Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Wasiotaka kukosoa ukweli ni wale wanaofaidika na uwongo.Kuna watu waliumizwa sana na utawala wake leo wakijitokeza sijui kama CCM watawafanya nini?Ni wengi mno.Unakumbuka wakati wauhujumu uchumi,je ni wangapi waliowekwa ndani walikuwa na hatia na wangapi walikuwa hawana?Je,waliruhusiwa kutetea au kufunguliwa kesi wajibu mahakamani?Ni kwa nini hawakupelekwa mahakamani,sababu hawakuwa binadamu?AU kwa sababu ya sheri alizokuwa anatunga yeye mwenyewe hazikuwa na impact kwa viongozi aliokuwa nao karibu bali watu wakawaida ndiyo alioumia,kuwekwa magerezani nk.

Kungekuwa na haki hata leo wanasheria wangeanza kuwatetea hawa waliodhulumiwa enzi za uongozi wa Mwalimu ili wapate haki zao hasa familia zao ambapo watoto walioswekwa ndani ndiyo walioumia kwa kukosa ada za shule,malazi,na hata chakula wazazi wao wakiwa jela.

Simlaumu Lissu hata kidogo ni bora ukweli utoke sasa kuliko baadaye.

Nafarijika sana kuona watu tunakuwa objective sikuhizi. Kiukweli mwalimu anasifa zake lakini madhara yake yamekuwa makubwa sana. Hakutaka kufikiri kuwa ipo siku si kiongozi tena katika taifa hili. Ninapomjadili Nyerere moyo wangu unauma sana kwani kaliharibu taifa na wananchi wake kuwafarakanisha.
 
Wengine hatujabadilishwa majina yetu ya asili na kufuata imani za kuletewa... Mimi bado ni katka generation ya Mfalme Suleiman kizazi cha malkia Sheba! Sihitaji kupewa majina ya kizungu na kirumi ili Mungu wetu anitambue! Imani yetu inasimama katika UKWELI na kamwe Mtu kama JKN hawezi kuwa kanuni kwani na yeye ni mja kama waja wengine wa Mungu wetu mmiliki wa kila kitu... Mhe Lisu tuko wengi nyuma yako! Hawa wenye kupigia magoti marehemu wacha waendelee ILA wakumbuke kuwa Hata Mhusika aliwahi kusema kuwa yeye si malaika na kuwa kuna mambo mengi ya kijinga aliyafanya na akawa anawashangaa inakuwaje wanakumbatia yale ya Kijinga mazuri wanayaacha?... HAO wenye kutaka kumfanya MTAKATIFU wanajulikana na Role ya kanisa haijawahi kubadilika toka Enzi zile za ukoloni ... Preach "Obedience" huku mali zetu zikisombwa na wamiliki wa hayo makanisa kwa karne nyingi mpaka sasa! Umewahi kusikia wanakemea na kuwa kemea wakwapuaji wa rasilimali zetu? THINK BIG ikiwezekana ondoa upogo wa udini ndipo unaweza kunielewa vema...
 
unachokiandika purely comes from witchcraft mentality. Hiyo aikili yenu ya kishirikina haiwezi kufannikiwa. Hafi mtu hapa. ViVA LISU, VIVAAA!!!!!!. Tatizo kubwa la viongozi wa ccm ni kushi kwa kupiga ramli na na kutoa kafara. Nani asiecjua kuwa viongozi wakubwa wa ccm kuwa ni washirikina wakutupwa?
 
Kishimbe, ebu sikiliza hotuba ya Mwalimu alivyoongelea Azimio la Zanzibar. Hapakuwa na ridhaa pale maana hasingesema ilifanyika kwa siri, lakini kwa wenye akili tulijua tu Azimio la Arusha limezikwa.

In NATIONAL AND INTERNATIONAL POLITICS you have to practice the art of reading between the lines!

KWELI KABISA MWALIMU ALILALAMIKA KUHUSU KUANGUKA KWA AZIMIO LA ARUSHA LAKINI KWAKUWA , KULINGANA NA WAKATI HUO, INTERNATIONAL PRESSURE N.K, HAKUWA NA JINSI ALIISHIA KULALAMIKA KIDOGO NA KUPETA HIYO FAULO!

LAKINI UKITAKA KUTHIBITISHA KWAMBA ALIRIDHIA KUZIKWA KWA AZIMIO LA ARUSHA BASI ANGALIA 'REACTION' YAKE KWA WAZEE G55! HAWA JAMAA, G55, WALICHIMBWA MKWARA AMBAO HAKUNA MTU ALIYESHUHUDIA MKWARA ULE ANAWEZA KUKUBALI SERIKALI TATU, LABDA WALE AMBAO WANAJUA UDHAIFU UNAOWEZA KUTOKANA NA SERIKALI TATU KWA MANUFAA YAO YA KISIASA!

NAKUSHAURI JARIBU KU'REFER' HAYA MATUKIO MAWILI HALAFU UJIJIBU! NJE YA HAPO KWA KWELI NA MIMI NI MAIMUNA MWINGINE TU!
 
Yote tu ni sahihi. Ukweli ni kuwa hakuna aliloridhia. Kama unavyosema reaction yake ilikuwa tofauti kulingana na mazingira ya wakati huo na jambo lenyewe. Unakumbuka alivyo react wakati anakataa kugeuka jiwe (kwa sababu ya masharti ya IMF/WB) na yaliyotokea muda mfupi baadaye. Itakupa picha ya mwanasiasa aliyebobea.
 
Sijaona wala kusikia mtu ambaye ameweza (hata kujaribu) kuja na hotuba mbadala ya kupinga hoja za Tundu Lisu. Tena akitumia taarifa za kitafiti....Hadi hapo tutakapompata mtu wa namna hiyo, ila kwa sasa Lisua ataendelea kuwatesa wanafiki!

Watanzania wengi na hasa wale wasiowafuatiliaji wa mambo yanayoendelea nchi hii wanaaminishwa kuwa Tundu Lissu alimtukana Mwalimu Nyerere,
lakn kinachonisikitisha ni kuwa hata wale wenye uelewa wa kati nao wanapokea kauli hii bila hata kufuatilia nn alisema TL
Aliyesikiliza Vzr ni kuwa TL yote aliyoyasema ni mambo ambayo yameandikwa na watu au matukio ambayo yamewahi kutokea.
kuhusu zile presidential decree alisema ameandika Msekwa kwny kitabu chake
Kauli ya kuwa hatawapiga mabomu wazanziba ni mahojiano aliyoyafanya mawalimu na gazeti la observer la uk, lkn tunaambiwa wapinga muungano waliteseka sana na wengine kuuawawa.
Kauli ya baraza la wawakilishi kutoridhia hati ya muungano ilitolewa na aliyekua katibu wa baraza la mapinduzi.
Kuhusu nyerere kwenda ha hati iliondaliwa kabisa tanganyika hiyo asubuhi ya tarehe 22/04/1964 imeandikwa kwenye kitabu cha Abdu Jumbe.
Sasa kosa la TL ni nn kusema vivyoandikwa ambayo watanganyika hatuvijui kwakua hatusomi vitabu au kosa lake ni nn??
Wale wote wanaoaminishwa kuwa mwalimu katukanwa wapanue akili zao na kufikiri kwa mapana.
 
Yote tu ni sahihi. Ukweli ni kuwa hakuna aliloridhia. Kama unavyosema reaction yake ilikuwa tofauti kulingana na mazingira ya wakati huo na jambo lenyewe. Unakumbuka alivyo react wakati anakataa kugeuka jiwe (kwa sababu ya masharti ya IMF/WB) na yaliyotokea muda mfupi baadaye. Itakupa picha ya mwanasiasa aliyebobea.

THAT WAS A 'TANTRUM'! (And I am sure he would laugh-it-off when alone!)

HIZO NDIO SIASA ZENYEWE!
images
 
Watanzania wengi na hasa wale wasiowafuatiliaji wa mambo yanayoendelea nchi hii wanaaminishwa kuwa Tundu Lissu alimtukana Mwalimu Nyerere,
lakn kinachonisikitisha ni kuwa hata wale wenye uelewa wa kati nao wanapokea kauli hii bila hata kufuatilia nn alisema TL
Aliyesikiliza Vzr ni kuwa TL yote aliyoyasema ni mambo ambayo yameandikwa na watu au matukio ambayo yamewahi kutokea.
kuhusu zile presidential decree alisema ameandika Msekwa kwny kitabu chake
Kauli ya kuwa hatawapiga mabomu wazanziba ni mahojiano aliyoyafanya mawalimu na gazeti la observer la uk, lkn tunaambiwa wapinga muungano waliteseka sana na wengine kuuawawa.
Kauli ya baraza la wawakilishi kutoridhia hati ya muungano ilitolewa na aliyekua katibu wa baraza la mapinduzi.
Kuhusu nyerere kwenda ha hati iliondaliwa kabisa tanganyika hiyo asubuhi ya tarehe 22/04/1964 imeandikwa kwenye kitabu cha Abdu Jumbe.
Sasa kosa la TL ni nn kusema vivyoandikwa ambayo watanganyika hatuvijui kwakua hatusomi vitabu au kosa lake ni nn??
Wale wote wanaoaminishwa kuwa mwalimu katukanwa wapanue akili zao na kufikiri kwa mapana.

Siyo hivyo tu mkuu, hotuba ya Tundu Lisu iliwekwa hapa hapa JF na pia kuchapishwa kwenye magazeti. Kwa kuwa nilitumia muda wangu kuisoma ile, naamini wengien walisoma na natamani kuona watu wenye na counter arguements ili tuwasikilize.

Badala yake wote wanakuja na style ya JK na Lukuvu, ambayo kwa namna yoyote ila haiwezi kutusaidia!
 
Nafarijika sana kuona watu tunakuwa objective sikuhizi. Kiukweli mwalimu anasifa zake lakini madhara yake yamekuwa makubwa sana. Hakutaka kufikiri kuwa ipo siku si kiongozi tena katika taifa hili. Ninapomjadili Nyerere moyo wangu unauma sana kwani kaliharibu taifa na wananchi wake kuwafarakanisha.

Tatizo linakuja kwa wale ambao tunajali zaidi vyama kuliko UTAIFA wetu. Tunadhani sisi tutaendelea kuishi mpaka lini?Hivi kiongozi una miaka 60-70 bado ni Mbunge unaenda kumtungia sheria mtoto wa siku au kijana wa miaka 18 unategema Katiba au sheria hizi atazikubali?Je tunauhakika Muungano huu bila marithiano utastawi?Je,ni kweli upande mmoja wa CCM unaweza kuwatungia Katiba Watanzania wote?

Hivi ninaingiwa na woga siku watakapopiga kura na kusema serikali mbili zimekubaliwa na wengi na 2/3 ya Zanzibar imefikiwa wakati kuna wabunge zaidi ya nusu wamesusia UUNDAJI huu wa Katiba?Kweli tunatafuta AMANI au tunatafuta matatizo?

Ninaumia kuona viongozi wetu wamekosa BUSARA kabisa ya hata kufikiria Katiba hii itapokelewaje upande wa pili.
 
Sasa hivi wajumbe wa bunge la katiba waliobaki bungeni ambao wengi ni CCM ni kama wamekubaliana kuwa kila anayesimama aanze kumshutumu Lissu kwa kumtukana Nyerere. Wanatumia muda mrefu sana kumshutumu Lissu na kujadili watu binafsi lakini hawajadili rasimu yenyewe Hata waliopo nje ikiwa ni pamoja na mwenyekiti wa CCM nao wanasema Lissu kamtukana Nyerere. Kwa kuwa Lissu aliongea bungeni mimi naomba wanaodai Lissu kamtukana Mwalimu Nyerere watupe na mifano ya maneno ambayo tunaweza kukubaliana kuwa hayo ni matusi maana mimi nimepata shida kupata hayo matusi katika hotuba ya Tundu Lissu. Naona wengi wanoongea wanaiga tu kutoka kwa wenzao lakini hawatoi ushahidi wa matusi hayo.

Jambo jingine ambalo nimegundua kwa wajumbe wa CCM wanotetea serikali mbili ni kuwa wanamtumia tu Mwalimu kinafiki kuwa eti wanataka serikali mbili ili kumuenzi Mwalimu. Wanazungumza serikali mbili lakini wanakwepa kuzungumza nchi mbili zilizopo sasa kama je ndio muungano wenyewe walioasisi Mwalimu na Karume?

Mimi binafsi nawaona viongozi wote wa CCM wanaodai kumuenzi Nyerere ni wanafiki wakubwa kwasababu yote aliyoanzisha Mwalimu wameyavuruga sasa wamebaki na kete ya muungano tu ambao nao ni kama haupo kwasababu Nyerere na Karume waliacha serikali 2 na nchi moja lakini sasa kuna serikali 2 na nchi 2.

Mwl Nyerere aliasisi mambo mengi yenye manufaa kiuchumi na kijamii kwa wananchi lakini leo manyang'au wanaojifanya kumuenzi wamesha yaua. Mwl aliasisi Azimio la Arusha ili kuleta usawa, haki, uadilifu na kuweka misingi imara ya kujitegemea lakini manyang'au wanaojifanya sasa kumuenzi Mwl ndio walioliua azimio la arusha ili waweze kuifisidi nchi hiii kwa kujilimbikizia mali na wizi kisha wakaanza kuuza na kubinafsisha misingi yote mikuu ya uchumi na jamii ambayo Nyerere alitumia nguvu kubwa kuianzisha na kuisimamia. Nyerere alijenga viwanda kila kona ya nchi hii ambavyo vilisaidia kuondoa tatizo la ajira lakini yalivyoingia mafisadi yanayojidai kumuenzi yakapiga mnada vyote. Manyang'au haya yamegawa raslimali zote kwa wageni kama migodi na mbuga za wanyama vitu ambavyo Nyerere alivisimamia kwa imani kuwa wananchi wakisha elimika watavisimamia na kuviendesha vyema. Nyerere alijenga nyumba za serikali kwa ajili ya watumishi wa serikali. Manyang'au yanayojifanya kumuenzi yamejibinafsishia nyumba na kuanza kuwapangishia watumishi au viongozi mahotelini. Huko ndiko kumuenzi Mwalimu?

Nyerere pia alisimamia vyema huduma za jamii kama elimu na afya. Ni katika wakati wake ndipo elimu ilikuwa bora sana na wengi waliosoma wakati ule walipata elimu bora bila malipo yoyote. Waliohitimu darasa la saba wakati ule waliweza kufanya kazi benki, TRA, Posta na kwenye mashirika mbali mbali kwa uwezo mkubwa kuliko hata form six wa sasa. Manyang'au yameua elimu na ndipo utayasikia eti yakisema wanafunzi 5200 wamefaulu kwenda kidato cha kwanza wakiwa hawajui kusoma wala kuandika na la ajabu utakuta yanapigiana makofi. Wakati wa Nyerere ndipo wananchi walipata huduma bora za matibabu bure lakini leo utashangaa mwananchi anakufa au kuteseka kwa kukosa laki tatu au tano za kutibiwa katika hospitali ya serikali na wakati huo huo kuna afisa mmoja wa bunge analipwa shilingi milioni moja na laki tano kila siku kwa eti kusimamia ufungaji wa viti katika ukumbi wa bunge la katiba na wakati hapo alipo ndipo ofisini kwake!

Nyerere wakati ule aliisimamia hasa siasa ya ujamaa na kujitegemea na hata alipolazimika kuomba msaada nje, aliomba ndoano ili aweze kuvua mwenyewe samaki na sio samaki ambapo baada ya kula unaenda tena kuomba. Hawa wa sasa wanazunguka dunia nzima kuomba omba na bila aibu wanajisifia eti wanahemea vibaba ili tusife njaa na wakisifiwa na Obama wanajiona ndio viongozi bora. Ndipo utashangaa kiongozi mzima anajisifia eti kuwa wa kwanza kuonana na Obama! So what? Nyerere alichukia sana tabia ya omba omba na ndio maana kila wakati alikuwa anasema hatuna mjomba huko nje. Hawa wa sasa wanafurahia kupewa net na wao kuachia madini yote na hata kuachia mali asili zetu kama wanyama kusafirishwa nje. Sasa wana muenzi mwalimu kwa lipi? Nyerere alipostaafu urais allirudi zake kijijini kulima. Jiulize wastaafu wengine wako wapi? Wengine wamekimbia mpaka vijiji vyao vyao vya asili na kwenda kuishi kwengine kana kwamba walipigwa uchawi.

Ukweli ni kuwa viongozi wote wa CCM wanaojifanya kumuenzi mwalimu ni wanafiki wakubwa na ni wa kuogopwa kama ukoma kwani wameua misingi yote muhimu aliyoanzisha mwalimu ikiwa ni pamoja na muungano wenyewe lakin bila haya yatasimama na kudai eti yana muenzi mwalimu. Yanakera sana na ukweli haya ndiyo yaliyopaswa kuwepo kwenye ile ndege ya Malaysia. Mimi nikisikia au kumuona kiongozi wa CCM eti anazungumzia kumuenzi Nyerere kama ilikuwa ni radio au TV natafuta station nyingine
 
Tukirejea "matusi" aliyotoa Lissu bungeni, basi tutakuwa tunashiriki kumtukana Mwalimu. Kama hukuyasikia, tulia tu na amini kuwa Mwalimu alitukanwa. Huwa hamtaki kusikiliza redio/televisheni mwisho wa siku mnaomba muelezwe matusi yalivyoporomoshwa.
 
Kwahiyo kama unatoa ushahidi mahakamani dhidi ya mtu aliyemtukana mlalamikaji na ukaambiwa useme kile ulichokisikia ambacho alikisema mshitakiwa na ukakisema kama alivyosema mshitakiwa na wewe utakuwa umemtukana mlalamikaji?! Na kwa maana hiyo na wewe shahidi unafunguliwa mashitaka hapo hapo kwa kumtukana mlalamikaji??!!
 
Tukirejea "matusi" aliyotoa Lissu bungeni, basi tutakuwa tunashiriki kumtukana Mwalimu. Kama hukuyasikia, tulia tu na amini kuwa Mwalimu alitukanwa. Huwa hamtaki kusikiliza redio/televisheni mwisho wa siku mnaomba muelezwe matusi yalivyoporomoshwa.
Mkuu waramba viatu wa mkubwa fulani walikimbia mbio kwenda mahakamani kumshitaki mwananchi mmoja kuwa eti kamtukana na kumkashifu mkubwa wao. Kule mahakamani ushahidi ukatolewa na neno likachambuliwa likaonekana ni neno la kawaida la kiswahili linalowafaa watu wenye tabia kama aliyoionesha bosi wao na hivyo yule mwananchi akaonekana hana hatia na lile neno ikaonekana ndio hasa linalofaa kumwelezea kiongozi kama yule. Wakati fulani Dr. Slaa alisimama pale mwembe yanga akati majina ya wakubwa fulani akiwemo na mkubwa mmoja maarufu sana kwa safari za kuhemea vibaba na kuiita ile ni "list of shame" kutokana na ufisadi mkubwa walioifanyia nchi. Kesho yake kila mmoja akasema kakashifiwa na kutukanwa hiyo wanakwenda mahakamani. Baada ya muda mfupi tukasikia wenyewe kwa wenyewe wanashitakina na wengine mpaka sasa wanaendelea na kesi mahakamani. Mmoja wao ghafla tukasikia anaumbwa na amekwenda kwa Obama na "kufia" huko. Wakati mwingine watu wanapoambiwa ukweli na wanapokuwa hawana hoja za kujitetea huwa wanageuza ukweli ule kuwa "matusi" Mbona hatujasikia hao hao CCM wakimlalamikia mmoja wao aliyesema bungeni na kusema"fakyu" au yule aliyema haongei na mbwa bali na mwenye mbwa! Maneno hayo angesema Lissu au Mnyika ingekuwaje. Jana mwingine naye kawataja Lipumba, Mbowe, Mbatia na Lissu kuwa ni watoto wa Shetani. Alipooambiwa afute kauli alikataa na imebaki hivyo. Fikiria maneno haya angetamka Lissu dhidi ya viongozi fulani wa CCM?? Mnyika wakati fulani alisema kiongozi fulani mkubwa kabisa ni dhaifu. Unajua kilichotokea? Alitimuliwa nje baada ya kukataa kufuta kauli. Hivi neno dhaifu toka lini likawa ni tusi hasa unapomuelezea mtu ambaye kweli kiutendaji ni dhaifu??!! Yaani nikiendelea kukupa matukio mengi ya maneno ambayo yakisemwa na mwanaccm huwa sio tusi lakini yakisemwa na mpinzani ni tusi nitamaliza mwezi mzima nikwa sija maliza

Tuko pamoja mkuu ulipoweka alama za kunukuu katika neno MATUSI nimekuelewa isipokuwa najaribu kuweka wazi kwa wale wakurupukaji
 
hawa watoto kwa matusi hawajambo.... sasa mtu mzima kama mie na mwanangu wa kutoa mgogoni kwangu eti nikanye kweli....??? haya kijana nimeshatoka kunya kama ulivyoshauri...... lakini wewe najua ni damu yangu labda tu mzazi mwenzangu hajakutaarifu
 
Vichaa hakika ni wengi Tz, unaweza je kumsifu mtu ayemtukana Mkombozi wa nchi yako kuwa ni msanii, mwongo, mtapeli... Je! kwanini asherekee tarehe ya uhuru ambayo mtu alimwita tapeli ali iomba? kwa nini anakuwa off siku ya kifo cha mwalimu? Lissu ni kichaa na msaliti wa nchi hii.

Mkombozix100! Akili ya ajabu ya wenye div.5. Je bila nyerere Tanzania isingekuwa huru? Je mawazo ya akina mkwawa na watemi wengine yako wapi? Lazima tuwe na mawazo huru tusikubali kuwekwa ndani ya kapu la akili ya mtu fulani.
 
Nadhani walioko bungeni wametawaliwa na nidhamu ya uoga, kwani wanajeshi si watanzania? Nani kawazuia kuchukua nchi hii, ni ccm? Ntakuwa na uwalakini nao kama watashindwa kuchukua nchi ktk kipindi hiki ambacho maoni ya wananchi yanapotoshwa, huku wakijidai kuwa ni walinzi wa wananchi wa Tanzania. Nashangaa kuona polisi inazuia watu kutoa maoni yao, huku nao wanamaisha magumu yasiyoelezeka, wametulia na kukubali kutumiwa vibaya. Igeni jeshi la Misri. Wale ndo watetezi wa wananchi. "Big up. Egypt navy"
 
Back
Top Bottom