U.S. warns Iran on Strait of Hormuz

umetukata..unafikiri wote sisi ni watoto?mimi nina rafiki zangu ni wa kurds..wanaipenda marekani kama nini kwa sababu iliwatoa kwenye mikono ya dikteta sadam hussein..unajua watu wangapi wanateseka nchini Iran?

Unajua watu wangapi wanateseka Tanzania? Tuiite Marekani?
Some arguments are hillarious!
 
Mchezo mgumu ni jinsi gani Iran atasukuma kete zake,ila Iran hana ubavu ,na kama anajua hivyo yanini kujiigiza kwenye matatizo zaidi,anajua kwamba haugwi mkono na mataifa ya kiarabu.mwisho wa siku ni wananchi wanaoteseka bila kosa lolote.
 
Haki za wapalestina ni zipi!!?

Hakuna vita ya III kwa wakati huu. Soma tena na tena uone ishara za World war III. Ni kutajie tu moja, all the nations of the world yatakapokuwa against Israel. bado USA inasupport Israel.

Wapalestina hawana haki? Unaishi wapi wewe? Hebu mwulize Membe.
Kwa kifupi, Azimio la Umoja wa Mataifa 242 linasema: Israel inabidi kuondoka katika maeneo yote iliyoyateka mwaka 1967.
Jee unapinga Umoja wa Mataifa (UN)? Kama si Umoja wa Mataifa pasingekuwepo Israel, kwa sababu ni UN ndiyo iliyotoa uamuzi wa kugawa Palestina, nusu ya Wayahudi na Nusu ya Waarabu mwaka 1947.
Huwezi kukubali uamuzi huo, ukakataaa huu (unless, tena, UDINI). Hata huo UDINI nishazungumza hapa kuwa usi confuse Wayahudi na Ukristo. Infact, Uislamu uko karibu zaidi na Ukristo kuliko Uyahudi na Ukristo. At least, Waislamu wanamkubali Yesu, Wayahudi hawakubali haata kama alizaliwa na wanamwita bi Maria (m) ...shakum......
Zaidi ya hayo, maeneo yote matakatifu ya Wakristo huko Palestina, ukitoa Jerusalem, Myahudi kaishawarudishia Wapalestina, kuonesha kuwa hataki kujihusisha na Ukristo. Maeneo kama Bethlehem, Nazaret nk. Kuna Wakristo wengi zaidi katika maeneo waliyonayo Wapalestina hivi sasa kuliko katika maeneo ya Wayahudi.
Na kama watetea Israel kwa misingi hiyo, hebu nenda leo Tel Aviv na Biblia yako uhubiri wazi kwa Waisrael uone kitu gani kitakufika! Baadhi ya mambo kwa kweli ni ujinga. Pana haja ya kusafiri!
 
Vyovyote itakavyokuwa, kama Iran inamatamanio ya kutengeneza silaha za nyuklia, basi asiruhusiwe. Huwezi kumruhusu kichaa akawa na silaha kama hizo. Kama hana matamanio wamuache!!!!!

Mkuu
Kichaa pekee ambaye amemiliki na kuzitumia silaha za nyuklia ni US. Au wewe una ushahidi mwengine?
 
Natumaini unaandika hivi kutokana na intellectual analysis na si kwa kufuata mkumbo tu au (kama ninavyodhania) kwa udini. Ukichaa wa Iran uko wapi? Hebu niambie, tangu babu yako alipozaliwa hadi leo umesikia/kuambiwa au kusoma kuwa Iran imeishambulia nchi yoyote? Hao wasio vichaa, wameshambulia nchi ngapi katika miaka 10 tu iliyopita?
Acha kufuata ushabiki tu, soma.

wengi wamepoteza ndugu na jamaa kwa kuruhusu waishi kawaida na vichaa,swala la kutaka kuifuta inchi nyingine kwenye ramani ya dunia wewe ni la umma wenye akili timamu ?
 
Wapalestina hawana haki? Unaishi wapi wewe? Hebu mwulize Memba.
Kwa kifupi, Azimio la Umoja wa Mataifa 242 linasema: Israel inabidi kuondoka katika maeneo yote iliyoyateka mwaka 1967.
Jee unapinga Umoja wa Mataifa (UN)? Kama si Umoja wa Mataifa pasingekuwepo Israel, kwa sababu ni UN ndiyo iliyotoa uamuzi wa kugawa Palestina, nusu ya Wayahudi na Nusu ya Waarabu mwaka 1947.
Huwezi kukubali uamuzi huo, ukakataaa huu (unless, tena, UDINI). Hata huo UDINI nishazungumza hapa kuwa usi confuse Wayahudi na Ukristo. Infact, Uislamu uko karibu zaidi na Uyahudi kuliko Ukristo.
Na kama watetea Israel kwa misingi hiyo, hebu nenda leo Tel Aviv na Biblia yako uhubiri wazi kwa Waisrael uone kitu gani kitakufika! Baadhi ya mambo kwa kweli ni ujinga. Pana haja ya kusafiri!

Mmmh hoja zinazotawaliwa na mapenzi zinakuwa na matatizo sana,hivi dunia hii ni wapalestina pekee ndiyo wanadhulumiwa haki zao ? Vipi wakurd ? Vipi watu wa sahara magharibi ? etc,lakini ni kwanini dunia nzima imewapa mgongo wengine wenye shida kubwa kuliko hata wapalestina na kushupalia palestina ambayo kimsingi hakuna matatizo kwani wapalestina matatizo yao kwa kiasi kikubwa ni ya kujitakia.
 
Iran inasema imefanya jaribio la kurusha kombora la masafa ya wastani.

Jaribio hilo lilifanywa wakati wa mazoezi ya jeshi karibu na Hormuz, mlango unaounganisha Ghuba na Bahari ya Hindi.
Jeshi la wanamaji la Iran linasema siku ya mwisho ya mazoezi Jumatatu, meli zitaweza kupita kwenye njia ya Hormuz, ikiwa tu jeshi hilo litaziruhusu.

Mkondo wa Hormuz ni njia inayopitwa na meli nyingi zinazobeba mafuta, na Iran inatishia kuifunga endapo itawekewa vikwazo zaidi.
 
wengi wamepoteza ndugu na jamaa kwa kuruhusu waishi kawaida na vichaa,swala la kutaka kuifuta inchi nyingine kwenye ramani ya dunia wewe ni la umma wenye akili timamu ?
Ah, sasa nimejua source (rubaa) ya habari zako.....
Nani kasema ataka kuifuta nchi kwenye ramani? Mimi najua kugha ya Kiajemi, hebu niletee ibara ya Amedinidjad iliyosema hivyo.
Hebu tuchukulie tu kuwa ni kweli , tangu lini neon la rais likahukumiwa kwa taifa zima kama unavyosema? Jee, matamshi ya JK ndiyo ya Watanzania wote?
Ukijadili na watu wanaojua, lazima ufanye utafiti, siyo kurudia habari za kuambiwa!
 
Heri na fanaka ya Mwaka Mpya JF.
Mwaka 2012 umeanza kwa ishara mbaya kwa wale wanofuatia masuala ya matangamano ya Kimataifa. Ndiyo kwanza rais Barack Obama amesaini kuwekewa vikwazo benki kuu ya Iran, eti kwa sababu nchi hiyo 'ina matamanio' ya kuunda silaha za nuklia. Nimeweka neno 'matamanio' (ambitions) ndani ya vibango kwa kusisitiza kuwa hadi sasa hakuna dalili yeyote kama Iran ina maatamanio hayo. Iran yenyewe inasema haina.
Lakini, hata kama inayo, so what? Kwa nini vikwazo hivyo haviwekewi wengine, ambao wanazo hasa?
Kama asemavyo Ron Paul 'ukianza mkondo wa vikwazo hatimaye utaishia vita' Hii ndivyo ilivyotokea kwa nchi zote- Iraq, Argentine,Libya.....

(Nchi pekee ambayo vikwazo havijapelekea vita ni Cuba- lakini hii ni special case- kwani Marekani ilipatana na Soviet ya wakati ule kuwa isiiguse Cuba na Soviet haitaigusa Uturuki).

Kwa mujibu wa wachunguzi wengi, vita dhidi ya Iran vitatokea kabla ya mwezi Machi mwaka huu, kutokana na sababu nyingi ambazo uki google utaelewa. Wengine watasema, matishio mengi ya namna hii yamekwishatolewa tangu 2005. Nasema safari hii ni tofauti, hasa Syria ikianguka katika miezi miwili ijayo.
Kwa wale wasio na naamna nyingine ya kupata habari za uhakika, uhasimu wa Marekani na Iran una sababu mbili muhimu

1- Iran kuwa msitari wa mbele wa kutetea haki za WaPalestine kwa vitendo (siyo kama Saudi Arabia na Waarabu wengine)

2- Hofu ya kuwa mfano wa Iran wa kujitegemea wenyewe utaigwa na madola mengine ya Mashariki Ya Kati, na hivyo kuathiri udhibiti wa Marekani wa eneo hili.

3- Kuwepo taifa lililo sawa kwa nguvu za kijeshi na Israel katika Mashariki ya Kati

Utaona kwamba suala la nuklia ni kisingizio tu. Kama unaona habari hizi hazikuhusu, fikiria tena. Iran siyo a 'push over' kama Iraq. Wairan- usi wa confuse na Waarabu- ni watu wenye ari kubwa ya kupigania nchi yao. Mfano ni katika vita vya Iran Iraq. Iraq ilikuwa inasaidiwa na nchi zote kubwa kwa silaha, na Waarabu kwa fedha. Iran ilikuwa pekee ikiwa na vikwazo vya silaha. Lakini ikaweza kumshinda Saddam na lau si kujiingiza Marekani dhahiri wangefika Baghdad, a la Tanzania!

Ninachotaka kusema ni kuwa itakapotokea vita, amini kuwa visima vyote vwa mafuta Mashariki ya Kati vitachomwa moto, na Israeli itashambuliwa kwa maelfu ya makombora- Israel itajibu kwa silaha za nuklia......

vita ya III ya dunia imeanza!

Lakini Israel hailindwai na Marekani ujue, ila inalindwa na Mungu Yehova-Shalom!
 
hapa kazi inaanza taratibu....
Movie litaanza in a very near future.
 
Mmmh hoja zinazotawaliwa na mapenzi zinakuwa na matatizo sana,hivi dunia hii ni wapalestina pekee ndiyo wanadhulumiwa haki zao ? Vipi wakurd ? Vipi watu wa sahara magharibi ? etc,lakini ni kwanini dunia nzima imewapa mgongo wengine wenye shida kubwa kuliko hata wapalestina na kushupalia palestina ambayo kimsingi hakuna matatizo kwani wapalestina matatizo yao kwa kiasi kikubwa ni ya kujitakia.

Kwa kifupi, si mapenzi au kusahau matatizo ya wengine. Hayo matatizo mawili uliyoyataja pia yanafuatiliwa na wapenda hakii duniani. Utafahamu kuwa hayo yamekuja baadaye katika international affairs kuliko hili. Pili hili la Palestina linahatarisha amani ya dunia. Hakuna amani ya dunia inayohatarishwa na matatizo uliyoyataja.
Kinachotia wasi wasi ni kuwa 'hutambui' haki za Wapalestina, kama unavyosema, matatizo ya kujitakia wenyewe. Kweli wewe ni mpenda haki? Unaonaje mtu akija nyumbani kwako akamchukua mkeo na watoto wako na kuwafukuzilia mbali na akaleta familia yake, utakubali?
Kuna Wapalestina milioni 3 walifukuzwa nyumbani kwao tangu 1948 wakati dola la Israel lilipozaliwa, na sasa wanaishi katika mahema ya wakimbizi Lebanon na Syria baada ya ardhi na nyumba zao kuhodhiwa na Wayahudi ambao hata hawakuzaliwa Palestina, wameletwa kutoka Russia, Poland na sehemu nyingine?
Utasema nini ikiwa Wajerumani waliokuwa Tanzania miaka 1900 leo watoto wao warudi na waseme wana haki ya Wilaya ya Usambara kwa vile babu zao waliishi huko miaka 100 iliyopita utakubali? Hukubali. Na hii ni miaaka 100 tu iliyopita. Wayahudi wanasema wana haki ya Palestina kwa vile babu zao waliishi huko miaka 2000 iliyopita!
Lazima ufahamu, kuna Wayahudi wa Mashariki ambao walibakia Palestina mika yote hii, hawa Waarabu hawana matatizo nao. Wenye matatizo ni Wayahudi wa Magharibi ( Ashkenazi) ambao walikuwa raia wa mataifa mengine kwa miaka maelfu na maelfu na leo wanarudi kudai Palestina.
Nadhani hii kwa muhtasari imekupa maelezo ya tatizo hili.
 
Wapalestina hawana haki? Unaishi wapi wewe? Hebu mwulize Membe.
Kwa kifupi, Azimio la Umoja wa Mataifa 242 linasema: Israel inabidi kuondoka katika maeneo yote iliyoyateka mwaka 1967.
Jee unapinga Umoja wa Mataifa (UN)? Kama si Umoja wa Mataifa pasingekuwepo Israel, kwa sababu ni UN ndiyo iliyotoa uamuzi wa kugawa Palestina, nusu ya Wayahudi na Nusu ya Waarabu mwaka 1947.
Huwezi kukubali uamuzi huo, ukakataaa huu (unless, tena, UDINI). Hata huo UDINI nishazungumza hapa kuwa usi confuse Wayahudi na Ukristo. Infact, Uislamu uko karibu zaidi na Uyahudi kuliko Ukristo.
Na kama watetea Israel kwa misingi hiyo, hebu nenda leo Tel Aviv na Biblia yako uhubiri wazi kwa Waisrael uone kitu gani kitakufika! Baadhi ya mambo kwa kweli ni ujinga. Pana haja ya kusafiri!

Kama udini (at least kwa mantiki ya Kitanzania) ina maana ya Ukristo dhidi ya uislamu then Israel si wakristo
 
Natumaini unaandika hivi kutokana na intellectual analysis na si kwa kufuata mkumbo tu au (kama ninavyodhania) kwa udini. Ukichaa wa Iran uko wapi? Hebu niambie, tangu babu yako alipozaliwa hadi leo umesikia/kuambiwa au kusoma kuwa Iran imeishambulia nchi yoyote? Hao wasio vichaa, wameshambulia nchi ngapi katika miaka 10 tu iliyopita?
Acha kufuata ushabiki tu, soma.

Unajipotezea muda tuu mkuu. Washabiki wa OBama wapo wengi humu ndani. Huwezi kuwaeleza kitu negative kuhusu Obama wakakuelewa.
 
Ah, sasa nimejua source (rubaa) ya habari zako.....
Nani kasema ataka kuifuta nchi kwenye ramani? Mimi najua kugha ya Kiajemi, hebu niletee ibara ya Amedinidjad iliyosema hivyo.
Hebu tuchukulie tu kuwa ni kweli , tangu lini neon la rais likahukumiwa kwa taifa zima kama unavyosema? Jee, matamshi ya JK ndiyo ya Watanzania wote?
Ukijadili na watu wanaojua,lazima ufanye utafiti, siyo kurudia habari za kuambiwa!

Unajua mkuu tofauti yako na huyo jamaa ni kubwa mno,its a waste of time trying to be rational to him, u will put logic into ur arguments but he/she will bring religius driven motives,dont abuse ur intelect trying to have a sensible dialogue with him.U just have to choose wether to play ignorant as he does or just let him go coz i assure u its not worth it.
 
Asante kwa ushauri huu. Wajua Waarabu wana msemo wao kwamba wajinga wako aina mbili. 'Jahl basiit na Jahl Murakkab' (kwa tafsiri ya haraka :yuko mjinga hafifu na mjinga mgando).
Mjinga hafifu ni mtu ambaye hajui na aanajua kuwa hajui- huyu anaweza kupatiwa dawa. Na ndio maana nikajitahidi hapa.
Ama mjinga mgando, huyu ni mtu ambaye hajui na hajijui kuwa hajui - huyu, kama ndugu yetu ni katika kundi hilo, Mungu awe na huruma naye, hana dawa!
 
Back
Top Bottom