TV 15 zaibwa hospitalini Njombe. Mkuu wa mkoa azunguka mitaani kuzisaka

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,126
4,169
20231126_203312.jpg

=======
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amemuelekeza Katibu Tawala wa Mkoa huo kuwasimamisha kazi baadhi ya Watumishi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe akiwemo Katibu wa Afya, Watu wa Idara ya manunuzi pamoja na Idara ya TEHAMA ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za wizi wa TV 15 pamoja na kompyuta tatu katika Hospitali hiyo.

Mtaka ametoa maagizo hayo mara baada ya kushtukiza katika Hospitali hiyo baada ya kupata taarifa ya upotevu wa vifaa hivyo vilivyopotea miezi mitano iliyopita huku akimtaka Afisa manunuzi wa Hospitali hiyo Aloyce Kavumika kulipa takribani shilingi milioni.11 kwa ajili ya kununua TV 15 zilizoibwa.

Awali Afisa manunuzi akitoa taarifa ya wizi huo alisema alipata taarifa ya wizi wa TV July 08,2023 akiwa nje ya ofisi ambapo baada ya kurejea ofisini hapo alilazimika kukaa na Watumishi wenzake kwa nyakati tofauti huku wakikubaliana Watumishi wa Idara hiyo kuingia gharama zao kulipa TV hizo.

Amesema baada ya makubaliano hayo walikwenda kwenye moja ya duka la Mfanyabiashara mmoja mjini Njombe na kuagiza TV nyingine ambazo walipewa kwa makubaliano ya kuzilipa baada ya miezi miwili yaani mpaka mwezi huu wa November na waliweza kupewa bila maandishi yoyote kwakuwa wamekuwa wakishirikiana katika shughuli mbalimbali ambapo mpaka sasa fedha hiyo pia bado haijalipwa kwa mwenye duka.
 
"Waliweza kupewa bila maandishi yoyote kwa kuwa wamekuwa wakishirikiana katika shughuli mbalimbali....." Ofisi ya serikali hakuna maandishi?

Huu ndio wizi. Huyu na Dangote wa Arusha aliyeuawa wametofautiana tu kiasi elimu na ofisi. Stupid in Mama's voice.
 
Naomba kujua majina ya shule za Njombe
 
Hospitali kama ina CCTV kamera,kitu ambacho nina uhakika zipo,walishindwaje kuwatrack wezi....?
Kuna namna hapo,wabanwe hasahasa.
Tatizo wizi
Kila mahali ni wizi mpaka wanaona cctv ni mfichua maovu kwa hiyo hata wakiziweka ( ambapo nina uhakika hakuna) wataziiba pia au kuzivunja aidha kupoteza ushahidi au hawataki kuumbuka

Nchi imejaa wizi hata unaemlisha anakuibia
 
Hospitali kama ina CCTV kamera,kitu ambacho nina uhakika zipo,walishindwaje kuwatrack wezi....?
Kuna namna hapo,wabanwe hasahasa.
Huu umeme hizo camera si ni mapambo tu!

Watu siyo wajinga waibe kiboya hivyo!
 
MaTV yote hayo yaibwe kwa mkupuo?

Hapo Kahama wameweka hadi TV showcase ngoja tuwape muda.
 
Wameambiwa wale kwa urefu wa kamba zao. Unategemea nini? Rais hafanyi ziara yoyote ya kushtukiza? Hakemei vikali wizi, rushwa, ufisadi. Angalau ingewapa watu hofu na kupunguza wizi.

Ndio kwanza yeye anawapa vyeo, promotion mafisadi, wezi na wala rushwa, wahuni ndio washauri wake wakuu.
 
"Waliweza kupewa bila maandishi yoyote kwa kuwa wamekuwa wakishirikiana katika shughuli mbalimbali....." Ofisi ya serikali hakuna maandishi?

Huu ndio wizi. Huyu na Dangote wa Arusha aliyeuawa wametofautiana tu kiasi elimu na ofisi. Stupid in Mama's voice.
Wewe ndiye hujaelewa, hizo walizopewa bila maandishi zimekopwa na wafanyakazi wa hospitali kwaajili ya kulipa zilizoibiwa ili walinde vibarua vyao
 
=======
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amemuelekeza Katibu Tawala wa Mkoa huo kuwasimamisha kazi baadhi ya Watumishi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe akiwemo Katibu wa Afya, Watu wa Idara ya manunuzi pamoja na Idara ya TEHAMA ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za wizi wa TV 15 pamoja na kompyuta tatu katika Hospitali hiyo.

Mtaka ametoa maagizo hayo mara baada ya kushtukiza katika Hospitali hiyo baada ya kupata taarifa ya upotevu wa vifaa hivyo vilivyopotea miezi mitano iliyopita huku akimtaka Afisa manunuzi wa Hospitali hiyo Aloyce Kavumika kulipa takribani shilingi milioni.11 kwa ajili ya kununua TV 15 zilizoibwa.

Awali Afisa manunuzi akitoa taarifa ya wizi huo alisema alipata taarifa ya wizi wa TV July 08,2023 akiwa nje ya ofisi ambapo baada ya kurejea ofisini hapo alilazimika kukaa na Watumishi wenzake kwa nyakati tofauti huku wakikubaliana Watumishi wa Idara hiyo kuingia gharama zao kulipa TV hizo.

Amesema baada ya makubaliano hayo walikwenda kwenye moja ya duka la Mfanyabiashara mmoja mjini Njombe na kuagiza TV nyingine ambazo walipewa kwa makubaliano ya kuzilipa baada ya miezi miwili yaani mpaka mwezi huu wa November na waliweza kupewa bila maandishi yoyote kwakuwa wamekuwa wakishirikiana katika shughuli mbalimbali ambapo mpaka sasa fedha hiyo pia bado haijalipwa kwa mwenye duka.
Angemuacha katibu wa afya, hao ni watu wa manunuzi tu. Ni wezi kila taasisi
 
Kwahiyo mkuu wa mkoa anaacha kazi zoote anaingia mtaani kusaka tv 15 tena kwa muda usiofahamika 😳

😂😂
 
Back
Top Bottom