Riwaya: Mpelelezi toka kuzimu

Ambakucha

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
277
445
MPELELEZI TOKA KUZIMU

UTANGULIZI
Poaba Wilabo, ni mfanyakazi kwenye taasisi nyeti ya upelelezi nchini inayoitwa Self Investigation Unit au kwa kifupi SIU akiwa ni shushu anayetegemewa sana.

Taasisi hii ni ya binafsi na imekuwa ikitumiwa na Jeshi la Askari nchini kuchunguza matukio yaliyofunguliwa majalada kwao, lakini yana utata mkubwa kama vile mauaji yanayotekelezwa na watu wasiyojulikana na mengine yenye mwelekeo huo.

Mara nyingi, Jeshi la Askari linapoonesha kushindwa kuwapata wahalifu ndani ya saa ishirini na nne ndipo huwatumia SIU kukamilisha kazi kwa malipo makubwa. Pia, wakati mwingine, SIU na Jeshi la Askari hufanya kazi ya uchunguzi kwa pamoja.

Aidha, wapo wafanyabiashara wakubwa nchini ambao huitumia taasisi hiyo kuwachunguzia mambo yao kwa malipo ya mamilioni ya fedha.

Kwa maana na sababu hiyo, Poaba Wilabo amejipatia sifa lukuki kutoka kwa askari wa Jeshi la Askari nchini mwake kwani katika kupeleleza matukio hajawahi kufyatua risasi wala kumwaga damu licha ya kumiliki bastola ya kisasa aina ya Roberto Negio yenye kiwambo cha sauti iliyotengenezwa nchini Korea. Yeye hutumia zaidi akili ya ziada aliyoipata kwenye mafunzo yake nje ya nchi.

Baadhi ya matukio yaliyomo kwenye kitabu hiki yalitukia hakika.
Sasa tuendelee....

MPELELEZI TOKA KUZIMU

MWAKA 2000, MGANGA WA KIENYEJI ACHINJA MKE NA MTOTO

Poaba Wilabo alijiweka katika umakini kusikia simu yake ya mkononi ikiita na jina la mpigaji lilisomeka Kwizera K. Kwizera ambaye ni bosi wake, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya SIU.

Kilichomshitua Poaba Wilabo ni kwamba, alivyojua yeye bosi wake yupo ofisini, hivyo asingepiga simu ya mkononi na kuacha ya mezani ambayo haikuwa na tatizo lolote. Kwa sababu hiyo, akaamini bosi wake hakuwepo ofisini kwake.

Kabla ya kupokea simu hiyo, alichungulia nje kupitia dirishani na kuliona gari la bosi wake aina ya Range Rover likiwa eneo la maegesho yake...

"Haloo mkuu," Poaba Wilabo alipokea...

"Njoo ofisini kwangu," sauti ya bosi wake, Kwizera K. Kwizera au KK kama wafanyakazi wake ofisini walivyozoea kumwita, ilisema na kukata simu bila kusubiri jibu.

Ilikuwa tabia isiyoeleweka ya bosi wake huyo. Kuna wakati akiwa nje ya ofisi alimpigia Poaba Wilabo simu ya mezani kupitia sekretari na kumuunganisha, hali ambayo iliweza kumfanya Poaba aamini bosi wake huyo yupo ofisini kumbe sivyo.

Ni mpaka pale Poaba Wilabo alipokosa kuliona gari nje ndipo alijua mkuu wake wa kazi aliunga kwa sekretari.

"Ndiyo bosi..." Poaba Wilabo aliitikia wito akiwa ameshakaa kwenye kiti akimtazama KK kwa macho yaliyojaa nidhamu ya hali ya juu.

"Aaa..! Una taarifa gani mpya?" KK alianza kwa kuuliza...

"Bado nafuatilia mkuu. Lakini ndani ya siku mbili itakuwa tayari," alijibu Poaba Wilabo huku akimwangalia KK kwa macho ya kusubiri kukosolewa kwa maneno kwamba ni mzembe na mvivu wa kazi japokuwa kiasili, Poaba Wilabo hakuwa na tabia ya uzembe na uvivu na ofisi imekuwa ikimpeleka yeye kwenye kazi ngumu na za hatari lakini zinazotaka akili na maarifa badala ya nguvu...

"Una taarifa gani mpya za leo?" KK aliuliza tena, safari hii sauti yake ilitoka kwa nguvu na alifafanua kidogo...

"Ooh! Hapana mkuu, sina...sina..."

"Kuna mauaji ya kutisha..."

"Hee!" alishtuka Poaba Wilabo huku akimkazia macho bosi wake...

"Mkuu wa Jeshi la Maaskari Nchini, yaani Inspekta Samweli Bonaventure amenipigia simu, anasema Kigamboni, kuna kijiji kinaitwa Kimbiji. Mganga mmoja wa kienyeji amewaua mkewe na mwanaye kwa kuwachinja na kitu chenye ncha kali kisha yeye ametokomea kusikojulikana," alimaliza kusema KK na kunyoosha mkono ili kuchukua gazeti la siku hiyo lililokuwa mezani kwake...

"Du! Mauaji makubwa sana. Maiti za marehemu ziko wapi?" aliuliza Poaba Wilabo...

"Marehemu wanazikwa leo, Temeke. Mauaji yalitokea juzi mtuhumiwa hajakamatwa."

"Wote?" aliuliza Poaba Wilabo lakini bosi wake hakumjibu swali hilo na kubaki akimwangalia tu kama ambaye moyoni alisema, 'swali gani hilo wakati nimekwambia wanazikwa leo. Kama angekuwa mmoja si ningesema anazikwa leo.'

"Sawa bosi, najipanga ili kesho asubuhi nifuatilie," alisema Poaba Wilabo akisimama na kuondoka zake.

Alijua swali lake la mwisho kwa bosi wake lilikuwa la kipuuzi na ndiyo maana hakumjibu.

Alipofika mlangoni, Poaba alisita kufungua, akageuka kumwangalia KK akitaka kumuuliza swali, kwamba akifika Kimbiji amuulizie nani lakini akapuuza kwa sababu kwa vyovyote vile, sehemu iliyotokea mauaji makubwa kama yale haiwezi kujificha.

Aliwaita wafanyakazi wenzake watatu ambao kwa ngazi ya utendaji walikuwa chini yake, Charles John, maarufu kama Mkongo, Venance Mkude na dereva Fanueli Makweta.

"Kesho asubuhi tunakwenda Kijiji cha Kimbiji, kipo nje kidogo ya Kigamboni. Kuna mauaji makubwa. Mganga wa kienyeji anadaiwa kumchinja mkewe na mtoto wao. Naamini kila mmoja wenu anajua aandae nini..." Poaba Wilabo aliwaambia.

"Ndiyo bosi," wote waliitika kwa pamoja. Wakaondoka zao.

************

Barabara haikuwa nzuri sana kwenye baadhi ya maeneo, hivyo ilimlazimu dereva Fanueli kutumia ustadi kuhakikisha Kijiji cha Kimbiji kinafikiwa na kazi iliyowapeleka inafanyika. Hapo ni baada ya Poaba Wilabo kumpigia simu Mkuu wa Jeshi la Askari, Samweli Bonaventure na kuomba baadhi ya taariza za awali.

Mbele ya safari, barabara inayoweza kupitika na magari ilifikia mwisho, ikabaki njia inayoweza kupitisha waenda kwa miguu, baskeli au pikipiki kama kutakosa namna.

"Jamani tumepotea nini?" aliuliza dereva Fanueli huku akifunga breki.

Mbele yake yalisimama majani ya kuweza kufika usawa wa mabegani kwa mtu mfupi ambaye angetaka kupita.

"Jana KK aliniambia askari walifika hadi kijijini na kuchukua miili. Sasa mbona hakuna dalili kama kuna gari lilipita?" alihoji Poaba Wilabo kwa sauti yenye mshangao.

"Au labda askari walisimama hapahapa tulipo, wakafuata miili kwa miguu, " alisema Venance.

Wote wakacheka wakiamini ni utani na kuchangamsha waliyomo ndani ya gari lao aina ya Rocky.

Mara, walitokea wanawake wawili wakiwa na watoto watatu wenye umri wa makadirio kati ya miaka sita, tisa na kumi na moja. Wale watoto walikimbilia porini baada ya kuliona gari limesimama na ndani kuna watu wanne. Wanawake walijipa ujasiri, wakasalimia...

"Eti, barabara ya kwenda Kimbiji ni ipi?" aliuliza Fanueli baada ya sekunde kadhaa za salamu...

"Ni hiihii. Gari linapita kwenye hayo majani. Kule mbele mtakuta barabara nzuri," mmoja wa wale wanawake alijibu kwa sauti iliyojaa unyenyekevu wa malezi...

"Mbona hakuoneshi kama magari yanapita," aliuliza Poaba Wilabo.

"Yanapita. Juzi kuna gari la askari lilipita, sema kwa sababu usiku wa kuamkia leo kuna mvua ilinyesha ndiyo maana hakuna alama za magurudumu," aliendelea kujibu yule mwanamke.

Poaba Wilabo na wenzake walimwelewa, wakashukuru kwa sauti, wakaendelea na safari yao wakipita na gari ndani ya majani marefu. Walitokea sehemu yenye barabara iliyo dhahiri, lakini siyo kwa kiwango cha lami.

MAITI JUU YA MKANJU

Kijiji cha Kimbiji kilikuwa umbali wa kilomita zisizopungua hamsini na tano kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Kijiji kilitulia ingawa ulikuwa muda wa harakati za watu kutembea huku na kule kwa ajili ya kujitafutia riziki ya siku hiyo. Hakukuonekana ubize wa wananchi kutoka sehemu moja kwenda nyingine kama zilivyo desturi za watu katika maeneo yao.

Baadhi ya watu wazima walisimama katika vikundi kwenye maeneo mbalimbali kama vile nje ya nyumba, chini ya miti na katika vibaraza vya maduka. Hali hiyo peke yake ilidhihirisha kuwa, kweli katika kijiji hicho kuna mauaji yalitokea.

Wanakijiji walipoliona gari, waliacha kuongea na kulikazia macho. Hakuna aliyeonesha kulifuata.

Poaba Wilabo alishuka sanjari na wenzake huku akitoa maelekezo kadhaa ya kikazi. Walitembea kuelekea kwa wazee watatu waliosimama nje ya nyumba moja, jirani na walipoegesha gari...

"Shikamoni wazazi," alisalimia Poaba Wilabo huku akichomekea shati vizuri ndani ya suruali ya kadeti nyeusi aliyoivaa siku hiyo...

"Marahaba...marahaba...marahaba, karibuni."

Marahaba zilikuwa nyingi kwa sababu, baada ya Poaba Wilabo kusalimia, wenzake nao walisalimia kama yeye.

"Asanteni, tumekaribia. Aaa...sisi tunatokea Dar, Taasisi ya Self Investigation Unit au kitupi, SIU. Tumekuja kufuatilia mauaji ya mwanamke na mtoto wake, waliyochinjwa na anayedaiwa ni mganga wa kienyeji ambaye ni mume wa mwanamke huyo na baba wa mtoto," alisema Poaba Wilabo akiinyoosha lugha ili aeleweke sawasawa.

Hakusita kuitaja taasisi yao kwa vile ni maarufu sana nchini.

Wale wazee watatu waliangaliana kwa nyuso zilizomaanisha kutaka kujua, kati yao nani awe mzungumzaji na wageni hao...

"Aaah! Ni kweli. Mauaji yametokea kwenye nyumba ile pale juu. Lakini mwenyekiti wa kijiji hiki angesaidia sana kuongea na nyinyi," alisema mzee mmoja kwa sauti iliyojaa hali ya kusumbuliwa na uvutaji mbovu wa sigara, kwani hata wakati huo alikuwa ameshika sigara baghairi ya kukohoa...

"Ni kweli, hata sisi ilikuwa tufike hadi huko kwa mwenyekiti," alisema Poaba Wilabo.

'Ngoja nikamuite," alisema mzee mwingine huku akiondoka.

Wakati anaondoka mzee huyo anakwenda kumwita mwenyekiti, yule mzee wa kwanza kujibu, aliwachukua Poaba Wilabo na wenzake na kwenda nao kwenye nyumba yalipotekelezwa mauaji ya kutisha na mganga huyo.

Ni nyumba ya miti na udongo, iliyoezekwa kwa makuti na kuifanya kuwa na sifa ya nyumba ya kijijini kwa asilimia mia moja.

Mlango wa mbele ulikuwa wazi, hivyo kutoa nafasi ya mtu wa nje kuona ndani bila kizuizi. Poaba Wilabo aliweza kuona vizuri ndani na kubaini kuwa, ukiingia unakuwa umefika sebuleni. Kushoto na kulia, kuna vyumba. Kwa hiyo, ni sawa kusema nyumba hiyo ina vyumba viwili na sebule. Hakukuwa na mlango wa kutokea uani. Hakukuwa na ua.

Kuanzia nje ya mlango kuelekea ndani damu zilizoganda ziliifanya ardhi ionekane nyeusi. Hali ilitisha! Ilitisha kwa maana ya kutisha! Hata mzee aliyempekeka Poaba Wilabo na wenzake, alisimama kwa mbali kama aliyetarajia kutokea kwa lolote na kwa muda wowote.

"Eti ni kweli mganga mwenyewe alikimbilia kusikojulikana?" aliuliza Poaba Wilabo swali lililoonesha ni la kupotezea muda wakati wakimsubiri mwenyekiti wa kijiji.

"Ndiyo. Kuna madai kwamba alikimbilia hukohuko mlikotokea nyiye," alijibu mzee yule akimaanisha mtuhumiwa alikimbilia Dar es Salaam baada ya kuua.

Kutokea upande wa chini wa kijiji hicho, mzee aliyemfuata mwenyekiti alitokea akiwa ameongozana na wazee wengine wawili. Ni hakika mmoja katika wazee hao, ndiye mwenyekiti wa kijiji hicho.

"Hamjambo?" mzee mmoja alisalimia.

"Hatujambo mzazi," Poaba Wilabo aliitikia na kumalizia na shikamoo kutoka kwenye vinywa vya wote waliotoka Dar kufuatilia mauaji hayo.

Poaba Wilabo alionesha bila shaka uso wenye subira ya kutambuliswa kati ya wale wazee wawili wapya, mwenyekiti ni yupi!

'Jamani, mimi naitwa Abdallah Mngaya. Ni mwenyekiti wa Kijiji cha Kimbiji. Karibuni sana."

Utambulisho huo haukumfanya Poaba Wilabo kuongeza neno, ila akasema:

"Asante mzazi. Mimi naitwa Poaba Wilabo...huyu Charles John...yule Venance Mkude...huyu huku Fanueli Makweta...

Wakati Poaba Wilabo akitambulisha, mwenyekiti alikuwa akitingisha kichwa kwamba, anaelewa...

"Wote ni maafisa kutokea Dar es Salaam. Ila mimi ni mpelelezi wa kutokea mbali sana..." Poaba Wilabo alijikuta akisema hivyo...

"Mbali...kuzimu au?" mwenyekiti alidakia. Wote walicheka kibinadamu, halafu Poaba Wilabo akaendelea...

"Tumekuja kufuatilia mauaji yanayodaiwa kufanywa na mganga wa kienyeji kwa kumchinja mkewe na mwanawe..."
Sura ya Poaba Wilabo ilionesha simanzi na pole.

Mwenyekiti alitingisha kichwa. Ni wazi alionesha kusubiri maswali...maana alisema tena 'karibuni sana'.

"Labda tu kwa kuanzia mwenyekiti, baada ya mauaji, askari walipofika walisemaje kabla ya kuchukua miili?" alianza kuuliza Poada Wilabo huku akimwangalia mwenyekiti kwa macho pima kumuonesha kuwa, swali hilo ni lake bila shaka yoyote...

"Askari walisema muuaji ameshakimbia mbali. Kwamba, hawezi kufanya mauaji makubwa kama haya halafu akabaki," alijibu mwenyekiti...

"Turekebishe hapo kwanza mwenyekiti. Mganga kwa sasa si muuaji, ni mtuhumiwa wa mauaji. Inawezekana hata yeye hakuua na walioua walimchukua mganga kwenda naye kusikojulikana," alisema Poaba Wilabo kwa uso wenye uhakika...

"Sawasawa ndugu mpelelezi kutoka kuzimu," mwenyekiti alijikuta amembatiza jina Poaba Wilabo.

Baadhi ya wanakijiji walifika kwenye nyumba hiyo baada ya taarifa kuenea kwamba, kuna wapelelezi wametokea Dar es Salaam.

"Je, mwenyekiti...haiwezekani kwamba baada ya mauaji, mtuhumiwa alikimbilia kwenye mashamba yale kule juu kwa ajili ya kujificha?" Poaba Wilabo aliuliza swali lililomfanya mwenyekiti kuachia tabasamu la dharau na kukosoa uelewa wake...

"Haiwezekani! Hata askari wamekataa. Hata mimi nakataa. Kila mtu hapa atakataa," alijibu mwenyekiti huku akigeuka kuwaangalia wananchi wake, kila mmoja kwa zamu yake kama aliyekuwa akiomba maoni yaliyofanana na yake na si kinyume cha hapo.

Baadhi ya wananchi aliyokutana nao macho walitingisha vichwa kukubaliana na yeye.

"Oke. Inasemekana kuwa, siku ya tukio, mtuhumiwa alitokea shamba. Na usiku wake ndiyo mauaji yakafanyika baada ya.mzozo mkubwa. Kweli si kweli?"

"Kweli," alijibu mwenyekiti.

"Pia kuna madai kwamba, mtuhumiwa alikimbia, lakini ameacha baskeli yake ndani! Amekimbia amevaa nguo alizotoka nazo shamba, kwani moja ya suruali zake nzuri ndani, ilikutwa ina noti ya shilingi elfu mbili. Kweli si kweli?"

Mwenyekiti alianza kuonesha uso wenye umakini kuliko awali. Hakujua maswali ya Poaba Wilabo yanakwenda kumalizikia wapi!

"Ni kweli."

"Askari wanajua yote haya?"

""Ndiyo, askari wanajua yote. Tulikuwa wote wakati tukiyagundua," alijibu mwenyekiti.

Poaba Wilabo aligeuka kuangalia nyuma kwa mbali. Mteremko mkali kuelekea bonde lenye shamba kubwa la miwa na ukivuka, ni kilima kuelekea katika shamba la mahindi na mikanju au miti ya mikorosho ya hapa na pale ndicho alichoona...

"Mwenyekiti mimi nakataa kwa kusema kwamba, mtuhumiwa hajakimbia. Sababu za kukataa ziko mbili kama siyo tatu. Kwanza, kwa sababu tunajua mtuhumiwa alifanya tukio lile usiku, kwa hiyo katika kukimbia asingeacha baskeli yake maana ndiyo angeitumia kukimbilia huko...

"Pili, mtuhumiwa asingeweza kukimbia bila kuchukua ile noti ya shilingi elfu mbili kwenye mfuko wa suruali. Kwani ingemsaidia mbele ya safari," alisema Poaba kwa sauti isiyojaa mzaha.

"Lakini askari walisema amekimbia zake. Tena na wao wametumia vigezo vyao vya kitaalam," mwenyekiti alipingana na mtazamo wa Poaba Wilabo.

Kisha maneno ya; 'atakuwa amekimbia' yalitawala kutoka kwa wanakijiji waliyokuwepo...'amekimbia...amekimbia....amekimbia yule...'

"Hajakimbia. Mimi nashauri kitu kimoja. Tuingieni kwenye mashamba yale kule juu tukamtafute, awe amekufa au yu mzima," alisema Poaba.

Baadhi ya wanakijiji walichekea kwa chini kicheko cha kumshangaa Poaba. Lakini wengine waliunga mkono wazo lake, kwamba ni sahihi wakamtafute kwa hiyo kwao ikawa siyo muhali.

"Tena jamani! Lile shamba la miwa na lile kule juu la mahindi lenye mikorosho, ni ya mtuhumiwa," alisema yule mzee aliyemfuata mwenyekiti nyumbani kwake.

Poaba Wilabo na timu yake, wanakijiji nao wakiongozwa na mwenyekiti walishuka bondeni wakikatiza kwenye shamba la miwa na kutokea katika shamba la mahindi na mikorosho.

Walitembea kwa safu safu au makundi. Mfano, mwenyekiti alikuwa na wazee wenzake watatu, Poaba Wilabo yeye aliongozana na maafisa wenzake aliyokwenda nao, akina Charles na kadhalika na kadhalika.

Licha ya mazungumzo, lakini karibia kila mtu alikuwa akitembea kwa tahadhari kubwa kwa kile ambacho kinaweza kutokea ghafla. Hasahasa ilikuwa ni picha ya mtuhumiwa huenda angetokea akiwa ameshika kisu chenye damu nyingi na sura yake ikionesha ukatili wa hali ya juu ya nia ya kutaka kuua tena

"Huyu hapa huyu," kijana mmoja aliyekuwa mbele kabisa alisema kwa sauti yenye mshtuko huku akikimbia kuwaelekea watu wengine wa nyuma yake ambao nao walitimua mbio wakiamini mtuhumiwa yuko nyuma ya kijana huyo akiwakimbiza na kisu mkononi tayari kwa kuchinja mwingine.

Itaendelea...

osanjelus@gmail.com
IMG_20220410_001338_752~5.jpg
 
osanjelus@gmail.comView attachment 2182157

Safi sana, tuongezee kipande kingine
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom