Tusikubali kulazimishwa wimbo wetu wa Taifa kuwa na ubeti mmoja

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
21,498
37,792
Muda mfupi uliopita kabla ya mechi ya CHAN 2021 kati ya Zambia na Tanzania, kama ilivyo ada zimepigwa nyimbo za Taifa za mataifa hayo mawili.

Umetangulia wimbo wa Taifa la Zambia na umepigwa wote kama ulivyo, lakini ilipofika zamu ya wimbo wa Tanzania wenye beti 2 umepigwa ubeti mmoja tu na kwa vile umepigwa kwa ala hatujui ni ubeti gani kati ya ubeti wa kwanza na wa pili. Wakati wachezaji na viongozi wakianza ubeti wa pili ghafla vyombo vikazimwa na ukawa mwisho wa wimbo.

Ninachotaka kusema hapa ni kwa nini wimbo wetu wa Taifa upigwe ubeti mmoja pekee? Je, hili ni la makusudi au menejimenti ya CAF inajua wimbo wetu wa Taifa una ubeti mmoja?
 
Naunga mkono hoja. Tususie michuano yote ya CAF, na wakituzingua, tususie hata ya FIFA.
 
Muda mfupi uliopita kabla ya mechi ya CHAN 2021kati ya Zambia na Tanzania, kama ilivyo ada zimepigwa nyimbo za Taifa za mataifa hayo mawili.
Umetangulia wimbo wa Taifa la Zambia na umepigwa wote kama ulivyo...
Ndiyo tatizo la kukopi nyimbo za watu!
 
Hivi wimbo wetu na wa zambia unafanana make kipindi wanapiga wa zambia ndo nilijua wetu
 
Nahangalia hapa kupitia KBC na mtangazaji alikua akiitaja zaidi Dar es salam Young African kama ndio timu kubwa na nembo la soka la bongo
Itakuwa kbc ya tandale ambayo mtangazaji wake ni maulid kitenge, hawawezi kuzungumzia timba ambayo hata kwenye 50 bora ya caf haipo
 
Muda mfupi uliopita kabla ya mechi ya CHAN 2021 kati ya Zambia na Tanzania, kama ilivyo ada zimepigwa nyimbo za Taifa za mataifa hayo mawili.

Umetangulia wimbo wa Taifa la Zambia na umepigwa wote kama ulivyo, lakini ilipofika zamu ya wimbo wa Tanzania wenye beti 2 umepigwa ubeti mmoja tu na kwa vile umepigwa kwa ala hatujui ni ubeti gani kati ya ubeti wa kwanza na wa pili. Wakati wachezaji na viongozi wakianza ubeti wa pili ghafla vyombo vikazimwa na ukawa mwisho wa wimbo.

Ninachotaka kusema hapa ni kwa nini wimbo wetu wa Taifa upigwe ubeti mmoja pekee? Je, hili ni la makusudi au menejimenti ya CAF inajua wimbo wetu wa Taifa una ubeti mmoja?
Wimbo wa Afrika Kusini uliotafsiriwa kwa Kiswahili
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom