CHAMVIGA
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 7,687
- 2,238
Wasiotaka kukosoa ukweli ni wale wanaofaidika na uwongo.Kuna watu waliumizwa sana na utawala wake leo wakijitokeza sijui kama CCM watawafanya nini?Ni wengi mno.Unakumbuka wakati wauhujumu uchumi,je ni wangapi waliowekwa ndani walikuwa na hatia na wangapi walikuwa hawana?Je,waliruhusiwa kutetea au kufunguliwa kesi wajibu mahakamani?Ni kwa nini hawakupelekwa mahakamani,sababu hawakuwa binadamu?AU kwa sababu ya sheri alizokuwa anatunga yeye mwenyewe hazikuwa na impact kwa viongozi aliokuwa nao karibu bali watu wakawaida ndiyo alioumia,kuwekwa magerezani nk.
Kungekuwa na haki hata leo wanasheria wangeanza kuwatetea hawa waliodhulumiwa enzi za uongozi wa Mwalimu ili wapate haki zao hasa familia zao ambapo watoto walioswekwa ndani ndiyo walioumia kwa kukosa ada za shule,malazi,na hata chakula wazazi wao wakiwa jela.
Simlaumu Lissu hata kidogo ni bora ukweli utoke sasa kuliko baadaye.
Nafarijika sana kuona watu tunakuwa objective sikuhizi. Kiukweli mwalimu anasifa zake lakini madhara yake yamekuwa makubwa sana. Hakutaka kufikiri kuwa ipo siku si kiongozi tena katika taifa hili. Ninapomjadili Nyerere moyo wangu unauma sana kwani kaliharibu taifa na wananchi wake kuwafarakanisha.