Tupe mtazamo wako!

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Mfungwa mmoja baada ya kutoroka jela,alikuwa akitembea barabarani huku akiwa kavaa uniform za kifungwa.Mara ghafla mbele yake umbali wa mita 200 akaliona gari la polisi likimjia.Uamuzi aliochukua ni kukimbilia upande ule ule linakotokea gari lile gari kwa hatua kama 10 halafu akachepuka porini na kutokomea kusikojulikana. (SWALI);Unafikiri ni kwa nini alikimbilia ule upande linakotokea gari na kuchepuka porini badala ya kulipa mgongo,akimbie kurudi alikotoka halafu ndo achepuke porini?
 
it's obvious, aenda opposite direction na gari, mpaka lisimame au limake u turn atakuwa keshachepukia porini!
 
Kukimbia kulielekea gari ni sawa na kujiongezea masafa ya kulikimbia gereza. Na angeliingia porini mapema ndo mwanya wa kukamatwa ungelikuwa mkubwa coz askari na wao wangelingia porini wakiwa mbele ili kumzingira asipate kwenda mbali zaidi vyenginevyo iwe ni kurudi tu.
 
Je, huyo mfungwa alikuwa bado na minyororo?
Je, alikuwa anaact movie/
Je, urefu wa huyo mfungwa ni kimo gani?
 
angekimbia kwa kulipa gari kisogo, polisi wangefyatua risasi,,,, soo ndo maana akawaface ili wamuone kwamba anataka kujisalimisha,, then polisi wakapumbazika, yeye akajisepea zake porini
 
simpo, ni kwasababu mpaka gari lifunge brek litaenda mbali zaidi, na atakuwa tayari kapotea..
 
aaaah jamani mbona hiyo ni rahis sana...itakua jezi za hyo magereza alokua amevaa ina namba nyuma. So kama ange geuka na kuwapa mgongo askar basi wangeweza kusoma namba. Hakuna posho jamani maana nimefanya kazi kubwa.
 
d5 sijakubaliana na wewe,hao askari hawakaagi mbele wote,so wale maafande walioko nyuma wangeruka wangemkamata tu fasta,kama gari lilikua halikimbii,tuumize kichwa kidogo zaidi
 
Mkuu polise wasingewez kumkamata kwa sababu awana mamlaka na mfugwa awapo ndani ya uniform au akiwa jela iyo ni kazi ya askar magerez.labda fafanua walikuwa police trafic au police wa usalama wa raia.
 
angekimbia kwa kulipa gari kisogo, polisi wangefyatua risasi,,,, soo ndo maana akawaface ili wamuone kwamba anataka kujisalimisha,, then polisi wakapumbazika, yeye akajisepea zake porini
Hii nimeipenda,lakini kama alitaka kujisalimisha angesubiri pale pale alipo na kuinua mikono juu,hakupaswa kulikimbilia!
 
Mkuu polise wasingewez kumkamata kwa sababu awana mamlaka na mfugwa awapo ndani ya uniform au akiwa jela iyo ni kazi ya askar magerez.labda fafanua walikuwa police trafic au police wa usalama wa raia.
Japokuwa sikufafanua ni polisi wa aina gani,ukweli ni kwamba mfungwa yoyote aliyetoroka jela atakuwa na hisia kwamba anatafutwa,hivyo kila polisi kwake ni simba.
 
Mfungwa mmoja baada ya kutoroka jela,alikuwa akitembea barabarani huku akiwa kavaa uniform za kifungwa.Mara ghafla mbele yake umbali wa mita 200 akaliona gari la polisi likimjia.Uamuzi aliochukua ni kukimbilia upande ule ule linakotokea gari lile gari kwa hatua kama 10 halafu akachepuka porini na kutokomea kusikojulikana. (SWALI);Unafikiri ni kwa nini alikimbilia ule upande linakotokea gari na kuchepuka porini badala ya kulipa mgongo,akimbie kurudi alikotoka halafu ndo achepuke porini?
Polisi wetu wameshajulikana ukiwakimbia ndo wanakukamata ukiwafuata hata hawakuulizi ndo maana huyo msegerea akawafuata halafu akajisepea..
 
Sitaki kutoa jibu mwenyewe,natoa hint ifuatayo;katika moment ambayo mfungwa aliiona gari ikija mbele yake,alikuwa akitembea juu ya daraja refu lenye kingo ndefu pande zote mbili!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom