Tusali....

Magehema

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
428
27
Eee Mungu baba wa rehema, asante kwa kuwa wewe ni mwema. Mungu/Allah/Yehova/Jah tumekuja kwako kukuomba yafuatayo.


Mola tunakuomba UWALAANI wale wote wanaojifanya kumuenzi Baba wa Taifa, huku wakijua fika ni longolongo tu, ndio hao hao walilivunja Azimio la Arusha, ndio hao hao wamechanganya siasa na biashara, ndio hao hao wamejimilikisha ranchi zilizoanzishwa na baba wa taifa, ndio hao hao wameleta ubaguzi katika elimu, leo tuna shule za Kanumba aka Msondo na FM Academia, Ee Mungu walaani!

Allah tunakuomba UWALAANI wale wote wanaoapa kwa kutumia kitabu chako kitakatifu (Biblia/Quran) kudai kwamba watailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wakati huo huo baada ya kiapo wanafanya kinyume na kiapo! Ndio hao wanawalinda wavunja sheria kwa madai “eti suala la Deepgreen, Meremeta ni masuala nyeti ya kiusalama ambayo hayafai kujadiliwa na Bunge, eti wanapata tabu na nyaraka mbali mbali za kutoa miongozo kuelekea uchanguzi, eti kwa kisingizio nchi yetu ni Secular State, wanasahau kwamba demokrasia sio Secular!

Yehova tunaomba washindwe na walegee, eti wanaogopa hata tangazo la Sidanganyiki wamefikia mahali wanalipiga marufuku, eti hawataki wananchi wapewe elimu ya uraia, taasisi nyingi zimenyimwa vibali vya kuendesha civic education mikoani bila sababu za msingi, eee Yehova tunaomba washindwe na walegee na watoe hivyo vibali!

Mungu tunakuomba upumbaze akili zao hasa wale ambao wana nia chafu ya kutaka kununua/kuhonga vyombo vya habari au waandishi ambao ni critical, watie uzuzu ili washindwe kufanya hivyo, tazama Mungu kwa takribani muongo mmoja tumepoteza waandishi ambao walikuwa very critical pamoja na vyombo vya habari. Ee Mungu watie uzuzu!

Mola tunakuomba uwatie UBUBU wale wanaojifanya nao wanapinga ufisadi huku moyoni wanabariki na kuwalinda mafisadi. Ni hao hao walikuja juu na kuikandia LIST OF SHAME iliyotajwa na Dr. Slaa pale Mwembeyanga, ndio hao hao walitishia eti kufungua mashtaka kwamba wamekashfiwa, ndio hao hao waliwaandalia wanaotuhumiwa kwa ufisadi mapokezi ya kishujaa katika majimbo yao, twakuomba MUNGU uwatie UBUBU pindi watakapojaribu kuzungumzia ufisadi kinafiki.
Endeleza sala hii….
 
Kumuomba mungu ni feel good therapy tu, you have to take care of your own business. Mungu mwenyewe hajawahi kuwepo hayupo na wala hatakuwapo.
 
Kumuomba mungu ni feel good therapy tu, you have to take care of your own business. Mungu mwenyewe hajawahi kuwepo hayupo na wala hatakuwapo.

Bluray umeshaanza kutokota kama kawaida yako
 
Kumuomba mungu ni feel good therapy tu, you have to take care of your own business. Mungu mwenyewe hajawahi kuwepo hayupo na wala hatakuwapo.

Hivi huyo Mungu ambaye hayupo, ni kivipi amekuwa Mungu mwenyewe?
 
Nitakuwa nikisali hii sala kila siku, Nimekumbuka wale jamaa waliosema watamshitaki Dr Slaa wako wapi?
 
Nitakuwa nikisali hii sala kila siku, Nimekumbuka wale jamaa waliosema watamshitaki Dr Slaa wako wapi?
Hata mimi nimewakumbuka. Nasikia walikwenda mahakamani wakakuta mlango umefungwa. Pia namkumbuka Rostum na kesi yake aliyoanzisha/aliyotaka kuanzisha dhidi ya Mengi. Naye aliishia njiani.
 
Mkuu bado wanaandaa mashtaka labda watafungua kesi 2015!

Nina chuki sana na mfumo tulionao Tanzania, usanii hata kwenye mambo ya Msingi, JK ni mzigo na wasaidizi wake ni kashata! issue ndogo hawezi amua ni kucheka tu na sasa anaumwa hali itakuwa mbaya zaidi!
 
Bluray umeshaanza kutokota kama kawaida yako

Hizi zinaitwa argumentum ad hominem.

Nimetokota wapi? Kivipi? Una ushahidi gani unaoweza kusimama dhidi ya uchambuzi mkali kwamba nimetokota?

Kati yangu niliyetoa msimamo unaoteteeka kutokana na observance ya phenomena na weye uliyerukia argumentum ad hominem nani anatokota sasa?

Sala zingekuwa zinafanya kazi Nyerere asingekufa, na wala nchi yetu isingekuwa na ukame.
 
eee mungu baba wa rehema, asante kwa kuwa wewe ni mwema. Mungu/allah/yehova/jah tumekuja kwako kukuomba yafuatayo.


mola tunakuomba uwalaani wale wote wanaojifanya kumuenzi baba wa taifa, huku wakijua fika ni longolongo tu, ndio hao hao walilivunja azimio la arusha, ndio hao hao wamechanganya siasa na biashara, ndio hao hao wamejimilikisha ranchi zilizoanzishwa na baba wa taifa, ndio hao hao wameleta ubaguzi katika elimu, leo tuna shule za kanumba aka msondo na fm academia, ee mungu walaani!

allah tunakuomba uwalaani wale wote wanaoapa kwa kutumia kitabu chako kitakatifu (biblia/quran) kudai kwamba watailinda na kuitetea katiba ya jamhuri ya muungano wakati huo huo baada ya kiapo wanafanya kinyume na kiapo! Ndio hao wanawalinda wavunja sheria kwa madai “eti suala la deepgreen, meremeta ni masuala nyeti ya kiusalama ambayo hayafai kujadiliwa na bunge, eti wanapata tabu na nyaraka mbali mbali za kutoa miongozo kuelekea uchanguzi, eti kwa kisingizio nchi yetu ni secular state, wanasahau kwamba demokrasia sio secular!

yehova tunaomba washindwe na walegee, eti wanaogopa hata tangazo la sidanganyiki wamefikia mahali wanalipiga marufuku, eti hawataki wananchi wapewe elimu ya uraia, taasisi nyingi zimenyimwa vibali vya kuendesha civic education mikoani bila sababu za msingi, eee yehova tunaomba washindwe na walegee na watoe hivyo vibali!

mungu tunakuomba upumbaze akili zao hasa wale ambao wana nia chafu ya kutaka kununua/kuhonga vyombo vya habari au waandishi ambao ni critical, watie uzuzu ili washindwe kufanya hivyo, tazama mungu kwa takribani muongo mmoja tumepoteza waandishi ambao walikuwa very critical pamoja na vyombo vya habari. Ee mungu watie uzuzu!

mola tunakuomba uwatie ububu wale wanaojifanya nao wanapinga ufisadi huku moyoni wanabariki na kuwalinda mafisadi. Ni hao hao walikuja juu na kuikandia list of shame iliyotajwa na dr. Slaa pale mwembeyanga, ndio hao hao walitishia eti kufungua mashtaka kwamba wamekashfiwa, ndio hao hao waliwaandalia wanaotuhumiwa kwa ufisadi mapokezi ya kishujaa katika majimbo yao, twakuomba mungu uwatie ububu pindi watakapojaribu kuzungumzia ufisadi kinafiki.
endeleza sala hii….

mweh !!!
 
kumuomba mungu ni feel good therapy tu, you have to take care of your own business. Mungu mwenyewe hajawahi kuwepo hayupo na wala hatakuwapo.

kila mtu na imani yake lakini unanitatiza na maneno yako
hii inaonyesha husali kabisa ..

Sijui ndo kizazi chenye imani haba hiki?
 
Kumuomba mungu ni feel good therapy tu, you have to take care of your own business. Mungu mwenyewe hajawahi kuwepo hayupo na wala hatakuwapo.

Tatizo lako hujawahi kukutana naye wala kumuona,hivyo waachie waliokutana nae na Mungu wao.
 
Maombi ya kuwalaani wengine au kuwaombea mabaya wale waliokukosea(maadui) imepitwa na wakati.
Kama kuna watu wanaotakiwa kuombewa kupita wengine basi ni viongozi.Kuwalaani haitasaidia bali waombewe wapewe hekima ya kuongoza kama akina King David na king Suleiman.
 
Kumuomba mungu ni feel good therapy tu, you have to take care of your own business. Mungu mwenyewe hajawahi kuwepo hayupo na wala hatakuwapo.

Sometimes it better keep quite, dont you think so?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom