Tunashuhudia amani kwa mara ya mwisho Tanzania

Kwa mwendo huu, hata Iraq inaweza kujiita nchi ya amani. I don't like this development in Tanzania. With the current data on attacks in churches in Tanzania, I am afraid we can no longer boast about being the haven of peace in Africa.That is for sure
 
I declare my interest kwa kusema mimi ni Mkiristu Mkatoliki.

Je mfumo wa usalama wa nchi hii umeanguka?

Kuna matukio mengi yametokea ambayo haijawahi kuyasikia nchini mwetu.sasa najiuliza je ni kweli mfumo wa wetu wa usalama nchini umepoteza muelekeo?

Padri alijeruhiwa kwa risasi huko Zanzibar hakuna aliyetabiri na pia hakuna aliyewajibishwa katika hili.

Padre akauawa huko huko Zanzibar hakuna aliyewajibishwa mpaka leo !kwa sasa kuna kesi inaendelea kuke zanzibar.

Mchungaji alichinjwa huko Geita hakuna aliyewajbishwa!

Leo hii Parokia Bikra imehujumiwa kwa kupigwa bomu hakuna aliyewajibishwa.

Ukiachana na matukio hayo kuna matukio kadhaa kama ya kutekwa na kuteswa kwa Dr Ulimboka na Kibanda lakini muhusika hajulkani!

Hivi ni kwa nini tumeshindwa kuwatambua na kuwawajibisha wahusika wa matukio haya ya kipekee na ya ajabu nchini?

Je serikali kupitia usalama wa taifa inakiri kushindwa katika hili?
 
Kufuatia matukio ya uvunjifu na upotevu wa amani katika maeneo anuai nchini kwa sasa, na kwa upande mwingine tabia za viongozi kufuatia matukio haya; yanatuacha wananchi wa Tanzania tukifikiri Tanzania si shwari?

Mathalan mlipuko wa bomu Arusha na hali ya viongozi wetu kutuma pole kwenye Twitter je ni sahihi. Inatia hasira sana.

Hata hivyo inatuamsha watanzania kuwa macho zaidi na kizazi hiki cha viongozi; wapenda raha, wasiojali kazi, kuangalia maslahi binafsi, kujilimbikizia mali na ufisadi uliotukuka ndiyo vinavyowajaa vichwani.

Lakini potelea kwa mbali 2015 tutawachagua kwenye Twitter pia.
 
[h=5]USALAMA WA WATANZANIA HAUPO LAKINI USALAMA WA TAIFA UPO.
Kwa mujibu wa Sheria ya Bunge namba 15 ya mwaka 1996(intelligence & security services act number 15 of 1996)iliyosainiwa na kupitishwa rasmi kuwa sheria na rais wa 3 Benjamin Mkapa tarehe 20/1/1997,pamoja na kazi nyingine na majukumu mengine ya kiusalama kazi ya taasisi hii itakuwa ni,
1:kutafuta na kukusanya taarifa zote za kijasusi kutoka nje na ndani ya nchi,
2:kuchambua,kuainisha hatari zinazo likabili taifa kutoka kwenye maadui wa ndani na nje ya nchi,
3:kutekeleza mipango ya kukabiliana na hatari hizo .
So kutokana na mambo mbalimbali yanayoendelea nchini mwetu je idala hii nyeti imekufa,imelala,imekosa weledi,imesisinzia,inatumiwa na kutumika kisiasa ama inajua kinachoendelea?matukio makubwa ambayo yalipaswa yazibitiwe na idala kama ufisad wa Richmond,Tanglord,Meremeta,EPA,DOWNS na utoroshwaji wa wanyama hai na ndege za kijeshi za nje?Mauji na vitendo vya kikatili zidi ya watu na viongozi maarufu kama kuteswa na kupigwa kwa Dk Ulimboka na Absalom Kibanda,kupigwa risasi na kujeruhiwa kwa padri Ambros,kumwagiwa tindikali kwa shekhe huko Zanzibar,kukabiliana na mihemko ya kidini,kisiasa na kikabila ni jukumu lao pia na sasa limetokea leo huko Arusha,
kama kweli idala hii ingekuwa macho na hai ingewezekana vipi kwa mharifu wa leo aliefanya kitendo hiki kupanga na kutekeleza kitendo cha kulipua mlipuko huo bila hata kutiliwa mashaka na kukamatwa,ama watuambie imekuwaje,ama wanatufanyia ajenda setting kutusahaulisha kashfa inayomkabili katibu mkuu wa CCM bwana Kinana kutuhumiwa bungeni kwa kashfa ya ujangili wa meno ya tembo?watuambie ukweli na vipi kwa viongozi wake kuwajibika hapa namaanisha mkuu wa kitengo hiki Othman Rashidi na naibu wake Jack Zoka,wanasubiri nini kuwajibika?[/h]:pray2:Kwa hisani ya john Mnyika FB group
 
Watanzania wenzangu tuichunge amani ya nchi yetu kama mboni ya jicho letu,tusishawishike wala kurubuniwa na walafi wa madaraka na uchu wa rasilimali tuliyo nayo.
Wahenga walituusia kuwa kama hujui kufa chungulia kaburi,tuna mifano mingi ya athari na madhira makubwa waliyopata jirani zetu wa DRC,Burundi na Rwanda.hii yote ni kwa sababu ya kuichezea amani.Tusithubutu kuichezea amani yetu Watanzania.
mungu Ibariki Tanzania
 
Umeongea kitu cha maana sana, ubarikiwe kwa ujumbe mzuri.
Lakini wasioipenda Amani watakuja hapa na mawazo yao kama Maryenge ya Mbowe utawaona tu.
 
linapokuja suala la usalama wa nchi yetu sipati picha kwanini ccm na kushindwa kote wanashindwa omba msaada toka serikati kivuli?

Watu wanauwawa ,mali zinaharibi ccm wanazunguka km pia wakisubiri mambo yaishe yenyewe,na kunyamazisha wahanga kwa hofu eti muovu akisikia amani itatoweka.

Kutunza usalama na rasilimali ya nchi ni jukumu la wote,ccm wanakua kuwa hilo halihitaji chama.nadhadhani watoe kiburi na kuomba msaada.unaona aibu kufa wakati kila mtu lazima afe?
 
amani tz ipo na itaendelea kuwepo sana tu wasiwasi chadema ikiingia ikulu duuhh!! Vita itakuwepo maana wanauchu wa madaraka na vijana tunasukumwa tu na wanasiasa wala hata hakuna sera na mawazo ya vijana ila ni kufuata tu!

Wakiitwa vijana na wewe unaweza kwenda kweli?.Hakuna kijana mwenye narrow thinking capacity kama hiyo uliyonayo wewe.Lazima utakuwa above 80 years old.
 
Wadau wenzangu kuna swali najiuliza tokea jana na sijapata jibu sahihi pengine mlioko huku mnaweza kunisadia... Hivi intelligence ya Police ni kwa ajili ya mikutano ya CHADEMA NA LEMA au ni kwa ajili ya matukio kama hili lililotokea jana la mabomu??
Nawasilisha......
 
Hivi Mlipuko wa Bomu kwenye mkutano wa Chadema Arusha ni mkakati mpya wa CCM kutishia na kuangamiza wanachama na wapenzi wa Chadema? au ni matokeo ya propaganda ile ya kusema Chademe ni chama cha wakristo ili chama kiandamwe na magaidi? Hivi polisi huwa wanafanya nini katika mikutano hii kwa nini wanashindwa kuzuia vitendo hivi? au wamekuwa POLICCM? Tusiichezee amani, Kuna umuhimu wa kupinga vitendo hivi kwa nguvu zote kwani wanaopoteza maisha ni watanzania bila kujali itikadi zao za vyama. Siasa ni watu, kama watu wataikimbia mikutano ya siasa tunakaribisha utawala wa kidikteta.
 

Attachments

  • 1.jpg
    1.jpg
    47 KB · Views: 170
Hakuna demokrasia Tanzania. Kauli na matendo ya Rais Kikwete vinaonyesha wazi kuwa hawezi kulinda demokrasia.
 
Back
Top Bottom