Tupige kidogo ‘mastori’ ya Mchungaji Christopher Reuben Mtikila

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,848
15,196
Kufuatia kauli aliyoitoa hadharani siku chache baada ya muasisi wa Tanzania, Julius Nyerere kufariki Oktoba 14, 1999 Mtikila alisema “Nyerere alifariki kwa ugonjwa wa UKIMWI, ni mzoga, nyamafu na ameenda jehanamu”.

Mtikila alisema maneno hayo siku zote za Maisha. Kesi hiyo ilifutwa. Kesi nyingine ya kutoa maneno ya uchochezi alivyoshitakiwa nayo Mtikila enzi za uhai wake ni Jamhuri dhidi ya Christopher Mtikila .

Mtikila alishtakiwa kwa kesi nyingine ya uchochezi ilidaiwa na upande wa jamhuri kuwa Mtikila akihutubia mkutano viwanja vya Jangwani Dar Es Salaam, Alisema maneno yaliyochapishwa Gazeti la Mtanzania

Miongoni wa mashahidi wa upande wa jamhuri alikuwa ni Mhariri wa gazeti Hilo Badra Masoud ambaye baadae aliajiriwa serikalini kuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari Cha Wizara ya Nishati na Madini na Askari Polisi pia.

Maneno yaliyotolewa na Mchungaji Christopher Mtikila ambayo upande wa Jamhuri ulidai ni maneno ya kichochezi ni; “Rais Benjamin Mkapa siyo Raia wa Tanzania ni Raia wa Msumbiji”.

Kesi iliunguruma na mwisho Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilifuta kesi hiyo dhidi ya Mtikila kwa sababu ilichukua muda mrefu kumalizika na mashahidi upande jamhuri ukawa hauleti mashahidi.

Wakati Kesi ikisikilizwa, mapolisi walipokuwa wakifika kutoa ushahidi, Mtikila alikuwa akiomba Mahakama isipokee ushahidi wa mapolisi wale kwa sababu wao sio Rais Benjamin William Mkapa.

Mtikila aliomba Mahakama itoe hati ya kumlazimisha Rais Benjamin William Mkapa kwa amri ya mahakama afike Mahakamani atoe ushahidi wake wa kupinga yeye siyo Raia wa Msumbiji.

“Rais Mkapa anaishi hapo SVU -Upanga, ni karibu na Mahakama ya Kisutu. Kwanini asipelekewe samansi maana ni karibu na anaweza kutembea hata kwa miguu aje akatae siyo Raia wa Msumbiji”

“Mimi ninao ushahidi Mkapa ni Raia wa Msumbiji ndio maana hana uchungu na taifa hili anauza viwanda vyetu kwa wazungu hovyo tu”. Alisisitiza Mchungaji Mtikila

Wakati Mtikila akitoa maombi hayo amesimama kizimbani Mkapa akiwa bado ni Rais wa nchi, waandishi waliokuwa wameketi mahakamani wanafuatilia Kesi hiyo walikuwa wanainama wakicheka bila kutoa sauti.

Kesi nyingine ya uchochezi Na.132/2011. Mtikila alidaiwa kutoa maneno ya uchochezi na kashfa dhidi ya Rais Kikwete kwa kumuita ‘gaidi’ serikali anayoiongoza inataka kuanzisha Mahakama ya kadhi,

kati ya Januari 2009 na Aprili 17, 2010 jijini DSM kwa nia ya uchochezi mshtakiwa alisambaza kwa umma nyaraka zilizosema “Kikwete kuuangamiza ukristo”, wakristo waungane kuweka mtu Ikulu”

Katika shtaka la pili, Aprili 16, 2010 eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam, bila kibali alikutwa akimiliki waraka wenye uchochezi kwa jamii. Katika kesi hii Mtikila hana wakili wa kumtetea na anajitetea mwenyewe.

Polisi walivamia nyumbani kwa Mtikila alfajiri kufanya upekuzi kwa kusaka waraka huo na kumkamata, mke wa Mtikila. Kesi hiyo ambayo ilisikilizwa na Mahakimu watatu tofauti.

Mahakimu wote watatu walilazimika wajitoe katika kuendesha kesi hiyo kwa sababu Mchungaji Mtikila aliwaomba mahakimu wawili wajitoe kwa sababu anaamini hawana hadhi na hawawezi kumtendea haki.

Akapangiwa Hakimu Mfawidhi kwa Elvin Mugeta aliisikiliza kesi hiyo na Septemba 25, 2012, alitoa hukumu ya kumuachilia huru Mtikila baada ya upande wa jamhuri kushindwa kuthibitisha uchochezi.

Mtikila kizimbani alipaza sauti mahakamani “Hallelujah”. Wafuasi wake walishangilia. Polisi wenye vyeo vya chini walijipanga nje wakataka kumuweka chini ya Ulinzi, aliwaeleza maneno yaliyosababisha jaribio la Polisi kufutika

“Polisi hamna uwezo wa kunikamata mnavyo vyeo vya chini sana.... Kama mnataka kanifungulia kesi nitakwenda polisi mwenyewe. Hata boss wenu IGP Mwema ananiita kwa heshima kwa kunipigia simu, toeni ujinga wenu hapa”

Alisema Mtikila na watu kuangua vicheko na Polisi wale waliokuwa wamepanga kumkamata kumuacha Mtikila aende zake nyumbani akapumzike huku wafuasi wake wakiimba “saa ya ukombozi ni sasa”

Kesi hiyo ya kumtolea kashfa Rais Jakaya Mrisho Kikwete mwanzo alipangiwa Hakimu Mkazi Waliarwande Lema, Januari 11, 2010 alitoa amri ya kumfutia dhamana Mtikila kwa madai ya kushindwa kujiheshimu.

Amri ya kumfutia dhamana ilitolewa na Hakimu Waliarwande Lema baada ya kusikiliza utetezi wa mshtakiwa aliyefika mahakamani saa tano asubuhi akiwa amechelewa na alijikuta akikamatwa na askari polisi.

Mtikila alipaswa kufika mahakamani hapo majira ya saa tatu asubuhi wakati kesi hiyo ilipotajwa, lakini hakuwepo, ndipo Wakili wa Serikali, Beatrice Mpangala aliomba hati ya kukamatwa kwa mshtakiwa.

Kabla ya Mtikila kukamatwa, alieleza mahakama kwamba alidamka mapema na kumtafuta daktari wake aliyemtaja kwa jina moja la Katembo, ambaye alimfanyia upasuaji baada ya kugongwa na nyoka aina ya COBRA.

Mchungaji Christopher Reuben Mtikila alieleza mahakam hiyo mbele ya Hakimu mkazi Waliarwande Lema kwamba aligongwa na COBRA wakati alipokuwa katika shughuli za kidini nchini Zimbabwe mwaka 2009.

Mtikila alisema alijitahidi kuwatafuta wadhamini wake ili wafike mahakamani kwa niaba yake, lakini hakuweza kuwapata, ndiyo maana alikuja mwenyewe mahakamani hapo akiwa na maumivu makali mwilini mwake.

Hata hivyo hakimu waliarwande Lema alieleza kutoridhishwa na utetezi huo wa mchungaji Christopher Reuben mtikila na kuamuru Mtikila atupwe rumande hadi Januari 25, 2010 kesi yake itakapotajwa tena ndiyo atarudishwa.

Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa Mchungaji Mtikila kushindwa kufika mahakamani wala wadhamini wake. Mara ya kwanza ilikuwa Oktoba 22, 2009. Mchungaji Mtikila alikuwa akikabiliwa na kesi hiyo ya uchochezi Na.132/2011

Ilipofika saa saa tano mchana, Mtikila aliwasili mahakamani hapo anashuka Kwenye Bajaji, marafiki zake waandishi wa habari wakamuwahi kule kule Kwenye bajaji na wakampa taarifa Kuwa

Hakimu mkazi waliarwande Lema alitoa Hati ya Mchungaji Mtikila kukamatwa hivyo mapolisi Wakimuona watamkamata. Utetezi wake huo haukumsaidia Mtikila ,Hakimu Lema aliamuru aepelekwe mahabusu.

Mtikila alienda mahabusu na alipotoka alipiga simu kuwajulisha watu wake kuwa anakusudia kuwasilisha ombi la kumkataa Hakimu Lema ajitoe Kwenye Kesi yake kwa sababu Hana utu na Hakimu Lema alijitoa .

Kesi ilipohamishiwa kwa Hakimu Sundi Fimbo pia, Mtikila kupitia barua yake alimuomba hakimu Fimbo ajitoe kwenye kesi yake kwa sababu amebaini hawezi kumtendea haki katika kesi hiyo.

katika kesi hiyo aliwasilisha ombi la kuomba usikilizwaji wa kesi hiyo usimame hadi kesi ya Kikatiba mbele ya Jopo la Majaji wa tatu wa mahakama Kuu wanaongozwa na Jaji Fakhi Jundu na Profesa Ibrahim Juma isikilizwe.

Ambapo katika kesi hiyo anaiomba Mahakama hiyo izifute sheria za makosa ya uchochezi kwa kuwa zinanyima haki wananachi ya kutoa maoni yao itakapotolewa uamuzi lakini hakimu huyo alilikataa ombi la mtikila.

Mchungaji Christopher Reuben Mtikila kupitia barua yake alisema kwamba kuna kesi tatu za Kikatiba zilizokuwa zimefunguliwa mahakama kuu na washtakiwa wanaokabiliwa na kesi za jinai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Aliwataja washtakiwa hao ambao ni Jayantkumar Patel ‘Jeetu Patel’, Profesa Costa Mahalu na mahakama ya Kisutu ilisitisha usikilizwaji wa kesi zinazowakabili hadio mahakama kuu ilipozitolea uamuzi kesi zao za Kikatiba.

“Na huyu Hakimu Sundi Fimbo anafahamu fika nimefungua kesi ya Kikatiba Mahakama Kuu kuzipinga sheria za uchochezi ambao sheria hizo ndizo zimetumika kunifungulia kesi ya uchochezi iliyopo mbele yake,”

“kesi ya aina hiyo ikishafunguliwa mahakama ya juu, mahakama ya chini inatakiwa isitishe usikilizaji hadi mahakama hiyo ya juu itakapotoa uamuzi lakini amelikataa ombi langu na kwa kitendo hicho amevunja mwenendo wa kesi”

“ukiukwaji wa maadili ya sheria za nchi na haki na nimuomba ajitoe kwenye kesi yangu kwani tayari ameishaonyesha hawezi kunitendea haki ”alidai Mchungaji Christopher Reube. Mtikila katika barua yake kwa msajili wa mahakama

Mtikila alidai sababu nyingine ya kumkataa hakimu Fimbo, ni kwamba wakati kesi hiyo ikiendeshwa aliwai kuwasilisha ombi kutaka afutiwe kesi hiyo ya uchochezi kwa sababu kesi hiyo ilifunguliwa nje ya muda

kwani kesi za uchochezi zinatakiwa zifunguliwe mahakamani ndani ya miezi sita tangu mshtakiwa alituhumiwa kutenda kosa hilo na kwamba kesi hiyo inafanana na kesi ya madai ya fidia Na.166/2004 inayosikilizwa na Jaji Robert Makaramba,

Ambapo katika kesi hiyo anamdai Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa alikamatwa kinyume na sheria na kwamba kesi ambayo nayo ni ya uchochezi iliyokuwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ilifunguliwa nje ya muda.

Na kweli Ilipofika Machi 22, 2013 Hakimu Fimbo alitangaza kujitoa kusikiliza kesi hiyo ikapangwa kwa Hakimu Elvin Mugeta ambaye aliisikiliza kesi hiyo hadi akatoa hukumu ya kumwachilia huru Mtikila.

Mtikila alipotoa utetezi wake, kama kawaida alikanusha madai ya upande wa jamhuri kuwa ule waraka wake uliokuwa na kichwa cha Habari kisemacho (KIKWETE KUANGAMIZA UKRISTO) kuwa ni wa uchochezi,

Mchungaji Christopher Mtikila alikubali kuwa ule waraka ni wake na aliundaa yeye na siyo wa uchochezi na kwamba hawezi kuukana waraka ule kwa sababu kuukana waraka ule ni sawa na kumkana YESU KRISTO.

Mtikila alijipambanua wazi kupambana na serikali ya Jakaya Kikwete na hakuogopa kumtaja hadharani. Mashambulizi yake aliyaita mabomu ya Hiroshima dhidi ya serikali ya ‘msanii’ Rais Jakaya Kikwete.

Mchungaji Christopher Reuben Mtikila kabla na baada ya Kikwete awe Rais, alikuwa akimuita Kikwete ni ‘RAIS MSANII’, Reginald Mengi, Rostam Aziz na wengine aliwajumuisha katika kundi hilo la wasanii.

Juni 2013, Mchungaji, Christopher Mtikila, aliibwaga serikali katika kesi Na. 09 na 011/2011, aliyokuwa ameifungua Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika (AfCHPR) kutaka kuruhusiwa kwa mgombea binafsi, ikiwamo Rais

Mtikila alifungua kesi (AfCHPR) baada ya Juni 17 2010, Mahakama ya Rufani ya Tanzania, kutoa hukumu ya rufaa ya Madai Na. 45/2009 ambayo ilifunguliwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Mchungaji Christopher Mtikila.

Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Tanzania ambaye alikuwa akitetewa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania ambaye baadae alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju

Katika rufaa hiyo alikuwa akiomba Mahakama kutengua hukumu ya Mahakama Kuu katika kesi ya madai Na.10/2005 mbele ya jopo la Majaji Amir Manento, Salum Massati na Thomas Mihayo ambayo ilitangaza Ibara ya 39, 67, 77 zinavunja Haki ya za watu

Kwamba, kupitia kuvunjwa kwa hizo ibara za katiba ya Jamhuri ya muungano wa tanzania wasiokuwa wanachama wa vyama vyovyote vya siasa kugombea Urais na hivyo hukumu ile ikaruhusu mgombea binafsi.

Juni 17, 2010 jopo la Majaji saba wa Mahakama ya Rufani likiongozwa na Jaji Mkuu Augustino Ramadhani, walitoa hukumu ambapo walitengua hukumu ya Mahakama Kuu kwamba Mahakama haina mamlaka ya kutunga Sheria,

Mhimili wenye mamlaka ya kufanyia marekebisho Katiba ni Bunge hivyo suala la kuwepo kwa mgombea binafsi litapelekwa bungeni kwasababu mhimili wa Mahakama haina mamlaka ya kufanyia marekebisho Katiba ya nchi.

Ieleweke kuwa Katiba ya Tanzania hadi sasa hairuhusu kuwepo kwa mgombea binafsi kwa sababu Ibara ya 39(1) (c) inasomeka hivi : “(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa”

Hukumu ya rufaa mgombea binafsi ilipotolewa Mtikila alikasirika sana na alihojiwa na vyombo vya habari na alikuwa akisema majaji wote saba waliokataa kuhurusu mgombea binafsi ni Yuda Eskarioti ni vibaraka wa serikali.

Kesi nyingine ya mchungaji Christopher Mtikila ni ile Kesi ya Madai ya fidia ya Sh. Bilioni Moja ambayo anataka Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dk. Valentino Mokiwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Katika Kesi hiyo Mchungaji Mtikila alidai Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dk. Valentino Mokiwa alimdhalilisha kwa kumshika makalio Mtikila na kwamba kitendo hicho kilichotokea Juni 25 2013 ni udhalishaji.

Mchungaji Christopher Mtikila alikuwa ameitwa na Askofu kujadili tamko la la Mtikila kwamba Kanisa la Anglican linajihusisha na ufisadi, ukiwemo wizi wa vifaa vya Hospitali ya Mission ya Millo iliyoko Ludewa mkoani Njombe.

Mtikila alisema alivyoitwa na Askofu Mokiwa ili kujadili hilo alifika na wenzake watatu wa taasisi ya Liberty International Foundation na wakakaribishwa kwenye moja ya jengo la dayosisi ya St. Nicholaus, usiku wa saa 03:00.

“Muda mfupi baada ya kikao kuanza, Askofu Valentino Mokiwa ambaye alikuwa na wenzake saba, alisimama na kuwataka wajumbe wote wakaguliwe kama kuna mtu ana kinasa sauti.” Hayo ni maelezo ya Mtikila

“Askofu Mokiwa alisimama na kuungana na wenzake kutukagua baada ya kuhakikisha mlango umefungwa.Katika upekuzi huo ndipo tuhuma hizo zilipopatikana, operesheni hiyo ilienda mbali zaidi ya lengo la kawaida.”

“Askofu Valentino Mokiwa alianza kupenyeza mikono yake kwenye shingo yangu kuelekea chini kisha huko chini mikono ya mlalamikiwa ilionekana waziwazi ikipapasa makalio ya yangu” alidai Mchungaji Mtikila .

Mtikila aliomba Mahakama imuamuru Askofu Mokiwa amlipe kiasi hicho cha fidia kwa sababu alimdhalilisha na alimletea madhara zaidi ya kitendo hicho ni pamoja na mfadhaiko, masikitiko, wasiwasi, aibu katika jamii

Mchungaji Christopher Mtikila alikwenda mbali zaidi katika madai yake na kusema kwamba baadabya ukaguzi alipata shinikizo la damu la mara kwa mara na matatizo ya moyo kila anapokumbuka kitendo hicho.

Mtikila alisema ana shauku kubwa siku ifike aanze kutoa utetezi katika kesi hiyo maana atavua nguo zote na huyo wakili wa Mokiwa atakuwa tayari kunishuhudi mzee wake nikivua nguo zote mahakamani kumuonyesha makalio yangu

Maana akinishuhudia nipo uchi nikimuonyesha hakimu makalio yangu atakuwa amepata laana huyo wakili wa Askofu Mokiwa ambaye ni kijana wangu. Basi wafuasi wake na waandishi wa habari wanafurahi kweli, wakisubiri kesi kuanza.

Mtikila alitaka Scotland Yard lifike Tanzania, kuchunguza kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba aliyefariki ghafla. Mtikila aliamini Kolimba aliuwawa na CCM. Ilifunguliwa Kesi, Mahakama yaKinondoni Dar Es Salaam,

Hakimu Gabriel Mirumbe (ni marehemu kwa sasa ambapo alipofariki Mtikila alisema amefuraishwa na kifo hicho kwa sababu hakimu huyo alimfunga gerezani kwa kumuonea kifungo cha mwaka mmoja gereza la Keko.

Mtikila aliwahi kuomba Mahakama ya Kisutu itoe amri ya kutolewa rumande (Habeas corpus) lilowasilishwa mahakamani hapo na Wakili wa kujitegemea Hurbet Nyange dhidi ya Jamhuri Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Nyange alikuwa akimtetea aliyekuwa mgombea Urais Burundi na Mtangazaji (Radio Publique Africaine) Burundi, Alexis Sinduhije. Alikuwa ni rafiki wa Mtikila na aliposhindwa uchaguzi nchini Burundi alikimbilia Tanzania kujificha.

Serikali ya Burundi ilimsaka Alexis Sinduhije kwa kutenda makosa ya jinai wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu Burundi. Alikamatwa na Interpol ili jamhuri iwasilishe ombi la Mahakama itoe Kibali cha kumrejesha Kwao (extradition request)

Mwaka 2007, Alexis Sinduhije aliacha uandishi wa habari ili kugombea Urais wa Burundi, lakini alikamatwa mwaka wa 2008 kwa shtaka la "kumtusi Rais," Pierre Nkurunziza, hakupatikana na hatia na kuachiliwa mnamo 2009

Filamu ya "Kamenge, Northern Quarters" inaeleza uhalisia wa maisha ya Alexis Sinduhije kabla, wakati na baada ya kufungwa kwake. Mwanasiasa na mwanahabari aliyelazimika kuondoka nyumbani kwake Kamenge kimya kimya.

Mchungaji Christopher Mtikila alikuwa akifika katika Mahakama hiyo na kujaribu kukaa karibu na eneo la mahabusu ya Mahakama hiyo lakini Askari Magereza walikuwa wakimtimua wakimtaka akae mbali na eneo hilo.

Waandishi wa habari walikwenda kuchekea mbali Mtikila asiwaone maana angewaona wanacheka angewashughulikia kwa maneno makali. Mwisho wa siku Mahakama ilitoa Kibali cha Alexis Sinduhije kurudishwa Burundi.

Mahakamani, Mtikila alikuwa anasema yeye anataka Sinduije abaki Tanzania kwa sababu endapo atarudishwa Burundi, serikali ya Burundi itaenda kumkata kichwa Sinduije. Hivyo akaiomba mahakama ilinde haki ya kuishi ya Sunduije

Mtikila alilipachika jina la “Mgodi” Kesi zote za madai alipokuwa amezifungua. Alisema jina la mgodi kwa sababu anaamini atashinda na akishinda na Mahakama itaamuru wadaiwa wamlipe fidia ya fedha kwa hiyo Fedha ndiyo mgodi.

Sebuleni kwa Mtikila makochi na meza zilikuwa zimepambwa na vitambaa vya kufumwa rangi za Bendera ya Tanganyika. Nje ya nyumba yake alitundika Bendera ya Tanganyika maana alikuwa akiamini na kuipenda Tanganyika.

Mtikila alilipenda sana vazi la suti na muda mwingi katika harakati zake alikuwa akivalia vazi hilo la suti na suspendeer. Miaka ya nyuma alienda Marekani Kwenye mkutano wa watumishi wa Mungu akiwa bado hajaanza kuvaa suspenders.

Huko aliwakuta watumishi wenzake wa Mungu, wakiwa wamevalia vazi la suspenders na aliwauliza kwanini wanapenda kuvaa suspenders. Walimueleza wanapenda kuvaa hivyo kwa sababu wao hupenda kufunga ili wawe karibu na Mungu

Wanapomaliza kufunga, uzito hupungua na kusababisha nguo kuwapwaya na kuwaletea Usumbufu wa kwenda kwa fundi kupunguza nguo. Kuondokona na tatizo hilo la kupeleka kwa fundi kupunguza nguo, wanaamua kuvaa suspenders

Mtikila alikuwa na komputa na printa nyumbani kwake tangu alipokuwa akiishi Ilala na Mikocheni na alikuwa na chumba chake kimoja amekitenga kama ofisi ambacho alikuwa akikitumia kufanyia shughuli zake.

Alikuwa ametenga kufanya shughuli ikiwemo shughuli kubwa aliyokuwa akiipenda sana ya uandishi wa nyaraka mbalimbali ambazo zimebeba maovu ambayo ameyachunguza na kuyabaini. Alitumia maisha yake vizuri.

Licha nyaraka zake hizo za maovu aliyokuwa anadai ameyagundua yalikuwa na maneno makali ambayo wahariri wengi waliogopa kutumia habari zinatokana na nyaraka zile alizokuwa akiziandika.

askari polisi pindi wapatapo taarifa za siri kuwa Mtikila anaandaa waraka mbalimbali za kuja kuwavua nguo viongozi wa serikali, walivamia nyumba yake asubuhi na kufanya upekuzi ndani ya nyumba yake.

Askari hao walipofika nyumbani kwake kwa ajili ya upekuzi walimueleza kwamba nyaraka zingine azifiche ili asiwe na Kesi nyingi. Walipenda kazi yake ya kukosoa serikali na kutetea jamii na maslahi ya kazi zao za upolisi.

kuna siku alifika getini Ofisi za Msajili wa Vyama Vya Siasa akiwa John Tendwa, Mlinzi aliyekuwa akilinda zamu walipishana Kiswahili (lugha) na Mtikila, Mtikila alimchapa vibao vya kutosha.

Baadhi ya wahariri wa vyombo vya Habari walifanya kikao na walipitisha azimio la kutochapisha habari zinazotolewa na Mtikila, Mtikila alivyopata taarifa hizo alitembelea baadhi ya vyombo Vya Habari.

Huko aliwakuta wahariri na kuanza kuwasemea hovyo katika ofisi zao. Mtikila aliwaambia waache kujipendekeza kwa watawala, watumie nguvu zao nyingi kutetea haki na maslahi ya jamii siyo watawala.

Mtikila alikuwa anasema Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, siyo Raia wa Tanzania, ni Raia wa Iran na anaitwa "Sakalili" na alikuwa akifanya biashara ya ngozi eti ni mtu hatari sana. Mtikila alisisitiza hivyo wakati wote.

Mtikila alifungua kesi nyinginne ya Kikatiba kuomba Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), apunguziwe mamlaka kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya 2002, DPP amepewa mamlaka makubwa sana

Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya 2002 Kifungu 91(1) cha Sheria hiyo kilitoa madaraka kwa DPP kumfutia Klkesi mshtakiwa wa kesi ya jinai bila kuhojiwa na mtu wala taasisi yoyote ile.

Pia, Mchungaji Christopher Reuben Mtikila alifungua kesi nyingine Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, akiomba Mahakama Kuu ya Tanzania izuie uuzwaji wa jengo la Mahakama ya Rufani Dar Es Salaam.

Maana kulikuwa na tarifa kuwa uongozi wa mahakama una mpango wa kuliuza jengo hilo la Mahakama ya Rufani ambalo ni jengo la kihistoria ambalo zamani jengo hilo lilikuwa likijulikana kama Forodhani Hoteli.

Mtikila alifungua kesi Na.14/2015 kupinga muswada wa mabadiliko ya sheria kuitambua Mahakama ya Kadhi. Muswada huo ulipangwa kuwasilishwa, kujadiliwa bungeni lakini haukuweza kuruhusiwa kujadiliwa bungeni tena.

Mtikila ni muasisi wa neno la “Magabacholi”, Wahindi ambapo Mtikila alitaka Wahindi wote wanaokaa Katika maghorofa ya NHC Katikati ya Jiji la Dar Es Salaam waondolewe na Watanganyika ndio waishi katika maghorofa hayo.

Kutokana na ujasiri na misimamo mikali aliyokuwa tangu zamani yalisababisha kutengenezewa kwa propaganda yakuwaaminisha Watanzania wapuuze yote yanayosemwa na Mtikila kwa sababu Mtikila ni kichaa.

Mwanzoni propaganda hiyo iliwangia watu waliikubali ila kadri siku zilivyokuwa zinaenda watu walipuuza propaganda hiyo na kusema Mtikila ni mzima siyo chizi anasema ukweli ila serikali haitaki kusikia ukweli huo

Hatua ya Mtikila kwenda mahakamani Mara kwa Mara Kufungua Kesi mbalimbali dhidi ya serikali, na serikali kumfungulia Kesi za jinai Mtikali mahakamani, pia kulisababisha kukuza Utawala wa Sheria nchini.

Aidha baadhi ya Kesi zilizofunguliwa na Mtikila zimekuwa zikitumiwa na wahadhiri wa Sheria Katika Vyuo Vikuu kufundishia wanafunzi wa kozi ya Sheria hususani katika somo la Sheria ya Katiba (Constitution Law).

Wahadhiri wa fani ya Sheria wamekuwa wakifundisha masomo mbalimbali ya Sheria ikifika somo la Sheria ya Katiba, wahadhiri hao huelekeza wanafunzi wa Sheria wasome na kuelewa Kesi ya Mtikila one na Mtikila Two.

Mtikila one ni kesi Na.10/2015 ambayo Mahakama Kuu iliruhurusu mgombea binafsi. Mtikila Two ni rufaa ya Madai Na.45/2009 Mahakama ya Rufaa ilitengua hukumu ya Mahakama Kuu iliyoruhusu uwepo wa mgombea binafsi.

Kesi za kikatiba nyingine alizowahi kuzifungua ni pamoja na kesi ya wananchi wa Tanzania Bara kuruhusiwa kwenda Zanzibar bila pasipoti na vyama vya siasa kuruhusiwa kufanya mikutano bila kuomba kibali toka kwa Mkuu wa Wilaya na polisi.

Chama chake cha Democratic Party (DP). hakikuweza kupata usajili wa kudumu kutokana na Mchungaji Mtikila kutoitambua Zanzibar. Alikuwa akisisitiza kuwa chama chake ni cha Tanganyika na si Tanzania ambayo haipo.

Mchungaji Christopher Mtikila alibadili msimamo wake katika miaka iliyofuata kwa kukubali kutafuta wanachama toka Zanzibar (kama sheria ya uchaguzi inavyotaka) na hivyo chama chake kuweza kupata usajili wa kudumu.

Katika sherehe za siku ya Sheria Mtikila alikuwa alishiriki Katika sherehe hiyo kwasababu naye ni mdau wa Mahakama na Mara zote alikuwa akishangiliwa umma ambao umekuwa umeshiriki Katika maadhimisho hayo.

Mtikila alikuwa Akizungumza lugha ya Kiingereza kwa ufasaha utafikiri kazaliwa Buckingham Palace. Na pindi azungumzapo lugha hiyo ya Kiingereza alipenda sana kutamka sana neno hili la Kiingereza “WELL”

Mtikila asubuhi alifanya mihadhara ya kisiasa viwanja vya Mnazi Mmoja, mchana anaondoka kwa maandamano na umati wake, wanakwenda kufanya mkutano wa hadhara viwanja vya Jangwani. Watu wanakula darasa.

Mtikila hajawahi kusomea sheria popote lakini aliyekuwa Msajili wa vyama vya siasa, Christopher Lihundi, nyakati za jioni, mwanzoni mwa Miaka 1990 walikuwa wakakutana na Mtikila sehemu anamfundisha kuvisoma vifungu

Msajili wa vyama vya siasa, Christopher Lihundi, alimfundisha kusoma hivyo vifungu na Ibara za Katiba na kumuelimisha zilikuwa zinataka afanye nini na jinsi ya kuzidai Haki zake. Mtikila akajikuta amekwiva kweli.

Mtikila aliwahi kusema Mawakili Richard Rweyongeza na Mpare Mpoki walikuwa msaada mkubwa kwake kwa sababu ndio walikuwa wakijitolea kumpa msaada wa kisheria hata kama alikuwa hana fedha zakuwalipia.

Sifa moja ya Mtikila, ambayo ilimfanya waandishi wengi wa habari wampende sana, hata siku Moja hawezi kumruka mwandishi aliyeandika taarifa inayomnukuu Mtikila. Hawezi kusema hajampa hiyo taarifa akishtakiwa mahakamani.

Mtikila alikuwa na mchezo wakuandika waraka kuhusu tuhuma za mtu fulani kwa maneno makali kisha anaitisha mkutano na waandishi wa Habari. Badhi ya vyombo ya Habari vilisita kutumia waraka kwa sababu maneno makali.

Baada mitandao ya kijamii kuanza kutumika kwa wingi na ukubwa kidogo nchini Tanzania, Mchungaji Mtikila alichokuwa anafanya, anaandaa waraka wake kisha anawatumia watu Kwenye email zao wasome wenyewe na kusambaza.

Mtikila alikuwa hajui kuficha hisia zake, anawapasha ukweli waandishi wa Habari hawataki kutoa Habari na kuhudhuria mikutano yake na waandishi wa Habari kwa sababu chama chake ni maskini Hakina uwezo wa kuwapatia “mshiko”

Wakati Mtikila anapambana Mahakama Kuu kanda ya Dodoma na Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam kutaka mgombea binafsi aruhusiwe walikuwa Wakimuona Mwendawazimu na wala walikuwa hawa thamani,

Lakini siku Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, iliporuhusu uwepo wa mgombea binafsi, wale wote waliokuwa wakimuona Mchungaji Christopher Mtikila ni chizi walianza kumthamini na kumuona Mtu wa maana sana.

Mtikila alikuwa mwanzilishi na mkuu wa kanisa la Kipentekoste la Full Salvation Church.alijihusisha pia na harakati za haki za binadamu kwa kupitia kitengo cha haki za binadamu cha kanisa hilo kiitwacho Liberty Desk.

Mchungaji Christopher Mtikila alifariki Oktoba 4, 2015 kwa ajali ya gari, Msolwa, Chalinze mkoani Pwani wakati akitoka kwenye shughuli za kisiasa, alizaliwa June 9, 1950. Mtikila alizaliwa Iringa, Tanzania.

Cc: Martin Maranja Masese, MMM.
 
Mandela alimtaja katika harakati zao,kwamba reveland alipiga kazi, viongozi wa waasi wa fdlr waliopo DRC walikuja,wakafikia kwake,kifo chake hakishangazi
Ni kweli alipoanza kuongelea mambo ya bwana slim ndo akaenda?
 
Hongera kwa kutoa credit kwa mwandish
 
Nilikuwa bado sijajipata sana wakati mtikila anakimbiza mjini. Nilikuwa pia simjui vzr ila huu unanipa mwanga kwamba alikuwa afisa kipenyo. Huwezi challenge mihimili halafu ukaendelea kidunda mitaani tu kirahisi rahisi
 
Mtikila alikua afisa kipenyo,usihadaike na mengine,ukifanya nusu ya aliyofanya mtikila utaishi jela milele
Sidhani kama kuna ukweli kuhusu suala hili, lakini hata kama ni kweli kwamba alikuwa Afisa Kipenyo, Basi alikuwa Afisa anayejitambua sana na Mwerevu, huwezi kumfananisha na Afisa mwingine yoyote yule ktk historia ya kada hiyo.

Mandela alimtaja katika harakati zao,kwamba reveland alipiga kazi, viongozi wa waasi wa fdlr waliopo DRC walikuja,wakafikia kwake,kifo chake hakishangazi
Ni kweli alipoanza kuongelea mambo ya bwana slim ndo akaenda?
Hizo zilikuwa ni 'Spinning Propaganda' tu za wale waliopanga Mpango wa Mauaji yake, yule amekuwa 'eliminated if not assassinated' kutokana na hizi harakati zake za 'Kupigania Haki,' alionekana Kama 'msumbufu' kwa 'wenye nchi.' Alikuwa 'eliminated' kwa tuhuma zinazodaiwa kuwa ni 'alikuwa mtata Sana,' 'anaisumbua mamlaka,' na tuhuma za kwamba 'alikuwa siyo mtiifu kwa mamlaka'.

Aliondolewa pamoja sambamba na wale watu wake wa karibu ambao nao 'Wadhalimu" waliowaona Kama "Mentors" wake kwenye suala zima la harakati zake za 'Kupigania Haki' na kuzidai kwa vitendo. Baada ya kuwa Mchiungaji na Mentors wake kuwa 'eliminated' ndipo zilitungwa 'Spinning Propaganda' nyingi zikiwa kama "Cover Story" ili kuwazuga watu na kuwatoa kwenye reli makusudi ili kuwapoteza maboya wasijue vyanzo halisi vya vifo vyao.
Kuna gharama kubwa Sana ktk kudai au Kupigania Haki, hususani kwenye hizi nchi zetu zenye tawala za 'mabavu.'

KUMBUKA NA MUHIMU KUZINGATIA:
'Ukiwa mkweli Sana, mnyoofu, mpinga wizi, rushwa, ufisadi, na dhuluma, tambua ya kwamba kwako Afrika siyo mahali salama pa kuishi.

RIP Mchungaji Dkt. Christopher Mtikila.
RIP Dkt. Sengondo Mvungi.
RIP Prof. Juan Mwaikusa.
 
Kuna kisa kimoja cha mtikila

mtikila alikuwa amepanda BASI(daladala) usishangae mtikila kupanda DALADALA alikuwa ni mtu anayejichanganya na JAMII na very humble hakuwa na makuu kabisa unless uende kinyume na sheria
Basi bana Anatokea zake GONGO LA MBOTO anaenda mjini Posta Enzi hizo DCM nyingi sana
Ilikuwa moja imeandikwa MZEE KASRI
Kufika tazara TRAFFIC akaisimamisha gari sijui ilikutwa na KOSA gani akaamulu watu washushwe wapande gari nyingine
Ikabidi MTIKILA ashuke akamfata TRAFFIC na kuanza kumuhoji "wewe unatuamulu sisi tushuke tupande gari nyingine kama nani"
Yule traffic polisi akang'aka na kujibu "mimi ni askari wa usalama barabarabi"
Mtikila akamtwanga Swali "nionyeshe mkataba tuliongia mimi na wewe wa kunisafirisha kutoka GONGO LA MBOTO mpaka POSTA"
kabla hata hajajibu hilo swali MTIKILA akamuonesha TIKETI akamuambia "unaona hii
Huu ndio mkataba niliongia na DEREVA wa kunitoa GONGO LA MBOTO mpaka POSTA wewe huna mamlaka yoyote ya kuvunja mkataba huu"

Watu wakaanza kumshangilia MTIKILA MTIKILA
polisi kuona hvyo na kumtambua anayebishana nae ni mtikila akaamua kula kona na mtikila akapanda GARI aliongia nayo mkataba Baina yake na dereva wa kumfikisha POSTA
Hao wakaseleleka zao POSTA

Jamaa alikuwa mtata na anajiamini
Nchi ingekuwa na Aina ya watu DIZAINI ya mtikila kama wa 5 hivi ingependeza sana
Kifo cha MTIKILA kimefanya TASNIA ya mahakama na ipooze sana zile hamsha hamsha za kuifungulia kesi serikali zimepotea

Pumzika kwa AMANI mzarendo na mtanganganyika halisi haswa
Mwafrika haswaa aliyeipenda NCHI yake na UAFRCA wake pamoja na DINI yake
 
Sidhani kama kuna ukweli kuhusu suala hili, lakini hata kama ni kweli kwamba alikuwa Afisa Kipenyo, Basi alikuwa Afisa anayejitambua sana na Mwerevu, huwezi kumfananisha na Afisa mwingine yoyote yule ktk historia ya kada hiyo.

Hizo zilikuwa ni 'Spinning Propaganda' tu za wale waliopanga Mpango wa Mauaji yake, yule amekuwa 'eliminated if not assassinated' kutokana na hizi harakati zake za 'Kupigania Haki,' alionekana Kama 'msumbufu' kwa 'wenye nchi.' Alikuwa 'eliminated' kwa tuhuma zinazodaiwa kuwa ni 'alikuwa mtata Sana,' 'anaisumbua mamlaka,' na tuhuma za kwamba 'alikuwa siyo mtiifu kwa mamlaka'.

Aliondolewa pamoja sambamba na wale watu wake wa karibu ambao nao 'Wadhalimu" waliowaona Kama "Mentors" wake kwenye suala zima la harakati zake za 'Kupigania Haki' na kuzidai kwa vitendo. Baada ya kuwa Mchiungaji na Mentors wake kuwa 'eliminated' ndipo zilitungwa 'Spinning Propaganda' nyingi zikiwa kama "Cover Story" ili kuwazuga watu na kuwatoa kwenye reli makusudi ili kuwapoteza maboya wasijue vyanzo halisi vya vifo vyao.
Kuna gharama kubwa Sana ktk kudai au Kupigania Haki, hususani kwenye hizi nchi zetu zenye tawala za 'mabavu.'

KUMBUKA NA MUHIMU KUZINGATIA:
'Ukiwa mkweli Sana, mnyoofu, mpinga wizi, rushwa, ufisadi, na dhuluma, tambua ya kwamba kwako Afrika siyo mahali salama pa kuishi.

RIP Mchungaji Dkt. Christopher Mtikila.
RIP Dkt. Sengondo Mvungi.
RIP Prof. Juan Mwaikusa.
Amini hilo
 
Kuna kisa kimoja cha mtikila

mtikila alikuwa amepanda BASI(daladala) usishangae mtikila kupanda DALADALA alikuwa ni mtu anayejichanganya na JAMII na very humble hakuwa na makuu kabisa unless uende kinyume na sheria
Basi bana Anatokea zake GONGO LA MBOTO anaenda mjini Posta Enzi hizo DCM nyingi sana
Ilikuwa moja imeandikwa MZEE KASRI
Kufika tazara TRAFFIC akaisimamisha gari sijui ilikutwa na KOSA gani akaamulu watu washushwe wapande gari nyingine
Ikabidi MTIKILA ashuke akamfata TRAFFIC na kuanza kumuhoji "wewe unatuamulu sisi tushuke tupande gari nyingine kama nani"
Yule traffic polisi akang'aka na kujibu "mimi ni askari wa usalama barabarabi"
Mtikila akamtwanga Swali "nionyeshe mkataba tuliongia mimi na wewe wa kunisafirisha kutoka GONGO LA MBOTO mpaka POSTA"
kabla hata hajajibu hilo swali MTIKILA akamuonesha TIKETI akamuambia "unaona hii
Huu ndio mkataba niliongia na DEREVA wa kunitoa GONGO LA MBOTO mpaka POSTA wewe huna mamlaka yoyote ya kuvunja mkataba huu"

Watu wakaanza kumshangilia MTIKILA MTIKILA
polisi kuona hvyo na kumtambua anayebishana nae ni mtikila akaamua kula kona na mtikila akapanda GARI aliongia nayo mkataba Baina yake na dereva wa kumfikisha POSTA
Hao wakaseleleka zao POSTA

Jamaa alikuwa mtata na anajiamini
Nchi ingekuwa na Aina ya watu DIZAINI ya mtikila kama wa 5 hivi ingependeza sana
Kifo cha MTIKILA kimefanya TASNIA ya mahakama na ipooze sana zile hamsha hamsha za kuifungulia kesi serikali zimepotea

Pumzika kwa AMANI mzarendo na mtanganganyika halisi haswa
Mwafrika haswaa aliyeipenda NCHI yake na UAFRCA wake pamoja na DINI yake
Hili tatizo la 'l' na 'r',h na a litaisha lini
 
Kufuatia kauli aliyoitoa hadharani siku chache baada ya muasisi wa Tanzania, Julius Nyerere kufariki Oktoba 14, 1999 Mtikila alisema “Nyerere alifariki kwa ugonjwa wa UKIMWI, ni mzoga, nyamafu na ameenda jehanamu”.

Mtikila alisema maneno hayo siku zote za Maisha. Kesi hiyo ilifutwa. Kesi nyingine ya kutoa maneno ya uchochezi alivyoshitakiwa nayo Mtikila enzi za uhai wake ni Jamhuri dhidi ya Christopher Mtikila .

Mtikila alishtakiwa kwa kesi nyingine ya uchochezi ilidaiwa na upande wa jamhuri kuwa Mtikila akihutubia mkutano viwanja vya Jangwani Dar Es Salaam, Alisema maneno yaliyochapishwa Gazeti la Mtanzania

Miongoni wa mashahidi wa upande wa jamhuri alikuwa ni Mhariri wa gazeti Hilo Badra Masoud ambaye baadae aliajiriwa serikalini kuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari Cha Wizara ya Nishati na Madini na Askari Polisi pia.

Maneno yaliyotolewa na Mchungaji Christopher Mtikila ambayo upande wa Jamhuri ulidai ni maneno ya kichochezi ni; “Rais Benjamin Mkapa siyo Raia wa Tanzania ni Raia wa Msumbiji”.

Kesi iliunguruma na mwisho Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilifuta kesi hiyo dhidi ya Mtikila kwa sababu ilichukua muda mrefu kumalizika na mashahidi upande jamhuri ukawa hauleti mashahidi.

Wakati Kesi ikisikilizwa, mapolisi walipokuwa wakifika kutoa ushahidi, Mtikila alikuwa akiomba Mahakama isipokee ushahidi wa mapolisi wale kwa sababu wao sio Rais Benjamin William Mkapa.

Mtikila aliomba Mahakama itoe hati ya kumlazimisha Rais Benjamin William Mkapa kwa amri ya mahakama afike Mahakamani atoe ushahidi wake wa kupinga yeye siyo Raia wa Msumbiji.

“Rais Mkapa anaishi hapo SVU -Upanga, ni karibu na Mahakama ya Kisutu. Kwanini asipelekewe samansi maana ni karibu na anaweza kutembea hata kwa miguu aje akatae siyo Raia wa Msumbiji”

“Mimi ninao ushahidi Mkapa ni Raia wa Msumbiji ndio maana hana uchungu na taifa hili anauza viwanda vyetu kwa wazungu hovyo tu”. Alisisitiza Mchungaji Mtikila

Wakati Mtikila akitoa maombi hayo amesimama kizimbani Mkapa akiwa bado ni Rais wa nchi, waandishi waliokuwa wameketi mahakamani wanafuatilia Kesi hiyo walikuwa wanainama wakicheka bila kutoa sauti.

Kesi nyingine ya uchochezi Na.132/2011. Mtikila alidaiwa kutoa maneno ya uchochezi na kashfa dhidi ya Rais Kikwete kwa kumuita ‘gaidi’ serikali anayoiongoza inataka kuanzisha Mahakama ya kadhi,

kati ya Januari 2009 na Aprili 17, 2010 jijini DSM kwa nia ya uchochezi mshtakiwa alisambaza kwa umma nyaraka zilizosema “Kikwete kuuangamiza ukristo”, wakristo waungane kuweka mtu Ikulu”

Katika shtaka la pili, Aprili 16, 2010 eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam, bila kibali alikutwa akimiliki waraka wenye uchochezi kwa jamii. Katika kesi hii Mtikila hana wakili wa kumtetea na anajitetea mwenyewe.

Polisi walivamia nyumbani kwa Mtikila alfajiri kufanya upekuzi kwa kusaka waraka huo na kumkamata, mke wa Mtikila. Kesi hiyo ambayo ilisikilizwa na Mahakimu watatu tofauti.

Mahakimu wote watatu walilazimika wajitoe katika kuendesha kesi hiyo kwa sababu Mchungaji Mtikila aliwaomba mahakimu wawili wajitoe kwa sababu anaamini hawana hadhi na hawawezi kumtendea haki.

Akapangiwa Hakimu Mfawidhi kwa Elvin Mugeta aliisikiliza kesi hiyo na Septemba 25, 2012, alitoa hukumu ya kumuachilia huru Mtikila baada ya upande wa jamhuri kushindwa kuthibitisha uchochezi.

Mtikila kizimbani alipaza sauti mahakamani “Hallelujah”. Wafuasi wake walishangilia. Polisi wenye vyeo vya chini walijipanga nje wakataka kumuweka chini ya Ulinzi, aliwaeleza maneno yaliyosababisha jaribio la Polisi kufutika

“Polisi hamna uwezo wa kunikamata mnavyo vyeo vya chini sana.... Kama mnataka kanifungulia kesi nitakwenda polisi mwenyewe. Hata boss wenu IGP Mwema ananiita kwa heshima kwa kunipigia simu, toeni ujinga wenu hapa”

Alisema Mtikila na watu kuangua vicheko na Polisi wale waliokuwa wamepanga kumkamata kumuacha Mtikila aende zake nyumbani akapumzike huku wafuasi wake wakiimba “saa ya ukombozi ni sasa”

Kesi hiyo ya kumtolea kashfa Rais Jakaya Mrisho Kikwete mwanzo alipangiwa Hakimu Mkazi Waliarwande Lema, Januari 11, 2010 alitoa amri ya kumfutia dhamana Mtikila kwa madai ya kushindwa kujiheshimu.

Amri ya kumfutia dhamana ilitolewa na Hakimu Waliarwande Lema baada ya kusikiliza utetezi wa mshtakiwa aliyefika mahakamani saa tano asubuhi akiwa amechelewa na alijikuta akikamatwa na askari polisi.

Mtikila alipaswa kufika mahakamani hapo majira ya saa tatu asubuhi wakati kesi hiyo ilipotajwa, lakini hakuwepo, ndipo Wakili wa Serikali, Beatrice Mpangala aliomba hati ya kukamatwa kwa mshtakiwa.

Kabla ya Mtikila kukamatwa, alieleza mahakama kwamba alidamka mapema na kumtafuta daktari wake aliyemtaja kwa jina moja la Katembo, ambaye alimfanyia upasuaji baada ya kugongwa na nyoka aina ya COBRA.

Mchungaji Christopher Reuben Mtikila alieleza mahakam hiyo mbele ya Hakimu mkazi Waliarwande Lema kwamba aligongwa na COBRA wakati alipokuwa katika shughuli za kidini nchini Zimbabwe mwaka 2009.

Mtikila alisema alijitahidi kuwatafuta wadhamini wake ili wafike mahakamani kwa niaba yake, lakini hakuweza kuwapata, ndiyo maana alikuja mwenyewe mahakamani hapo akiwa na maumivu makali mwilini mwake.

Hata hivyo hakimu waliarwande Lema alieleza kutoridhishwa na utetezi huo wa mchungaji Christopher Reuben mtikila na kuamuru Mtikila atupwe rumande hadi Januari 25, 2010 kesi yake itakapotajwa tena ndiyo atarudishwa.

Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa Mchungaji Mtikila kushindwa kufika mahakamani wala wadhamini wake. Mara ya kwanza ilikuwa Oktoba 22, 2009. Mchungaji Mtikila alikuwa akikabiliwa na kesi hiyo ya uchochezi Na.132/2011

Ilipofika saa saa tano mchana, Mtikila aliwasili mahakamani hapo anashuka Kwenye Bajaji, marafiki zake waandishi wa habari wakamuwahi kule kule Kwenye bajaji na wakampa taarifa Kuwa

Hakimu mkazi waliarwande Lema alitoa Hati ya Mchungaji Mtikila kukamatwa hivyo mapolisi Wakimuona watamkamata. Utetezi wake huo haukumsaidia Mtikila ,Hakimu Lema aliamuru aepelekwe mahabusu.

Mtikila alienda mahabusu na alipotoka alipiga simu kuwajulisha watu wake kuwa anakusudia kuwasilisha ombi la kumkataa Hakimu Lema ajitoe Kwenye Kesi yake kwa sababu Hana utu na Hakimu Lema alijitoa .

Kesi ilipohamishiwa kwa Hakimu Sundi Fimbo pia, Mtikila kupitia barua yake alimuomba hakimu Fimbo ajitoe kwenye kesi yake kwa sababu amebaini hawezi kumtendea haki katika kesi hiyo.

katika kesi hiyo aliwasilisha ombi la kuomba usikilizwaji wa kesi hiyo usimame hadi kesi ya Kikatiba mbele ya Jopo la Majaji wa tatu wa mahakama Kuu wanaongozwa na Jaji Fakhi Jundu na Profesa Ibrahim Juma isikilizwe.

Ambapo katika kesi hiyo anaiomba Mahakama hiyo izifute sheria za makosa ya uchochezi kwa kuwa zinanyima haki wananachi ya kutoa maoni yao itakapotolewa uamuzi lakini hakimu huyo alilikataa ombi la mtikila.

Mchungaji Christopher Reuben Mtikila kupitia barua yake alisema kwamba kuna kesi tatu za Kikatiba zilizokuwa zimefunguliwa mahakama kuu na washtakiwa wanaokabiliwa na kesi za jinai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Aliwataja washtakiwa hao ambao ni Jayantkumar Patel ‘Jeetu Patel’, Profesa Costa Mahalu na mahakama ya Kisutu ilisitisha usikilizwaji wa kesi zinazowakabili hadio mahakama kuu ilipozitolea uamuzi kesi zao za Kikatiba.

“Na huyu Hakimu Sundi Fimbo anafahamu fika nimefungua kesi ya Kikatiba Mahakama Kuu kuzipinga sheria za uchochezi ambao sheria hizo ndizo zimetumika kunifungulia kesi ya uchochezi iliyopo mbele yake,”

“kesi ya aina hiyo ikishafunguliwa mahakama ya juu, mahakama ya chini inatakiwa isitishe usikilizaji hadi mahakama hiyo ya juu itakapotoa uamuzi lakini amelikataa ombi langu na kwa kitendo hicho amevunja mwenendo wa kesi”

“ukiukwaji wa maadili ya sheria za nchi na haki na nimuomba ajitoe kwenye kesi yangu kwani tayari ameishaonyesha hawezi kunitendea haki ”alidai Mchungaji Christopher Reube. Mtikila katika barua yake kwa msajili wa mahakama

Mtikila alidai sababu nyingine ya kumkataa hakimu Fimbo, ni kwamba wakati kesi hiyo ikiendeshwa aliwai kuwasilisha ombi kutaka afutiwe kesi hiyo ya uchochezi kwa sababu kesi hiyo ilifunguliwa nje ya muda

kwani kesi za uchochezi zinatakiwa zifunguliwe mahakamani ndani ya miezi sita tangu mshtakiwa alituhumiwa kutenda kosa hilo na kwamba kesi hiyo inafanana na kesi ya madai ya fidia Na.166/2004 inayosikilizwa na Jaji Robert Makaramba,

Ambapo katika kesi hiyo anamdai Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa alikamatwa kinyume na sheria na kwamba kesi ambayo nayo ni ya uchochezi iliyokuwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ilifunguliwa nje ya muda.

Na kweli Ilipofika Machi 22, 2013 Hakimu Fimbo alitangaza kujitoa kusikiliza kesi hiyo ikapangwa kwa Hakimu Elvin Mugeta ambaye aliisikiliza kesi hiyo hadi akatoa hukumu ya kumwachilia huru Mtikila.

Mtikila alipotoa utetezi wake, kama kawaida alikanusha madai ya upande wa jamhuri kuwa ule waraka wake uliokuwa na kichwa cha Habari kisemacho (KIKWETE KUANGAMIZA UKRISTO) kuwa ni wa uchochezi,

Mchungaji Christopher Mtikila alikubali kuwa ule waraka ni wake na aliundaa yeye na siyo wa uchochezi na kwamba hawezi kuukana waraka ule kwa sababu kuukana waraka ule ni sawa na kumkana YESU KRISTO.

Mtikila alijipambanua wazi kupambana na serikali ya Jakaya Kikwete na hakuogopa kumtaja hadharani. Mashambulizi yake aliyaita mabomu ya Hiroshima dhidi ya serikali ya ‘msanii’ Rais Jakaya Kikwete.

Mchungaji Christopher Reuben Mtikila kabla na baada ya Kikwete awe Rais, alikuwa akimuita Kikwete ni ‘RAIS MSANII’, Reginald Mengi, Rostam Aziz na wengine aliwajumuisha katika kundi hilo la wasanii.

Juni 2013, Mchungaji, Christopher Mtikila, aliibwaga serikali katika kesi Na. 09 na 011/2011, aliyokuwa ameifungua Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika (AfCHPR) kutaka kuruhusiwa kwa mgombea binafsi, ikiwamo Rais

Mtikila alifungua kesi (AfCHPR) baada ya Juni 17 2010, Mahakama ya Rufani ya Tanzania, kutoa hukumu ya rufaa ya Madai Na. 45/2009 ambayo ilifunguliwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Mchungaji Christopher Mtikila.

Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Tanzania ambaye alikuwa akitetewa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania ambaye baadae alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju

Katika rufaa hiyo alikuwa akiomba Mahakama kutengua hukumu ya Mahakama Kuu katika kesi ya madai Na.10/2005 mbele ya jopo la Majaji Amir Manento, Salum Massati na Thomas Mihayo ambayo ilitangaza Ibara ya 39, 67, 77 zinavunja Haki ya za watu

Kwamba, kupitia kuvunjwa kwa hizo ibara za katiba ya Jamhuri ya muungano wa tanzania wasiokuwa wanachama wa vyama vyovyote vya siasa kugombea Urais na hivyo hukumu ile ikaruhusu mgombea binafsi.

Juni 17, 2010 jopo la Majaji saba wa Mahakama ya Rufani likiongozwa na Jaji Mkuu Augustino Ramadhani, walitoa hukumu ambapo walitengua hukumu ya Mahakama Kuu kwamba Mahakama haina mamlaka ya kutunga Sheria,

Mhimili wenye mamlaka ya kufanyia marekebisho Katiba ni Bunge hivyo suala la kuwepo kwa mgombea binafsi litapelekwa bungeni kwasababu mhimili wa Mahakama haina mamlaka ya kufanyia marekebisho Katiba ya nchi.

Ieleweke kuwa Katiba ya Tanzania hadi sasa hairuhusu kuwepo kwa mgombea binafsi kwa sababu Ibara ya 39(1) (c) inasomeka hivi : “(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa”

Hukumu ya rufaa mgombea binafsi ilipotolewa Mtikila alikasirika sana na alihojiwa na vyombo vya habari na alikuwa akisema majaji wote saba waliokataa kuhurusu mgombea binafsi ni Yuda Eskarioti ni vibaraka wa serikali.

Kesi nyingine ya mchungaji Christopher Mtikila ni ile Kesi ya Madai ya fidia ya Sh. Bilioni Moja ambayo anataka Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dk. Valentino Mokiwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Katika Kesi hiyo Mchungaji Mtikila alidai Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dk. Valentino Mokiwa alimdhalilisha kwa kumshika makalio Mtikila na kwamba kitendo hicho kilichotokea Juni 25 2013 ni udhalishaji.

Mchungaji Christopher Mtikila alikuwa ameitwa na Askofu kujadili tamko la la Mtikila kwamba Kanisa la Anglican linajihusisha na ufisadi, ukiwemo wizi wa vifaa vya Hospitali ya Mission ya Millo iliyoko Ludewa mkoani Njombe.

Mtikila alisema alivyoitwa na Askofu Mokiwa ili kujadili hilo alifika na wenzake watatu wa taasisi ya Liberty International Foundation na wakakaribishwa kwenye moja ya jengo la dayosisi ya St. Nicholaus, usiku wa saa 03:00.

“Muda mfupi baada ya kikao kuanza, Askofu Valentino Mokiwa ambaye alikuwa na wenzake saba, alisimama na kuwataka wajumbe wote wakaguliwe kama kuna mtu ana kinasa sauti.” Hayo ni maelezo ya Mtikila

“Askofu Mokiwa alisimama na kuungana na wenzake kutukagua baada ya kuhakikisha mlango umefungwa.Katika upekuzi huo ndipo tuhuma hizo zilipopatikana, operesheni hiyo ilienda mbali zaidi ya lengo la kawaida.”

“Askofu Valentino Mokiwa alianza kupenyeza mikono yake kwenye shingo yangu kuelekea chini kisha huko chini mikono ya mlalamikiwa ilionekana waziwazi ikipapasa makalio ya yangu” alidai Mchungaji Mtikila .

Mtikila aliomba Mahakama imuamuru Askofu Mokiwa amlipe kiasi hicho cha fidia kwa sababu alimdhalilisha na alimletea madhara zaidi ya kitendo hicho ni pamoja na mfadhaiko, masikitiko, wasiwasi, aibu katika jamii

Mchungaji Christopher Mtikila alikwenda mbali zaidi katika madai yake na kusema kwamba baadabya ukaguzi alipata shinikizo la damu la mara kwa mara na matatizo ya moyo kila anapokumbuka kitendo hicho.

Mtikila alisema ana shauku kubwa siku ifike aanze kutoa utetezi katika kesi hiyo maana atavua nguo zote na huyo wakili wa Mokiwa atakuwa tayari kunishuhudi mzee wake nikivua nguo zote mahakamani kumuonyesha makalio yangu

Maana akinishuhudia nipo uchi nikimuonyesha hakimu makalio yangu atakuwa amepata laana huyo wakili wa Askofu Mokiwa ambaye ni kijana wangu. Basi wafuasi wake na waandishi wa habari wanafurahi kweli, wakisubiri kesi kuanza.

Mtikila alitaka Scotland Yard lifike Tanzania, kuchunguza kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba aliyefariki ghafla. Mtikila aliamini Kolimba aliuwawa na CCM. Ilifunguliwa Kesi, Mahakama yaKinondoni Dar Es Salaam,

Hakimu Gabriel Mirumbe (ni marehemu kwa sasa ambapo alipofariki Mtikila alisema amefuraishwa na kifo hicho kwa sababu hakimu huyo alimfunga gerezani kwa kumuonea kifungo cha mwaka mmoja gereza la Keko.

Mtikila aliwahi kuomba Mahakama ya Kisutu itoe amri ya kutolewa rumande (Habeas corpus) lilowasilishwa mahakamani hapo na Wakili wa kujitegemea Hurbet Nyange dhidi ya Jamhuri Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Nyange alikuwa akimtetea aliyekuwa mgombea Urais Burundi na Mtangazaji (Radio Publique Africaine) Burundi, Alexis Sinduhije. Alikuwa ni rafiki wa Mtikila na aliposhindwa uchaguzi nchini Burundi alikimbilia Tanzania kujificha.

Serikali ya Burundi ilimsaka Alexis Sinduhije kwa kutenda makosa ya jinai wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu Burundi. Alikamatwa na Interpol ili jamhuri iwasilishe ombi la Mahakama itoe Kibali cha kumrejesha Kwao (extradition request)

Mwaka 2007, Alexis Sinduhije aliacha uandishi wa habari ili kugombea Urais wa Burundi, lakini alikamatwa mwaka wa 2008 kwa shtaka la "kumtusi Rais," Pierre Nkurunziza, hakupatikana na hatia na kuachiliwa mnamo 2009

Filamu ya "Kamenge, Northern Quarters" inaeleza uhalisia wa maisha ya Alexis Sinduhije kabla, wakati na baada ya kufungwa kwake. Mwanasiasa na mwanahabari aliyelazimika kuondoka nyumbani kwake Kamenge kimya kimya.

Mchungaji Christopher Mtikila alikuwa akifika katika Mahakama hiyo na kujaribu kukaa karibu na eneo la mahabusu ya Mahakama hiyo lakini Askari Magereza walikuwa wakimtimua wakimtaka akae mbali na eneo hilo.

Waandishi wa habari walikwenda kuchekea mbali Mtikila asiwaone maana angewaona wanacheka angewashughulikia kwa maneno makali. Mwisho wa siku Mahakama ilitoa Kibali cha Alexis Sinduhije kurudishwa Burundi.

Mahakamani, Mtikila alikuwa anasema yeye anataka Sinduije abaki Tanzania kwa sababu endapo atarudishwa Burundi, serikali ya Burundi itaenda kumkata kichwa Sinduije. Hivyo akaiomba mahakama ilinde haki ya kuishi ya Sunduije

Mtikila alilipachika jina la “Mgodi” Kesi zote za madai alipokuwa amezifungua. Alisema jina la mgodi kwa sababu anaamini atashinda na akishinda na Mahakama itaamuru wadaiwa wamlipe fidia ya fedha kwa hiyo Fedha ndiyo mgodi.

Sebuleni kwa Mtikila makochi na meza zilikuwa zimepambwa na vitambaa vya kufumwa rangi za Bendera ya Tanganyika. Nje ya nyumba yake alitundika Bendera ya Tanganyika maana alikuwa akiamini na kuipenda Tanganyika.

Mtikila alilipenda sana vazi la suti na muda mwingi katika harakati zake alikuwa akivalia vazi hilo la suti na suspendeer. Miaka ya nyuma alienda Marekani Kwenye mkutano wa watumishi wa Mungu akiwa bado hajaanza kuvaa suspenders.

Huko aliwakuta watumishi wenzake wa Mungu, wakiwa wamevalia vazi la suspenders na aliwauliza kwanini wanapenda kuvaa suspenders. Walimueleza wanapenda kuvaa hivyo kwa sababu wao hupenda kufunga ili wawe karibu na Mungu

Wanapomaliza kufunga, uzito hupungua na kusababisha nguo kuwapwaya na kuwaletea Usumbufu wa kwenda kwa fundi kupunguza nguo. Kuondokona na tatizo hilo la kupeleka kwa fundi kupunguza nguo, wanaamua kuvaa suspenders

Mtikila alikuwa na komputa na printa nyumbani kwake tangu alipokuwa akiishi Ilala na Mikocheni na alikuwa na chumba chake kimoja amekitenga kama ofisi ambacho alikuwa akikitumia kufanyia shughuli zake.

Alikuwa ametenga kufanya shughuli ikiwemo shughuli kubwa aliyokuwa akiipenda sana ya uandishi wa nyaraka mbalimbali ambazo zimebeba maovu ambayo ameyachunguza na kuyabaini. Alitumia maisha yake vizuri.

Licha nyaraka zake hizo za maovu aliyokuwa anadai ameyagundua yalikuwa na maneno makali ambayo wahariri wengi waliogopa kutumia habari zinatokana na nyaraka zile alizokuwa akiziandika.

askari polisi pindi wapatapo taarifa za siri kuwa Mtikila anaandaa waraka mbalimbali za kuja kuwavua nguo viongozi wa serikali, walivamia nyumba yake asubuhi na kufanya upekuzi ndani ya nyumba yake.

Askari hao walipofika nyumbani kwake kwa ajili ya upekuzi walimueleza kwamba nyaraka zingine azifiche ili asiwe na Kesi nyingi. Walipenda kazi yake ya kukosoa serikali na kutetea jamii na maslahi ya kazi zao za upolisi.

kuna siku alifika getini Ofisi za Msajili wa Vyama Vya Siasa akiwa John Tendwa, Mlinzi aliyekuwa akilinda zamu walipishana Kiswahili (lugha) na Mtikila, Mtikila alimchapa vibao vya kutosha.

Baadhi ya wahariri wa vyombo vya Habari walifanya kikao na walipitisha azimio la kutochapisha habari zinazotolewa na Mtikila, Mtikila alivyopata taarifa hizo alitembelea baadhi ya vyombo Vya Habari.

Huko aliwakuta wahariri na kuanza kuwasemea hovyo katika ofisi zao. Mtikila aliwaambia waache kujipendekeza kwa watawala, watumie nguvu zao nyingi kutetea haki na maslahi ya jamii siyo watawala.

Mtikila alikuwa anasema Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, siyo Raia wa Tanzania, ni Raia wa Iran na anaitwa "Sakalili" na alikuwa akifanya biashara ya ngozi eti ni mtu hatari sana. Mtikila alisisitiza hivyo wakati wote.

Mtikila alifungua kesi nyinginne ya Kikatiba kuomba Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), apunguziwe mamlaka kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya 2002, DPP amepewa mamlaka makubwa sana

Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya 2002 Kifungu 91(1) cha Sheria hiyo kilitoa madaraka kwa DPP kumfutia Klkesi mshtakiwa wa kesi ya jinai bila kuhojiwa na mtu wala taasisi yoyote ile.

Pia, Mchungaji Christopher Reuben Mtikila alifungua kesi nyingine Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, akiomba Mahakama Kuu ya Tanzania izuie uuzwaji wa jengo la Mahakama ya Rufani Dar Es Salaam.

Maana kulikuwa na tarifa kuwa uongozi wa mahakama una mpango wa kuliuza jengo hilo la Mahakama ya Rufani ambalo ni jengo la kihistoria ambalo zamani jengo hilo lilikuwa likijulikana kama Forodhani Hoteli.

Mtikila alifungua kesi Na.14/2015 kupinga muswada wa mabadiliko ya sheria kuitambua Mahakama ya Kadhi. Muswada huo ulipangwa kuwasilishwa, kujadiliwa bungeni lakini haukuweza kuruhusiwa kujadiliwa bungeni tena.

Mtikila ni muasisi wa neno la “Magabacholi”, Wahindi ambapo Mtikila alitaka Wahindi wote wanaokaa Katika maghorofa ya NHC Katikati ya Jiji la Dar Es Salaam waondolewe na Watanganyika ndio waishi katika maghorofa hayo.

Kutokana na ujasiri na misimamo mikali aliyokuwa tangu zamani yalisababisha kutengenezewa kwa propaganda yakuwaaminisha Watanzania wapuuze yote yanayosemwa na Mtikila kwa sababu Mtikila ni kichaa.

Mwanzoni propaganda hiyo iliwangia watu waliikubali ila kadri siku zilivyokuwa zinaenda watu walipuuza propaganda hiyo na kusema Mtikila ni mzima siyo chizi anasema ukweli ila serikali haitaki kusikia ukweli huo

Hatua ya Mtikila kwenda mahakamani Mara kwa Mara Kufungua Kesi mbalimbali dhidi ya serikali, na serikali kumfungulia Kesi za jinai Mtikali mahakamani, pia kulisababisha kukuza Utawala wa Sheria nchini.

Aidha baadhi ya Kesi zilizofunguliwa na Mtikila zimekuwa zikitumiwa na wahadhiri wa Sheria Katika Vyuo Vikuu kufundishia wanafunzi wa kozi ya Sheria hususani katika somo la Sheria ya Katiba (Constitution Law).

Wahadhiri wa fani ya Sheria wamekuwa wakifundisha masomo mbalimbali ya Sheria ikifika somo la Sheria ya Katiba, wahadhiri hao huelekeza wanafunzi wa Sheria wasome na kuelewa Kesi ya Mtikila one na Mtikila Two.

Mtikila one ni kesi Na.10/2015 ambayo Mahakama Kuu iliruhurusu mgombea binafsi. Mtikila Two ni rufaa ya Madai Na.45/2009 Mahakama ya Rufaa ilitengua hukumu ya Mahakama Kuu iliyoruhusu uwepo wa mgombea binafsi.

Kesi za kikatiba nyingine alizowahi kuzifungua ni pamoja na kesi ya wananchi wa Tanzania Bara kuruhusiwa kwenda Zanzibar bila pasipoti na vyama vya siasa kuruhusiwa kufanya mikutano bila kuomba kibali toka kwa Mkuu wa Wilaya na polisi.

Chama chake cha Democratic Party (DP). hakikuweza kupata usajili wa kudumu kutokana na Mchungaji Mtikila kutoitambua Zanzibar. Alikuwa akisisitiza kuwa chama chake ni cha Tanganyika na si Tanzania ambayo haipo.

Mchungaji Christopher Mtikila alibadili msimamo wake katika miaka iliyofuata kwa kukubali kutafuta wanachama toka Zanzibar (kama sheria ya uchaguzi inavyotaka) na hivyo chama chake kuweza kupata usajili wa kudumu.

Katika sherehe za siku ya Sheria Mtikila alikuwa alishiriki Katika sherehe hiyo kwasababu naye ni mdau wa Mahakama na Mara zote alikuwa akishangiliwa umma ambao umekuwa umeshiriki Katika maadhimisho hayo.

Mtikila alikuwa Akizungumza lugha ya Kiingereza kwa ufasaha utafikiri kazaliwa Buckingham Palace. Na pindi azungumzapo lugha hiyo ya Kiingereza alipenda sana kutamka sana neno hili la Kiingereza “WELL”

Mtikila asubuhi alifanya mihadhara ya kisiasa viwanja vya Mnazi Mmoja, mchana anaondoka kwa maandamano na umati wake, wanakwenda kufanya mkutano wa hadhara viwanja vya Jangwani. Watu wanakula darasa.

Mtikila hajawahi kusomea sheria popote lakini aliyekuwa Msajili wa vyama vya siasa, Christopher Lihundi, nyakati za jioni, mwanzoni mwa Miaka 1990 walikuwa wakakutana na Mtikila sehemu anamfundisha kuvisoma vifungu

Msajili wa vyama vya siasa, Christopher Lihundi, alimfundisha kusoma hivyo vifungu na Ibara za Katiba na kumuelimisha zilikuwa zinataka afanye nini na jinsi ya kuzidai Haki zake. Mtikila akajikuta amekwiva kweli.

Mtikila aliwahi kusema Mawakili Richard Rweyongeza na Mpare Mpoki walikuwa msaada mkubwa kwake kwa sababu ndio walikuwa wakijitolea kumpa msaada wa kisheria hata kama alikuwa hana fedha zakuwalipia.

Sifa moja ya Mtikila, ambayo ilimfanya waandishi wengi wa habari wampende sana, hata siku Moja hawezi kumruka mwandishi aliyeandika taarifa inayomnukuu Mtikila. Hawezi kusema hajampa hiyo taarifa akishtakiwa mahakamani.

Mtikila alikuwa na mchezo wakuandika waraka kuhusu tuhuma za mtu fulani kwa maneno makali kisha anaitisha mkutano na waandishi wa Habari. Badhi ya vyombo ya Habari vilisita kutumia waraka kwa sababu maneno makali.

Baada mitandao ya kijamii kuanza kutumika kwa wingi na ukubwa kidogo nchini Tanzania, Mchungaji Mtikila alichokuwa anafanya, anaandaa waraka wake kisha anawatumia watu Kwenye email zao wasome wenyewe na kusambaza.

Mtikila alikuwa hajui kuficha hisia zake, anawapasha ukweli waandishi wa Habari hawataki kutoa Habari na kuhudhuria mikutano yake na waandishi wa Habari kwa sababu chama chake ni maskini Hakina uwezo wa kuwapatia “mshiko”

Wakati Mtikila anapambana Mahakama Kuu kanda ya Dodoma na Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam kutaka mgombea binafsi aruhusiwe walikuwa Wakimuona Mwendawazimu na wala walikuwa hawa thamani,

Lakini siku Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, iliporuhusu uwepo wa mgombea binafsi, wale wote waliokuwa wakimuona Mchungaji Christopher Mtikila ni chizi walianza kumthamini na kumuona Mtu wa maana sana.

Mtikila alikuwa mwanzilishi na mkuu wa kanisa la Kipentekoste la Full Salvation Church.alijihusisha pia na harakati za haki za binadamu kwa kupitia kitengo cha haki za binadamu cha kanisa hilo kiitwacho Liberty Desk.

Mchungaji Christopher Mtikila alifariki Oktoba 4, 2015 kwa ajali ya gari, Msolwa, Chalinze mkoani Pwani wakati akitoka kwenye shughuli za kisiasa, alizaliwa June 9, 1950. Mtikila alizaliwa Iringa, Tanzania.

Cc: Martin Maranja Masese, MMM.
Daaaaaah jamaa inaonekana alikuwa ni nguli wa sheria kuliko TL,
Hivi aliuliwa na kundi lipi?
Kundi la Edo, Born to town au PK?
 
Tunajadili vitu msingi na tunasoma vitu vya maana usilete usenge silabi hapa ,kafungue twisheni nyumbani kwako ya kufundishq silabi k wewe!!
 
Back
Top Bottom