legally yes; madaraka yake ya kutangaza hali ya hatari ni ya kwake mwenyewe lakini ana uwezo wa kuyakasimu kwenye baadhi ya mambo n.k lakini vile vile yanaweza kutolewa na mtu ambaye atatoa kwa jina la Rais. Lakini kikiwaka hiyo safari nyingine akiendelea nayo basi ndio itakuwa imekula kwetu.
Mkuu wangu kumbuka maneno yako kuwa tumepanda mbegu hizi na sasa tunavuna na wala hayakuwa magugu yalojiotea yenyewe - Tumepanda sisi wenyewe kwa kufikiri ni mtishamba kama ile dawa ya mzee wa Loliondo.. Na hakika kuna Ulazima wa kutangaza hali ya hatari lakini UDINI tayari imewekwa ktk maghala yetu ya chakula (Rohoni) hivyo inatakiwa kazi kubwa zaidi ya kutangaza hali ya hatari, hekima na busara inatakiwa na sidhani kama kuna mmoja CCM mwenye uwezo huo maana wote ni walevi na mateja wa Udini..Tusipoangalia vizuri tutashuhudia jambo ambalo halijawahi kutokea nchini tangu maasi ya jeshi 1964 na pengine pia tangu vita ya Kagera; kutangazwa kwa hali ya hatari (state of emergency) ili hatimaye kurudisha hali ya usalama nchini. Kutangazwa kwa hali ya hatari na rais kunatoa nafasi kwa vyombo mbalimbali kufanya kazi katika ulinzi wa sheria za juu zaidi na ambapo sheria nyingine zinaweza kuwa suspended na hata haki ya habeas corpus kusitishwa.
I hope hatutafika huko maana tukifika itakuwa ni doa kubwa zaidi la utawala wa Kikwete... maana tayari madoa yapo..
Ama kweli jf ni zaidi ya darasa kwqni sikuwa nayajua hayo
Wewe ni mtu mmojawapo utakayekuwa uko responsible kwa machafuko yoyote kwenye nchi ya kidini.Wewe na huyo Mohammed Said wadini wakubwa kabisa.Nimefuatilia hiyo linki nikakutana na udini mtupu,na hakuna pahala nilipoona hayo uliyoya quote!Kweli una shida sana,unabugia tu bila ya kutafuna.Unaweza kuniambia a hiyo paragraph umeitoa wapi?Usidhani humu watu ni wavivu wa kusoma,nimeiptia na sijaona huo ujinga hapo kuhusu mapinduzi ya 1964,tafadhali mkuu,do not insult our intelligence.
Umeweka link ukisema ndipo ulipoyatoa hayo maneno ya Dosa Azizi na mwalimu Nyerere wakati wa jaribio la kuipindua serikali la 1964,nimeifuatilia hiyo linki sijaona hayo maneno zaidi ya chuki za kidini za Mohammed Said.Sasa umechanganya madesa wewe mwenyewe.Unasema ninakutafuta,nikutafute nikupeleke wapi wewe?Lipi la uongo katika hiyo nukuu?
Ulikuwa unantafuta umenipata, unaanza kutoa povu. Unanchekesha - Courtesy FF
teh teh, yamekukuta nini? Pole, but kama kweli ni shushushu, basi tumlaumu kwa nguvu zetu zote kwa kushindwa kuisaidia nchi hadi ameiacha ifikie hapa ilipo. Binafsi sina kabisa imani na usalama wa taifa, maana ni siku nyingi hapa jf, tunajadili hatari ya radio imaan, gazeti la al-nuur pamoja na ponda, lakini hakuna hata mmoja wa hao usalama wa taifa aliyechukua hatua. Sasa leo watasema wamefanya kazi ipi ya kulisaidia taifa?
Mambo yanabadilika kwa haraka sana. Busara ingetumika ili viongozi wote wakuu walio nje ya nchi warudi nyumbani haraka. Najua State visit inaandaliwa kwa muda mrefu lakini rais anatakiwa akatishe hiyo visit arudi, haraka na ahutubie taifa.
mmh.. na wewe nawe; mnatishwa mno. Mtu akisema yuko Usalama wa Taifa mnaogopa, mtu akizungumza hivi mnadhani ni shushushu. Mashushushu wa kweli hawajulikani na wala huwezi hata kumhisi! Mtanipa ujiko ambao hata sina wala sifikirii kuwa nao.
MMM nani anaweza kutangaza hali ya hatari kama Rais wa nchi hayupo nchini?kuna taarifa tumepata baada ya huko uarabuni ataelekea Japan
NI dhaifu dhaifu ndo maana anazunguka kama Vasco Dagama!!!!