Nsabhi
JF-Expert Member
- Feb 23, 2011
- 1,093
- 162
Tatizo tulilo nalo kwa sasa ni kwamba viongozi wetu wakuu wanapenda sana udini na wanaulea. Na sijui wanafanya hivi kwa maslahi ya nani.Sheikh Ponda kaanza uchokozi siku nyingi lakini akina mwema wamekuwa wakimchekea tu. Anatukana Wakristo lakini Mwema na viongozi wengine wa juu wanamchekea tu. Uamusho nao wameanza uchochezi muda mrefu lakini si Rais wa Jamhuri wa wa Zanzibar aliyewakemea. Wameachwa mpaka amani ya nchi inatishiwa. Lakini viongozi wamekuwa hawachukui hatua zozote. Jamani hii nchi viongozi mnaipeleka wapi? Mnataka Watanzania wachinjane? Mnaongoza kwa kufuata katiba ipi ambayo mliapa kuilinda? aaT
Viongozi wa kasheshe hizi sio wazawa kumbe wa TZ ??? Mhh kweli changanya na zako. Mimi naamini bado tunaweza kuilinda amani yetu. Ila ukweli kabisa serikali inahusika kabisa kuvuraga amani hii. Lazima wote tuheshimu sheria za nchi na uhuru wa kuabudu. Vikundi vyote vya kichochezi na ambavyo havifanyi kazi kwa mujibu ya maombi ya usajili wao vifutwe. Na wale wote wanaotumia dini kuvunja sheria waathibiwe kwa kosa lao sio kosa la kidini. Mungu atusaidie kwani wote walianza hivi hivi mwisho wakimbizi. Hauna sehemu nzuri ya kuishi kama TZ kama hamwamini leteni kasheshe tuwe wakimbizi halafu tutasomanamba.