Asilimia 75 ya miradi ya maendeleo Njombe yakutwa na kasoro baada ukaguzi wa Takukuru

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,505
3,038
Jumla ya miradi ya ujenzi ya maendeleo 12 kati ya 16 ( sawa na asilimia 75) katika mkoa wa Njombe imekutwa na kasoro mbalimbali katika utekelezaji wake baada ya Taasisi ya upambana na kuzuia rushwa mkoa wa Njombe kufanya ukaguzi.

Akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi katika kipindi cha miezi mitatu, Kaimu Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Njombe, Noel Mseo amesema miradi hiyo ni pamoja na ile ya ujenzi wa shule, barabara pamoja na vituo vya afya ambapo baada ya ukaguzi huo wamebaini kuwapo kwa kasoro kadha wa kadha zikiwemo za ukiukwaji wa sheria za manunuzi pamoja na matumizi ya mashine za kukusanyia mapato (POS) kinyume na taratibu zilizowekwa.
img-accountability.jpeg
 
Back
Top Bottom