Tundu Lissu: Hizi Pikipiki zinatengenezwa China kwa Mamilioni lakini China hakuna Bodaboda hivyo Siyo Ajira

Viwanda gani vya kulipana ef 7 siku nzima. Kama viwanda vitaanza kulipa elfu 7 kwa lisaa limoja hutaona mtu anapurukushana barabarani na maboda boda. Hata wakilipa elf 4 kwa lisaa bado ni pesa nzuri ambayo itapu nguza kundi kubwa kwenye betting na boda boda.
Betting itaongezeka pia
 
Hakuna hoja ambayo mtu yeyote anaweza kuleta kuhusu kuhalalisha bodaboda kama usafiri wa umma. Hoja hiyo itakuwa na mashiko, labda mbele ya watu wenye uelewa duni.

Watengenezaji wenyewe wanatoa tahadhari kuhusu matumizi ya pikipiki wanazotengeneza kuwa kwaajili ya usalama, pikipiki itumike na mtu mmoja tu kwa sababu kukiwa na abiria nyuma, mwendesha pikipiki akifunga break ghafla, abiria atamsukuma mbele dereva.
Pia barabara ni nyembamba wengi wanasukumiwa mitaroni,
 
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema China inatengeneza Mamilioni ya Pikipiki lakini nchi hiyo haina Bodaboda.

Lissu anasema, Vietnam inatengeneza Pikipiki lakini nchi hiyo haina usafiri wa Bodaboda.

Mwisho Lissu anamuunga mkono Lema kwamba Bodaboda siyo Ajira.

Chanzo: Jambo TV
Kwa maana halisi ya neno ajira... "Ajira (kutoka neno la Kiarabu) ni kazi yoyote ambayo mtu anafanya kwa malipo katika kampuni, ofisi za serikali au kwa mtu mwingine binafsi." Kwa maana hii hutoona hizo boda huko China na Vietnam
 
Viwanda gani vya kulipana ef 7 siku nzima. Kama viwanda vitaanza kulipa elfu 7 kwa lisaa limoja hutaona mtu anapurukushana barabarani na maboda boda. Hata wakilipa elf 4 kwa lisaa bado ni pesa nzuri ambayo itapu nguza kundi kubwa kwenye betting na boda boda.
Walipwe buku 7 lakini wana uhakika wa kuzeeka wakiwa na miguu yote miwili na vidole vyake
 
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema China inatengeneza Mamilioni ya Pikipiki lakini nchi hiyo haina Bodaboda.

Lissu anasema, Vietnam inatengeneza Pikipiki lakini nchi hiyo haina usafiri wa Bodaboda.

Mwisho Lissu anamuunga mkono Lema kwamba Bodaboda siyo Ajira.

Chanzo: Jambo TV
hivi nyie chadema kweli hii ya bodaboda ndo hoja ya msingi kwa watanzania lisu na lema na cdm
 
hivi nyie chadema kweli hii ya bodaboda ndo hoja ya msingi kwa watanzania lisu na lema na cdm
Msingi wa hoja yao ni kwamba ccm walianzisha boda boda ili kuwakomoa chadema kwa kuwafanya vijana kuwa bize wasishiriki haraki za chadema.
 
HAWA WANASIASA WAKIMPATA MTU MPUMBAVU WANACHEZEA KICHWA CHAKE KAMA NGOMA,
Hawa ni bodaboda wapo Beijing, China wanasubiri kula vichwa,
#BODABODA TANZANIA RISEUP, TUIKATAE CHADEMA TUPO WENGI TUNATOSHA TUSIDHARAULIWE!
FB_IMG_1678257216428.jpg
 
HAWA WANASIASA WAKIMPATA MTU MPUMBAVU WANACHEZEA KICHWA CHAKE KAMA NGOMA,
Hawa ni bodaboda wapo Beijing, China wanasubiri kula vichwa,
#BODABODA TANZANIA RISEUP, TUIKATAE CHADEMA TUPO WENGI TUNATOSHA TUSIDHARAULIWE! View attachment 2541400
Acha ujinga wako mkuu, wamesema boda siyo ajira sasa mihemko ya nini! Leo hii wewe apo unaweza mruhusu mwanao akaifanye boda kama kazi yake au unawajaza hao boda ujinga wako ndg,
 
Chadema siku zote wao ni kupinga maendeleo tu
Kwa hiyo wewe unaona ni sawa kwa vijana woote wa kitanzania kutumia boda kama ajira huku wakimalizwa au kufanywa vilema watokanao na ajari za pikipiki hasa ukifikiria kwamba ajira yenyewe haina bima kama ajira zingine?
 
Hizo ajali hazina suluhisho la kuzipunguza?
 
China wanafundishwa maarifa ya kujitegemea na kujiajiri wenyewe kwa hiyo huo sio mfano hai. India na Nigeria zenye uchumi mkubwa kuliko Tanzania lakini wana usafiri wa bodaboda. Zanzibar zamani walijifanya wana ustaarabu kama Oman na Uarabuni wakapiga marufuku pikipiki za usafiri kibiashara lakini sasa hivi huko ndiko kuliko tamalaki usafiri wa bodaboda. Mzungu akija Tanzania ili afurahie matembezi katika mji husika hakodi taxi anachukua boadaboda.

Chanzo cha usafiri wa bodaboda Tanzania ni ukiritimba uliokuwepo miaka ya nyuma kati ya mpaka wa Tanzania na Uganda ndipo vijana wa huko wakabuni usafiri wa kupita vichochoroni hadi anafika nchi nyingine bila kusumbuliwa na mpakani kulipia ushuru na kodi.

Wanasiasa walipiga vita jitihada za JPM kuhamasisha kujengwa viwanda ili vijana wengi waajiririwe huko na serikali haina uwezo wa kuajiri kila kijana anayehitimu chuo sasa hivi ndio maana unakuta viongozi wanahamasisha pamoja na kupata maarifa ya nadharia chuoni lakini hawana uwezo wa kubuni mradi wakiwa kikundi na kuomba mkopo wakaanzisha shughuli za kiuchumi kujipatia kipato na maendeleo binafsi pamoja na kuchangia pato lataifa hivyo wanashauriwa kwenda VETA ambapo ukimaliza hakuna kitu kinashinda kufanya mtaani.
Nani alimpinga JPM kwenye ujenzi wa viwanda?? Viko wapi alivyojenga
 
Mgejua umhimu wa bodadoda vijijini katika shughuli za kilimo na usafilishaji wa mazao kutoka mashambani yani si kitu cha kureta utani cdm ilisha poteza mwelekeo imebaki kufa tu kama vingine
Kwa nini mkulima asiwe na pikipiki yake ya kumpeleka na kurudi shambani na mazao yake akijiendesha mwenyewe? Kwa sababu mifumo haijaruhusu kitu hicho!
 
Back
Top Bottom