Papua New Guinea: Hali ya hatari yatangazwa Mji Mkuu baada ya maandamano na uporaji kutokana na kupanda kwa gharama za maisha na malipo finyu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
4.jpeg

Papua New Guinea imekusanya vikosi vya usalama baada ya uporaji na ghasia nchini kote. Ufinyu wa ajira na kupanda kwa gharama ya maisha kumezua hali ya kufadhaika katika taifa hilo la Pasifiki Kusini

Waziri Mkuu wa Papua New Guinea James Marape alitangaza hali ya hatari ya wiki mbili katika mji mkuu wa Port Moresby siku ya Alhamisi baada ya kuenea kwa uporaji na kusababisha vifo vya takriban watu 15 nchini humo.

Agizo la waziri mkuu linasema kuwa zaidi ya wanausalama 1,000 walikuwa wamesimama tayari "kuingia popote inapobidi kuzuia ghasia hizo"

Marape mapema Alhamisi alisema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba Port Moresby ilikuwa "katika shinikizo." Takriban Wanajeshi 180 walitumwa baada ya ghasia siku ya Jumatano, kulingana na ripoti za awali.

"Ripoti ya hali kufikia leo asubuhi inaonesha kuwa hali ya wasiwasi imepungua jijini," Marape alisema katika mkutano huo wa wanahabari.

"Polisi hawakuwa kazini jana jijini na watu walifanya uvunjaji wa sheria - sio watu wote, lakini katika sehemu fulani za jiji letu," Marape alisema.

Kilichojiri tangu awali:

Ghasia zilizuka huko Port Moresby siku ya Jumatano baada ya mamia ya maafisa wa polisi, wanajeshi, wafanyikazi wa magereza na wafanyikazi wa umma kuacha kazi zao kupinga mzozo wa malipo.

Maduka yaliporwa na maghala kuchomwa moto katika mji mkuu, huku ghasia kama hizo pia zikiripotiwa katika mji wa pili kwa ukubwa nchini humo wa Lae.

3.jpg

Shirika la Utangazaji la Australia liliripoti kuwa machafuko yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 15 huko Port Moresby na Lae.

Maduka mengi na huduma za benki bado zimefungwa huku wamiliki wa biashara wakirekebisha uharibifu.

Mvutano nchini umeongezeka huku kukiwa na ukosefu mkubwa wa ajira na kuongezeka kwa gharama za maisha.

Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese aliomba utulivu. Alisema serikali yake haijapokea maombi yoyote ya usaidizi kutoka kwa jirani yake wa karibu.

Papua New Guinea, nchi yenye watu milioni 10, ndiyo taifa lenye watu wengi zaidi katika Pasifiki Kusini baada ya Australia.
 
ccmu wanatupeleka huku , hayo machafuko yana mkono wa wamatajiri , kama una akili fupi huez elewa
 
Back
Top Bottom