Tundu Lissu noma, auliza swali jipya bungeni, waziri ashangaa ashindwa kujibu

Hamuelewi bunge linavoendeshwa na sheria za maswali zikoje, kama ni swali la nyongeza na halihusiani na swali la msingi hilo huwa swali jipya, na swali jipya lina njia zake za kufikishwa ili lijibiwe kwa kina. Upo hapo ulipo?

Dada/kaka hivi angekua waziri mpenda kucheza na jukwaa (ndugu Makomeo) hangeshindwa kujibu swali kama ilo? Au unataka kutetea utendaji mbovu wa waziri Maige?
 
Haiingii akilini, madini ni yetu halafu mabepari hawa wanaoitwa wawekezaji tunawapa misamaha ya kodi as if we are benefiting more than them, looh ndiyo maana wakagundua kuwa sisi ni majuha wanajirukia kwa ndege kutoka migodini huku wakikomba rasrimali zetu, mtu yeyot mwenye mawazo mazuri hawezi kushangilia hili suala!inauma sana unajua.
 
tushamzoea anatafuta jina nayeye ili 2015 agombee urais ameshaanza kutengeneza mtandao wake ndani ya cdm
wewe upo kundi gani kati ya hayo yaliyopo? Sio dhambi kugombea urais kama anaona ana uwezo. Wapiga kura ndio watakao amua.
 
Tatizo liko wapi? anafaa, na kura yangu anastahili endapo atasimama,
kifupi hawa ndio watu naoweza kuwapa kura yangu Ya urais endapo watasimama 2015
1.SAMUEL SITA
2. DR. SLAA
3. MAGUFULI
4. ZITTO/MBOWE/LISSU
Mkuu hizo red sijakubali
 
Ameshtukizwa. Ni ushahidi kwamba majibu wanaandaliwa, wao ni kusoma tu kama kasuku. Hovyo!!!!!!!!!!!!!
 
pamoja na hayo kujua specific date, month and year ni shughuli kwa mtu yeyote sana sana angekumbuka mwaka.
 
Waziri mwenye akili ni mmoja tu, nae anaharufu ya ufisadi ! Ccm ni kusanyiko la wezi na wadokozi na wajinga waliokubuhu. Huwezi kuwa timamu ukabaki ccm aka The Gambaz
 
Hee leo nimeona maajabu ya bunge baada ya mh waziri kushindwa kujibu swali la mh Lissu kwa madai eti ni SWALI jipya, kumbe serikali inataka maswali ya zamani tu.

Hili lilikuwa swali la nyongeza, ambapo Mh. Lissu alisimama na kuuliza kwa kuwa Sheria yeyote ya Hifadhi ya Misitu inatakiwa kutangazwa kwenye gazeti la serikali, Je, Ni Tarehe gani, mwezi gani mwaka gani, ilitangazwa sheria ya kuanzishwa kwa Hifadhi ya Msitu ulioko Singida mashariki


Kama ni swali la nyongeza, then ingekuwa ngumu kupata tarehe, mwezi na mwaka on the spot. Inawezekana Lissu ana point nzuri, lakini asingeuliza kama swali la nyongeza b'se hata kama yeye angekuwa ni waziri asingeweza kukremisha hizo tarehe.

Kawaida sheria zote, na sio tuu sheria za hifadhi ya misitu, inabidi zitangazwe kwenye gazeti la serikali kabla ya ya kuanza kutumika. Waziri hawezi kukremisha sheria zote zilitangazwa lini kwneye gazeti la serikali. Na waziri asingejibu kuwa ni swali jipya.

Angemweleza vizuri tuu kuwa kwa kuwa lilikuwa swali la nyongeza, then hakuwa na hizo data on the spot lakini atazitafuta na kumpatia mheshimiwa. Simple, unless kama hiyo sheria hakutangazwa kwenye gazeti la serikali.
 
Hebu acha uwongo wewe kijana!
Rev, nijuavyo mimi ni kweli kabisa, maswali hupelekwa mapema kutafutiwa majibu yake na ndo maana ukifuatilia vema utasikia ikisemwa "hilo ni swali jipya". Hapo ujue halikupelekwa mapema! Kimbembe huwa kwenye swali la nyongeza, mara chache mawaziri wetu wamekuwa mahiri kwenye maswali hayo ya nyongeza.
 
swali lililoulizwa ni zuri....na si kweli kuwa lazima jibu lipatikane hapo hapo.......hata muulizaji sidhani kama alitegemea Waziri angejibu hapo hapo..........whats a big deal here.......!!
 
Viongozi wetu kwa kiasi kikubwa wamerihti namna wakoloni walivyokuwa wakitutawala.Mkoloni aliweka sheria na taratibu za kuwabana colonised people,pamoja na ujanja ujanja kama wanavyofanya huko bungeni kwenye hizo kanuni ambazo zinaulinda upuuzi wowote alimradi umefanywa na chama na serikali.Bado sana....kama tunataka kujikomboa,basi kazi ipo na si kidogo.
 
Hee leo nimeona maajabu ya bunge baada ya mh waziri kushindwa kujibu swali la mh Lissu kwa madai eti ni SWALI jipya, kumbe serikali inataka maswali ya zamani tu.

Hili lilikuwa swali la nyongeza, ambapo Mh. Lissu alisimama na kuuliza kwa kuwa Sheria yeyote ya Hifadhi ya Misitu inatakiwa kutangazwa kwenye gazeti la serikali, Je, Ni Tarehe gani, mwezi gani mwaka gani, ilitangazwa sheria ya kuanzishwa kwa Hifadhi ya Msitu ulioko Singida mashariki

wamesha zoea maswali ambayo tayari yapo solved. ukileta swali jipya halijibiki, ndio maana uwaziri wanapewa hata wasiokuwa na uwezo kwa vile wanajua maswali yote yapo kwenye past papers na yapo solved. waziri mkuu nahisi alikuwa amesha zoea kuwapanga watu wa kumuuliza maswali na akawa anayasolve vizuri, sasa hivi naona watu wanamshuti ambao hakuwategemea ndio maana alisema kuwa posho wanayoichukua kuishia mlangoni kuwa wananchi tunaenda kuwaomba. umemuona mwana sheria alipokuwa akichemka kuhusu miaka ya kusamehe kodi, mnyika anamwambia miaka mitano yeye anang'anga'ania kumi tena akajichomeka kuwa walikubaliana nchi5 za africa mashariki lakini kenya wao wamepunguza sasa najiuliza sisi watanzania lipi linatuzuia tusipunguze? halafu kwanini serikali siku zote inaona hoja zake ziko sahihi tu? mimi inanikera. mtu unamsamehe miaka kumi anaendesha business bure that means kuanzia Richmond+dowans+symbioni mpaka sasa serikali haijapata hata shilingi moja ila dowanz inadai pesa nyingi mno serikali.
 
Huyo naibu waziri astahili pongezi kwani wanasiasa wengi hupenda majibu rahisi kwa maswali magumu na pengine ninyi mnaoshangaa ni kutokana na kujengeka vibaya kwamba kiongozi anajua yote
 
Huyo naibu waziri astahili pongezi kwani wanasiasa wengi hupenda majibu rahisi kwa maswali magumu na pengine ninyi mnaoshangaa ni kutokana na kujengeka vibaya kwamba kiongozi anajua yote

Wee vipi yaani asijue issue ya kitaifa iliyo chini yake?Kweli JK alisema uwaziri hausomewi yeyote hata chizi anaweza kwani ni kudesa tu!!!!!!!!!
 
Wewe ndio mjinga kwa sababu hujui taratibu za Bunge, usiwe mshahabiki hata kwa mambo usiayoyajua.
shiiit! Unatafuta nini huku mheshimiwa? Umeshasaini posho? Salamu zao bungeni, waambie magamba tunawasubiri kikao kikiisha, mwendo mndundo kitarimetarime tu.
 
Maswali haya Tundu anataka watu lawama . Watu wanampeleka Simba bunge la SADC bila kumhoji kama wenzake leo anategemea kumbukumbu ziwepo ?
 
Hahahaha! kwani wewe jzi hujamsikia yule mbunge wa Mtera akilalamika bungeni kuwa dodoma imelaaniwa kwasababu dodoma kuna gereza la Isanga linaloweka wafungwa wanaotakiwa kunyongwa!!

Halafu akachangia tena kwamba tanzania imelaaniwa Coz imeweka wanyama----specifically Nyoka kwenye note coz nyoka ni alama ya shetani!!!

CCM Hoyeeee!!.................imagine huo ndo mchango wa mbunge wa CCM kwenye budget.

Tena akaongeza kwa kusema, Dodoma inaonewa sana kwani hata Hospital ya Vichaa-Milembe imejengwa hapo. Akasema wakayajenge sehemu nyingine kama Tabora, ..., nk! Ila Lusinde inaonekana thinking capacity yake ni ndogo sana. Hilo ndo alilo ona linakwamisha maendeleo ya nchi?
 
Back
Top Bottom