tupo kwenye mahusiano huu ni mwaka wa saba bado hatujaoana.

DA, mimi silazimishi ushauriano unaoudhani kama ulivyoandika! I am a true follwer of the principle of consultation katika nyanja zote za maisha. Na hii haimaanishi kuwa siwezi kufanya maamuzi.

Sasa niliona kama umemaanisha uanamme ndo unatumika kuamua kana kwamba lisemwalo na mwanaume ndo ssahihi!

What if in this given scenario, huyo dada yeye ana mbumba? Wakishauriana si wanaweza tu kufikia uamuzi kuwa wafanye harusi ya kifahari?

Otherwise me and you are kinda in the same line!

wakuu nina umri wa miaka 32 male, na mwenzangu ana miaka 27: mwenzangu ni mpare mi mnyakyusa. tulianza mahusiano mwaka 2006; kabla hatujaanza mikakati ya ndoa nikaenda masomoni mwaka 2008. ikawa vigumu kuendelea na mchakato, lakini baada ya kumaliza chuo naona bado hakuna dalili ya kufunga ndoa hivi karibuni kwani mwenzangu anahitaji ndoa ya kifahari wakati mimi uwezo huo sina, inanibidi nifanye kazi sana ili nijiweke fiti kwa hilo. natamani saana kuwa na mke jamani
NISAIDIENI WAKUU UMRI UNAENDA.


@ BHT msome jamaa hapo kwenye red utamwelewa.

siku njema
 
We unaoa mke au unaoa sherehe ?
Kama unakosa maamuzi asubuhi (wakati hujaoa) ukioa ndiyo kabisa! Utakosa hata maamuzi ya kununua suruali. Mpaka uruhusiwe!
 
Kaka huyo wa bei ghali atusumbua kama hawezi maisha ya uwezo wenu utakalia kuti kavu.
Ongea nae mweleze hali yako kama hawezi tafuta mwngne.
 
Miaka saba katika mahusiano ni mingi.Lazima upime uzito wa tabia zake,umri wa tabia zake na madhara yanayotokana na tabia zake.Baada ya hapo ufanye maamuzi.Kuna uwezekano mkubwa huyu binti alikuwa mzuri wa tabia na asiye na makeke,ila kutokana na tabia za kuiga(westernisation),na tabia za mashosti anabadilika.Hivyo huna budi kupima mwenendo,mlipoanzia,mlipo na mwendako.Kuna vitu vingine vinarekebishika tu.
 
Unajitesa sanaaaaaaaaaaaa sijui kwanini,kama anakupenda kweli hawezi kutaka kitu ambacho huna uwezo nacho,au kama umemwambia wewe mtoto wa boss wa BOT hapo ndio utajiju! ebu jikune unapojifikia......
 
he,kwani anavokwambia anataka ndoa yakifahari inamaana hajui uwezo wako kifedha?pamoja na mapenzi ya muda wa miaka yote saba?:A S 465:
 
Huyo usimuoe mkuu bora muendelee kukaa kama mtu na gf/bf wake kwakuwa mmeshazoea hali hiyo.

Mkiingia kwenye ndoa tu hamtakaa sana mtaachana pengine hata mwaka msifike!
 
wakuu nina umri wa miaka 32 male, na mwenzangu ana miaka 27: mwenzangu ni mpare mi mnyakyusa. tulianza mahusiano mwaka 2006; kabla hatujaanza mikakati ya ndoa nikaenda masomoni mwaka 2008. ikawa vigumu kuendelea na mchakato, lakini baada ya kumaliza chuo naona bado hakuna dalili ya kufunga ndoa hivi karibuni kwani mwenzangu anahitaji ndoa ya kifahari wakati mimi uwezo huo sina, inanibidi nifanye kazi sana ili nijiweke fiti kwa hilo. natamani saana kuwa na mke jamani
NISAIDIENI WAKUU UMRI UNAENDA.
Huyo anayehitaji ndoa ya kifahari hata maisha atahitaji ya kifahari kwa hiyo uwe macho akitokea anayeweza funga ndoa ya kifahari unaweza mpoteza tafuta mwingine.
 
Mie mwanaume asiyekuwa na maamuzi huwa ananikera sana.
Utakuja kushindwa hata kufanya maamuzi ndani ya nyumba kisa mke???
Kwani anayeoa mwenzie ni nani?? Au wewe ndo unaolewa???

Fanya maamuzi na wewe ukiamua umeamua unangoja eti anataka ndoa ya kifahari???

Acha hizo bana sema nimeamua ndoa itafanyika hivi na hivi kwisha kama hataki huyo ana lake jambo??

Dena akisema hivi now,hii biashara itamkata.huu ndio utakuwa utaratibu wa maisha ya ndoa yao kwa maisha yao yote!!ni kitu kizuri kuwa na mahusiano safi ambapo mke anakuwa sio KITU bali mwenza wa kweli wa maisha.akifanya hivi sasa na akamuoa huyu dada,basi kila kitu chao baadae kitahitaji huyu jamaa kutumia ubabe kufanya maamuzi na niamini mimi,ndoa ya hivyo ni jehanamu ndogo in disguise.....naungana na wadau waliomshauri kuzungumza na mwenzake ili kujua vipaumbele vyake katika maisha,hasa ya ndoa ili kuweka msingi mzuri wa kanuni zitakazoongoza mahusiano yao ya ndoa hapoi baadae!
 
Back
Top Bottom