Uamuzi wa CHADEMA dhidi ya madiwani: "A Big Mistake!"

mkuu
chadema hawajui kabisa politics behind the door
wanahitaji kujifunza hilo somo
unamuona raila odinga,amefikaje hapo????
wangejifunza hawa watu....

wakati wa reagan,marekani waliwauzia silaha iran
unaweza shangaa hapo inakuwaje,wakati iran ndio adu wao mkubwa?
ni politics behind the door,na kuwa na strategy za mtazamo wa mbali

hivi tmesahau pia jinsi chadema walivyompoteza mwenyekiti wa bawacha....
hawajifunzi kabisa....

Kwamba chadema hawajui politics, hizi ni kauli za wanamagamba na washabiki wao.

chadema wameondoka wangapi na chama kinazidi kusonga mbele? unamzungumzia mwenyekiti wa bawacha wakati alishaondoka makamu mwenyekiti Dr. Kabouru lakini chama kimezidi kusonga mbele.

Hizo siasa mnazotaka chadema ifanye ni za huko huko mliko, wao wana siasa zao wenyewe, mtu akishindwa kujiheshimu kwa kiwango cha utovu wa nidhamu wa waliokuwa madiwani, hakuna namna ya kuwasaidia zaidi ya kuwavua uanachama. Ili watafute mahali pengine wanapoweza kufanya siasa bila kuheshimu viongozi wao wa juu.
 
Pasco naamini unatambua kwamba uamuzi wa kuwavua uanachama ulifikiwa na kamati kuu ambayo ina watu wa kutosha, makini kabisa na wasomi wazuri sana vile vile.

Haya mambo unayojaribu kuyaorodhesha hata wao waliyaona, wakayajadili na kupima consequences za uamuzi wao, and they knew that there should be a price to pay.

Suala la wananchi kunyimwa haki ya watu waliowachagua huwezi hata siku moja kuinyooshea kidole chadema, hiyo ndiyo sheria tuliyonayo na wengi tunakubaliana kwamba ni mbaya.

Sasa njia bora ya kubadilisha sheria mbaya ni kuwaona wahusika na najua unawafahamu. Hapa unachojaribu kufanya ni kulalalmikia matokeo ya sheria mbaya ambayo chadema wameikuta.

Na kwa kuzingatia kwamba hao madiwani walikuwa wanafahamu kwamba walidhaminiwa na chadema ili kuwania udiwani walipaswa kuzingatia maelekezo ya kamati kuu kwa kujua kwamba hao ndio wenye dhamana ya mwisho juu ya uendeshaji wa chama. Sasa kama walikaidi kwa bahati mbaya ama makusudi pamoja na kupewa muda wa kujirudi lakini wakakaidi, na walisikilizwa ingawa unajaribu kupindisha kwamba principle of natural justice haikufuatwa, kulikuwa hakuna uamuzi mwingine chama kingechukua zaidi ya huo uliochukuliwa.

Muhimu hapa ni aheri kuwa na jeshi dogo lenye nidhamu kuliko kuwa na lundo la wanajeshi wasiokuwa na nidhamu, hamuwezi kushinda vita yoyote.

Mwisho, nimeshangazwa na utabiri wako kwamba watakwenda mahakamani na watashinda, bila shaka unaelekea kuchukua mikoba ya marehemu sheikh yahya!!

Mkuu,

kwenye true democracy hiyo unayoita nidham ya jeshi hakuna
tazama marekani leo,wapo wabunge wanapinga mpaka miswada ya obama bungeni na ni wabunge wa chama cha democdrats

Sio kila atakae pinga maamuzi ya chama ahukumiwe kuwa msaliti
nini maana ya demokrasia sasa,
si tofauti ya mawazo na misimamo?
 
nilikuwa najua chadema watafanya hivi
wana hamu kubwa mno ya kuionesha jamii kwamba wao sio waoga wa kufanya maamuzi

hata kama yatawa cost ,hii inanikumbusha uchaguzi uliopita walivyopoteza jimbo la tarime

chadema sio wanasiasa kabisa,
mwanasiasa lazima ujue ku commpromise kwa maslahi yenu na chama

obama aliposhinda urais na chama chake kuwa na nguvu kubwa,
alikuwa na option ya kumuondoa joe lieberman kwenye kamati za congres
lakini ali compromise na kumuacha tu,licha ya joe lieberman kuungana na republicans kumponda obama wakati wa uchaguzi.....
chadema ni kama mtoto mdogo anaejaribu ku prove kuwa yeye ni mtu mzima
mwisho hufanya madudu tu mengi.....
ukiwa mtu mzima huitaji ku prove anything.....
itwacost mno hiiiii,mark my words

Naheshimu maoni yako yote, sikubliani nayo hata chembe. Sijui msimamo wako wa kisiasa. Kilichotokea ndizo siasa za Chadema, kama wewe ni mwanachama wa CDM ebu jitahidi kutumia forum za CDM kupenyeza mawazo yako hayo.

Ila kama nitakuwepo kujadili mawazo yako hayo nitakupinga kwa nguvu zote.
 
Mzee wa Rula, sehemu kubwa ya andiko langu ni opinion tuu backed by facts na trends, hivyo sio hisia.
Maadamu umeweka kipimo ni hizo chaguzi ndogo, tusubiri na tuone, time will tell.
Nakubaliana nawe kabisa Pasco usahihi wa maamuzi hayo ni suala la muda na si malumbano tena.

Nashukuru kwa mtazamo wako mzuri lakini kwa taarifa muafaka ule uliongiwa na wale madiwani wa CDM ulikuwa na mawaa kiasi hivyo kujenga sintofahamu nyingi. Kuhusu principle of natural justice ulisoyosema, mimi nadhani walipewa, ila ni ujeuri wao walijaribu kuonyesha kuwa hakuna jambo kubwa linaloweza kuwasibu zaidi ya kupewa onyo au karipio kali.

Binafsi naamini kabisa kuwa hakuna maamuzi yasiyokuwa na gharama kabisa hivyo ni tumaini langu katika hili ni lazima kutakuwa na gharama ikizingatiwa kuwa wale jamaa wanasiri kiasi za chama hivyo ni lazima watazitoa ili kukinukisha chama.
Mwisho time will tell.
 
Pasco naamini unatambua kwamba uamuzi wa kuwavua uanachama ulifikiwa na kamati kuu ambayo ina watu wa kutosha, makini kabisa na wasomi wazuri sana vile vile.

Haya mambo unayojaribu kuyaorodhesha hata wao waliyaona, wakayajadili na kupima consequences za uamuzi wao, and they knew that there should be a price to pay.

Suala la wananchi kunyimwa haki ya watu waliowachagua huwezi hata siku moja kuinyooshea kidole chadema, hiyo ndiyo sheria tuliyonayo na wengi tunakubaliana kwamba ni mbaya.

Sasa njia bora ya kubadilisha sheria mbaya ni kuwaona wahusika na najua unawafahamu. Hapa unachojaribu kufanya ni kulalalmikia matokeo ya sheria mbaya ambayo chadema wameikuta.

Na kwa kuzingatia kwamba hao madiwani walikuwa wanafahamu kwamba walidhaminiwa na chadema ili kuwania udiwani walipaswa kuzingatia maelekezo ya kamati kuu kwa kujua kwamba hao ndio wenye dhamana ya mwisho juu ya uendeshaji wa chama. Sasa kama walikaidi kwa bahati mbaya ama makusudi pamoja na kupewa muda wa kujirudi lakini wakakaidi, na walisikilizwa ingawa unajaribu kupindisha kwamba principle of natural justice haikufuatwa, kulikuwa hakuna uamuzi mwingine chama kingechukua zaidi ya huo uliochukuliwa.

Muhimu hapa ni aheri kuwa na jeshi dogo lenye nidhamu kuliko kuwa na lundo la wanajeshi wasiokuwa na nidhamu, hamuwezi kushinda vita yoyote.

Mwisho, nimeshangazwa na utabiri wako kwamba watakwenda mahakamani na watashinda, bila shaka unaelekea kuchukua mikoba ya marehemu sheikh yahya!!

Mwita Maranya, kwanza asante kwa kulitambua hili la sheria kandamizi.

Nakubaliana na wewe kuwa Chadema wameikuta hiyo sheria mbovu, nilichosema, ni kwa vile Chadema wanaijua hiyo ni sheria kandamizi, na inakwenda kinyume cha katiba ya JMT, mimi niliwategemea Chadema kuwa wao ni chama cha watendahaki, hivyo sikuwategemea kuitumia sheria hiyo kandamizi kuwakandamiza wananchi wa Arusha walioipa Chadema dhamana kubwa ile.

Nilitegemea Chadema kwa vile ina jeshi dogo kuliko mahasimu wao, basi fighting strategy yake, ingekuwa 'consolidation' of whatever little it has on its hands, kumbe its the other way around, ndio maana kuna mahali nimesema, "safari bado ni ndefu".
 
Mimibaba, Yes chama kina haki kuchukua maamuzi yoyote kwa mujibu wa katiba yake, kitu muhimu kwangu ni 'what for'?. I thought Chadema is party of the people, by the people and for the people!. Jee uamuzi huo wa Kamati Kuu ya Chadema is it for the people of Arusha or for the party?. Maamuzi yanayofanywa regardless of what come out may, ndiyo yatakuja kuicost zaidi Chadema, na what come out may, ni kuishia kulalamika na kulalama!. 2015 siyo mbali kihivyo!.

Pasco,itakapotokea kile unachokidhania kikawa sivyo (najua hofu yako ni CDM kupoteza viti vya udiwani),utakuja tena kutupa analysis tofauti na hii? Maana unaonekana kabisa ku underestimate the thinking capacity ya wana A-Town.
 
Kwamba chadema hawajui politics, hizi ni kauli za wanamagamba na washabiki wao.

chadema wameondoka wangapi na chama kinazidi kusonga mbele? unamzungumzia mwenyekiti wa bawacha wakati alishaondoka makamu mwenyekiti Dr. Kabouru lakini chama kimezidi kusonga mbele.

Hizo siasa mnazotaka chadema ifanye ni za huko huko mliko, wao wana siasa zao wenyewe, mtu akishindwa kujiheshimu kwa kiwango cha utovu wa nidhamu wa waliokuwa madiwani, hakuna namna ya kuwasaidia zaidi ya kuwavua uanachama. Ili watafute mahali pengine wanapoweza kufanya siasa bila kuheshimu viongozi wao wa juu.

kama wote walioondoka walienda ccm
ungekuwa na pointi but wote tunajua
kafulila na yule mwenyekiti wa bawacha wameenda wapi na wenye akili wanaona hasara ambayo chadema wamepata
 
Pasco,itakapotokea kile unachokidhania kikawa sivyo (najua hofu yako ni CDM kupoteza viti vya udiwani),utakuja tena kutupa analysis tofauti na hii? Maana unaonekana kabisa ku underestimate the thinking capacity ya wana A-Town.

wewe unazungumza nini??????
tarime ipo wapi now??????
 
Mwita Maranya, kwanza asante kwa kulitambua hili la sheria kandamizi. Nakubaliana na wewe kuwa Chadema wameikuta hiyo sheria mbovu, nilichosema, ni kwa vile Chadema wanaijua hiyo ni sheria kandamizi, na inakwenda kinyume cha katiba ya JMT, mimi niliwategemea Chadema kuwa wao ni chama cha watendahaki, hivyo sikuwategemea kuitumia sheria hiyo kandamizi kuwakandamiza wananchi wa Arusha walioipa Chadema dhamana kubwa ile. Nilitegemea Chadema kwa vile ina jeshi dogo kuliko mahasimu wao, basi fighting strategy yake, ingekuwa 'consolidation' of whatever little it has on its hands, kumbe its the other way around, ndio maana kuna mahali nimesema, "safari bado ni ndefu".

Sheria hiyo kandamiziambayo hata mimi siiungi mkono inawanyima wananchi haki ya kuendelea kupata huduma ya mwakilishi wao waliyemchagua, sheria hiyo haiwaelekezi madiwani kutotii maamuzi yaliyotolewa na viongozi wao wa chama, nadhani uchore mstari kati ya hivyo viwili.

Najaribu kutaka kuelewa pendekezo lako ni lipi kwa hali kama hii iliyotokea kwa madiwani kukaidi maelekezo ya kamati kuu. Labda kwa ufupi tu,unaweza kuniambia wewe kwa mtazamo wako kamati kuu ya chadema ilipaswa kutoa uamuzi gani?
 
Udhamini wa chama kwa viongozi ni kinyume cha katiba, kiongozi akishachaguliwa ni kiongozi wa watu na sio kiongozi wa chama, ni mtumishi wa watu na sio mtumishi wa chama. Muafaka wa madiwani wale ni kwa maslahi ya wananchi wao na sio maslahi ya chama. Wote mnaopongeza hatua hii kwa sasa, mtanielewa ninasema nini, pale yatakapoikuta Chadema, hayo ya kuikuta!.

Ok, sijui utanisaidiaje suala la collective responsibilities, sera za chama na kama wamekiuka katiba sijui pia utanielimishaje kuhusu kutekeleza ilani ya chama chako badala ya ilani ya wananchi

kumbuka kila chama kina misingi yake na pale inapogeukwa tena bila nidhamu lazima hili lifanyike

do you want to justify kwamba as long as walichagulia basi wabaki tu hata kama hawawakilishi chama kilichowasimamia??

YOUR ARGUMENTS WOULD HOLD WATER KAMA TUNGEKUA NA WAGOMBEA BINAFSI

anyway ngoja tujifunze zaidi
 
wewe unazungumza nini??????
tarime ipo wapi now??????

Kwani wewe unazungumza nini?? Tarime iko mkoani Mara, au una taarifa za kuhamia mkoa mwingine? Tarime na arusha ni maeneo mawili tofauti, siasa za tarime na arusha huwezi kuzifananisha.

Halafu usipende kutanguliza hisia kuliko ukweli halisi. Usisahau kwamba mwera alihama kwenda cuf kutokana na hali iliyojitokeza wakati wa mchakato wa kura za maoni na hakufukuzwa na kwahiyo aliondoka na watu wake wengi plus hujuma kadhaa alizofanya baada ya kugundua kwamba nafasi yake ya ushindi ni finyu. Hawa madiwani wamekaidi maamuzi ya viongozi wa juu wa chadema na wananchi wengi hususan wanachama na wapenzi wa chadema wanaunga mkono uamuzi huo.

Mazingira ya uchaguzi wa ubunge tarime 2010 na haya ya madiwani arusha ni tofauti sana, na hata hivyo chadema wameamua ni bora kuwa na madiwani wachache wenye kuheshimu mamalaka za chama kuliko kundi kubwa la watu wasio na nidhamu wala heshima kwa viongozi wao.
 
Kwa nini povu likutoke kaka/dada? Hebu vuta subira,tusubiri uchaguzi mdogo ndio mje na analysis zenu,otherwise naona kama mnajaribu kupaka upepo rangi.

wewe unazungumza siasa za kitoto
kuna jimbo chadema walikuwa na nguvu kama tarime?
walipogawanyika tu,wakapoteza....
kuwa na heshima,umeona avatar inakupa jinsia
 
Pasco naamini unatambua kwamba uamuzi wa kuwavua uanachama ulifikiwa na kamati kuu ambayo ina watu wa kutosha, makini kabisa na wasomi wazuri sana vile vile.

Mwisho, nimeshangazwa na utabiri wako kwamba watakwenda mahakamani na watashinda, bila shaka unaelekea kuchukua mikoba ya marehemu sheikh yahya!!
Mwita Maranya, hili la kushinda, sio utabiri wa Sheikh Yahya, bali nilibahatika kufuta Tongotongo la tasnia ya sheria. Ingekuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa sheria wanaruhusiwa kuwa ma advocate, then, kesi ya madiwani hawa ingefunguliwa na kutetewa na advocate mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa sheria, na kushinda right away.

Kwa kumbukumbu zangu za darasa la sheria, siku ya kwanza, somo la kwanza, ukurusa wa kwanza ni What is law, ikifuatiwa na principles of natural, principle kuu ya kwanza ni
  1. No man shall be condemned unheard.
ya Hivyo kitendo tuu cha jamaa kutuhumiwa na kuhukumiwa bila kusikizwa, kunatosha kuifanya mahakama kutengua uamuzi wa CC ya Chadema.
 
mkuu
chadema hawajui kabisa politics behind the door
wanahitaji kujifunza hilo somo
unamuona raila odinga,amefikaje hapo????
wangejifunza hawa watu....

wakati wa reagan,marekani waliwauzia silaha iran
unaweza shangaa hapo inakuwaje,wakati iran ndio adu wao mkubwa?
ni politics behind the door,na kuwa na strategy za mtazamo wa mbali

hivi tmesahau pia jinsi chadema walivyompoteza mwenyekiti wa bawacha....
hawajifunzi kabisa....

bOSS,

YOU PICKED A VERY WRONG EXAMPLE... RAILA NI JAMBAZI, NA KWA MTIZAMO WA CCM, YULE JAMAA KAMA NI BONGO WANGESHAMUUA TENA KABLA HAJAFIKISHA HATA MIAKA 45

GIVE US ANOTHER EXAMPLE
 
wewe unazungumza siasa za kitoto
kuna jimbo chadema walikuwa na nguvu kama tarime?
walipogawanyika tu,wakapoteza....
kuwa na heshima,umeona avatar inakupa jinsia

Kwa hiyo Tarime ni Arusha siku hizi? Si mleta maada kasema wazi kuwa siasa za kaskazini ni tofauti kabisa na maeneo mengine? Iweje wewe ulete mfano wa Tarime kwa siasa za Arusha?
 
kama wote walioondoka walienda ccm
ungekuwa na pointi
but wote tunajua
kafulila.na yule mwenyekiti wa bawacha wameenda wapi
na wenye akili wanaona hasara ambayo chadema wamepata

Hivi wewe unaongea vitu gani hivi vya kuchekesha.

Suala si kwamba walienda magamba ama wapi, suala ni kwamba waliondoka na chadema haikutetereka.

Yani chadema kutoka kuwa na wabunge wa kuchaguliwa watano hadi 23 ndio wewe unaona ni hasara?? basi kama nyongeza ya wabunge ni 18 ni hasara basi mwalimu wangu wa hisabati kibeyo p/s alikuwa hajui kitu!!

Nadhani kimsingi wengi mnaopingana na chadema kwa uamuzi huu hamkuzoea maamuzi kama haya, mmezoea kupeana siku tisini kisha mkaongezeana siku baadae mnapotezea. Sasa chadema imefanya uamuzi ambao unawasuta sana wanamagamba na hii ni turufu kubwa sana ya chadema kisiasa dhidi ya magamba.
 
Mwita Maranya, hili la kushinda, sio utabiri wa Sheikh Yahya, bali nilibahatika kufuta Tongotongo la tasnia ya sheria. Ingekuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa sheria wanaruhusiwa kuwa ma advocate, then, kesi ya madiwani hawa ingefunguliwa na kutetewa na advocate mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa sheria, na kushinda right away.

Kwa kumbukumbu zangu za darasa la sheria, siku ya kwanza, somo la kwanza, ukurusa wa kwanza ni What is law, ikifuatiwa na principles of natural, principle kuu ya kwanza ni
  1. No man shall be condemned unheard.
ya Hivyo kitendo tuu cha jamaa kutuhumiwa na kuhukumiwa bila kusikizwa, kunatosha kuifanya mahakama kutengua uamuzi wa CC ya Chadema.

Hapo nilipobold,kwa hiyo Mahakama itaiamuru CC iwarudishie uanachama? Na kwa nini mpaka waende mahakamani kupinga wakati umesema siasa za kaskazini watu wanachagua mtu na si chama? Kwa nini wasihamie tu chama kingine na kugombea kupitia huko?
 
Sikushangai mkuu najua huu msimamo wa cdm ni mgeni kwako, but kumbuka kila jumuiya au taasisi lazima ziwepo taratibu za kufuatwa, huwezi kwenda nje ya utaratibu halafu ukasema kuwa bado ni mwanajumuiya hata baada ya kushauriwa kubadilika. So Utazoea tu!
 
Mwita Maranya, hili la kushinda, sio utabiri wa Sheikh Yahya, bali nilibahatika kufuta Tongotongo la tasnia ya sheria. Ingekuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa sheria wanaruhusiwa kuwa ma advocate, then, kesi ya madiwani hawa ingefunguliwa na kutetewa na advocate mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa sheria, na kushinda right away.

Kwa kumbukumbu zangu za darasa la sheria, siku ya kwanza, somo la kwanza, ukurusa wa kwanza ni What is law, ikifuatiwa na principles of natural, principle kuu ya kwanza ni
  1. No man shall be condemned unheard.
ya Hivyo kitendo tuu cha jamaa kutuhumiwa na kuhukumiwa bila kusikizwa, kunatosha kuifanya mahakama kutengua uamuzi wa CC ya Chadema.

Pasco kama unasomea sheria na uko ndani ya nchi hii hii lakini hujafanya jitihada za kujua ni kwa kiasi gani hao jamaa walipewa nafasi namuda wa kusikilizwa, basi nina shaka kwamba unaweza kuhitimu na kupata cheti cha sheria lakini isikusaidie sana wewe binafsi na taifa kwa ujumla wake.

Kamati ya marando ilikwenda arusha na ikawasikiliza madiwani wote wa arusha, na bado jana kabla ya kufikiwa uamuzi huumadiwani wakaidi waliitwa dodoma na kupewa nafasi nyingine tena ya kusikilizwa.

Sasa unaposema hiyo principle of natural justice haikuzingatiwa basi hapo ndo napata mashaka na uelewa wako wa hiyo principle of natural justice.
 
Back
Top Bottom