Tushauriane: Kuoa bila kuwa na misingi imara ni sawa na kutafuta kifo

pakamwam

JF-Expert Member
May 28, 2013
516
651
Heshima kwenu wakuu

Leo nimependa tushauriane kwenye mitazamo hii

Nianze tu kusema naamini kuoa/kuolewa bila kuweka misingi imara ya kuhakikisha maisha ya wawili au watatu yaani familia yanasonga ni sawa na kutafuta kifo au kuua

Ninaamini pamoja na ahadi zote mnazoweza kupeana na hasa mwanamke lazima tukumbuke hawa viumbe hawajaumbiwa shida.

Hakuna mwanamke anayependa kung'ang'ania mwendokasi maisha yake yote. Hakuna mwanamke anayependa kukaa na wakwe au kufia kwenye nyumba za wakwe, hakuna mwanamke anayependa kuishi bila kuwa na mji wake.

Tofauti na mafunzo mengi yanavyosema oa kupata ni majaliwa, mifano toka kwa jamaa wengi ukioa/kuolewa hujajipanga kimaishi, itakuchukua muda sana kufikia malengo na mara nyingine unaweza kupotea kabisa ndio maana nasema kama unafikiri elimu itakutoa kimaisha basi malizia elimu yako na pata chanzo ya hela ndio oa/kuolewa.

Kama ni biashara basi isimamishe vizuri na ndio oa/kuolewa na kama namalengo ya kujenga basi nunua kiwanja ndio anza hizo mishe

Kwa lolote lite mimi naamini, mipango yako ni rahisi kutimiza ukiwa peke yako kuliko mkiwa wawili.

Wenzangu mnalitazamaje hili?
 
Tafuta chapaa kwanza bro,weka uchumi vzr ndio uoe,tena oa mwenye akili,hata kama hana ajira,awe na ujasiriamali ndani yake,awe tayari kuchakalika na kuongeza kipato cha familia,
Chonde chonde mdogo wangu,usioe wale wanaoamini Kazi ya kutafuta ni ya Baba tu,yeye anaweka miguu juu,hata ushauri wa jinsi ya kupata pesa zaidi,hakupi!
Oa mwanamke ambaye yupo tayari 'to get dirty" ,katika kusaka pesa,ili maisha ya familia yawe bora,ambaye anawiwa,ana kiu ya kuweka uchumi wa familia vzr.Usiwe na haraka tafuta taratiiiibu.ukimpata huyo,umepata dhahabu.
Kinyume chake,utajuta kuzaliwa.I speak from experience !!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli unachosema. Kuna jamii ukizitembelea utaona maisha ya tofauti kabisa. Waishio mjini mambo ndio mengi
Shida kubwa inaanza pale ambapo huwa tunaiona tz kuwa inaishia dar "

Mkuu watu wengi wapo mikoani huko na wana enjoy maisha yao ' huku wakiwa hawana kitu ..nyumba za nyasi " maji ya mtoni" wana shindia mapapai ... maisha yanasonga

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha hayana formula.

Mara nyingi wanaoishi mijini ndiyo huwaza mawazo kama yako. Ila vijijini wanaoana bila hata ramani lakini wana-fight pamoja mashambani ndiyo wanatusua.

Mfano mzuri ni dadangu. Alikataa school akaolewa na jamaa hakuwa na A wala B, tena waliishi nyumba ya baba mdogo dah!

Ila leo hii wako vizuri financially, nyumba nzuri, maduka na mashamba hadi watu wanawaonea wivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
iwe mjini au vijijini huko,,maisha kabla ya ndoa lazima mwanaume ujiandae kiuchumi

wale mnaosema life halina formula mnatakiwa muelewe kwamba ndoa za vijana wengi siku hizi mjini na kijijini zinavunjika kwa sababu ya umasikini wa mwanaume

mwanaume tafuta pesa ndio uoe utaona raha ya uanaume wako
 
Kwani huyo mwanamke alivyokua nyumbani kwao alikua anapata shida au hapati? Haiwezekani mtu awe ameishi kwa shida kwa wazazi wake kisa umemuoa ndo ajifanyishe hapendi shida au hajazoea shida vitu vingine ni vya kawaida tu..shida zipo sehemu zote kwenye ndoa na hata nje ya ndoa wanaume tuachekuchukulia wanawake kwamba ni watu special saana...ndoa yako unaiharibu mwenyewe kwa jinsi unavyoiopelekesha...
 
nakuunga mkono 100%
ndoa Sio jambo la kulikimbilia
Una takiwa ujipange kiuchumi.
Kidogo hata uwe na kibanda.
Unaoa huku umepanga chumba kimoja.unaoa huna kazi ya maana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli unachosema. Kuna jamii ukizitembelea utaona maisha ya tofauti kabisa. Waishio mjini mambo ndio mengi

Sent using Jamii Forums mobile app
Saana " ndio maana tunashauriwa tutembee ili tuweze kujionea namna ambavyo maisha yalivyo " tunatofauti kubwa kwetu sisi watu wa mijini namna tunavyo ishi na jinsi ambavyo watu wa vijijini huishi pia ...

Kuna sehemu unaweza ukaenda (vijijini) zaidi ya kutumika kama nauli pesa haina umuhimu kabisa. Ukiwa na 10k unaweza kuitumia week nzima

So ukienda kwa watu wanaoishi kwenye mazingira haya ukianza kuwaambia habari za kuoana ni mpaka Sijui ujipange na blaa blaa kibao hawawezi kukuelewa katu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom