Tuzungumze kuhusu luku./ tanesco

dfreym

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
342
87
Wadau najua kuna thread nyingi tofauti tofauti, ila nimeona nifanye kitu hiki kwani mimi ni mmoja wa wahanga wa luku. ninaishi kwenye nyumba ya kupanga, sina vitu vya kiviile vinavyotumia umeme mkubwa, kwani nina subwoofer watt 250. laptop moja, taa mbili energe server (sebuleni na chumbani) na pasi (ambayo huitumia kunyooshea nguo ninapotaka kwenda kazini, na sio kila siku).

Tuko wapangani wawili, mpangaji mwenzangu ana kiredio kidogo (huwa hakiwashi mara kwa mara japo kinatumia umeme), duka, ndani ya duka kuna friji, taa na huwa anachajisha simu, pia kuna saloon, ina tv, redio na mashine za kunyolea,

Mama mwenye nyumba ana friji, tv, pasi , na ana kimedical chenye taa na feni tu. ila juzi nimesikia kama kanunua brender kwani nilisikia kelele za brenda zikitokea kwake.

Tangu nihamie nina kama miezi mitatu hivi, mwanzoni nilikaa kama mwezi hivi bila kudaiwa hela ya umeme, nilifurahi nikajua hapa si kwenye gharama kubwa za umeme, then baada ya mwezi nikaambiwa umeme umeisha then nitoe tsh. 5000, nikatoa after 15 days, nikaambiwa tena nitoe 5000, ya umeme, nikatoa, sasa mwezi huu(june 2012, tarehe 8), umeme ukakata, nikaambiwa nitoe tena 5000, kishingo upande nikatoa, jana tena (17 june,)umeme ukakata tena, mi sikusema kitu ila nilijikuta natumbukia kwenye dimbwi la mawazo mwenyewe tu, then naambiwa tena hela ya luku 5000, nikaishiwa pozi. SIKU TISA! luku gani hii?

sasa wanabodi hebu tushauriane, tatizo ni tanesco au mama mwenye nyumba? kwani inaonesha huwa ananunua umeme kwa njia ya m-pesa, anajaza mwenyewe, au huwa ananunua wa elfu mbili mbili?

NINGEPENDA KUJUA YAFUATAYO,

1. UNIT @ MOJA HUWA INAUZWA SHILINGI NGAPI?
2. KUNA TOFAUTI GANI KATI YA MTU AKINUNUA UMEME KATI KATI YA MWEZI, MWANZONI AU MWISHONI?
3. KUNA TOFAUTI YOYOTE MTU AKINUNUA UMEME KWA MAX MALIPO AU M PESA?
4. KUNA TOFAUTI YOYOTE MTU AKINUA UMEME WA 25000, KUSHUKA CHINI, NA MTU AKINUNUA UMEME WA SH. 25000 KUPANDA? (INTERMS OF UNITS).

nawasilisha.........
 
Mkuu nyie mnanyonywa na hao wenye vifaa vikubwa vya umeme, kiufupi hapo hapa kufai au labda akubali kufanya partition ya meter ili msilipie garama zisizo zenu.
 
Tembelea hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...acholipa-kwa-umeme-unaotumia.html#post2351480
huenda ukakuta kitu cha kukufaa

1. ukinunua umeme itazame vizur risit utaona bei ya unit moja
2. ukinunua umeme katikati ya mwez na mwisho wa mwezi haukatwi services charge, hivyo utapata unit nyingi. ukinunua umeme mwanzoni mwa mwezi utakatwa service charges na kodi zingine, mfano kodi za ewura. hivyo utapata unit chache
3. hakuna tofauti. njia yoyote utakayotumia ni sawa tu. ila ukinunua umeme kwa tigo pesa leo basi kesho utazawadiwa dakika 10 za maongezi tigo kwenda tigo
4. nenda ofis ya tanesco ilokarib nawe utaelezwa kuhusu makundi ya watumiaji umeme. ila kuna kundi la watumiaji wadogo, watumiaji wakubwa na watumiaji wa kati.
natumai umeelewa
 
Tehe tehe tehe kaka ndio unaanza maisha!!! Hata me ni muanga hilo swala sio pekeako na nitatizo kwa kila nyumba ya kupanga ambayo mnashare luku moja hakuna uwiano wa matumizi ya umeme, na usitegemee hatakuta tatizo hilo kwenye nyumba ya kupanga cha msingi nikufight ujenge kibanda chako tu!
 
Pole sana kaka ni vzr huyo mother house anapo nunua Umeme awape risit muone au SMS ya manunuzi ya Umeme na kama hauto baini chochote fika office za Tanesco zilizo jaribu nawe upate kufaham yalio mengi kuhusu
 
Back
Top Bottom