Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,744
Huwa napenda sana kutazama TV zetu hizi za hapa nchini .ITV,EATV mTBC lakini sasa naona zinazidisha matatizo kichwani.
SHida na matatizo yaliyo nchini unahisi ukiangalia Tv labda yatatulia kutokana na vipindi mbalimbali vya kufurahisha ,kinachosikitisha na kunihuzunisha ni vipindi hivi kuwa vimekalia fujofujo ,kwa maana hakuna unachokisikia kwa makini ,utaona unatazama mchezo au kipindi halafu kuna mziki nyuma yake, mziki na maneno ya kipindi hujenga fujo na kukuchanganya na kujiona hujui unasikiliza kitu gani.
Kama humu mna watu ambao ni watazamaji wazuri wa Tv bila ya shaka yeyote ile mtaweza kuliona jambo hili ,yaani unakuta kipindi ni kizuri tu ,na unatamani kusikia wanayozungumza washiriki ,lakini mziki ulionyuma au tuseme mziki unaochomekewa huwa unavuluga kila kitu ,hakuna kinachosikilikana ni fujo tupu ,hujui uzidishe sauti au upunguze.
Ningependelea wahusika kama mnasoma hapa JF basi muangalie vipindi vya wengine au TV za wengine muone ,kama mna habari za mitaani basi ziwe habari tu na sio na muziki juu yake ,kama ni igizo basi zisikike sauti za waigizaji pekee zisizo ingiliana na muziki unaovuka sauti za waigizaji au usiwepo mziki kabisa.
Hivi sasa kuna kipindi EATV ,aloo kuna mziki unaharibu kipindi kizima na ni ovyo kabisa ,yaani huwezi kuzidisha, sauti inakuwa ni balaa. sijui wanafikiaria watu wako baa.