Tundu Lissu noma, auliza swali jipya bungeni, waziri ashangaa ashindwa kujibu

Yule Livingstone Lusinde uwezo wake ni mdogo sana, yani alichangia vitu vya ajabu sana
kwa hili ninaamini nilimsikia......... ndio maana mzee JSM alisema hajui kilchotokea wakati wa kura za maoni.... nimesikia tetesi kariakoo kuwa alisaidiwa kushinda na wanamuziki (Mapacha3)
 
Usipotoshe watu, pengine kwa kutojua au kwa ushabiki tu wa makusudi. Katika Maswali ya Bunge , Mbunge anpouliza swali la msingi, Mbunge huyo au mwingine yeyote anapaswa kuuliza swali la nyongeza ambalo linaendana na swali lamsingi.

Asubuhi wakati Naibu Waziri wa Viwanda akijibu swali la msingi la Prof. Mwakyusa kwa niaba ya waziri wa Maliasili kuhusu Hifadhi ya Kitulo, Mh. Lissu alisimama na kuuliza kuwa kwa kuwa Sheria yeyote ya Hifadhi ya Misitu inatakiwa kutangazwa kwenye government gazzette, Je, Ni Tarehe gani, mwezi gani mwaka gani, ilitangazwa sheria ya kuanzishwa kwa Hifadhi ya Msitu ulioko Singida.

Kimsingi kwa mujibu wa Kanuni za Bunge ,toleo la Mwaka 2007, hili ni swali jipya ambalo linahitaji ufuatiliaji wa tarehe, mwezi na mwaka wa sheria hiyo ilipotangazwa kwenye gazzette la Serikali. Swali hili linapaswa kuandika kwa maadishi na kupelekwa wizarani ili kutafutiwa majibu.
 
Hamuelewi bunge linavoendeshwa na sheria za maswali zikoje, kama ni swali la nyongeza na halihusiani na swali la msingi hilo huwa swali jipya, na swali jipya lina njia zake za kufikishwa ili lijibiwe kwa kina. Upo hapo ulipo?
 
"Upinzani dhidi ya ukandamizaji ni utii kwa Mungu". Kayasema haya maneno leo bungeni akiwa anaponda misamaha ya kodi kwa makampuni ya madini katika muswada wa sheria ya fedha 2011.
 
Utaratibu ni kwamba Maswali hupelekwa mapema ili yatafutiwe majibu ya kina kabla muhusika hajaingia bungeni, kwa mfano kuna maswali yanahitaji mpaka analysis of data je laweza kujibiwa papo kwa papo?. Kama lilikuwa ni swali la papo kwa papo basi hawajamtendea haki Lisu.
Ni mtazamo tu
Nakubaliana na wewe kuhusu utaratibu wa kuuliza maswali na ukiangalia swali la Lisu ni kati ya maswali yanayohitajika kuwa yamefikishwa mapema kwani lina hitaji tarehe na hakuna anayeweza kukumbuka out of the head dates ambapo mswada au sheria ilipitishwa. Hapa naona Lisu aliteleza maana huwezi kutaka that level of details kutoka kwenye swali la nyongeza.
 
Maswali yote ni lazima yapitie kwa Mh. Microphone then yale ya nyongeza lazima yawe yanahusiana kwa ukaribu na swali la msingi ili kupata ufafanuzi kutoka jibu la kwanza hasa kwa upande wa jimboni mwa mbuge ambaye hakuuliza swali la msingi.
 
Maswali yote ni lazima yapitie kwa Mh. Microphone then yale ya nyongeza lazima yawe yanahusiana kwa ukaribu na swali la msingi ili kupata ufafanuzi kutoka jibu la kwanza hasa kwa upande wa jimboni mwa mbuge ambaye hakuuliza swali la msingi.
 
JAMANI NIMEMSIKIA MHE. TUNDU LISSU, JAMAA KAONGEA VIZURI SANA. ANASEMA

"SERIKALI HAITAKI KUJIFUNZA NA MAKOSA ILIYOFANYA NYUMA ILI HALI INAJUA NI WAPI TULIKOSEA. SASA SERIKALI INATAKA KUWASAMEHE KODI WAWEKEZAJI WA EPZ NA SEZ, KWA MIAKA KUMI.

KWA HILI TUNDU LISSU SI TU KUSEMA BALI NI KUWAAMSHA WATANZANIA KWAMBA KUPIGANA NA UDHARIMU NI UTII KWA MUNGU. NANUKUU MANENO YAKE
" Resistance to oppression can only be obedience to GOD". Hiyo ni nukuu ya Mama mmoja wa Kimarekani aliyefngwa kwa kupiga kura enzi za wanawake wa kimarekani hawaruhusiwi kupiga kura.

wakati akiongea magamba wote kimya!!!!!!!!!!!!! jamani ukumbozi wa pili wa taifa hili upo miguuni mwetu hawa jamaa watatafuna kila kitu,,,,,,,,,,, wasije wajukuu zetu wakajakuchapa makabuli yetu wakitulaumu hatukufanya kitu kutetea rasilimali kwa ajili ya maisha yao baadae.

VIVA TUNDU LISSU,
VIVA UKOMBOZI
VIVA CHADEMA

NIA TUNAYO, TUNAWEZA NA TUTASHINDA
 
Swali lenyewe ni hili hapa.Sheria yeyote ya Hifadhi ya Misitu inatakiwa kutangazwa kwenye gazeti la serikali, Je, Ni Tarehe gani, mwezi gani mwaka gani, ilitangazwa sheria ya kuanzishwa kwa Hifadhi ya Msitu ulioko Singida mashariki
 
tushamzoea anatafuta jina nayeye ili 2015 agombee urais ameshaanza kutengeneza mtandao wake ndani ya cdm
 
Sasa jamani mawziri wengine, sasa hilo swali ni jipya gani hilo!!!!!!!! tena ni swali ambalo alitakiwa kulitegemea
 
tushamzoea anatafuta jina nayeye ili 2015 agombee urais ameshaanza kutengeneza mtandao wake ndani ya cdm

Tatizo liko wapi? anafaa, na kura yangu anastahili endapo atasimama,
kifupi hawa ndio watu naoweza kuwapa kura yangu Ya urais endapo watasimama 2015
1. SAMUEL SITA
2. DR. SLAA
3. MAGUFULI
4. ZITTO/MBOWE/LISSU
 
Katika cross examination kuna technique inaitwa building up, yaani unauliza swali lisilokuwa la msingi ilikujenga msingi.With all due respect to Mr. Lissu MP, the additional question was, unless carried a hidden intended purpose, unecessary as far as Forestry industry for the betterment of Tanzanians is concerned.

I remember during the interview of the then aspiring MPs for representation in the SADC, if I have not mistaken, he asked similar dates years questions. I belive it is high time MP's stop turning the House into Celtel challenge contest. Ask qustions which has merits and not mere test of credibility or memory of the Ministers. I hope CDM MPs may wish to borrow this.My humbled submission.

End of the mission...
 
tushamzoea anatafuta jina nayeye ili 2015 agombee urais ameshaanza kutengeneza mtandao wake ndani ya cdm


Sasa mtu kutetea mustakabali wa nchi ni kutafuta jina kwaajili ya 2015????? Wewe ulipaswa ungekuwa Mombasa tungekunaninihiii huna maana au umetumwa na magamba??? Kumbe tanzania bado kuna watu kama wewe. Hongera CDM iko siku mungu atawalipa haki yenu hata kama Watanzania hatutatambua kazi yenu lakini fanyeni hivi kwa faida ya vizazi vijavyo
 
tushamzoea anatafuta jina nayeye ili 2015 agombee urais ameshaanza kutengeneza mtandao wake ndani ya cdm

tatizo kubwa hapa ni mental slavery- huwezi kuchangia hoja hii ya mtanzania anaesimamia haki kwa statement hii hapa juu ni unafiki na uzandiki
 
Ukombozi wa mwafrika /mtanzania /binaadamu unaanza pale anapojitambua na anapoona maana ya vitu/kitu.huwezi kupata haki/ukombozi wa kweli kama nafsi yako haiko safi na huru ndipo uanagalie ya wenzako.ndio maana siku ya siku hata hao wanaofikiri wao ndio wao nao watatambua wale ni sawa hawa
 
Back
Top Bottom