Tutashuhudia kutangazwa kwa hali ya hatari?

Tukitoa yote na udhaifu wote tujuavyo,hivi tuna WAZIRI MKUU? Mh Pinda ameshindwa walau kupunguza hili ombwe la uongozi! Huyu mtoto wa mkulima yupo yupo tu utafikiri mbunge wa kuteuliwa!
 
zomba

Wewe ni mtu mmojawapo utakayekuwa uko responsible kwa machafuko yoyote kwenye nchi ya kidini.Wewe na huyo Mohammed Said wadini wakubwa kabisa.

Nimefuatilia hiyo linki nikakutana na udini mtupu, na hakuna pahala nilipoona hayo uliyoya quote!Kweli una shida sana,unabugia tu bila ya kutafuna. Unaweza kuniambia a hiyo paragraph umeitoa wapi?

Usidhani humu watu ni wavivu wa kusoma, nimeiptia na sijaona huo ujinga hapo kuhusu mapinduzi ya 1964, tafadhali mkuu, do not insult our intelligence.
 
Last edited by a moderator:
legally yes; madaraka yake ya kutangaza hali ya hatari ni ya kwake mwenyewe lakini ana uwezo wa kuyakasimu kwenye baadhi ya mambo n.k lakini vile vile yanaweza kutolewa na mtu ambaye atatoa kwa jina la Rais. Lakini kikiwaka hiyo safari nyingine akiendelea nayo basi ndio itakuwa imekula kwetu.

What scares me is that masses, millions of people in this country are still voting for these corrupt, thieving bastards who are throwing our country to the dogs. To think there are still people who support and defend them, when those same people are suffering the consequences of their refusal to deliver basic services because they are too busy preaching about religion getting fat and rich. That is what makes me worry.

That a person who is clever enough to use a computer and comment on JF or FB, people with access to information on how corrupt our government is, still defends them.. That is something to worry about! People who think they don't deserve better, people who think they can't get better, people who think it is okay for their children to go to bed hungry, as long as their president sleeps in a 1billion house with his family members, those are the people who really scare me. Those who stand in the way of those who pay taxes, those who want to hold this thieving government accountable for their actions and mostly their in actions!!

People like zomba and Ritz, you allow this to happen to us!! You allow this to happen to our country. In fact, you are your own worse enemies!!!

Now we are seeing the result or preaching religion in politics, Thanks to CCM
 
Tusipoangalia vizuri tutashuhudia jambo ambalo halijawahi kutokea nchini tangu maasi ya jeshi 1964 na pengine pia tangu vita ya Kagera; kutangazwa kwa hali ya hatari (state of emergency) ili hatimaye kurudisha hali ya usalama nchini. Kutangazwa kwa hali ya hatari na rais kunatoa nafasi kwa vyombo mbalimbali kufanya kazi katika ulinzi wa sheria za juu zaidi na ambapo sheria nyingine zinaweza kuwa suspended na hata haki ya habeas corpus kusitishwa.

I hope hatutafika huko maana tukifika itakuwa ni doa kubwa zaidi la utawala wa Kikwete... maana tayari madoa yapo..
Mkuu wangu kumbuka maneno yako kuwa tumepanda mbegu hizi na sasa tunavuna na wala hayakuwa magugu yalojiotea yenyewe - Tumepanda sisi wenyewe kwa kufikiri ni mtishamba kama ile dawa ya mzee wa Loliondo.. Na hakika kuna Ulazima wa kutangaza hali ya hatari lakini UDINI tayari imewekwa ktk maghala yetu ya chakula (Rohoni) hivyo inatakiwa kazi kubwa zaidi ya kutangaza hali ya hatari, hekima na busara inatakiwa na sidhani kama kuna mmoja CCM mwenye uwezo huo maana wote ni walevi na mateja wa Udini..

Yeyote anayesema hakuliona hili basi huyo ni Mnafiki mkubwa maana tulipanda, kupapalia na kumwagilia maji sisi wenyewe sasa miiba imezaa na ndimo tunamoishi na kulala...
 
Wewe ni mtu mmojawapo utakayekuwa uko responsible kwa machafuko yoyote kwenye nchi ya kidini.Wewe na huyo Mohammed Said wadini wakubwa kabisa.Nimefuatilia hiyo linki nikakutana na udini mtupu,na hakuna pahala nilipoona hayo uliyoya quote!Kweli una shida sana,unabugia tu bila ya kutafuna.Unaweza kuniambia a hiyo paragraph umeitoa wapi?Usidhani humu watu ni wavivu wa kusoma,nimeiptia na sijaona huo ujinga hapo kuhusu mapinduzi ya 1964,tafadhali mkuu,do not insult our intelligence.

Lipi la uongo katika hiyo nukuu?

Ulikuwa unantafuta umenipata, unaanza kutoa povu. Unanchekesha - Courtesy FF
 
Lipi la uongo katika hiyo nukuu?

Ulikuwa unantafuta umenipata, unaanza kutoa povu. Unanchekesha - Courtesy FF
Umeweka link ukisema ndipo ulipoyatoa hayo maneno ya Dosa Azizi na mwalimu Nyerere wakati wa jaribio la kuipindua serikali la 1964,nimeifuatilia hiyo linki sijaona hayo maneno zaidi ya chuki za kidini za Mohammed Said.Sasa umechanganya madesa wewe mwenyewe.Unasema ninakutafuta,nikutafute nikupeleke wapi wewe?
 
teh teh, yamekukuta nini? Pole, but kama kweli ni shushushu, basi tumlaumu kwa nguvu zetu zote kwa kushindwa kuisaidia nchi hadi ameiacha ifikie hapa ilipo. Binafsi sina kabisa imani na usalama wa taifa, maana ni siku nyingi hapa jf, tunajadili hatari ya radio imaan, gazeti la al-nuur pamoja na ponda, lakini hakuna hata mmoja wa hao usalama wa taifa aliyechukua hatua. Sasa leo watasema wamefanya kazi ipi ya kulisaidia taifa?

hao walishaacha kazi yao wakajifunza kulimboka watu ndio wanachojua siku hizi imefikia mahali kila mwanasiasa ana kundi lake humo ndani ya usalama wanatumwa tu kwa maslahi binafsi
 
Marais wengi sana wawapo ziarani nje lakini nyumbani kukichafuka wanarejea haraka sana. JK kwa hili anatakiwa awe mkali sana unajua WAKRISTO mwisho watachoka hali ya vitisho. IJUMAA kesho unadhani wakisogelea MAKANISA watavumiliwa tena ni wazi hali yaweza kuwa tete.MBONA awamu ya MKAPA hakukuwa na huu upuuzi?
 
Mambo yanabadilika kwa haraka sana. Busara ingetumika ili viongozi wote wakuu walio nje ya nchi warudi nyumbani haraka. Najua State visit inaandaliwa kwa muda mrefu lakini rais anatakiwa akatishe hiyo visit arudi, haraka na ahutubie taifa.

Nashangaa ziara ni muhimu kuliko Amani ya nchi yetu.
 
Mi ngoja nianze kabisa kuandika heading ya taarifa za kesho baada ya swala ya ijumaa "BREAKING NEWS-WAISLAMU WAVAMIA GEREZA KUMKOMBOA sheikh ISSA PONDA"
 
mmh.. na wewe nawe; mnatishwa mno. Mtu akisema yuko Usalama wa Taifa mnaogopa, mtu akizungumza hivi mnadhani ni shushushu. Mashushushu wa kweli hawajulikani na wala huwezi hata kumhisi! Mtanipa ujiko ambao hata sina wala sifikirii kuwa nao.

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha...kamanda MM,unatisha mkuu. Heshima kwako.
 
Taifa liko tayari kwenye state of emergency (undeclared). Ila kama tutaendelea kutoa majibu mepesi kwenye maswali mazito basi itakuwa officially declared. Japo tulio wengi tusingependa kufikiswha huko.
 
Kweli kabisa Mwanakijiji...
Na sasa hivi ndio naielewa lile neno la Mh MNYIKA kuwa jeikei ni DHAIFU
 
MKJJ, huyu bwana tunavyozungumza wote tunajua yupo uarabuni! Sijajua ni kitu gani hasa anachofuata huko hata akakaa kwa amani namna hiyo wakati nchi yetu iko kwenye wimbi kubwa la machafuko ya kidini! Wakati makanisa yanachomwa yeye anawakenulia meno waarabu na kuwapa zawadi ya picha za tembo (ambao waarabu wanawaua kila siku na kuwapeleka huko huko kwa biashara ya pembe zao). Huyu haoni kama ni hatari! Nadhani kwake ni furaha. Udini aliotamani sasa umefika alipopataka!

Hawa uamsho wamekuwepo tokea lini? Vuguvugu la mambo ya kidini yamekuwepo toka lini? Si raisi huyu huyu aliyewachekea walipogomea sensa? Si raisi huyu huyu aliyewaachia huru aliowakamata kwa geresha kuwa wamegomea sensa? Huyu ninayemfahamu, kwa udhaifu wake, hawezi!
 
NI dhaifu dhaifu ndo maana anazunguka kama Vasco Dagama!!!!

Kila anaponusa kuwa kutakuwa na matatizo nchini ,anaandaa safari ili kukwepa kuwajibika!! The presidency is not for the weak in the head and at their heart!!
 
Back
Top Bottom