Tutashuhudia kutangazwa kwa hali ya hatari?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Tusipoangalia vizuri tutashuhudia jambo ambalo halijawahi kutokea nchini tangu maasi ya jeshi 1964 na pengine pia tangu vita ya Kagera; kutangazwa kwa hali ya hatari (state of emergency) ili hatimaye kurudisha hali ya usalama nchini.

Kutangazwa kwa hali ya hatari na rais kunatoa nafasi kwa vyombo mbalimbali kufanya kazi katika ulinzi wa sheria za juu zaidi na ambapo sheria nyingine zinaweza kuwa suspended na hata haki ya habeas corpus kusitishwa.

I hope hatutafika huko maana tukifika itakuwa ni doa kubwa zaidi la utawala wa Kikwete... maana tayari madoa yapo..
 
Mambo yanabadilika kwa haraka sana. Busara ingetumika ili viongozi wote wakuu walio nje ya nchi warudi nyumbani haraka. Najua State visit inaandaliwa kwa muda mrefu lakini rais anatakiwa akatishe hiyo visit arudi, haraka na ahutubie taifa.
 
Tusipoangalia vizuri tutashuhudia jambo ambalo halijawahi kutokea nchini tangu maasi ya jeshi 1964 na pengine pia tangu vita ya Kagera; kutangazwa kwa hali ya hatari (state of emergency) ili hatimaye kurudisha hali ya usalama nchini.
Kwasababu ya wahuni wachache? BTW hata vijana wa cozi pale CCP moshi wanatosha kuwa-silence hawa vibaka wa Manzese...
 
Ijapobidi kutangaza hali ya hatari ili kurudisha utangamano wa kitaifa hatuna budi kufanya hivo kila nyakati na kitabu chake! chuki za kidini zimepandikizwa na kulelewa na viongozi walio madarakani kwa sababu za kisiasa sasa ni lazima wamvalishe paka kengele!!
 
Kuanzia leo onward nakuwa makini kuchangia hoja za Mzee Mwanakijiji...nimegundua ni shushushu. Ukicheza nae utanyea debe. I salute you sir!!
 
Tusipoangalia vizuri tutashuhudia jambo ambalo halijawahi kutokea nchini tangu maasi ya jeshi 1964 na pengine pia tangu vita ya Kagera; kutangazwa kwa hali ya hatari (state of emergency) ili hatimaye kurudisha hali ya usalama nchini. Kutangazwa kwa hali ya hatari na rais kunatoa nafasi kwa vyombo mbalimbali kufanya kazi katika ulinzi wa sheria za juu zaidi na ambapo sheria nyingine zinaweza kuwa suspended na hata haki ya habeas corpus kusitishwa.

I hope hatutafika huko maana tukifika itakuwa ni doa kubwa zaidi la utawala wa Kikwete... maana tayari madoa yapo..

Mkuu hii post ingewekwa na mtu mwingine nahakika ingeondolewa mapema kabisa.Unaweza kuweka maoni yako mara ghafla mods wanaiondoa na hata sababu hupewi.
 
Mambo yanabadilika kwa haraka
sana. Busara ingetumika ili viongozi wote wakuu walio nje ya nchi warudi
nyumbani haraka. Najua State visit inaandaliwa kwa muda mrefu lakini
rais anatakiwa akatishe hiyo visit arudi, haraka na ahutubie
taifa.

mbona alivyokuwepo walishambulia makanisa dar? shein naye hayupo maana zanzibar ndiko kunakofuka moshi!
 
Wakati viongozi wa CCM wakiongoza jitihada za kupandikiza chuki za kidini dhidi ya CHADEMA ili kumsaidia Kikwete kuingia madarakani, yeye alikenua meno akaona hao ndo wenye akili. Ujumbe wa simu wa kupandikiza mbegu za chuki za kidini ulisambazwa kila mahali hakuna aliyesimama kukemea. Waislam wakatoa matamko yenye sura za udini hakuna aliyesimama kuyapinga, leo yamefika hapa ndo wanajifanya wanahamaki.

Kuna waliotabiri kwamba utawala wa Kikwete hautafika 2015, naona dalili ndo hizi, kama maaskofu wa makanisa yote wataamua kuungana na kutangaza wanachoweza kutangaza, naamini hapo tutamark the end of utawala wa Kikwete. And the worst think tukifikia huko, itamaanisha Kikwete hana jeshi tena la kusimama upande wake, maana hawa wanajeshi wana dini zao wanazoziamini. Worse enough asilimia karibu 80 ya wanajeshi ni wakristu. Kwakweli sipati picha hii vita itapiganwaje?

Tuombe Mungu tu atupe busara, ili kama ni hali ya hatari itangazwe mapema kabla hatujafika kubaya. Maana siamini kama wakristo wataendelea kufumbia macho hivi vitendo vya uchomaji wa makanisa vinavyoendelea kufanywa na hawa waabuduo majini.
 
Hali ya hatari itangazwe tu,hawa vibaka watatumaliza,wakristo waki react hapatatosha hapa.

Tumefika hapa tulipo kutokana na udhaifu wa Rais Kikwete-jj Mnyika.
 
Mambo yanabadilika kwa haraka sana. Busara ingetumika ili viongozi wote wakuu walio nje ya nchi warudi nyumbani haraka. Najua State visit inaandaliwa kwa muda mrefu lakini rais anatakiwa akatishe hiyo visit arudi, haraka na ahutubie taifa.

Mkuu, umenena. Tatizo la hapa TZ, nchi imekaa kama vile haina uongozi. Kila kiongozi na kila raia asimame katika zamu yake, hapatakuwa na shida tena.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Miemuko ya kisiasa ni kitu hatari sana,inaweza kutuangamiza si tu kifikra bali kimaendeleo.
 
Kuanzia leo onward nakuwa makini kuchangia hoja za Mzee Mwanakijiji...nimegundua ni shushushu. Ukicheza nae utanyea debe. I salute you sir!!
Teh teh, yamekukuta nini? Pole, but kama kweli ni shushushu, basi tumlaumu kwa nguvu zetu zote kwa kushindwa kuisaidia nchi hadi ameiacha ifikie hapa ilipo. Binafsi sina kabisa imani na usalama wa taifa, maana ni siku nyingi hapa JF, tunajadili hatari ya radio Imaan, gazeti la Al-nuur pamoja na Ponda, lakini hakuna hata mmoja wa hao usalama wa taifa aliyechukua hatua. Sasa leo watasema wamefanya kazi ipi ya kulisaidia taifa?
 
Back
Top Bottom