Tushauriane: Kuoa bila kuwa na misingi imara ni sawa na kutafuta kifo

Tafuta chapaa kwanza bro,weka uchumi vzr ndio uoe,tena oa mwenye akili,hata kama hana ajira,awe na ujasiriamali ndani yake,awe tayari kuchakalika na kuongeza kipato cha familia,
Chonde chonde mdogo wangu,usioe wale wanaoamini Kazi ya kutafuta ni ya Baba tu,yeye anaweka miguu juu,hata ushauri wa jinsi ya kupata pesa zaidi,hakupi!
Oa mwanamke ambaye yupo tayari 'to get dirty" ,katika kusaka pesa,ili maisha ya familia yawe bora,ambaye anawiwa,ana kiu ya kuweka uchumi wa familia vzr.Usiwe na haraka tafuta taratiiiibu.ukimpata huyo,umepata dhahabu.
Kinyume chake,utajuta kuzaliwa.I speak from experience !!!

Sent using Jamii Forums mobile app
umena na heshima kwako mkuu
 
Saana " ndio maana tunashauriwa tutembee ili tuweze kujionea namna ambavyo maisha yalivyo " tunatofauti kubwa kwetu sisi watu wa mijini namna tunavyo ishi na jinsi ambavyo watu wa vijijini huishi pia ...

Kuna sehemu unaweza ukaenda (vijijini) zaidi ya kutumika kama nauli pesa haina umuhimu kabisa. Ukiwa na 10k unaweza kuitumia week nzima

So ukienda kwa watu wanaoishi kwenye mazingira haya ukianza kuwaambia habari za kuoana ni mpaka Sijui ujipange na blaa blaa kibao hawawezi kukuelewa katu

Sent using Jamii Forums mobile app
kweli kabisa mkuuu
 
nakuunga mkono 100%
ndoa Sio jambo la kulikimbilia
Una takiwa ujipange kiuchumi.
Kidogo hata uwe na kibanda.
Unaoa huku umepanga chumba kimoja.unaoa huna kazi ya maana.


Sent using Jamii Forums mobile app
vijana wanasema eti muenze pamoja bila kitu. mimi nasema maisha ya wawili bila kitu ni taabu sana kuliko ya mmoja bila kitu. tena ndio ukute yuleee tege,ezi unaona rangi zote duniani
 
Maisha hayana formula.

Mara nyingi wanaoishi mijini ndiyo huwaza mawazo kama yako. Ila vijijini wanaoana bila hata ramani lakini wana-fight pamoja mashambani ndiyo wanatusua.

Mfano mzuri ni dadangu. Alikataa school akaolewa na jamaa hakuwa na A wala B, tena waliishi nyumba ya baba mdogo dah!

Ila leo hii wako vizuri financially, nyumba nzuri, maduka na mashamba hadi watu wanawaonea wivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
hizo kaka ni special cases au kwa lugha ya kitwakwimu tuanaita outliers
 
Sijali kuwa ukioa ni lazima uwe umejipanga

Ndoa kwangu ni suala la kiibada haswaaa

Nalifanya kwa ajili ya Allah na sio kutimiza matamanio yangu ni sunnah ya mtume wetu

So pale kwenye ugumu kutakuwa na wepesi
 
Kujiandaa huku kiuchumi ni kwa wanawake wa mjini na ujiandae pia kisaikolojia lazima wakutie uchizi. Wanawake wa vijijini madhali we mashine iko fiti owa hata kama kiuchumi hauko fresh, maisha yenu ya ndoa yataenda vizuri tu.
 
vijana wanasema eti muenze pamoja bila kitu. mimi nasema maisha ya wawili bila kitu ni taabu sana kuliko ya mmoja bila kitu. tena ndio ukute yuleee tege,ezi unaona rangi zote duniani
.mimi huwa siyawezi maisha ya namna hiyo ... kwanza nikiwa sina hela nakuwa hata genye sina pia
 
Sijali kuwa ukioa ni lazima uwe umejipanga

Ndoa kwangu ni suala la kiibada haswaaa

Nalifanya kwa ajili ya Allah na sio kutimiza matamanio yangu ni sunnah ya mtume wetu

So pale kwenye ugumu kutakuwa na wepesi
kwa imani yangu njaa na umaskini ni matokeo ya mipango mibaya na uvivu. biblia inasema asiyefanya kazi asile maana yake afe kabisa. kwa hiyo swala la kuhakikisha chakula cha familia kipo bila wasi wasi ni kazi yako mwanaume
 
Heshima kwenu wakuu

Leo nimependa tushauriane kwenye mitazamo hii

Nianze tu kusema naamini kuoa/kuolewa bila kuweka misingi imara ya kuhakikisha maisha ya wawili au watatu yaani familia yanasonga ni sawa na kutafuta kifo au kuua

Ninaamini pamoja na ahadi zote mnazoweza kupeana na hasa mwanamke lazima tukumbuke hawa viumbe hawajaumbiwa shida.

Hakuna mwanamke anayependa kung'ang'ania mwendokasi maisha yake yote. Hakuna mwanamke anayependa kukaa na wakwe au kufia kwenye nyumba za wakwe, hakuna mwanamke anayependa kuishi bila kuwa na mji wake.

Tofauti na mafunzo mengi yanavyosema oa kupata ni majaliwa, mifano toka kwa jamaa wengi ukioa/kuolewa hujajipanga kimaishi, itakuchukua muda sana kufikia malengo na mara nyingine unaweza kupotea kabisa ndio maana nasema kama unafikiri elimu itakutoa kimaisha basi malizia elimu yako na pata chanzo ya hela ndio oa/kuolewa.

Kama ni biashara basi isimamishe vizuri na ndio oa/kuolewa na kama namalengo ya kujenga basi nunua kiwanja ndio anza hizo mishe

Kwa lolote lite mimi naamini, mipango yako ni rahisi kutimiza ukiwa peke yako kuliko mkiwa wawili.

Wenzangu mnalitazamaje hili?

Kwa maisha ya sasa yalivyobadilika, mawazo yako yako sahihi Mkuu maana hiki kipindi tulichonacho na tunachopitia vijana wa sasa mambo yamebadilika sana.. bila kuwa na misingi mizuri ya kiuchumi ndipo uoe ni shida Juuuuu ya shida. Na mimi naongezea kwamba kwa kijana ni vyema kuanza kujipanga vizuri kiuchumi ndipo uchukue uamuzi wa kuoa.
 
Back
Top Bottom