thought Chadema is party of the people, by the people and for the people!. Jee uamuzi huo wa Kamati Kuu ya Chadema is it for the people of Arusha or for the party?. Maamuzi yanayofanywa regardless of what come out may, ndiyo yatakuja kuicost zaidi Chadema, na what come out may, ni kuishia kulalamika na kulalama!. 2015 siyo mbali kihivyo!.

Natumaini humaanishi CDM wanataka anything for free. THEY DONT and are ready for the outcome with respect
 
Back
Top Bottom