Tundu Lissu Umepotoka!

MUUNGANO WENU MNAOBISHANIANA UPO HIVI:

TANGANYIKA + ZANZIBAR = TANZANIA + ZANZIBAR.

Tanganyika ilikuwa nchi
Zanzibar ilikuwa nchi.

Baada ya Muungano matokeo

Tanzania ni Jamuhuri ya muungano wa nchi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar then Zanzibar inabakia kuwa ni nchi huru ndani ya muungano.

Hapa ndipo kwenye kiini cha matatizo yenu yote na hayatakaa yaishe mpaka mkae muamue mfumo mwingine.
 
Hivi si wazanzibar hawautaki muungano? Ni vipi tena wanalilia kushiriki ktk hili?! Ingekuwa njia rahisi sana kwao kujitoa kwa amani kwa kukataa kushiriki ktk mchakato huu.

Nafikiri unahitaji kujifunza japo kiduchu sheria za nchi yako.

Kumbuka kuwa Wabunge kutoka Zanzibar wapo hapo Bungeni kwa mujibu wa sheria za JMT kama ambavyo wenzao wa bara walivyo. Usikae na kujidanganya kuwa wapo hapo kwa Ihsani za watu wa Bara.

Na kumbuka inayojadiliwa hapo ni Katiba ya Muungano sio ya tanganyika. Hivyo wapo hapo kutetea maslahi ya Zanzibar katika muungano.
 
<font size="4">Kwani</font> <font size="4">issue hapa ni nini???</font>
&lt;br /&gt;<br />
&lt;br /&gt;<br />
ISSUE NI KAMA IFUATAVYO MENGINE YOTE MNAKANYAGA VICHAKA TU,KWANINI<br />
1.TANGANYIKA + ZANZIBAR= TANZANIA<br />
2.TANZANIA-TANGANYIKA= ZANZIBAR<br />
3.TANZANIA-ZANZIBAR=TANZANIA? KWA NINI ISIWE TANGANYIKA ?UKIWEZA KUJIBU SWALI HILI UTAKUWA UMEMALIZA MZIZI WA FITINA NA MALUMBANO YOTE
 
Rais wa Zanzibar ni waziri katika serekali ya JMT ni makosa makubwa sana kumpatia madaraka sawa na rais wa JMT.Zanzibar walibadili katiba yao wakaunda serekali ya umoja wa kitaifa Tanzania bara haikuhusika kuwamulia jambo lolote Zanzibar iweje mambo yasiyohusu muungano waZanzibar watuamulie ?.

Katiba ya Tanzania ni jambo la Muungano
 
Namuunga mkono lisu mia kwa mia, alichoengea mambo ya msingi, na huo usawa wanaotaka wazbr mbona haupo! Kwani wao wenyewe tunawasikia wakilalama kwy mambo kazaa ya kazaa kama vle kuna mbunge alihoji juu ya timu ya taifa kutokuwa na mchezaji kutoka kwy club za znz, hata pia kulalamikia kwy mambo mengi tu ya kudai wabara wanawanyonya waznbr. Mi naona bora hata huo muungano uvunjwe kila mtu afe na chake.
 
Tundu Antipas Mungwali Lissu, (Mb-Chadema) na msemaji wa kambi ya upinzani katika wizara ya katiba na sheria, jana akiwasilisha hotuba ya kambi ya upinzani ya wizara ya hiyo alisema kati ya mengi mambo ya upotofu, upotoshaji hivyo itahalis tukisema Tundu Lissu amepotoka.

Katika hotuba hiyo , wakati akitoa maelezo kuhusu mswada wa kuandaa utaratibu wa kutoa maoni ya mabadiliko ya katiba mpya ya JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, Mhe. Lissu alisema muswada huo bado una dosari hivyo kambi ya upinzani haikubaliani nao.

Kati ya dosari nyingi alizozitaja miongoni mwao ni uwepo au ushiriki wa Zanzibar kama mshiriki kamili wa mustakbai wa mabadiliko ya katiba hiyo. Mhe. Lissu alipotoka na kujipotosha aliposema:

a). kuwa mamlaka sawa aliyopewa rais wa Zanzibar na rais wa muungano hayakubaliki kwa kuwa yamefanywa "...kuwaonea huruma Wazanzibari baada ya kulalamika, kwa vile ilitosha rais wa zanzibar "...kuhusishwa tu.." na siyo kuwa na mamlaka sawa na rais wa muungano.

b). Wazanzibari wasishirika katika mchakato wa marekebishoa ya katiba katika mambo ya Tanzania bara kama vile Tanzania bara ilivyokuwa haikushirika katika mabadiliko ya katiba yao (mabadiliko ya kumi ya ktiba ya zanzibar ya 1984).

c). Katika uamuzi wa kupitisha katiba kilelezo "utaweka rehani " mustakbali wa mabadiliko hayo kwa vile iwapo Wazanzibari wakikataa na wabara wakikubali katiba hiyo haitapita, hivyo mchakato huu usiwekwe reheni na "siasa za Zanzibar".

MAWAZO YANGU:

Naamini Mhe. Tundu Lissu amefanya upotofu wa makusudi na anayefanya upotofu wa makusudi hawa amepotoka yy mwenyewe kwa vile:

a. Mhe. Lissu anajuwa kuwa muungano huu umeundwa kwa mkataba na siyo katiba na mkataba huo ndiyo unaotoa usawa wa mamlaka za nchi mbili kati ya Jamhuri ya watu wa zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika, katika yale mambo tuliyokualiana likiwamo la katiba ya Jamhuri ya Muungano.

b. Ushiriki wa Zanzibar katika mabadiliko ya katiba ya muungano siyo wa "hisani" bali haki yao na usawa walionao kwa mujibu wa makubaliano ya muungano na katiba hii hii mbovu, Mhe Lissu, kusema kuwa Zanzibar isihusike na mambo yasiyo kuwa ya muungano katika katiba hii ni kauli yakichekesho na aibu (nachelea kusema ya kipumbavu) kutoka kwa kinywa cha mwanasheria msomi aliyebobea. Mhe. Lissu anajuwa kuwa kinachofanyiwa marekebisho/mabadiliko hapa ni KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SIYO YA TANGANYIKA?

Hapa alikuwa Mhe, Lissu, aje na hoja nyingine ya IPO WAPI KATIBA YA TANGANYIKA WAKATI ZANZIBAR WANAYO KATIBA YAO? ambayo itakuwa na mambo ya Tanganyika kama vile Zanzibar na Wazanzibari haitawahusu.

Ndiyo hapa wazanzibar wanapata na watapata uhalali wa kuikubali au kuikataa katiba ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ambayo hatutakubali tena iingizwe mambo yasiyokuwa ya muungano, hivyo wala hatutakuwa na sababu ya kuyagusa.

c. Mhe. Lissu, anasema mambo kwa ujumla jumla, nani ataweka rehani hapa upitishwaji wa katiba hii? ni Wazanzibari au walioweka utaratibu huo kuwa katiba hiyo haitatumika mpaka ipate ridhaa ya pande mbili za muungano na kila upande kivyake! kwa akili ya Tundu Lissu watakao kataa ni wazanzibari tu,wakikataa Watanganyika je? si na wao watakuwa wameweka rehani mustakabali wa mabadiko haya kwa "siasa za Tanganyika?"

Hata hivyo, bado nakubaliana na maelezo mengine ya Mhe. Tundu Lissu kuwa mchakato huu uwape fursa watanzania waamuwe kama wanautaka muungano na wa aina gani?

wewe na magamba wenzako ndo wapotoshaji kabisa hamna lolote nyinyi mnataka kuhodhi mchakato wa katiba ili muweke matakwa yenu. hatukubali wewe ndo mpotoshaji pamoja na wazir wako
 
Mfumo mzima wa muungano unawalakini japo ni lazima muungano uendelee. Nilishawahi kulizungumzi hili kwa undani ila nitarudia tena leo ni kwa nini hatunabudi kuendelea na muungano huu hata kama tunauona ni batili.

Jiulize ni kwa nini Hongkong na Tibet zinabaki katika Jamhuri ya watu wa china japo wachina wangependa kupunguza ukubwa wa nchi yao na wingi wa watu je isingekuwa vyema kuziacha Hongkong na Tibet zikajiendesha zenyewe? Jibu ni sawa na Zanzibar na Tanganyika na Jamhuri ya muungano wa Tz.

Zanzibar ni vital land katika maswala ya ulinzi kama zilivyo Hongkong na Tibet. Leo hii Zanzibar ikijitenga na muungano wa Tanganyika na kubaki Zanzibar itakuwa ni vigumu kwa Tanganyika kukaa kwa amani kwani kushambuliwa kutokea Zanzibar ni vyepesi na itakuwa na advantage kubwa kwa adui. ( Maelezo zaidi siwezi yaweka hapa ila jaribu kutafuta wataalam wa jeshi letu watakueleza kwa marefu na mapana ni kwa nini watafia kuulinda muungano kwa sababu za kiusalama.)

Kisha tujiulize ni kwanini historia ya zanzibar haifundishwi zanzibar katika shule zao? Wazee wa Zanzibar wanajua nini hasa kiini chake na ni aibu kufahamika kwa waliyokuwa wanafanyiwa na waarabu enzi za kutawaliwa. Hofu na busara za kuilinda Zanzibar isirudi kwa waarabu ndio msingi mwingine wa muungano.

Mahitaji mengi ya vyakula yanatoka bara kwa kiasi kikubwa hivyo kimantik zanzibar inalishwa na bara kwani zanzibar sio wakulima wazuri wa mazao ya vyakula na wanyama kama tulivyo bara. Leo hii kariakoo imejaa wafanyabiashara kutoka zanzibar ambao ni wapemba hivi muungano ukivunjika hawa tutawarudisha vipi kwao. Kuna wanasiasa wengi ambao wamepata misaada mingi kutoka Omani kujaribu kuleta hoja za kuuvunja muungano lakini wameshindwa kwani pindi muungano ukivunjika tu waarabu wa Omani wengi watajipenyeza na kulichukua taifa la zanzibar na kufufua historia iliyokufa na inayoelekea kusahaulika.

Nadhani ipo haja ya kuirudisha historia ya Zanzibar na ifundishwe kwa uwazi tuone kama kuna mzanzibar atakayethubutu kujaribu kuumba muungano uvunjike. Au leo tuseme tunaenda kufanya uchaguzi zanzibar na tuondoe majeshi ya bar yaliyoko zanzibar tuone kama waarabu wa Omani hawajajipenyeza na kuichukua zanzibar kwa njia yoyote.

Ipo haja ya dhati kuupita muundo mzima wa muungano ili kuondoa migogoro japo serikali iliyoko madarakani imeshindwa kufanya hata hili japo inatambua mchango wa muungano wa faida zake za kiusalama kwa taifa kwa ujumla. Tukiweza kuunda mfumo wa muungano ambao wazanzibar watajadili mambo yao na watanganyika wakajadili mambo yao kisha wakashirikiana kwa upamoja katika maswala nyeti ya kimuungano basi chuki na hasira zote zitakwishwa na upendo na amani vitaongozeka.
 
Wazanzibari wamekuwa wakisema kila mara wanapopata nafasi ya kuzungumzia muungano kwamba hawautaki. Lakini akitokea mtu wa bara akagusia juu ya huo muungano hasa ushiriki wao katika mamboi yasiyo ya muungano wanakuja juu kama moto wa kifuu.

Pamoja na faida zilizopatikana na zinazoendelea kupatikana kwa Tanganyika na watanganyika kutokana na huu muungano kama vile za kiulinzi na kiusalama kama tunazoelezwa,kwa hapa tulipofika ni afadhali wabaki na zanzibar yao na sisi tubaki na Tanganyika yetu. Hatuna sababu ya kuendelea kuwalea wazanzibar, hapo tulipofika inatosha wachukue hamsini zao na sisi tuchukue hamsini zetu.
 
Kwa maana hiyo mabadiliko ya katiba yanayo wasilishwa na serikali yanamtambua raisi wa ZNZ ni raisi wa taifa kamili na sio sehemu ya muungano na raisi wa Muungano ni Raisi wa Tanganyika (Danganyika)???? Lissu pambana nenda kwa mzee Mtikila akupe falsfa za Danganyikan yetu ilipo potea na namna ya kuipata kwa kuwa mzee huyu hajachoka kuipigania taifa letu
 
Kwa Katiba na muundo wa Tanzania ya sasa inawezekana Zanzibar kufanya mambo yao wenyewe kwa yale mambo yasiyohusu Muungano. Lakini haiwezekani "Tanganyika" kufanya mambo yake nje ya muungano. Hii ni kwa sababu Tanganyika haipo tena, sasa kuna "Tanzania Bara". Kwa mujibu wa katiba mambo ya Tanzania Bara yanashughulikiwa na serikali ya muungano. Sasa kwa vile serikali ya muungano inaihusisha Zanzibar pia basi unakuta kwamba hakuna jambo la Tanzania bara ambalo twaweza lifanya bila Wazanzibari kushiriki. Dawa hapa ilikua ni kwanza kuirudisha serikali ya Tanganyika halafu sasa ndo tukae kujadili kama twataka huo muungano na je uwe katika umbo gani? Kutokuwepo kwa serikali ya Tanganyika kumetuondolea Watanganyika haki na usawa mbele ya Wanzibari ambao wana serikali yao.
 
Tundu yupo right!
Mambo ya Tanzania yatajadiliwa na watanzania wenyewe, ambao ni akina kikwete, Membe, Nahodha, Omar Nundu etc. Bali mambo ya Zanzibar kama yalivyotokea kwenye katiba yao tumeona yalijadiliwa na kumalizwa na Wazanzibar wenyewe.
Sijaona tatizo lolote katika statement za Tundu. Rais wa Zanzibar hawezi kuwaamulia watanzania mambo yao, kwa sababu watanzania wanaye rais wao ambaye alipigiwa kura na watanzania wote (akiwemo rais wa zanzibar). Huwa ninashangaa sana ninapoona protocal ya Urais inapovunjwa kule Zanzibar ambapo rais wa Zanzibar anapokuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za mapinduzi ilhali rais wake yupo hapo hapo kiwanjani!

Inavyoonyesha wazanzibari wengi hawaelewi advantage waliyonayo kwenye muungano huu. Wao ni Wazanzibari kwanza (kwa kuzaliwa) na kisha ni watanzania kwa muungano huu wa kisiasa. Ningekuwa mtanzania/mzanzibari ningempongeza sana Tundu
 
naunga mkono hoja ya Lissu. Hawa wa Rais na Wazanzibar wakazi hawapaswi kuhusishwa ktk kutoa maoni wala kupiga kura mambo yasiyohusu muungano. Wale wanaoishi huku bara 'Wazanzibara' ndio wahusishwe tuu kwani mambo hayo hayawahusu kabisaaaaaaa.....
KWA SISI WATANZANIA BARA HUYO RAISI WA ZANZIBAR NI RAIA TU WA KAWAIDA NA TENA NI RAISI KAMA WA REAL MADRID AU BARCELONA TUUUU.
 
Ndio maana mimi naunga mkono Serikali Tatu kama sio Moja. Maana haya yote yanatokea kwa sababu ya kiini macho cha serikali mbili (ya Zanzibar na Muungano). Inaumiza upande wa Bara
 
Mhe. Lissu yuko sahihi 100% wazanzibar washiriki mambao yanayohusu muungano tu yasiyohusu muungano watuachie wenyewe sasa tatizo ni nini? Mbona wao wazenj wamebadili katiba yao kwa mambo yao bila kutuhusisha sisi.
 
Tundu Antipas Mungwali Lissu, (Mb-Chadema) na msemaji wa kambi ya upinzani katika wizara ya katiba na sheria, jana akiwasilisha hotuba ya kambi ya upinzani ya wizara ya hiyo alisema kati ya mengi mambo ya upotofu, upotoshaji hivyo itahalis tukisema Tundu Lissu amepotoka.

Katika hotuba hiyo , wakati akitoa maelezo kuhusu mswada wa kuandaa utaratibu wa kutoa maoni ya mabadiliko ya katiba mpya ya JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, Mhe. Lissu alisema muswada huo bado una dosari hivyo kambi ya upinzani haikubaliani nao.

Kati ya dosari nyingi alizozitaja miongoni mwao ni uwepo au ushiriki wa Zanzibar kama mshiriki kamili wa mustakbai wa mabadiliko ya katiba hiyo. Mhe. Lissu alipotoka na kujipotosha aliposema:

a). kuwa mamlaka sawa aliyopewa rais wa Zanzibar na rais wa muungano hayakubaliki kwa kuwa yamefanywa "...kuwaonea huruma Wazanzibari baada ya kulalamika, kwa vile ilitosha rais wa zanzibar "...kuhusishwa tu.." na siyo kuwa na mamlaka sawa na rais wa muungano.

b). Wazanzibari wasishirika katika mchakato wa marekebishoa ya katiba katika mambo ya Tanzania bara kama vile Tanzania bara ilivyokuwa haikushirika katika mabadiliko ya katiba yao (mabadiliko ya kumi ya ktiba ya zanzibar ya 1984).

c). Katika uamuzi wa kupitisha katiba kilelezo "utaweka rehani " mustakbali wa mabadiliko hayo kwa vile iwapo Wazanzibari wakikataa na wabara wakikubali katiba hiyo haitapita, hivyo mchakato huu usiwekwe reheni na "siasa za Zanzibar".

MAWAZO YANGU:

Naamini Mhe. Tundu Lissu amefanya upotofu wa makusudi na anayefanya upotofu wa makusudi hawa amepotoka yy mwenyewe kwa vile:

a. Mhe. Lissu anajuwa kuwa muungano huu umeundwa kwa mkataba na siyo katiba na mkataba huo ndiyo unaotoa usawa wa mamlaka za nchi mbili kati ya Jamhuri ya watu wa zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika, katika yale mambo tuliyokualiana likiwamo la katiba ya Jamhuri ya Muungano.

b. Ushiriki wa Zanzibar katika mabadiliko ya katiba ya muungano siyo wa "hisani" bali haki yao na usawa walionao kwa mujibu wa makubaliano ya muungano na katiba hii hii mbovu, Mhe Lissu, kusema kuwa Zanzibar isihusike na mambo yasiyo kuwa ya muungano katika katiba hii ni kauli yakichekesho na aibu (nachelea kusema ya kipumbavu) kutoka kwa kinywa cha mwanasheria msomi aliyebobea. Mhe. Lissu anajuwa kuwa kinachofanyiwa marekebisho/mabadiliko hapa ni KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SIYO YA TANGANYIKA?

Hapa alikuwa Mhe, Lissu, aje na hoja nyingine ya IPO WAPI KATIBA YA TANGANYIKA WAKATI ZANZIBAR WANAYO KATIBA YAO? ambayo itakuwa na mambo ya Tanganyika kama vile Zanzibar na Wazanzibari haitawahusu.

Ndiyo hapa wazanzibar wanapata na watapata uhalali wa kuikubali au kuikataa katiba ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ambayo hatutakubali tena iingizwe mambo yasiyokuwa ya muungano, hivyo wala hatutakuwa na sababu ya kuyagusa.

c. Mhe. Lissu, anasema mambo kwa ujumla jumla, nani ataweka rehani hapa upitishwaji wa katiba hii? ni Wazanzibari au walioweka utaratibu huo kuwa katiba hiyo haitatumika mpaka ipate ridhaa ya pande mbili za muungano na kila upande kivyake! kwa akili ya Tundu Lissu watakao kataa ni wazanzibari tu,wakikataa Watanganyika je? si na wao watakuwa wameweka rehani mustakabali wa mabadiko haya kwa "siasa za Tanganyika?"

Hata hivyo, bado nakubaliana na maelezo mengine ya Mhe. Tundu Lissu kuwa mchakato huu uwape fursa watanzania waamuwe kama wanautaka muungano na wa aina gani?

Upumbavu tu umeandika,mambo yasiyo ya muungano mnataka mjadili ya nini?
 
Bro,
nakubaliana na mawazo yako kifungu I & II ila cha III bado ninakitafakari - ila cha kwanza kina kasoro kidogo - nitajaribu kueleza : RAIS wa Zanzibar katika mabadiliko yanayohusu katiba ya MUUNGANO hapaswi KUPEWA madaraka sawa na Rais wa Jamhuri bali ANAPASWA KUWA NAYO KIKATIBA - mimi ninapinga hii notion ya KUPEANA ina uenyeji ndani yake!!! Kama mimi na wewe tukijenga condominial flat pamoja halafu nikaku-delegate ku-administer na "hisa zangu" basi mimi na wewe tuna haki sawa. Kabla ya Muungano Zanzibar ilikuwa nchi huru kama ilivyokuwa Tanganyika na katika makubaliano yao ni kuwa Rais wa "Tanganyika" ndiye atakuwa Rais wa Muungano - lakini haina maana kuwa awaamulie hata Wazanzibar without any consultation! Tanzania haipo bila ya Zanzibar!!!!

Nimesoma hoja kuwa mbona bara haikushiriki katika kujadili mabadiliko ya katiba ya Zanzibar??? if you read btn the lines utaona hata hili jibu lake lipo katika maelezo niliyojaribu kutoa hapo juu.

Muungano una kasoro nyingi mno na ninafikiri ni wajibu wetu sote kuzijadili bila kufikiri kuwa solutions za matatizo yetu anazo Mh. Lissu pekee - nafikiri kila mmoja ana haki ya kushiriki hata kama si mwanasheria kitaaluma - by the way Tanzania ni ya Watanzania wote bila kujali taaluma zao.

naachia hapo kwa sasa.
 
Upumbavu tu umeandika,mambo yasiyo ya muungano mnataka mjadili ya nini?

badala ya kumwita mwenzio mpumbavu si utoe mawazo/maoni yako??

I think Tanzania as a country has really a rough and long way to go if even those of your kind are considered to be (great????) thinkers!!! God forbid!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom