TUONGEE ASUBUHI: TV Live interaction on Star TV Yazinduliwa Rasmi

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
Naona Star TV wamezindua mpango mpya katika Kipindi cha Tuongee Asubuhi, Kwanza Hongereni na pia kazeni uzi na isiwe ni nguvu ya soda.

Nimemsikia Yahya analalamika kuwa account yake ya JF hawezi kuifungua tena, hivi na huku hackers wapo au nia je mkuu invicible?

Tuwape ushauri, mie binafsi nimependa mtindo huu ila nahisi wangebadili na mfumo wa Studio yao ikawa na maandhari mpya.


ADIOS
 
Mimi naitwa Fredy Kayombo nipo Arusha.

Ninapenda kutoa pongezi nyingi kwa waganda kutengeza hiyo gari, ingawa inatumia muda mrefu kuichaji lakini inaenda kilomita chache, good start.
 
Kuhusu muonekano, ule uaisilia umekwenda wapi?

Na kuhusu ARV bandia ni hao hao serikali na hao watu wao wa procurement ndio wabanwe. Na tatizo linasababishwa na uwepo wa kampuni tofauti, mara india, mara wapi.

Zingekuwa zinatoka nchi moja na kampuni moja haya yasingetokea.
 
Kuhusu kipindi:
Jambo lolote linapoanza huwa na challenges nyingi; lakini bado nadhani kupokea simu LIVE studio ni issue ambayo inabidi iangaliwe. Zina risks zake nyingi.

Kwa ARV bandia:
Yahya, nchi yetu tuna kitengo cha "Medical Intelligence"? Kama kipo, kazi yake nini? Ni kitengo muhimu kwa idara ya kijasusi ya Tanzania (TISS) na kama kipo basi kime-prove failure!
 
Yahya napongeza Star TV kwa kukubali kushiriki kuelimisha Watanzania juu ya mabadiliko, naomba mafundi wenu wajitahidi kupata uzoefu.

Kuna mambo mbalimbali ambayo hawabadilishi, kwa mfano utakuta Yahya au mtangazaji anaongea na mgeni studio lakini camera inammulika mtangazaji ambaye wakati huo haongei badala ya kummulika mzungumzaji, sasa najiuliza kama wanajisahau au wanafanya makusudi au hawapo smart?

Naomba Program Manager awe makini kufuatilia mambo madogo kama hayo kwani yanaondoa ule utamu wa kipindi
.
 
Mmependeza

1. Mkuu wa wilaya anatakiwa ashtakiwe kwa kutokuwa na choo. Anaposema hana choo, paa linavunja anataka nani amchimbie choo na nani amjengee nyumba? Ashtakiwe tafadhali

2. Dawa yoyote ambayo haitoi tiba sahihi ni feki/bandia. Acheni maneno yenu hapo studio. Kwani neno bandia lina maana gain. Kwanza inakuwaje tunasikia kuna dawa zisizo na viwango zimekamatwa lakini hatusii mtu yeyote kakamatwa kuhusiana na dawa hizo

3. Kilimanjaro International Airport ipo mkoa wa Kilimanjaro sio Arusha.

4. Uwanja wa ndege wa Mwanza hata ukiitwa "Igembe Nsabo" kama kuna nia ya dhati ya kuvutia watalii wakuja tuu. Kubadili jina sio solution. Kwanza kanini watalii watufanye tubadilishe jina la uwanja wetu? Acheni hizo.

Filemoni Tenu
 
Yahya napongeza Star TV kwa kukubali kushiriki kuelimisha Watanzania juu ya mabadiliko, naomba mafundi wenu wajitahidi kupata uzoefu, kuna mambo mbalimbali ambayo hawabadilishi, kwa mfano utakuta Yahya au mtangazaji anaongea na mgeni studio lakini camera inammulika mtangazaji ambaye wakati huo haongei badala ya kummulika mzungumzaji, sasa najiuliza kama wanajisahau au wanafanya makusudi au hawapo smart?

Naomba Program Manager awe makini kufatilia mambo madogo kama hayo kwani yanaondoa ule utamu wa kipindi

very critical
 
Mkuu wa wilaya anapoishi nyumba haina choo, je anawezaje kuhamasisha wananchi wawe na vyoo?

Mh huyo ameshindwa kuchimba choo kwa kutegemea awekewe na serikali ambayo sasa inaonekana imezidiwa majukumu yake, anapashwa kuwa mbunifu siyo kulalamika kwa mambo kama haya anaidharirisha serikali yetu ndani na nje ya nchi.
 
Niwashukuru sana G.T's wote kwa michango yenu mizuri sana

Tumeanza awamu hii mpya kama alivyobainisha hapo juu ya ufupi GR. Tutakuwa na interaction na wadau wetu kwa karibu sana sasa kuliko wakati mwingine.

Na utaratibu huu utakuwa unatumika kwa juma zima kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.

Utaratibu wetu wa JUmapili unabaki kama ulivyo, bila kusahau tutakuwa katika mada ya Ipi Misingi ya Amani Sehemu ya NNE.

Niwashukuru sana na tukutane kesho katika mjadala wa kipindi kwa yote yanayojitokeza, kuanzia item za habari, uchambuzi wa magazeti, makala fupi ndani ya kipindi na hatimaye katika mjadala wa kina wa siku.

Kwa niaba ya Timu iliyoshiriki leo katika matangazo ya moja kwa moja niwashukuru sana na kuwatakika siku njema


Ahsanteni sana
 
Swali zuri sana mkuu lakini wanahabari kuuliza mambo yanayohusu TISS wanaogopa kweli wakati enzi za intelligence system kufanya kazi kwa usiri mno zimepita!

Umehoji jambo jema sana lakini nani apulize filimbi?
 
Hii news ya ARV Bandia ndugu yetu Kibonde imemkasirisha sana na anaikemea sana kila siku.... na sio hizo tu Walianzia kwenye dawa za Malaria wakapata faida Serikali yetu haina mkono mrefu so wameingia kwa wenye HIV hii nchi inaenda ndivyo sivyo...

Kuwe na sehemu maalum zinazotoa hizo dawa original na wengine wakikutwa nazo washitakiwe mara moja sio kesi iendeshwe miaka na miaka hadi watu wanasahau...
 
Ni ukweli unaosikitisha hili swala la madawa feki serikali inahusika ndio maana wako kimya kwa nchi hii chini ya CCM kila kitu ni deal hii ndiyo sera ya CCM .UFISADI KILA KONA.
 
Back
Top Bottom