Tundu Lissu na Wenzake waachiwa kwa dhamana na masharti magumu

delabuta

Senior Member
May 23, 2011
178
46
Wana JF Habari za kuaminika nilizozipata sasa hivi tundu lisu na wenzake wameachiwa kwa dhamani kutoka mahama ya tarime.na ameambiwa asionekane nyamongo from today. source redio one breaking news. mwenye taarifa kamili atujuze.
 
hivi Katiba ya nchi hii inasemaje kuhusu movement!!!
Hawa wehu kweli hawa!!
 
Asionekane Nyamongo kwa sheria ipi? Huyu hakimu atakuwa anatekeleza amri za mtu fulani. Kwa kitendo cha kushindwa kutoa dhamana jana, huyu hana sifa ya kuendelea na kesi hii.
 
Unapolewa na siasa za kikandamizaji badala ya kutumia utaalam uliosomea kama mwanasheria madhara yake ni kama ya mtu mwenye ukurutu kwani haufichiki. Hawa mahakimu waliotoa hukumu ya namna hiyo inabidi wakafanyiwe vipimo kwani huku wakijua kabisa mtanzania ana uhuru wa kwenda popote wameamua maksudi kuanzisha siasa za kimajimbo na huu ni ubaguzi.

CCM wanaweza kukumbatia hii kwani ina wapemndelea kisiasa ila in the long run watajuta kwani kila mkoa utapiga marufuku wanasiasa wasiotokea mkoa huo na zaidi sana kuwanyima kura. Matokeo yake ni kila mkoa kuwa na rais wake n.k. Kama kweli mahakama imetoa hukumu ya namna hii ni ishara kwamba nchi sasa haitawaliki na kila mmoja anatoa amri yake ilimradi inaisaidia CCM
 
Hivi leo hii imefika mahali Mtanzania anapigwa marufuku kutembea nchini kwake!

Kweli si muda mrefu, The Hague itajaa viongozi wa Afrika na Viongozi wengi watapelekwa huko kwa Ujinga wao kwa kuruhusu watu kutumia majina yao kwa manufaa ya Matumbo yao.
 
Wana JF Habari za kuaminika nilizozipata sasa hivi tundu lisu na wenzake wameachiwa kwa dhamani kutoka mahama ya tarime.na ameambiwa asionekane nyamongo from today. source redio one breaking news. mwenye taarifa kamili atujuze.

Sitoshangaa kusikia huyu hakimu ana elimu ndogo (elimu ya sheria) kuliko Lissu. Kwangu mimi naona haya ni masharti ya kisiasa zaidi kuliko sheria. Katiba mpya inakuja. Hawa mahakimu wa elimu ya Kata basi.
 
Asionekane Nyamongo kwa sheria ipi? Huyu hakimu atakuwa anatekeleza amri za mtu fulani. Kwa kitendo cha kushindwa kutoa dhamana jana, huyu hana sifa ya kuendelea na kesi hii.

CHADEMA tuna watu wengi smart, kama hawataki lissu aonekane nyamongo tutakwenda wengine, wakituzuia watakwenda wengina. nakumbuka kuna wakati mafarisayo walitaka wanafunzi wa Yesu wanyamaze. Yesu akawajibu hivi "wakinyamaza hawa, haya mawe yatasema". CCM wasidhani kwamba akinyamaza lissu ndo chadema imenyamaza, au akinyamaza slaa PhD ndo chadema inatanyamaza. Kila mwanachadema wa ukweli ni smart. aluta continua
 
Wote wanajua wazi kuwa huyu **** ndio amesababisha maiti zisizikwe, hana dini huyo lasivyo angeheshimu maiti na kuweka uroho wa madaraka nyuma. Lakini kwaajili yeye ni CHADEMA basi wote mnaona hajakosea.
 
masharti magumu ya dhamana ni pamoja na kutokwenda mbai na eneo uliloshitakiwa na kuripoti mara kwa mara ...

hii kali kweli kweli
 
Nimempenda huyo hakimu kwa masharti yake ya dhamana, hapo tunajenga hoja kwamba hata mahakama imeingiliwa na siasa (ccm) na mafisadi wake. Huwezi kufanya maamuzi ya kitaaluma kijinga namna hiyo, huyo hakimu pia nikipofu haoni mbali hakika asingechukua uamuzi huo.
 
Asionekane Nyamongo kwa sababu zipi au kwa kifungu kipi cha Sheria au Katiba yetu Tanzania inasemaje kuhusu uhuru wa raia wa Tanzania kuishi eneo lolote ndani ya Jamhuri bila kubugudhiwa!!?.Huyo hakimu katumia sheria za nchi gani?
 
Asionekane Nyamongo kwa sababu zipi au kwa kifungu kipi cha Sheria au Katiba yetu Tanzania inasemaje kuhusu uhuru wa raia wa Tanzania kuishi eneo lolote ndani ya Jamhuri bila kubugudhiwa!!?.Huyo hakimu katumia sheria za nchi gani?Au nnaota vile yaani kazuiwa asionekane Nyamongo!!!!?
 
Hivi leo hii imefika mahali Mtanzania anapigwa marufuku kutembea nchini kwake!

Kweli si muda mrefu, The Hague itajaa viongozi wa Afrika na Viongozi wengi watapelekwa huko kwa Ujinga wao kwa kuruhusu watu kutumia majina yao kwa manufaa ya Matumbo yao.

Tindu ni kansa kwenye nchi yetu ambayo ni kisiwa cha amani na utulivu..........hakimu mwenye hekima alitakiwa kumzuia kwenda mara kabisa kwa kuwa ni mchochezi wa uvunjaji wa amani na mtetezi wa majambazi
 
Back
Top Bottom