Tundu Lissu ambana RPC mahakamani, RPC ashikwa kigugumizi (Shein na Seif) nao wahitajika mahakamani

Hii article ungeiweka vizuri kwa sasa kuna eneo linajirudia rudia zaidi ya Mara tatu edit basi.
Kama umeshasoma na kuelewa kunasehemu inajirudia shida inakuwa wapi?Lengo hapo nikukupa yaliojiri Mahakamani na sio kujuchapishia hadithi na kukupangia utakavyo wewe.
Wakati mwingine inakatisha sana tamaa,mtu anakupa kitu ambacho ulikuwa hukijui badala ya kumwambia asante kwa ujumbe au taarifa unaanza na maneno kumkatisha mtu tamaa.
Mmmmmh vichwa hivi jamani Mungu atusaidie
 
Ultimately gymnastics za Tundu zitafika mwisho.Anadhani ana akili kupita watu wote ! Ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu, wahenga walisema !




Ili kumnasa Lissu inatakiwa Amri(maelekezo)kutoka juu(kuzimu)kama yale waliyoekezwa waliokuwa wanamshikilia Lema kwa miezi minne,au yale yaliyotolewa dhidi ya Lijualikali au Suleiman Mathew,vinginevyo hakuna namna mnavyoweza kumtia Lissu hatiani.

Anayeifahamu njia ya Maji hawezi kusombwa na maji,Lissu kwa uelewa wake wa sheria hawezi kunena/kutenda yale yanayoweza kumtia matatani,kama angekuwa ametenda kosa lolote hata la bahati mbaya,kwa jinsi anavyoidharirisha serikali katika uringo wa sheria,hakika wangekuwa wameshamhukumu kwenda jela bila faini.
 
Hako ni ka irregularity kadogo sana ambacho hakiaribu substance ya ushahidi mzima , ni curable kabisa kwani ushahidi huwa haunyoooki asilimia 100 kama rula
Heh! Unaongea kisheria au kisiasa. Umefuatilia hukumu iliyomwachia kasusura msingi wake ilikuwa nini!? Ok. We are here to learn.
 
Jamaa elimu yake ikoje kama anashindwa kuhesabu aya? hatari sana



Matokeo ya Elimu huwekwa kwenye cheti(makaratasi)Usiliamini kila karatasi liitwalo cheti ukadhani lina matokeo sahihi,yawezekana kilichomo kwenye cheti ni zao la Bashilelism.

Nimeyadharau sana Makaratasi yanayoitwa vyeti vya elimu,tena yale yenye "Title" kubwa kama PhDs,Bachelors na nyinginezo.Ulishawahi kujiuliza PhD ya mafuta ya maganda ya korosho imeleta tija gani kwa Taifa tangu atunukiwe mwenye nayo?Au yule aliyepewa PhD baada ya "kukokotoa" umuhimu na faida za serikali tatu na baadae akalikana andiko lake lililompatia cheti chake cha " Permanent Head Dissoder(PhD)"?
 
Kama umeshasoma na kuelewa kunasehemu inajirudia shida inakuwa wapi?Lengo hapo nikukupa yaliojiri Mahakamani na sio kujuchapishia hadithi na kukupangia utakavyo wewe.
Wakati mwingine inakatisha sana tamaa,mtu anakupa kitu ambacho ulikuwa hukijui badala ya kumwambia asante kwa ujumbe au taarifa unaanza na maneno kumkatisha mtu tamaa.
Mmmmmh vichwa hivi jamani Mungu atusaidie

Niliyemuomba amenieleza tatizo na amenielewa,tatizo ni chanzo.Tena nimemuomba kwa nidhamusiyo kwa kumkatisha tamaa.

Nisamehe bure basi
 
HABARI
pic+lissu+ambana+RPC.jpg

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamdani
  • Lissu alimuuliza swali hilo Kamanda Hamdani aliyekuwa akitoa ushahidi jana kwenye kesi ya tuhuma za uchochezi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba katika Mahakama ya Kisutu.

Dar es Salaam. Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amemhoji Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamdani sababu za kutoshtakiwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif, Rais Ali Mohamed Shein na Hassan Nassor Moyo waliotajwa kwenye makala inayodaiwa ya uchochezi.

Lissu alimuuliza swali hilo Kamanda Hamdani aliyekuwa akitoa ushahidi jana kwenye kesi ya tuhuma za uchochezi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba katika Mahakama ya Kisutu.

Kamanda Hamdani aliyekuwa akiongozwa kutoa ushahidi na Wakili wa Serikali, Paul Kadushi alikumbana na swali hilo ulipofika wakati wa maswali ya kuhoji kutoka upande wa utetezi.

Lissu alitilia mkazo swali hilo kwa maelezo kwamba Kamanda Hamdani ndiye mlalamikaji na kiini cha kesi hiyo. Washtakiwa wengine ni, Jabir Idrissa na Simon Mkina ambao kwa pamoja wanadaiwa kuandika na kuchapisha taarifa‎ za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.

Akijibu swali hilo la Lissu, Kamanda Hamdani alisema Rais Shein, Maalim Seif na Moyo hawajashtakiwa katika shauri hilo na kwamba yeye hana jukumu la kuwafungulia mashtaka.

Lissu aliendelea kumuuliza shahidi huyo wa upande wa mashtaka kwamba katika maelezo yake (Kamanda Hamdani) ya polisi aliwataja Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad, Rais Dk Ali Mohamed Shein na Mwanasiasa Mkongwe, Hassan Nassor Moyo na kusema maneno yao hayakuwa ya uchochezi.

Hata hivyo, Kamanda Hamdani alijibu swali hilo kwa kusema kuwa hakuwataja.

Lissu alimuonyesha shahidi huyo gazeti la Mawio la Januari 14, 2016 na kumtaka amweleze Hakimu Simba idadi ya aya za makala inayodaiwa kuwa ya uchochezi iliyokuwa na kichwa cha habari cha ‘Machafuko yaja Zanzibar’.

Baada ya kuulizwa swali hilo, Kamanda Hamdani alimueleza Lissu kuwa hawezi kuzihesabu, lakini mahakama ilitoa maelekezo azihesabu, akaomba muda akapewa, akazihesabu kuwa zipo nane.

Lissu alidai kuwa yeye amezisoma zipo 55 na kwamba aya 37 ni za maneno ya Maalim Seif, aya nane ni za maneno ya Tundu Lissu, aya nne ni za maneno ya Moyo na kwamba kwenye aya tatu, ametajwa Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Kamanda Hamdani alidai kuwa ni sawa.

Aliendelea kumhoji shahidi huyo wa upande wa mashtaka kwamba:

Lissu: Kwa uelewa wa akili yako anayetajwa mara nyingi kwenye makala hiyo inayodaiwa kuwa ni ya uchochezi ni nani?

Kamanda Hamdani: Maalim Seif.

Lissu: Wakati unaisoma makala hiyo ulibaini kuwapo kwa matamshi ya chuki na uchochezi dhidi ya Serikali ni kweli ama si kweli?

Kamanda Hamdani: Ni kweli.

Lissu: Kwa uelewa wako mtu anayetoa matamshi yenye kuibua hamasa au chuki dhidi ya Serikali ni lazima uwe uchochezi?

Kamanda Hamdani: Kwa uelewa wangu ni lazima uwe uchochezi.

Lissu: Alimuonesha shahidi huyo hati ya mashtaka na ya maelezo ya awali (PH) na kuuliza ni sawa nikisema makala nzima ya ‘Machafuko yaja Zanzibar’ ilikuwa ni makala ya uchochezi?

Kamanda Hamdani: Ni kweli.

Lissu kama makala yote ni ya kichochezi wote walioshiriki ni wachochezi?

Kamanda Hamdani: Ni sahihi.

Lissu: Ni kwa nini Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad, Rais Dk Ali Mohamed Shein na mwanasiasa mkongwe, Hassan Nassor Moyo hawajashtakiwa, kwa nini Tundu Lissu pekee ameshtakiwa?

Kamanda Hamdani: Jukumu hilo siyo la kwangu, mimi ni mlalamikaji.

Lissu: Kwenye lengo lako mbaya wako alikuwa ni Tundu Lissu?

Kamanda Hamdani: Hapana sina ubaya na Lissu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 3, itakapoendelea kusikilizwa.

Chanzo: Mwananchi
Duuu aiseee lisu ni sooo sijawahi ona walahi ningekuwa na muda ningekuwa nahudhuria kesi zake.
Ndio maaana mapolis wanakufa haraka
 
Duh Lissu anafinyanza atakavyo. Elimu Elimu Elimu. Lissu defines future ya Tanzania, Tanzania ya ukweli siyo Tanzania ya CCM ya utapeli ulio kubuhu.
 
Hahaha huyu ndiye yule alikuwa anasema sijui kila swali na leo hapo tena kabananishwa hadi anatia huruma

Serikali mkiwa na kesi za namna hii kwa mtu kama Lisu basi jitahidini kuwaweka mashaidi wanaojielewa ,sasa huyu hata kuhesabu aya ya kwenye makala hawezi ndio atatoa ushahidi wa kumuweka Tundu hatiani ?

Savage
inawezekana hata makala hajui ni nini, maana kama zipo 55 lakini yeye kaona ni nane? mimi wala simlaumu yeye, wote mnajua nani wa kulaumiwa, huyo katumwa tu masikini wala hana hatia baba wa watu, huyo hata angeulizwa kafata nini mahakamani angejibu sijui
 
Haa ha ha ha, LIssu ni shidaaa, khaa. Kumbe police wakiwa mtaani wababe, wakikutana mahakamani kwa wenye ofisi zao huko wanakua wapole hivi? NImeelewa kwanini Dr. Mwanafyale hataki jamaa awe raisi wa kile chama cha manguli wa sheria aise.
 
Kamanda hajui kuhesabu aya?, acheni masihara bhana. Nimejiuliza hiyo ni makala ya namna gani ya aya 8 tu tena kwa gazette la makala. Ubaya wa kutumika badala ya weledi ni aibu.
 
Ultimately gymnastics za Tundu zitafika mwisho.Anadhani ana akili kupita watu wote ! Ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu, wahenga walisema !
Mie nilijua unafuatilia mwenendo wa kesi kumbe una hasira na lissu?? Sheria sio taarabu .
 
Back
Top Bottom