Polisi watatu wafungwa miaka 20 jela kwa Rushwa

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,834
18,836
Askari hawa walikuwa wakifanya mambo aliyokuwa anayependa Magufuli kipindi chake . =================================================
IMG_20240107_071348.jpg

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewahukumu Askari Polisi watatu wa zamani wa Jeshi hilo Mkoa wa Arusha ( Inspekta Hillary Ferdinand Komba, Bartholomeo Augustine Maya na PC Apornary Proches Burretta ) kifungo cha miaka 20 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka.


Kosa lao hilo la matumizi mabaya ya madaraka walilifanya tarehe 19 March 2021 walipokwenda nyumbani kwa Profesa Justin Maeda Wilayani Arumeru, Arusha na kufanya upekuzi pasipo kufuata utaratibu kisha kutumia nguvu na kumchukua Profesa huyo hadi kwenye Benki mbili pamoja duka lake moja la vifaa vya ujenzi walikomlazimisha atoe pesa ( anazodai ni milioni 100) na kuwapatia ili wasimfikishe kwenye vyombo vya sheria wakimtuhumu kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo na ngozi ya chui.


Profesa Maeda kwenye mahojiano ya @AyoTV_ April 2021 alisema Askari hao walimtaka awape kiasi hicho cha pesa lasivyo atashtakiwa kwa uhujumu uchumi na walimtisha kuwa jela inamuhusu, kitisho ambacho kilimfanya awape pesa hiyo harakaharaka ili kuepuka kupelekwa mahabusu au jela akihofia hali yake mbaya ya kiafya aliyokuwa nayo wakati huo.


Japokuwa Profesa Maeda alidai kuwapa Askari hao milioni 100 kwa tuhuma hizo alizodai ni za uongo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ikitoa hukumu kwa Askari hao leo imesema kiwango cha pesa walichokichukua kwa Profesa huyo ni shilingi milioni 73.


Sakata hili la Askari hao watatu liligundulika kwenye Vyombo vya dola baada ya Profesa Maeda ( pichani kulia) kujitokeza na kufikisha malalamiko yake kwa Vyombo hivyo ikiwemo TAKUKURU na Jeshi la Polisi ambalo baada ya uchunguzi wake liliamua kuwafukuza kazi Askari hao mwezi mmoja baadae. #MillardAyoMAHAKAMANI
 
Walitakiwa wapate Mvua 30 na kuendelea kitendo cha kwenda kutupa kipande cha Jino la Tembo kwenye shamba lake ni kosa kubwa sana na je hao Polisi kupatikana na Jino la Tembo sio kosa walilipata wapi mpaka kulitumia mbona kama kesi imefunikwafunikwa majani...
 
Back
Top Bottom