Tusitumie tena "Division Zero" kwenye matokeo ya Elimu ya Sekondari...

Mzee Mwanakijiji,tusitake kubadilisha mada hapa!
Elimu iliyo tolewa kwa miaka 4 ni elimu ya darasani,na vigezo vya kufaulu au kufeli vinapangwa kwa kuzingatia elimu hiyo iliyo tolewa darasani.
Hivyo aliye pata Div 1 ana uwezo mkubwa katika elimu ya darasani;na aliye pata FLD(Sijui ndio div 0) haina maana ni dumb,bali katika elimu iliyo tolewa darasani ndio hana uwezo.
Alternative sio kubadili jina la FLD,bali kutafuta options nyingine kama elimu ya ufundi,elimu ya kilimo,vyuo vya sanaa nk ili watoto walio pata FLD darasani waende kulingana na uwezo wao.
 
Last edited by a moderator:
Mimi nakubaliana na wewe mwanakijiji kabisa. Ila pia hata km zero itaendelea kuwepo basi wapewe cheti kwani hata zero ni namba. Japokua mtu kapata zero yan "F" haimaanishi kua hana kitu alichojifunza na kuelewa kwa muda wa miaka minne au sita ambacho kitaisaidia jamii. Inawezekana huyu mtu yuko kwenye lile kundi la "iron" kulingana na Plato ambaye aliwagawa katika makundi matatu. GOLD Hawa ni intelligence people wanaotumia akili kuliko nguvu mara nyingi huishia kuwa watawala. Pili ni SILVER hawa ni wa kati na wanaotumia nguvu pamoja na akili na hawa alitolea mfano kua huishia kua askari. Kundi la mwisho ni hawa iron ambao hutumia zaidi nguvu kuliko akili japo wanazo akili. Hawa ni wale wafanyao kazi ngumu kama ufundi.
Serikali yetu imeliacha hili kundi la watoto ambao ni iron kwa kuwatunukia division zero kwa kusahau kua ndio wengi na wanaohitajika kulijenga taifa. Kwani ndio nguvu kazi
 
Division zero lazima iendelee kuwapo, inasaidia wanafunzi, wazazi, walimu na serikali kwa ujumla.
Kwa mwanafunzi makini mwenye kujua anachokifanya lazima baada ya matokeo ya namna hii kutoka lazima ataongeza juhudi katika masomo yake ya darasani na hii hakika itamsaidia kujikwamua na janga kama hili la mwaka huu.

Kwa upande wa wazazi hasa ambao kwa namna moja ama nyingine huwa hawatimizi wajibu wao mfano kulipa ada na michango mbalimbali kwa wakati nadhani watatimiza wajibu huo, kukagua nini watoto wao wanafanya mashuleni, kuwahimiza watoto katika kuzingatia masomo nk. Hakika sisi kwa pamoja tukitimiza wajibu wetu kama wazazi walau tutachangia kuleta matokeo mazuri kwa watoto wetu, tutimize wajibu wetu, hakuna aliyezaliwa kufeli kwa kiwango cha kutisha namna hii ya mwaka huu.

Kwa upande wa ndg zetu walimu, tunajuwa kwa mwaka huu ujumbe wao umekuwa delivered kwa vitendo lakini lakini hakika walimu wengi ni wazazi pia, watoto wao wamo kwenye hili kundi la 60%. Kwa mkutadha huo sio wote wenye kufurahia matokeo hayo hata kidogo, wataendelea kutimiza majukumu/wajibu yao ipasavyo ambao ni kufundisha watoto wetu kwa moyo, nguvu, akili yao yote.

Na mwisho kwa upande wa serikali, wazee wa tume, hakika wanabidi watimize wajibu wao ipasavyo. Wamejisahau sana sina hakika hiyo tume itakuja na jibu gani ambalo wao serikali na hata sisi wananchi hatulijui, any way ngoja tuwasubiri, ili hakika hawa nakula pesa wa walipa kodi pasipo sababu ya msingi.
*Nani hajui kuwa kwenye shule zetu msingi hadi sekondari kuna upungufu mkubwa wa walimu na hasa wa masomo ya Sayansi,

*Nani hajui kuwa kwenye mashule yetu hakuna vitabu vya kufundishia, Ni nani hajui kuwa kwenye shule zetu hakuna nyumba za walimu za kutosha,

*Ni nani hajui kuwa walimu wetu kila kukicha wanalalamika kuwa mishahara yao ni midogo na haikidhi mahitaji ya maisha na wanadai malimbikizo mengi mf, uhamisho, likizo nk, jambo ambalo linafanya maisha yao kuwa magumu na kuishia kuwa watu wa madeni na madeni na wao.

*Serikali iliwahi kusema itakuwa inapeleka ruzuku mashuleni kulingana na idadi ya wanafunzi ili kusaidia uendeshaji wa shule, mf manunuzi ya chaki, kalamu, karatasi, vifaa vya ofisi nk, lakini hayo yote hayatekelezwi ipasavyo.

*Idara za ukaguzi zilikwisha kufa kabisa, maana hawana hata bajeti ya kuweka mafuta kwenye gari ili wazungukie mashule na hapo ni tofauti na posho ya kujikimu wawapo huko.

*Kuna kitu kinaitwa maabara kwa masomo ya Sayansi, hili hata takwimu zake zikitolewa na ukilinganisha na idadi ya shule za sekondari tulizonazo nadhani ni masikitiko makubwa, na huu ni wajibu wa serikali. Na hata zile shule kongwe tulizoachiwa na mkoloni zina maabara lakini hazina vifaa vya maabara (laboratory apparatus) na chemicals kwa ajili ya majaribio nk.

Muulizeni mkuu PM (Pinda) aulize ile shule yake aliyosoma A level, japo yeye hakuwa mtu wa Sayansi kama maabara zina vifaa.
Hakika hiyo tume haitakuja na jipya ambalo serikali hailijui, labda kama ni vipofu na hawajui kusoma pia.

Mwisho kabisa acha divishen zero ziwepo zitatusaidia katika kutumbusha wajibu wetu sote, yaani wanafunzi, wazazi, walimu na serikali.
 
... Inawaambia watoto hawa kuwa wao hawana uwezo. Na hii ni kweli hasa pale inapoonekana kuwa katika mtihani ule ule kuna watoto wamepata Division 1 za Juu. Kimsingi mfumo huu unasema kuwa watoto waliofaulu ndio wana akili sana na wale waliopata division zero hawana akili. Lakini ni akili gani tumepima - ni ile ya darasani....
Lakini najaribu kujiuliza pia, ni kwa nini baadhi yao (au pengine niseme, wengi wao) wakiamua kurudia (resit) wanafanya vizuri?
 
Lengo la elimu iwe kufaulisha siyo kufelisha. Matokeo ya elimu yawe ni wanafunzi kuelimika siyo kutoelimika. Alama ya "zero" kwenye matokeo ya mtihani wa Sekondari ya Kawaida (O Level) na Sekondari ya Juu (A Level) ni alama yenye kuonesha kushindwa. Inaonesha kushindwa kwa wanafunzi, shule, wazazi na jamii. Ni alama ambayo haioneshi juhudi za watoto wetu ambao kwa miaka minne wamejitahidi kukaa darasani kujifunza; na haioneshi uwezo wa watoto katika mambo mengine (sanaa, kujitolea, utumishi, n.k). Tunasema mtoto kafeli mtihani basi "hana akili".

Kwa wale ambao tunaamini katika nadharia ya "Multiple Intelligencies" binadamu wana tofauti katika akili. Mtu ambaye anaweza asiwe mzuri sana kwenye baadhi ya masomo (na hivyo kuonekana hana akili sana) anaweza kuwa na uwezo mkubwa kwenye fani nyingine nje ya darasani. Na hata darasani watu wanajifunza tofauti tofauti. Mfumo wetu wa sasa ambapo mwalimu anahutubia mbele ya darasa ni mfumo wa kizamani wa kufundishia kwani haujali sana tofauti ya namna ya watu mbalimbali kujifunza (una assume kuwa watu wote wanaelewa sawasawa na wakati mmoja). Hivyo matokeo ya "zero" kimsingi yanatupa picha ya uongo.

Kuondokana na 'division zero' haina maana ni kuondokana na kipimo cha watu kufanya vibaya. Bali ni kuondokana na kipimo chenye kudunisha, kudhalilisha na kuwawekea alama watoto wetu isiyofutika (indelible mark) ya kushindwa. Mtoto aliyepata zero ndio kapata zero maisha yake yote. Alama hii ni alama ya aibu.

Ninasema hivi hasa katika taarifa za safari hii (na imewahi kutokea huko nyuma) baadhi ya watoto wamejiua kwa sababu pamoja na jitihada zao zote wamepata 'zero". Binafsi siamini kuwa alama hii inastahili kuwepo hata kwa mtoto mmoja tu kujiua kwa sababu "kafeli". Kweli kupata "zero" ni kufeli maisha, ni kufeli katika njozi, ni kufeli katika kujaribu? Kwa wengine, 'zero' ndio alama ya wao kushindwa katika maisha; hawahitaji hata kujaribu. Lakini kweli "zero" ni kushindwa?

Tume ya Waziri Mkuu inapoanza kazi ya kufikiria chanzo na mapendekezo ya nini cha kufanya ni matumaini yangu itafikiria pia namna ya kuondokana na "division zero" kama alama ya chini kabisa. Ifikirie namna ya kupima watahiniwa na kuwapanga katika madaraja ambayo hayatakuwa na alama hii ya aibu na fedheha.

Tangu matokeo haya mapya ya kidato cha nne yalivyotoka nimekuwa nikiwaza sana na hatimaye ninaweza kusema pasi ya shaka kuwa pamoja na mabadiliko mengine yatakayopendekezwa ili kuboresha elimu nipendekeze kuwa mojawapo ya vitu vya kuondolewa ni hili la watu kupata "division zero".

Watu wanapopata alama hiyo manake ni kuwa "wamefeli". Kwamba kwa miaka yao minne ya elimu ya sekondari watoto hawa wametoka kapa. Na hii ina maana siyo tu wamefeli lakini wazazi nao wamefeli, na walimu nao wamefeli. Inawezekana vipi pamoja na gharama na juhudi zote za taifa, wazazi na shule watoto watoke shuleni na "zero"?

Ni alama mbaya Kisaikolojia vile vile. Inawaambia watoto hawa kuwa wao hawana uwezo. Na hii ni kweli hasa pale inapoonekana kuwa katika mtihani ule ule kuna watoto wamepata Division 1 za Juu. Kimsingi mfumo huu unasema kuwa watoto waliofaulu ndio wana akili sana na wale waliopata division zero hawana akili. Lakini ni akili gani tumepima - ni ile ya darasani.

Tuondokane na alama ya 'division zero'.

Unakubali au unakataa?

Mwanakijiji umeongea kitu cha maana sana. Kuongeza ulichosema ni kwamba wanafunzi wa sekondari kila mwisho wa term hufanyiwa assessment ikiwa ni pamoja na mitihani na mambo mengine. Hiyo assessment hutumwa wizarani na baraza la mitihani. Sasa kama mwanafunzi amefanya hii mitihani na amekuwa akipata marksi zake (hata kama siyo A) kwa nini uje baadaye umpime kwa mitihani ya taifa tu peke yake? Hapo kwa kweli nakuunga mkono
 
Mzee Mwanakijiji napingana na wewe kwa asilimi mia.Kigezo cha zero kiwepo kwani mtoto anayeiona division "Zero" inadhalilisha atajitahidi kusoma na kuzingatia shule.

Na tatizo la pili kwa wale watoto ambao hawapati haki kamili ya kufundishwa walimu,vifaa vya kujifunzia ,majengo,maktaba,labs hao ndio wakuwatafutia ufumbuzi ni nini wafanyiwe.

Division Zero inamfanya mtu kuwa muoga na kusoma kwa bidii ukiitoa watoto wetu watazmbea.Ilikuwepo toka enzi hizo na waliopta walikuwa ni asilimia ndogo sana,iendelee tu kuwepo hakuna jinsi.

Mkuu naona unapinga labda kwa kupenda au hujui,na kama ungekuwa umesoma psychology usingepnga na hapa ungekuwa unajua mamb meng!
 
Hatuna sababu ya kushughulika na majina, ni bora jina libaki hivyo hivyo ili watoto wajitahidi kusoma ili wasitumbukie kwenye hilo kundi.
 
nakataa 100% mtanzania mwenzangu kuondoa division zero ni sawa na kupulizia pafyumu mwili wenye kunuka jasho harufu itabadilika ila itakuwa kali zaidi yenye kuleta mafua.

maoni yangu ni wahusika wote wazazi, wanafunzi, seikali na jamii kwa ujumla tutimize wajibu wetu
 
Mkuu naona unapinga labda kwa kupenda au hujui,na kama ungekuwa umesoma psychology usingepnga na hapa ungekuwa unajua mamb meng!
naamin brain ya binadamu hufanya kazi zaidi inapo hisi "sense of fear" kupaka rangi division zero ni kutengeneza mazigira ya wanafunzi kutojituma akijua mwishoni hakuna aibu.
 
Labda kuendeleza alichosema Mkodoleaji hapo (kama kuna mtu anaweza kutusaidia) - je mitihani ya nyuma ya mwanafunzi (miaka yake minne yote) na Mtihani wa form two (sijui kama upo) inajulimshwa vipi katika matokeo ya mwisho wa kuhitimu? Yaani alama zake za nyuma zina nafasi gani katika kuamua matokeo ya mwisho ya mtoto? Au mtoto anahukumiwa kwa matokeo ya ule mtihani wa mwisho tu?
 
Excellent mtoa mada, binafsi nina kaka yangu ambaye alipata iyo div-0 lakin alikuwa na uwezo na kipaji kikubwa kwenye uchoraji.. Alipelekwa chuo cha sanaa ya uchoraji na kufanya vizuri cna kwa sasa anakampuni ya uchoraji yenye mafanikio sana akiwapita kwa mbali sana kiuchumi na kiufanisi wa kazi wale ambao walipata div-1 na wengine wakiwa na madegree yao.. Ni sahihi kuangalia upya mfumo we2 wa elim na kuwa na masomo ya ufundi,sanaa na michezo yakiwa yenye practical sana kisha kipimo kiwe kwa kuwafanyia assessment kutoka kidto 1-4.. Naamin hakutakuwa na mtu kufeli hapo huku tukiwa na hazina kubwa ya rasili mali watu yenye tija kwa taifa. Hata nchi za asia ya kati zinazokua kwa kasi kiuchumi inatokana kuwa na mfumo wa elim wa kuthamini kipaji cha mtu.. Hiyo tume haina jipya la kutueleza kwani kila kitu kinajieleza..
 
mwanakijiji napingana na wewe kwa kiwango kikubwa sana sana sana labda nianze hivi katika kundoi lolote lazima kuna kiongozi na lazima kuna wa mwisho. na kawaida mwisho uitwe nini bado utabaki kuwa mwisho tu. so far hata kwenye michezo kuna timu inayoshoinda na inayosindwa na haimaanish kwamba inayoshindwa basi itakaa mkiani milele la hasha ipo siku itakuja juu kama tu itatambua makosa yake na kuyasahihisha.

Binafsi kama mwl ambaye nimefanaya kazi hii kwa miaka 10 sasa nimeona mengi ambayo siasa kama hizi yanayaharibu. Hapa mtakuja na hoja isiwepo div 0 wala baraza halina zero bali lina fail. na hili ndilo jina pekee analostahili kuitwa yule aliyeshindwa mtihan na ndo maana education evaluators waliiweka hii grade.

mantiki ya hili kundi ni kuwakumbusha waliofeli ku pull up their socks ili wawe sawa na wenzao huku tukiamini kwamba elimu sio lazima wote wapitie formal education hapana wap watakao divergelkn mwisho wa siku tunakutana nao.

mathalan wapo wanafunzi wanaofeli mtihani kabisa ila wananzia ngazi ya cheti kusoma may be unesi ama ufundi, mwisho wsiku tunakutana vyuoni wakiwa ni wanafunzi. hivi umesha wah kujiuliza wale anaofanya mature entry wana kuwa wamepita wapi b4??

nakupa mfano halisi kuna mwl wangu asasa ni prof tena anacheo kikubwa sana serikalini yeye alianza alisoma hakufaulu darasa la saba, akaenda ualimu wa UPE miaka hiyo, akajitahd akaup grade hadi akafikia ngazi ya diploma, kisha akaja chuo kama mature entry akasoma degree ya kwanza, hadi phd na sasa ni prof.

sasa fikiria mtu kama huyu na huu ni mfano mmoja tu ninaye mdogo wangu kabisaa yeye alisoma form 4 akazungusha nikamwambia maisha hayajaishia hapo, twende nikamsomesha cheti cha Nacte akafaulu, nikampeleka dip huko mbeya TIA akasoma akafaulu vzr nikamwambia bado nenda TIA soma degree sasa ni mwaka wa 3 na anafanya vzr. swala sio zero swala ni nafasi aliyonayao mtu binafsi kwenye kutaka kubadilika
 
Na ni kwanini Serikali isimpe cheti mtoto pamoja na result zake? kupata Division zero kuna uhusiano gani na kubatilisha ukweli kwamba mtoto amehitimu form 4?

amehitimu nini wakati ameshindwa hata kupata D mbili sijui tatu
 
Labda kuendeleza alichosema Mkodoleaji hapo (kama kuna mtu anaweza kutusaidia) - je mitihani ya nyuma ya mwanafunzi (miaka yake minne yote) na Mtihani wa form two (sijui kama upo) inajulimshwa vipi katika matokeo ya mwisho wa kuhitimu? Yaani alama zake za nyuma zina nafasi gani katika kuamua matokeo ya mwisho ya mtoto? Au mtoto anahukumiwa kwa matokeo ya ule mtihani wa mwisho tu?

nimekupa like kwasababu hili ni swala nyeti ila watu huwaga hawajiulizi. siku zote waalimu huwa tunajaza CA za wanafunzi na hizi ni toka form 1 hadi form 4 mock. matokeo haya huwa yale ta form two na yale ya form 4 mock pamja na ya annual ya kila form huwa yanaccount kwenye kituambacho huitwa majaribio haya huhesabiwa kwenye mtihani wa mwisho. na hizi ni muhimu sana ingawa watu huona kama hayana kazi na hivyo wazazi pamoja watoto hudharau na kuaona kana kwamba hakuna sababu ya kuyawekea mkazo haya.

ila matokeo ya mwisho huwa yana carry big percent kuliko haya majaribio na ndio maana bado wanafunzi wanafeli manake waweza kukuta kweye majaribio mtu ana f wastani wa f na ukijumlisha na national exam bado ana wastan F so ni bora mwanafunzi akawa mzuri toka siku ya kwanz aanapoingia darasani.
 
Labda kuendeleza alichosema Mkodoleaji hapo (kama kuna mtu anaweza kutusaidia) - je mitihani ya nyuma ya mwanafunzi (miaka yake minne yote) na Mtihani wa form two (sijui kama upo) inajulimshwa vipi katika matokeo ya mwisho wa kuhitimu? Yaani alama zake za nyuma zina nafasi gani katika kuamua matokeo ya mwisho ya mtoto? Au mtoto anahukumiwa kwa matokeo ya ule mtihani wa mwisho tu?
wako sahihi kabisa wanafunzi wakipimwa jinsi unavyotaka pendekeza hatutakuwa na wasomi.....walimu wata chakachua wanafunzi watapewa marksi nyingi za bure ili shule zionekane zinafanya vizuri.....tujiulize swali kama mtihani wa taifa watu wana nunua na kuwapa wanafunzi itakuwaje tukisema 40% ya mtihani wa mwisho iwe ni accumulation ya marks alizopata ndani ya miaka minne.
 
nimekupa like kwasababu hili ni swala nyeti ila watu huwaga hawajiulizi. siku zote waalimu huwa tunajaza CA za wanafunzi na hizi ni toka form 1 hadi form 4 mock. matokeo haya huwa yale ta form two na yale ya form 4 mock pamja na ya annual ya kila form huwa yanaccount kwenye kituambacho huitwa majaribio haya huhesabiwa kwenye mtihani wa mwisho. na hizi ni muhimu sana ingawa watu huona kama hayana kazi na hivyo wazazi pamoja watoto hudharau na kuaona kana kwamba hakuna sababu ya kuyawekea mkazo haya.

ila matokeo ya mwisho huwa yana carry big percent kuliko haya majaribio na ndio maana bado wanafunzi wanafeli manake waweza kukuta kweye majaribio mtu ana f wastani wa f na ukijumlisha na national exam bado ana wastan F so ni bora mwanafunzi akawa mzuri toka siku ya kwanz aanapoingia darasani.

gfsonwin unaweza kutusaidia kujua CA ina carry percent ngapi na mtihani wa mwisho una carry percent ngapi?
 
Labda kuendeleza alichosema Mkodoleaji hapo (kama kuna mtu anaweza kutusaidia) - je mitihani ya nyuma ya mwanafunzi (miaka yake minne yote) na Mtihani wa form two (sijui kama upo) inajulimshwa vipi katika matokeo ya mwisho wa kuhitimu? Yaani alama zake za nyuma zina nafasi gani katika kuamua matokeo ya mwisho ya mtoto? Au mtoto anahukumiwa kwa matokeo ya ule mtihani wa mwisho tu?
Katika nchi ambayo rushwa na ujanjanjanja umetawala hizo alama za mwanafunzi anazojaziwa ktk kipindi chake cha masomo siyo za kuhaminika kabisa. Kwa maoni yangu bado mtihani wa mwisho ni kielelezo muhimu cha muhusika yuko vipi! Tuache kutafuta sifa za kisiasa eti tuna maelfu ya wanafunzi ktk shule za sekondari. Tutafute njia nyingine mfano kuwa na vyuo vya ngazi ya chini na kati ambako vijana watajifunza uvuvi,kilimo,useremela,ujasirimali,fundi makenika,nk!
 
Katika nchi ambayo rushwa na ujanjanjanja umetawala hizo alama za mwanafunzi anazojaziwa ktk kipindi chake cha masomo siyo za kuhaminika kabisa. Kwa maoni yangu bado mtihani wa mwisho ni kielelezo muhimu cha muhusika yuko vipi! Tuache kutafuta sifa za kisiasa eti tuna maelfu ya wanafunzi ktk shule za sekondari. Tutafute njia nyingine mfano kuwa na vyuo vya ngazi ya chini na kati ambako vijana watajifunza uvuvi,kilimo,useremela,ujasirimali,fundi makenika,nk!

Kwa hiyo hiyo baraza haliyaamini hayo matokeo yanayojazwa na walimu, lakini linaamini kwamba wanafundisha kiasi cha kuwatungia wanafunzi wanaowafundisha mitihani? Na huo mtihani wa mwisho unatungwa na unasahihishwa na nani? Je hao nao unawaamini?
 
Back
Top Bottom