Tundu Lissu na Wenzake waachiwa kwa dhamana na masharti magumu

Great thinkers mbona hamjadili kivile ? Sheria inasemaje? Nini kifanyike? Mnejedili km mko kwenye club ya pombe za kienyeji! Aah !
 
Siku CDM ikishika nchi hawa Barrick lazima wafukuzwe na mikataba ikatishwe mara moja wakitaka waende kushitaki popote duniani. Inavyoelekea kila mfanya kazi wa serikali kule Tarime including mahakimu wako ktk payroll ya Barrick! Wamepumbazwa kutojali ndugu zao, bali hao Wacanada na familia zao kule Vancouver.
 
Ni sawa sawa na umepatika na hatia ya ujambazi Kigoma, mahakama inakuhukumu usionekane tena Kigoma. Yani nenda kaibe Tanga!
 
Hivi wewe unakichaa cha mbwa au!!! Una akili kweli. Kama watanzania wengi bado wako kama wewe kazi ipo. Tumekusamehe bure, manake ungekua milembe.

Wakuu
Kwa jinsi hii watanzania bado tunayosafari ndefu. Mimi ninaamini kwamba hakuna mtu yeyote ambaye ana afiki vitendo vilivyofanywa na Polisi wetu. Kazi yao kubwa ni kuhakikisha usalama wa raia na mali zao, ndo kazi kubwa Polisi wetu waliopewa.

Na nina amini kuwa kila mtu ana hasira na uchungu kutokana na kitendo hiki ambacho wale tuliowapa dhamana ya kulinda maisha yetu, mali zetu n.k ndo wanaopola maisha hayo na mali hizo,jambo hilo linanihudhunisha sana. Lakini zaidi nahudhunishwa na uelewa wa baadhi ya ndugu zetu(watanzania),mimi siamini kabisa kwamba kutukana, kutumia lugha mbaya kunatusaidia kutatua tatizo lililo mbele yetu.(kwa wale wanaosoma biblia kuna msemo kuwa Mpumbavu akinyamanza huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu...Mithali 17:28).

Sasa ninadhani kuna Lugha humu kwenye jamvi la wana falsafa(thinkers), zinatuondolea heshima si kwa mtu binafsi tu bali hata kwa vyama tunavyoviwakilisha kama wasemaji wake.
Kumbukeni msemo wa kelele za chura hazimkatazi mchota maji kuchota,sasa tuangalie hoja nyingine ambazo tunazitoa kwenye jamvi hili zizituaibishe na kuaibisha wale tunaodhania tunawasemea.

Mimi binafsi siafiki, kuhusu mwenendo mzima wa serikali yetu katika kulishughulikia hili swala, napia siafiki kuwa lugha tunayotumia inatusaidia katika kutafuta tulitatueje swala hili. Nina imani HOJA ZA NGUVU zikitolewa kwa staili nzuri zitawasuta hata wale ambao wanazibeza au kuziponda, lakini Hoja hizo zikitolewa kihunihuni basi hoja hizo zitachukuliwa kihunihuni.

nachotaka kusema ndg zangu hebu tuondoe lugha ya kwamba kama chama fulani kingekuwa madarakani ndo kingefanya hili na lile, na chama kilichopo hakifanyi, mimi naingiwa na wasiwasi kama vile tuonavyo kwenye mechi siku zote mtazamaji anaona makosa kuliko mchezaji.
Sisi tumeyaona makosa ya wenzetu sasa tujenge hoja za nguvu na wala siyo nguvu ya hoja.
na wale ambao wana kosolewa wayaone makosa yao na wakubali kukosolewa pasipo jazba.

Mwisho jamvi letu hili tulipe heshima kama lenyewe lilivyotangulia kujieleza kuwa ni jamvi la wanafalsafa wakuu(great thinkers). Mwanafalsafa aliyesema kwamba" Endapo wana falsafa hawatakuwa marais au marais kuwa wanafalsafa duniani hakutakuwepo na amani" nadhani au naamini kuwa alimaanisha kwamba watu walio na muda wa kufikiri,kutafakali ndo wanasitahili kuongoza nchi kwani hawatakurupuka katika maamuzi,vivyovyo kwetu wana jamvi tutumie hekima ya kutoa mawazo yetu pasipo kukulupuka hilo litatusaidia sana vinginevyo tunajichimbia kaburi wenyewe. Hizo nchi zote zisizo na amani walianza kidogokidogo hadi walipo sasa.

Wito vyama vyote vya siasa kumbukeni dhamana ambayo wananchi wamewapa, inapo bidi kukosolewa kubali kukosolewa, na mtu anapokosoa mwenzie iwe kwa staha kama jadi yetu ilivyo na si kwa jazba.
 
huyo hakimu akapimwe akili zake mirembe, du elimu za kata zina shida, nina doubt professional competence ya huyo akimu
 
kwahyo kesi yake anaenda kuisikilizia chumbani kwake kama amezuiwa kwenda nyamongo?huyo hakimu elimu ya sheria haijamkaa vizur ndo mana anakumbatia siasa za chama cha mafisadi.
 
mi sishangai cz kama hakimu huyo hakuwa na sifa yaani elimu ya kuungaunga na position hiyo kapewa na mkubwa lazima atekeleze maamuzi ya mkubwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Yaani there are hundreds of them including Judges. Kama umeshasikia "majaji wa vodafasta" this is actually the name insiders wa mahakama wanawaita majaji wale walioingia kwa mlango wa nyuma. Wale wanaoteuliwa bila kupendekezwa na tume and believe me there are many of them. Kama wameanza kuchemsha mapema hivi five years from now ndio itakua balaa.
 
Wote wanajua wazi kuwa huyu **** ndio amesababisha maiti zisizikwe, hana dini huyo lasivyo angeheshimu maiti na kuweka uroho wa madaraka nyuma. Lakini kwaajili yeye ni CHADEMA basi wote mnaona hajakosea.

Kuna dini inaruhusu watu kuuawa ovyo? Wewe dini yako ipi bwana..usianze kuzua hoja kwa kusingizia dini hapa... hatuwezi kukubali eti mtu asifanyiwe uchunguzi kisa dini... hiyo ni kuzidi kulea uovu na uozo uliopo.. ni bora mmoja atolewe sadaka ili wengine wapone.., kwa hizo maiti kufanyiwa uchunguzi na kujulikana ukweli, itasaidia kupunguza upuuzi mwingine next time..kwa hiyo acha tumia tuu busara yako, acha kukimbilia dini..
 
Wana JF Habari za kuaminika nilizozipata sasa hivi tundu lisu na wenzake wameachiwa kwa dhamani kutoka mahama ya tarime.na ameambiwa asionekane nyamongo from today. source redio one breaking news. mwenye taarifa kamili atujuze.

Safi sana hakimu kwa kutekeleza sheria za nchi !
 
Tindu ni kansa kwenye nchi yetu ambayo ni kisiwa cha amani na utulivu..........hakimu mwenye hekima alitakiwa kumzuia kwenda mara kabisa kwa kuwa ni mchochezi wa uvunjaji wa amani na mtetezi wa majambazi

Kwa mantiki hiyo "MAGAMBA" na mafisadi wote wa CCM akiwemo Rais JK wafukuzwe nchini wasikanyage nchini mpaka pale watakapofikiswa mahakamani kujibu mashitaka kwa makosa ya rushwa ufisadi ,uchochezi na mauaji ya polisi kwa raia wasio na hatia kwani kuwepo nchini hapa kunaingilia uchunguzi wa maovu yao kutokana na nafasi zao katika uongozi katika chama na serikali pia kutumia vyombo vya dola dhidi ya wananchi wasio na hatia kunasababisha mauaji .Mahakama ikifanya hayo basi kutakua na mantiki kwa uamuzi uliotolewa dhidi ya Lisu:mod::mod::mod::mod::mod::mod::mod::mod:

 
Tindu ni kansa kwenye nchi yetu ambayo ni kisiwa cha amani na utulivu..........hakimu mwenye hekima alitakiwa kumzuia kwenda mara kabisa kwa kuwa ni mchochezi wa uvunjaji wa amani na mtetezi wa majambazi

Na mwaka huu mtahama hii nchi....kwa sabab ka akili zenyewe ndo hizi mtapata taab sana...hata majambazi wana haki zao mbele ya sheria!!
 
Back
Top Bottom