Baada ya Tundu Lissu kutoa hoja nzito kuhusu baadhi ya vifungu ktk muswada huu wa Huduma za Vyombo vya Habari tunasubiri kuona kama Rais John Pombe Magufuli atatumia uwezo/mamlaka yake kutousaini.
Maana ijumaa tarehe 4 November 2016, katika mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari Mh. Rais ''alisema'' kuwa taasisi ya Urais ni kubwa kuliko mihimili mingine ya dola yaani Bunge na Mahakama. Na kama taasisi ya URais ina uwezo wa ''kupiga kura ya veto'' tunategemea Rais kutousaini muswada huu na badala yake ataurudisha Bungeni ufanyiwe marekebisho kuondoa ''mabaki'' ya ''kikoloni''.