KipimaPembe
JF-Expert Member
- Aug 5, 2007
- 1,285
- 696
Muundo wa muungano uko "flawed" na hilo linaeleweka. Muundo si mbaya kwa sababu muundo wa serikali mbili hauwezekani, la hasha; muundo ni mbaya kwa sababu walio madarakani wamekataa kuufanyia kazi muundo huo kuurekebisha. Mambo mawili muhimu sana ambayo hayajawekewa mipaka vya kutosha na ambayo yatakuja kuusambaratisha huu muungano ni yafuatayo;
Lakini mpango wa wanasiasa wetu wengi dhaifu dhaif imekuwa ni kuahirisha matatizo. Wengi wanasema "haya hata mwalimu yalimshinda". Hakuna kingozi yeyote ambaye ameonesha nia na mwenye uwezo wa kuyashughulikia mambo hayo makubwa mawili. Approach imekuwa ni kuahirisha matatizo na kutarajia yatajimaliza yenyewe, tujue kwa uhakika kabisa haya mambo hayatajimaliza yenyewe! Au yakijimaliza yenyewe yatajimaliza kwa njia ambayo wengi wetu hatutarajii.
- Mambo yasiyokuwa ya muungano kwa upande wa bara kushughulikiwa na serikali ya muungano bila muongozo wa aina yoyote (yaani inategemea busara ya viongozi waliopo) - Yaani hapa assumption ni kuwa siku zote rais wa muungano atatokea bara. Siku akitokea rais Zanzibar, G55 mpya itazaliwa na Mwalimu wa kuisambaratisha hatakuwepo - Muungano utatumbukia kaburini
- Nafasi ya Serikali ya mapinduzi zanzibar na rais wa Zanzibar ndani ya serikali ya Jamhuri ya Muungano ni ipi? Hapa kumekuwa na kufunga bandeji kidonda mara kwa mara bila kukitafutia tiba ya kudumu. Kila ikijitokeza migogoro hapa na pale wakubwa wanakubaliana makubaliano ya behind scenes ambayo mengi yanaishia watu kupewa vyeo vikubwa vikubwa bila kuweka wazi hasa makubaliano yalikuwa ni nini! Katika mambo ya muungano na ndani ya serikali ya muungano rais wa Zanzibar hatakiwi kupewa hadhi ya urais wa zanzibar - wakati wa karume alisimama kama makamu wa Rais. Sasa hivi ni waziri asiye na wizara ......... haha; hapa pana mushkeli sana tu!