Tundu Lissu achambua Muswada wa Huduma za Vyombo vya Habari bungeni

Sio kwa staili iyo mkuu,.
Kauli zake hazikua na uhalali wa kuaminiwa mpaka Mwakyembe atie neno la kukubali au kukataa.
Tunahitilafiana katika kuelewa mambo.Mimi naamini alikuwa anajaribu kumvua nguo mwalimu wake.
 
Mhe Lissu ni kichwa sana na anajua kuwa Mwakyembe kuwa anajua huo ukweli lakini tatizo sio Mwakyembe bali wameamua kujifanya wale malaika wa kuzima uhuru wa habari..

Nimeisikia ile clip ya hitimisho ya Nape.....yaani badala ya kujibu hoja za wabunge yeye alijibu hoja ya Zitto kwa vijembe.

Mimi navyoona hawa mawaziri sio wabunifu bali wanafanya mambo kwa matukio ili kumfurahisha mkulu na hili ni tatizo letu sisi weusi hatufanyi kitu kwa kuacha jina bali tunajali sana leo na matumbo basi.......
 
Sio kwa staili iyo mkuu,.
Kauli zake hazikua na uhalali wa kuaminiwa mpaka Mwakyembe atie neno la kukubali au kukataa.
Kaka Jambazi wewe utakuwa wale majambazi wanaovua viatu wakifika nyumba yenye zulia safi kuiba. Unaposema sio kweli si ni wajibu wako kuusema ukweli?
Usikute Mwakyembe haijui hata hiyo sheria ya 1928 na 1952 ndio kwanza anasikia hapo. Lazima mtu aliyefanya research ya jambo alisemalo tumpe credit zake maana kazungumzia jambo kisayansi.
 
Baada ya Tundu Lissu kutoa hoja nzito kuhusu baadhi ya vifungu ktk muswada huu wa Huduma za Vyombo vya Habari tunasubiri kuona kama Rais John Pombe Magufuli atatumia uwezo/mamlaka yake kutousaini.

Maana ijumaa tarehe 4 November 2016, katika mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari Mh. Rais ''alisema'' kuwa taasisi ya Urais ni kubwa kuliko mihimili mingine ya dola yaani Bunge na Mahakama. Na kama taasisi ya URais ina uwezo wa ''kupiga kura ya veto'' tunategemea Rais kutousaini muswada huu na badala yake ataurudisha Bungeni ufanyiwe marekebisho kuondoa ''mabaki'' ya ''kikoloni''.
Tanzania imeiga ukoloni alioukataa kila mwenye akili ya kibinadamu duniani , Hii ccm ipigwe vita kiukweli sana , mara zote tumesema humu kwamba TUNAPIGANIA UKOMBOZI nadhani sasa mmeelewa

Ipuuzeni kauli ya mkapa kwamba eti nchi ilishakombolewa , ushahidi ni huu hapa .

Hongera MAOKOLA MAJOGO , HONGERA TUNDU LISSU , Aibu kubwa iwapate HARISSON MWAKYEMBE na NAPE NNAUYE .
 
Lissu nakupenda sana kwa taaluma ako ya sheria hakika mungu kakupatia kipaji cha pekee na kama Tanzania tusingekuwa tunaangalia vyama wewe ndio ungekuwa waziri wa katiba na sheria au mwanasheria mkuu kulingana na uwezo wako wa sheria ni mkubwa sana
Nlishasema hiki kitu mkuu
 
Ajahahahaha umenifurahisha umetumia style ya kipekee kujaribu kumvuta lkn ametumia akili nyingi ya tundu lissu kujificha inaweza akawa anajua kua akuna cha kupinga hapo hata yeye ajafurahisha na sheria iyo pia
Ila kama angekuwa ametajwa Lowassa, dadadek angejaa kwenye screen
 
Lizabon kama hajapewa pesa huwa haingii JF yy hana kazi anaishi kwa kuwatetea ccm lakini pindi wakimlipa tu.
Ila akitajwa Lowassa, hata bila ujira lazima aje ajilipue, angalau amseme kidogo. Sijui huyo baba wa watu alimfanyaje Lizaboni.
 
Hatari iliopo nchi inaendeshwa Kichina china. Wachina wana manifesto yao ya ""the communist party""
"'Modern Chinese history well indicates that without the Communist Party, there would have been no New China. Neither would there be China's socialism. Only with the leadership of the Communist Party of China can there be victory of the socialist cause with Chinese characteristics. Only with the leadership of the Party can the Chinese people have a brighter and more hopeful future."" Na huu ndio msimamo wa watawala wetu, Ndugu zangu katika jamii forums, nimetafakari na nikajiuliza hizi siasa za kwetu mbona namna hii?. Nikakambuka zawadi waliopewa CCM kujengewa makao makuu na wachina kisha mchina akajisifia kuwa ana mwenzake. Ndipo nilipofungua manifesto yao kiabla hata sijasoma naanza kuona mafanano fulani fulani.
 
Only in Africa a Dr by Phd,Prof,Masters Holder or Degree Holder can argue like .... and .... can argue like Dr or prof ,Only in Africa things goes ant-clock wise
 
Lakini nikuulize swali bwana Lissu,wako wapi unaowatetea?Mbona wenye nchi wako kimya tu?Watanzania ni wa kuachwa tu,unajisumbua bure!Wameridhika wao hata wakitiwa kidole machoni wanakaa kimya.Wewe Lisu peleka sheria zako Ulaya huko ukapige pesa uenjoy maisha wewe na wanao na wajukuu na vitukuu vyako.Watanzania achana nao,wamelogwa na zile mbio za ile sanamu ya kuzunguushwa nchi nzima!Hopeless kabisa!
 
Back
Top Bottom